< Warumi 7 >

1 Ndugu zangu, bila shaka mtaelewa yafuatayo, maana ninawazungumzia watu wanaojua Sheria. Sheria humtawala mtu wakati akiwa hai.
Or do you not know, brothers, (now I am speaking to those who know the law) that the law has dominion over a man only so long as he lives?
2 Mathalan: mwanamke aliyeolewa anafungwa na sheria muda wote mumewe anapokuw hai; lakini mumewe akifa, hiyo sheria haimtawali tena huyo mwanamke.
For example, a woman who is subject to a husband is obligated by the law while her husband lives. But when her husband has died, she is released from the law of her husband.
3 Hivyo mwanamke huyo akiishi na mwanamume mwingine wakati mumewe yungali hai, ataitwa mzinzi; lakini mumewe akifa, mwanamke huyo yu huru kisheria, na akiolewa na mwanamume mwingine, yeye si mzinzi.
Therefore, while her husband lives, if she has been with another man, she should be called an adulteress. But when her husband has died, she is freed from the law of her husband, such that, if she has been with another man, she is not an adulteress.
4 Hali kadhalika ninyi ndugu zangu: ninyi pia mmekufa kuhusu Sheria kwa kuwa ninyi ni sehemu ya mwili wa Kristo; sasa mmekuwa wake yeye aliyefufuliwa kutoka wafu ili tupate kuzaa matunda mema kwa ajili ya Mungu.
And so, my brothers, you also have become dead to the law, through the body of Christ, so that you may be another one who has risen from the dead, in order that we may bear fruit for God.
5 Maana, tulipokuwa tukiishi kimaumbile tu, tamaa mbaya zikichochewa na Sheria, zilifanya kazi katika miili yetu, na kuchuma pato la kifo.
For when we were in the flesh, the passions of sins, which were under the law, operated within our bodies, so as to bear fruit unto death.
6 Lakini sasa tumekuwa huru kutoka vifungo vya Sheria, kwa sababu tumekufa kuhusu lile jambo lililotufanya sisi watumwa. Sasa tunatumikia kufuatana na maisha mapya ya Roho, na si kufuatana na hali ile ya kale ya Sheria iliyoandikwa.
But now we have been released from the law of death, by which we were being held, so that now we may serve with a renewed spirit, and not in the old way, by the letter.
7 Je, tuseme basi, kwamba Sheria ni dhambi? Hata kidogo! Lakini bila Sheria, mimi nisingalijua dhambi ni kitu gani. Maana, nisingalijua ni nini hasa kutamani mabaya, kama Sheria isingalikuwa imesema: “Usitamani.”
What should we say next? Is the law sin? Let it not be so! But I do not know sin, except through the law. For example, I would not have known about coveting, unless the law said: “You shall not covet.”
8 Kwa kuitumia hiyo amri, dhambi ilipata fursa ya kuamsha kila aina ya tamaa mbaya ndani yangu. Maana, bila Sheria dhambi ni kitu kilichokufa.
But sin, receiving an opportunity through the commandment, wrought in me all manner of coveting. For apart from the law, sin was dead.
9 Wakati mmoja mimi nilikuwa hai mbali na Sheria; lakini amri ilipokuja, dhambi ilifufuka,
Now I lived for some time apart from the law. But when the commandment had arrived, sin was revived,
10 nami nikafa. Hiyo amri ambayo shabaha yake ilikuwa kuleta uhai, kwangu imeleta kifo.
and I died. And the commandment, which was unto life, was itself found to be unto death for me.
11 Maana, dhambi ilichukua fursa iliyopatiwa na amri hiyo, ikanidanganya na kuniua.
For sin, receiving an opportunity through the commandment, seduced me, and, through the law, sin killed me.
12 Basi, Sheria yenyewe ni takatifu, na amri yenyewe ni takatifu, ni ya haki na nzuri.
And so, the law itself is indeed holy, and the commandment is holy and just and good.
13 Je, hii inamaanisha kwamba kile kilicho kizuri kimesababisha kifo changu? Hata kidogo! Iliyo ni kwamba, dhambi, ili ionekane dhahiri kuwa ni dhambi, imekitumia kile kilicho kizuri na kusababisha kifo changu. Hivyo dhambi, kwa njia ya ile amri, ilijionyesha kikamilifu jinsi ilivyo mbaya mno.
Then was what is good made into death for me? Let it not be so! But rather sin, in order that it might be known as sin by what is good, wrought death in me; so that sin, through the commandment, might become sinful beyond measure.
14 Tunajua kwamba Sheria ni ya kiroho, lakini mimi ni wa kidunia, mimi nimeuzwa kuwa mtumwa wa dhambi.
For we know that the law is spiritual. But I am carnal, having been sold under sin.
15 Sielewi nifanyacho, maana kile ninachotaka sikifanyi, bali kile ninachochukia ndicho nikifanyacho.
For I do things that I do not understand. For I do not do the good that I want to do. But the evil that I hate is what I do.
16 Ikiwa basi, ninatenda kinyume cha matakwa yangu, hii inamaanisha kwamba nakubali kuwa ile Sheria ni nzuri.
So, when I do what I do not want to do, I am in agreement with the law, that the law is good.
17 Basi, si mimi hasa ninayefanya kitu hicho, bali ile dhambi iliyo ndani yangu.
But I am then acting not according to the law, but according to the sin which lives within me.
18 Najua kwamba hamna jema lolote ndani yangu mimi, kadiri ya ubinadamu wangu. Kwa maana, ingawa nataka kufanya jambo jema, siwezi kulitekeleza.
For I know that what is good does not live within me, that is, within my flesh. For the willingness to do good lies close to me, but the carrying out of that good, I cannot reach.
19 Yaani, badala ya kufanya lile jambo jema ninalotaka, nafanya lile baya nisilotaka.
For I do not do the good that I want to do. But instead, I do the evil that I do not want to do.
20 Basi, kama ninafanya kinyume cha matakwa yangu, hii inamaanisha kwamba si mimi ninayefanya hayo, bali ni ile dhambi iliyo ndani yangu.
Now if I do what I am not willing to do, it is no longer I who am doing it, but the sin which lives within me.
21 Basi, nimegundua kanuni hii: ninataka kufanya jema, lakini najikuta kwamba lile lililo baya ndilo ninalochagua.
And so, I discover the law, by wanting to do good within myself, though evil lies close beside me.
22 Ndani kabisa katika moyo wangu naifurahia sheria ya Mungu.
For I am delighted with the law of God, according to the inner man.
23 Lakini naona kwamba kuna sheria nyingine inayofanya kazi mwilini mwangu, sheria ambayo inapingana na ile inayokubaliwa na akili yangu. Hiyo inanifanya niwe mtumwa wa sheria ya dhambi ifanyayo kazi mwilini mwangu.
But I perceive another law within my body, fighting against the law of my mind, and captivating me with the law of sin which is in my body.
24 Maskini miye! Nani atakayeniokoa kutoka katika mwili huu unaonipeleka kifoni?
Unhappy man that I am, who will free me from this body of death?
25 Shukrani kwa Mungu afanyaye hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo! Hii basi, ndiyo hali yangu: mimi binafsi, kwa akili yangu, ninaitumikia sheria ya dhambi.
The grace of God, by Jesus Christ our Lord! Therefore, I serve the law of God with my own mind; but with the flesh, the law of sin.

< Warumi 7 >