< Tito 2 >
1 Lakini wewe unapaswa kuhubiri mafundisho safi.
But do you, on your part, speak what becomes sound teaching;
2 Waambie wazee kwamba wanapaswa kuwa na kiasi, wawe na busara na wataratibu; wanapaswa kuwa timamu katika imani yao, upendo na uvumilivu.
that the older men be self-controlled, serious and sober-minded, sound in faith, in love, in patience;
3 Hali kadhalika waambie wanawake wazee wawe na mwenendo wa uchaji wa Mungu; wasiwe wachongezi, au watumwa wa pombe. Wanapaswa kufundisha mambo mema,
that older women likewise be reverent in demeanor, not slanderers or slaves to much wine, but teachers of what is right.
4 ili wawazoeze kina mama vijana kuwapenda waume zao na watoto,
They should train the younger women to love their husbands and children,
5 wawe na kiasi na safi, waangalie vizuri mambo ya nyumbani, na wawatii waume zao, ili ujumbe wa Mungu usije ukadharauliwa.
to be sober-minded, chaste, workers at home, kind and submissive to their husbands, in order that God’s message be not maligned.
6 Kadhalika, wahimize vijana wawe na kiasi.
The younger men exhort to be sober-minded; in every respect showing yourself an example of good works.
7 Katika mambo yote wewe mwenyewe unapaswa kuwa mfano wa matendo mema. Uwe mnyofu na uwe na uzito katika mafundisho yako.
In your teaching be serious and sincere.
8 Maneno yako yasiwe na hitilafu yoyote ili adui zako waaibike wasipopata chochote kibaya cha kusema juu yetu.
Let the instruction that you give be sound and above reproach, so that our opponents may be ashamed because they find no evil things to say about us.
9 Watumwa wanapaswa kuwatii wakuu wao na kuwapendeza katika mambo yote. Wasibishane nao,
Exhort slaves to be obedient to their own masters, and to be well- pleasing to them in every respect;
10 au kuiba vitu vyao. Badala yake wanapaswa kuonyesha kwamba wao ni wema na waaminifu daima, ili, kwa matendo yao yote, wayapatie sifa njema mafundisho juu ya Mungu, Mwokozi wetu.
not to contradict nor pilfer, but to exhibit praiseworthy trustworthiness in every thing, that they may adorn the doctrine of God our Saviour in all things.
11 Maana neema ya Mungu imedhihirishwa kwa ajili ya wokovu wa watu wote.
"For God’s grace has shined forth bringing salvation to all men
12 Neema hiyo yatufunza kuachana na uovu wote na tamaa za kidunia; tuwe na kiasi, tuishi maisha adili na ya kumcha Mungu katika ulimwengu huu wa sasa, (aiōn )
And schooling us to renounce impiety and evil passions, And to live soberly, righteously, and godly in this present age; (aiōn )
13 tukiwa tunangojea siku ile ya heri tunayoitumainia, wakati utakapotokea utukufu wa Mungu Mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo.
While we look for the blessed hope and epiphany of the glory of our great God and Saviour, Jesus Christ.
14 Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili atukomboe kutoka katika uovu wote na kutufanya watu safi walio wake yeye mwenyewe, watu walio na hamu ya kutenda mema.
He gave himself for us to redeem us from all iniquity, and to purify unto himself a people zealous of good works."
15 Basi, fundisha mambo hayo na tumia mamlaka yako yote ukiwahimiza na kuwaonya wasikilizaji wako. Mtu yeyote na asikudharau.
Thus speak, exhort, reprove with all authority. Let no one despise you.