< Ester 1 >
1 Ahaşveroş Hoddu'dan Kûş'a uzanan bölgedeki yüz yirmi yedi ilin kralıydı.
Katika siku za utawala wa Ahasuero (huyu ni Ahasuero aliyetawala toka India hadi Ethiopa, zaidi ya majimbo 127),
2 O sırada ülkeyi Sus Kalesi'ndeki tahtından yönetiyordu.
katika siku hizo Mfalme Ahasuero aliketi katika kiti chake cha utawala katika ngome ya Shushani.
3 Krallığının üçüncü yılında bütün önderlerinin ve görevlilerinin onuruna bir şölen verdi. Pers ve Med ordu komutanları, ileri gelenler ve il valileri de oradaydı.
mwaka wa tatu wa utawala wake aliwaandalia sherehe viongozi na watumwa wake wote. Waliohudhuria katika sherehe hiyo walikuwa wakuu wa jeshi la Uajemi na Umedi, watu wenye vyeo, na viongozi wa majimbo.
4 Ahaşveroş tam yüz seksen gün süren şenliklerle krallığının sonsuz zenginliğini, büyüklüğünün görkemini ve yüceliğini gösterdi.
Mfalme akaweka wazi utajiri na utukufu wa ufalme wake na heshima ya ukufu wa ukuu alio upata kwa siku nyingi, kwa siku180.
5 Bunun ardından, sarayının avlusunda küçük büyük ayırmadan, Sus Kalesi'nde bulunan bütün halka yedi gün süren bir şölen verdi.
Siku hizi zilipotimia, Mfalme aliaandaa karamu iliyodumu kwa siku saba. Karamu hii ilikuwa kwa watu wote walioishi katika ikulu ya Shushani, tangu mkubwa hadi mdogo. Behewa la bustani ya ikulu ya mfalme ndiyo karamu ilipofanyikia.
6 Mermer sütunlar üzerindeki gümüş çemberlere mor ve beyaz renkli iplikten yapılmış sicimlerle bağlanmış beyaz ve lacivert kumaşlar asılmıştı. Somaki, mermer, sedef ve pahalı taşlar döşenmiş avluya altın ve gümüş sedirler yerleştirilmişti.
Behewa la bustani lilipambwa kwa mapazia meupe ya pamba na urujuani, yalifungwa kwa kamba za kitani safi na zambarau, yakiwa yametundikwa kwa pete za fedha na nguzo za marimari. Kulikuwa na makochi ya dhahabu na fedha juu ya sakafu ya marimari, mawe mekundu na meupe, na ya manjano na meusi.
7 Sarayın en iyi şarabı kralın cömertliğine yaraşır biçimde bol bol ve her biri değişik altın kupalar içinde sunuluyordu.
Vinywaji viliandaliwa katika vikombe vya dhahabu. Na kila kikombe kilikuwa ni cha kipekee na kwa sababu ya ukarimu wa mfalme kulikuwa mvinyo mwingi.
8 Kralın buyruğu uyarınca, konuklar içki içmeye zorlanmadı. Kral saray hizmetkârlarına konukların dileklerini yerine getirmeleri için buyruk vermişti.
Mfalme aliwambia wahudumu watu wagawiwe vinywaji kwa kila mtu kulingana na matakwa yake. Maana tayari mfalme alikuwa ametoa agizo kwa watumishi wa ikulu kuwafanyia wageni kulingana na matakwa ya kila mgeni.
9 O sırada Kraliçe Vaşti de Kral Ahaşveroş'un sarayındaki kadınlara bir şölen veriyordu.
Wanawake nao walikuwa wamealikwa katika karamu na Malkia Vashiti katika ikulu ya Mfalme Ahusuero.
10 Yedinci gün, şarabın etkisiyle keyiflenen Kral Ahaşveroş, hizmetindeki yedi haremağasına –Mehuman, Bizta, Harvona, Bigta, Avagta, Zetar ve Karkas'a– Kraliçe Vaşti'yi başında tacıyla huzuruna getirmelerini buyurdu. Kraliçe Vaşti güzeldi. Kral halka ve önderlere onun ne kadar güzel olduğunu göstermek istiyordu.
katika siku ya saba moyo wa mfalme ulipokuwa na furaha kwa sababu ya mvinyo, aliwaagiza Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari na Karkas (hawa saba ndio waliohudumu mbele ya mfalme)
kumleta Malkia Vashiti akiwa katika mavazi yake ya kimalkia. Akiwa na lengo la kuwaonyesha watu na maakida urembo wake, maana alikuwa mrembo.
12 Ama Kraliçe Vaşti haremağalarının kraldan getirdiği buyruğu reddedip gitmedi. Bunun üzerine kral çok kızdı, öfkesinden küplere bindi.
Pamoja na maagizo ya Mfalme, Malkia Vashiti alikataa kwenda kama alivyokuwa amewaagiza viongozi wake. Hivyo mfalme akakasirika sana; ghadhabu yake ikawaka ndani yake
13 Kral yasaları bilen bilge kişilerle görüştü. Çünkü kralın, yasaları ve adaleti bilen kişilere danışması gelenektendi.
Mfalme akawandea wenye hekima, waliofahamu nyakati (kwa kuwa huu ndio uliokuwa utaratibu wa mfalme kuhusu wale waliokuwa watalaamu wa sheria na hukumu.
14 Kendisine en yakın olan Karşena, Şetar, Admata, Tarşiş, Meres, Marsena ve Memukan onunla yüzyüze görüşebiliyorlardı. Pers ve Med İmparatorluğu'nun bu yedi önderi krallığın en üst yöneticileriydi.
Carshena, Shethar, Admatha, Tarshish, Meres, Marsena, na Memucan, majimbo saba ya Uajemi na Umedi walikuwa karibu na mfalme na walikuwa na vyeo vikubwa katika ufalme.
15 Kral Ahaşveroş onlara, “Kralın haremağaları aracılığıyla gönderdiği buyruğa uymayan Kraliçe Vaşti'ye yasaya göre ne yapmalı?” diye sordu.
Katika kutafsiri nini kifanyike kwa mjibu wa sheria kutoka na mgomo wa Malkia Vashiti dhidi ya agizo la mfalme Ahusiero kwa Malkia Vashiti.
16 Memukan, kralın ve önderlerin önünde şu yanıtı verdi: “Kraliçe Vaşti yalnız krala karşı değil, bütün önderlere ve kralın bütün illerindeki halklara karşı suç işledi.
Mmoja wao aliyejulikana kwa jina la Memukani alisema mbele ya Mfalme na mbele ya viongozi, Malkia Vashiti hajamkosea tu mfame na wakuu na watu wote walio katika majimbo ya mfale Ahusiero.
17 Bütün kadınlar, kraliçenin davranışıyla ilgili haberi duyunca, ‘Kral Ahaşveroş Kraliçe Vaşti'nin huzuruna getirilmesini buyurdu, ama kraliçe gitmedi’ diyerek kocalarını küçümsemeye başlayacaklar.
kwa kuwa jambo la malkia litafahamika kwa wanawake wote. watawatendea waume zao vibaya. Watasema, 'Mfalme Ahusiero Malkia Vashiti hakumtii mme wake, Mfalme Ahusiero alipotaka ahudhurie mbele yake.'
18 Bugün kraliçenin davranışını öğrenen Pers ve Medli soylu kadınlar da kralın soylu adamlarına aynı biçimde davranacak. Bu da alabildiğine kadınların küçümsemesine, erkeklerin de öfkelenmesine yol açacak.
Kabla ya siku hii wanawake wa wakuu wa Uajemi na Umedi walipata taarifa ya mgomo wa malkia Vashiti watawatendea waume zao, viongozi wa mfalme. kutakuwa na ghasia na nyingi hasira.
19 Kral uygun görüyorsa ferman çıkarsın; bu ferman Persler'le Medler'in değişmeyen yasalarına eklensin. Buna göre Vaşti bir daha Kral Ahaşveroş'un huzuruna çıkmasın ve kral ondan daha iyi birini kraliçeliğe seçsin.
kama ni jambo jema kwa mfalme, ruhusu tangazo litolewe, na iwe katika sheria ya Waajemi na Wamedi, ambao haiwezi kutanguliwa, kwamba Vashiti hatakuja tena mbele za mfalme kama malkia. Nafasi ya Vashiti apewe mwingine ambaye ni bora zaidi ya Vashiti.
20 Kralın fermanı büyük krallığının dört bir yanına ulaşınca, ister soylu ister halktan olsun, bütün kadınlar kocalarına saygı gösterecektir.”
Tangazo la mfalme litakapotolewa katika ufalme wote, wanawake wote watawaheshimu waume zao, tangu mwenye cheo hadi asiye na cheo.”
21 Bu sözler kralın ve önderlerinin hoşuna gitti. Kral, Memukan'ın önerisine uyarak,
Ushauri huu ulikuwa mzuri kwa mfalme na wakuu wengine, mfalme akafamya kama Memkani alivyopendekeza.
22 krallığın bütün illerine yazılı buyruklar gönderdi. Her ile kendi işaretleriyle ve her halka kendi diliyle yazıldı. Her erkeğin kendi evinin egemeni olduğu her dilde vurgulandı.
Akatuma barua katika majimbo yote ya mfalme, kwa kilajambo na andiko lake, na watu kwa makabila yao. Aliamuru kwamba kila mme awe msimamizi katika nyumba yake mwenyewe. Tangazo hili lilitolewa katika lungha ya kila mtu katika ufalme.