< İbraniler 9 >
1 İlk antlaşmanın tapınma kuralları ve dünyasal tapınağı vardı.
Agano la kwanza lilikuwa na taratibu zake za ibada na pia mahali patakatifu pa ibada palipojengwa na watu.
2 Bir çadır kurulmuştu. Kutsal Yer denen birinci bölmede kandillik, masa ve adak ekmekleri bulunurdu.
Palitengenezwa hema ambayo sehemu yake ya nje iliitwa Mahali Patakatifu. Humo mlikuwa na kinara cha taa, meza na mikate iliyotolewa kwa Mungu.
3 İkinci perdenin arkasında En Kutsal Yer denen bir bölme vardı.
Nyuma ya pazia la pili, kulikuwa na hema iliyoitwa Mahali Patakatifu Kupita Pote.
4 Altın buhur sunağıyla her yanı altınla kaplanmış Antlaşma Sandığı buradaydı. Sandığın içinde altından yapılmış man testisi, Harun'un filizlenmiş değneği ve antlaşma levhaları vardı.
Humo mlikuwa na madhabahu ya dhahabu kwa ajili ya kufukizia ubani, na Sanduku la Agano, ambalo lilikuwa limepakwa dhahabu pande zote, na ndani yake mlikuwa na chungu cha dhahabu kilichokuwa na mana; fimbo ya Aroni iliyokuwa imechanua majani, na vile vibao viwili vilivyoandikwa agano.
5 Sandığın üstünde Bağışlanma Kapağı'nı gölgeleyen yüce Keruvlar dururdu. Ama şimdi bunların ayrıntılarına giremeyiz.
Juu ya hilo Sanduku kulikuwa na viumbe vilivyodhihirisha kuweko kwa Mungu, na mabawa yao yalitanda juu ya mahali ambapo dhambi huondolewa. Lakini sasa, hatuwezi kusema kinaganaga juu ya mambo hayo.
6 Her şey böyle düzenlendikten sonra kâhinler her zaman çadırın ilk bölmesine girer, tapınma görevlerini yerine getirirler.
Mipango hiyo ilitekelezwa kisha ikawa desturi kwa makuhani kuingia kila siku katika hema ya nje kutoa huduma zao.
7 Ama iç bölmeye yılda bir kez yalnız başkâhin girebilir. Üstelik kendisi için ve halkın bilmeden işlediği suçlar için sunacağı kurban kanı olmaksızın giremez.
Lakini kuhani Mkuu peke yake ndiye anayeingia katika lile hema la pili; naye hufanya hivyo mara moja tu kwa mwaka. Anapoingia ndani huwa amechukua damu ambayo anamtolea Mungu kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya dhambi ambazo watu wamezitenda bila wao wenyewe kujua.
8 Kutsal Ruh bununla çadırın ilk bölmesi durdukça, kutsal yere giden yolun henüz açıkça gösterilmediğini belirtiyor.
Kutokana na taratibu hizo Roho Mtakatifu anafundisha wazi kwamba wakati ile hema ya nje ingali ipo imesimama, njia ya kuingia Mahali Patakatifu haijafunguliwa.
9 Bu, şimdiki çağ için bir örnektir; sunulan kurbanlarla sunuların tapınan kişinin vicdanını yetkinleştiremediğini gösteriyor.
Jambo hili ni mfano wa nyakati za sasa. Linaonyesha kwamba zawadi na dhabihu zinazotolewa kwa Mungu haziwezi kuifanya mioyo ya wale wanaoabudu kuwa mikamilifu,
10 Bunlar yalnız yiyecek, içecek, çeşitli dinsel yıkanmalarla ilgilidir; yeni düzenin başlangıcına kadar geçerli olan bedensel kurallardır.
kwani haya yote yanahusika na vyakula, vinywaji na taratibu mbalimbali za kutawadha. Yote hayo ni maagizo ya njenje tu; na nguvu yake hukoma wakati Mungu atakaporekebisha vitu vyote.
11 Ama Mesih, gelecek iyi şeylerin başkâhini olarak ortaya çıktı. İnsan eliyle yapılmamış, yani bu yaratılıştan olmayan daha büyük, daha yetkin çadırdan geçti.
Lakini Kristo amekwisha fika, akiwa Kuhani Mkuu wa mambo yaliyo mema, ambayo sasa yamekwisha fika. Yeye anatoa huduma zake katika hema iliyo bora na kamilifu zaidi, isiyofanywa kwa mikono ya watu, yaani isiyo ya ulimwengu huu ulioumbwa.
12 Tekelerle danaların kanıyla değil, sonsuz kurtuluşu sağlayarak kendi kanıyla kutsal yere ilk ve son kez girdi. (aiōnios )
Yeye aliingia Mahali Patakatifu mara moja tu, tena hakuwa amechukua damu ya mbuzi wala ng'ombe, bali aliingia kwa damu yake yeye mwenyewe, akatupatia ukombozi wa milele. (aiōnios )
13 Tekelerle boğaların kanı ve serpilen düve külü murdar olanları kutsal kılıyor, bedensel açıdan temizliyor.
Watu waliokuwa najisi kidini waliweza kutakasika na kuwa safi waliponyunyiziwa damu ya mbuzi na ya ng'ombe pamoja na majivu ya ndama.
14 Öyleyse sonsuz Ruh aracılığıyla kendini lekesiz olarak Tanrı'ya sunmuş olan Mesih'in kanının, diri Tanrı'ya kulluk edebilmemiz için vicdanımızı ölü işlerden temizleyeceği ne kadar daha kesindir! (aiōnios )
Lakini, kwa damu ya Kristo, mambo makuu zaidi hufanyika! Kwa nguvu za Roho wa milele, Kristo alijitolea mwenyewe dhabihu kamilifu kwa Mungu. Damu yake itatutakasa dhamiri zetu kutokana na matendo yaletayo kifo, ili tupate kumtumikia Mungu aliye hai. (aiōnios )
15 Bu nedenle, çağrılmış olanların vaat edilen sonsuz mirası almaları için Mesih yeni antlaşmanın aracısı oldu. Kendisi onları ilk antlaşma zamanında işledikleri suçlardan kurtarmak için fidye olarak öldü. (aiōnios )
Kwa hiyo, Kristo ndiye aliyeratibisha agano jipya ili wale walioitwa na Mungu wazipokee baraka za milele walizoahidiwa. Watazipata, kwani kifo kimetokea ambacho huwakomboa watu kutoka yale makosa waliyofanya wakati wa lile agano la kale. (aiōnios )
16 Ortada bir vasiyet varsa, vasiyet edenin ölümünün kanıtlanması gerekir.
Kwa kawaida wosia hutambuliwa tu kama kifo cha yule aliyeufanya huo wosia kimethibitishwa.
17 Çünkü vasiyet ancak ölümden sonra geçerli olur. Vasiyet eden yaşadıkça, vasiyetin hiçbir etkinliği yoktur.
Wosia hauwezi kutekelezwa mpaka kumetokea kifo, kwani wosia hauna maana ikiwa mwenye kuufanya bado anaishi.
18 Bu nedenle ilk antlaşma bile kan akıtılmadan yürürlüğe girmedi.
Ndiyo maana hata lile agano la kwanza halikuwekwa bila damu kumwagwa.
19 Musa, Kutsal Yasa'nın her buyruğunu bütün halka bildirdikten sonra su, al yapağı, mercanköşkotu ile danaların ve tekelerin kanını alıp hem kitabın hem de bütün halkın üzerine serpti.
Kwanza Mose aliwatangazia watu wote amri zote kama ilivyokuwa katika Sheria; kisha akachukua damu ya ndama pamoja na maji, na kwa kutumia majani ya mti uitwao husopo na pamba nyekundu, akakinyunyizia kile kitabu cha Sheria na hao watu wote.
20 “Tanrı'nın uymanızı buyurduğu antlaşmanın kanı budur” dedi.
Mose alisema: “Hii ni damu inayothibitisha agano mliloamriwa na Mungu mlitii.”
21 Aynı biçimde çadırın ve tapınmada kullanılan bütün eşyaların üzerine kan serpti.
Vilevile Mose aliinyunyizia damu ile hema na vyombo vya ibada.
22 Nitekim Kutsal Yasa uyarınca hemen her şey kanla temiz kılınır, kan dökülmeden bağışlama olmaz.
Naam, kadiri ya Sheria karibu kila kitu chaweza kutakaswa kwa damu, na dhambi nazo zaondolewa tu ikiwa damu imemwagwa.
23 Böylelikle aslı göklerde olan örneklerin bu kurbanlarla, ama gökteki asıllarının bunlardan daha iyi kurbanlarla temiz kılınması gerekti.
Vitu hivi ambavyo ni mfano tu wa mambo halisi ya mbinguni, vililazimika kutakaswa kwa namna hiyo. Lakini vitu vya mbinguni huhitaji dhabihu iliyo bora zaidi.
24 Çünkü Mesih, asıl kutsal yerin örneği olup insan eliyle yapılan kutsal yere değil, ama şimdi bizim için Tanrı'nın önünde görünmek üzere asıl göğe girdi.
Maana Kristo hakuingia Mahali Patakatifu palipojengwa kwa mikono ya watu, ambapo ni mfano tu wa kile kilicho halisi. yeye aliingia mbinguni kwenyewe ambako sasa anasimama mbele ya Mungu kwa ajili yetu.
25 Başkâhin her yıl kendisinin olmayan kanla En Kutsal Yer'e girer; oysa Mesih kendisini tekrar tekrar sunmak için göğe girmedi.
Kuhani Mkuu wa Wayahudi huingia Mahali Patakatifu kila mwaka akiwa amechukua damu ya mnyama; lakini Kristo hakuingia humo ili ajitoe mwenyewe mara nyingi,
26 Öyle olsaydı, dünyanın kuruluşundan beri Mesih'in tekrar tekrar acı çekmesi gerekirdi. Oysa Mesih, kendisini bir kez kurban ederek günahı ortadan kaldırmak için çağların sonunda ortaya çıkmıştır. (aiōn )
maana ingalikuwa hivyo, Kristo angalipaswa kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa ulimwengu. Lakini sasa nyakati hizi zinapokaribia mwisho wake, yeye ametokea mara moja tu, kuondoa dhambi kwa kujitoa yeye mwenyewe dhabihu. (aiōn )
27 İnsanın bir kez ölmesi, sonra da yargılanması kaçınılmaz olduğu gibi, Mesih de birçoklarının günahlarını yüklenmek için bir kez kurban edildi. İkinci kez, günah yüklenmek için değil, kurtuluş getirmek için kendisini bekleyenlere görünecektir.
Basi, kama vile kila mtu hufa mara moja tu, kisha husimama mbele ya hukumu ya Mungu,
vivyo hivyo Kristo naye alijitoa dhabihu mara moja tu kwa ajili ya kuziondoa dhambi za wengi. Atakapotokea mara ya pili si kwa ajili ya kupambana na dhambi, bali ni kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaomngojea.