< Tito 3 >

1 Wakumbushe watu kuwastahi watawala na wenye mamlaka, kuwatii na kuwa tayari kwa kila namna kutenda mambo yote mema.
你要醒寤人服從執政的官長,聽從命令,準備行各種善事。
2 Waambie wasimtukane mtu yeyote; bali waishi kwa amani na masikizano, wawe daima wapole kwa kila mtu.
不要辱罵,不要爭吵,但要謙讓,對眾人表示極其溫和,
3 Maana, wakati mmoja sisi tulikuwa wapumbavu, wakaidi na wapotovu. Tulikuwa watumwa wa tamaa na anasa za kila aina. Tuliishi maisha ya uovu na wivu; watu walituchukia nasi tukawachukia.
因為我們從前也是昏愚的,悖逆的,迷途的,受各種貪慾和逸樂所奴役,在邪惡和嫉妒中度日,自己是可憎惡的,又彼此仇恨。
4 Lakini wakati wema na upendo wa Mungu, Mwokozi wetu, ulipofunuliwa,
但當我們的救主的良善,和衪對人的慈愛出現時,
5 alituokoa. alituokoa si kwa sababu ya jambo lolote jema tulilotenda sisi, bali alituokoa kwa sababu ya huruma yake, kwa njia ya Roho Mtakatifu anayetujalia tuzaliwe upya na kuwa na maisha mapya kwa kutuosha kwa maji.
衪救了我們,並不是我們本著義德所立的功勞,而出於衪的憐憫,藉聖神所施行的重生和更新的洗禮,救了我們。
6 Mungu alitumiminia Roho Mtakatifu bila kipimo kwa njia ya Yesu Kristo, Mwokozi wetu,
這聖神是天藉我們的救主耶穌基督,豐富地傾注在我們身上,
7 ili kwa neema yake tupate kukubaliwa kuwa waadilifu na kuupokea uzima wa milele tunaoutumainia. (aiōnios g166)
好使我們因衪的恩寵成義.本著希望成為永生的繼承人。 (aiōnios g166)
8 Jambo hili ni kweli. Ninakutaka uyatilie mkazo mambo haya, ili wale wanaomwamini Mungu, wawe na hamu ya kuutumia wakati wao katika kutenda mema, ambayo ni mambo mazuri na ya manufaa kwa watu.
這話是確實的,我願意你堅持這些事,好使那些已信奉天主的人,熱心專行善:這些都是美好而為人有益的事;
9 Lakini jiepushe na ubishi wa kipumbavu, ugomvi na mabishano juu ya Sheria. Mambo hayo hayana faida yoyote na ni ya bure tu.
至於那些愚昧的辯論,祖譜、爭執和關於法律的爭論,你務要躲避,因為這些都是無益的空談。
10 Mtu anayesababisha mafarakano mpe onyo la kwanza na la pili, kisha achana naye.
對異端人,在譴責過一次兩次以後,就應該遠離他。
11 Wajua kwamba mtu wa namna hiyo amepotoka kabisa, na dhambi zake zathibitisha kwamba amekosea.
該知道:這樣的人已背棄正道,犯罪做惡,自己給定了罪案。
12 Baada ya kumtuma kwako Artema au Tukiko, fanya bidii kuja Nikopoli unione, maana nimeamua kukaa huko wakati wa majira ya baridi.
當我打發阿爾特瑪或提希苛到你那裏以後,你趕快到尼苛頗里來見我,因為我已決定在那裏過冬。
13 Jitahidi kumsaidia mwana sheria Zena na Apolo ili waweze kuanza ziara zao na uhakikishe kwamba wana kila kitu wanachohitaji.
你打發法學士則納和阿頗羅上路,要照顧周到,使他們什麼也不缺少。
14 Ni lazima watu wetu wajifunze kuutumia wakati wao katika kutenda mema ili wasaidie katika mahitaji ya kweli, na maisha yao yawe ya kufaa.
我們人也應當學習行善,為應付一切急需,免得成為不結果實的人。
15 Watu wote walio pamoja nami wanakusalimu. Wasalimu rafiki zetu katika imani. Nawatakieni nyote neema ya Mungu.
同我在一起的弟兄都問候你;請問候那些在信德內愛我們的弟兄。願恩寵你與們同在!

< Tito 3 >