< Tito 1 >

1 Mimi Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo naandika. Mimi nimechaguliwa kuijenga imani ya wateule wa Mungu na kuwaongoza waufahamu ukweli wa dini yetu,
Paul, a servant of God and an apostle of Jesus Christ, for the faith of God's chosen people and the knowledge of the truth that agrees with godliness,
2 ambayo msingi wake ni tumaini la kupata uzima wa milele. Mungu ambaye hasemi uongo, alituahidia uzima huo kabla ya mwanzo wa nyakati, (aiōnios g166)
with the certain hope of everlasting life that God, who does not lie, promised before all the ages of time. (aiōnios g166)
3 na wakati ufaao ulipowadia, akaudhihirisha katika ujumbe wake. Mimi nilikabidhiwa ujumbe huo nuutangaze kufuatana na amri ya Mungu, Mwokozi wetu.
At the right time, he revealed his word by the message that he trusted me to deliver. I was to do this by the command of God our savior.
4 Ninakuandikia wewe Tito, mwanangu wa kweli katika imani tunayoshiriki. Nakutakia neema na amani kutoka kwa Mungu Baba, na kutoka kwa Kristo Yesu, Mkombozi wetu.
To Titus, a true son in our common faith. Grace and peace from God the Father and Christ Jesus our savior.
5 Nilikuacha Krete ili urekebishe yale mambo ambayo hayakuwa yamekamilika bado, na kuwateua wazee wa kanisa katika kila mji. Kumbuka maagizo yangu:
For this purpose I left you in Crete, that you might set in order things not yet complete and ordain elders in every city as I directed you.
6 mzee wa kanisa anapaswa kuwa mtu asiye na hatia; aliye na mke mmoja tu, na watoto wake wanapaswa kuwa waumini, wasiojulikana kuwa wakorofi au wakaidi.
An elder must be without blame, the husband of one wife, with faithful children who do not have the reputation of being reckless or undisciplined.
7 Maana kwa vile kiongozi wa kanisa ni mkurugenzi wa kazi ya Mungu, anapaswa kuwa mtu asiye na hatia. Asiwe mwenye majivuno, mwepesi wa hasira, mlevi, mkorofi au mchoyo.
It is necessary for the overseer, as God's household manager, to be blameless. He must not be arrogant, not be easily angered, not addicted to wine, not a brawler, and not a greedy man.
8 Anapaswa kuwa mkarimu na anayependa mambo mema. Anapaswa kuwa mtu mtaratibu, mwadilifu, mtakatifu na mwenye nidhamu.
Instead, he should be hospitable and a friend of what is good. He must be sensible, righteous, godly, and self-controlled.
9 Ni lazima ashike kikamilifu ujumbe ule wa kuaminika kama unavyofundishwa. Ndivyo atakavyoweza kuwatia wengine moyo kwa mafundisho ya kweli na kuyafichua makosa ya wale wanaoyapinga mafundisho hayo.
He should hold tightly to the trustworthy message that was taught, so that he may be able to encourage others with good teaching and correct those who oppose him.
10 Maana, wako watu wengi, hasa wale walioongoka kutoka dini ya Kiyahudi, ambao ni wakaidi, wanaowapotosha wengine kwa upumbavu wao.
For there are many rebellious people, empty talkers and deceivers, especially those of the circumcision.
11 Lazima kukomesha maneno yao, kwani wanavuruga jumuiya nzima kwa kufundisha mambo ambayo hawapaswi kufundisha; wanafanya hivyo kwa nia mbaya ya kupata faida ya fedha.
It is necessary to stop them. They are upsetting whole families by teaching for shameful profit what they should not teach.
12 Hata mmoja wa manabii wao, ambaye naye pia ni Mkrete, alisema: “Wakrete, husema uongo daima; ni kama wanyama wabaya, walafi na wavivu!”
One of their own prophets has said, “Cretans are always liars, evil beasts, lazy gluttons.”
13 Naye alitoboa ukweli kwa sababu hiyo, unapaswa kuwakaripia vikali, ili wawe na imani kamilifu.
This statement is true. Therefore, correct them severely, so that they may be sound in the faith,
14 Wasiendelee kushikilia hadithi tupu za Kiyahudi na maagizo ya kibinadamu yanayozuka kwa watu walioukataa ukweli.
not paying any attention to Jewish myths or to the commands of people who turn away from the truth.
15 Kila kitu ni safi kwa watu walio safi; lakini hakuna chochote kilicho safi kwa wale waliochafuliwa na wasioamini, maana dhamiri na akili zao zimechafuliwa.
To those who are pure, all things are pure. But to those who are corrupt and unbelieving, nothing is pure, but both their minds and their consciences have been corrupted.
16 Watu kama hao hujidai kwamba wanamjua Mungu, lakini kwa matendo yao humkana. Ni watu wa kuchukiza mno na wakaidi, hawafai kwa jambo lolote jema.
They profess to know God, but they deny him by their actions. They are detestable, disobedient, and unfit for doing any good work.

< Tito 1 >