< Warumi 6 >
1 Tuseme nini basi? Je, twendelee kubaki katika dhambi ili neema ya Mungu iongezeke?
Then what shall we say? must we abide in sin, in order that grace may abound?
2 Hata kidogo! Kuhusu dhambi sisi tumekufa—tutaendeleaje kuishi tena katika dhambi?
It could not be so. How shall we, who are dead unto sin, live any longer in it?
3 Maana, mnajua kwamba sisi tuliobatizwa tukaungana na Kristo Yesu, tulibatizwa na kuungana na kifo chake.
Whether do you not know, that so many of us as were baptized unto Jesus Christ were baptized into His death?
4 Tulipobatizwa tuliungana na kifo chake, tukazikwa pamoja naye, ili kama vile Kristo alivyofufuliwa kutoka wafu kwa kitendo kitukufu cha Baba, sisi pia tuweze kuishi maisha mapya.
Therefore we were buried with him by baptism into death: in order that as Christ was raised from the dead by the glory of the Father, so must we also walk in newness of life.
5 Maana, kama sisi tumeungana naye katika kufa kama yeye, vivyo hivyo tutaungana naye kwa kufufuliwa kutoka wafu kama yeye.
For if we have grown together in the likeness of His death, we shall also be in the likeness of his resurrection:
6 Tunajua kwamba utu wetu wa kale ulisulubiwa pamoja na Kristo, ili hali ya dhambi iharibiwe, tusiwe tena watumwa wa dhambi.
knowing this, that our old man is crucified along with him, in order that the body of sin may be destroyed, that we may no longer serve sin;
7 Kwa maana, mtu aliyekufa, amenasuliwa kutoka katika nguvu ya dhambi.
for the one having died has been made free from sin.
8 Basi, ikiwa tumekufa pamoja na Kristo, tunaamini kwamba tutaishi pia pamoja naye.
But if we died along with Christ, we believe that we will also live with him:
9 Maana, tunajua kwamba Kristo amekwisha fufuliwa kutoka wafu na hafi tena; kifo hakimtawali tena.
knowing that Christ having risen from the dead dies no more; death no longer has dominion over him.
10 Hivyo, kwa kuwa alikufa—mara moja tu—dhambi haina nguvu tena juu yake; na sasa anaishi maisha yake katika umoja na Mungu.
For the death that he died, he died unto sin once: but the life that he lives, he lives unto God.
11 Hali kadhalika nanyi lazima mjione kuwa mmekufa kuhusu dhambi, lakini kama mnaoishi katika umoja na Mungu kwa njia ya Kristo Yesu.
So you also thus reckon yourselves dead unto sin, but alive unto God through Jesus Christ.
12 Kwa hiyo, dhambi isiitawale tena miili yenu ambayo hufa, na hivyo kuzitii tamaa zake.
Let not sin therefore reign in your mortal body that you should obey the lusts of it:
13 Wala msitoe hata sehemu moja ya miili yenu iwe chombo cha kutenda uovu na dhambi. Badala yake, jitoleeni ninyi wenyewe kwa Mungu kama watu waliofufuliwa kutoka wafu; toeni nafsi zenu zote kwa Mungu kwa ajili ya uadilifu.
neither present your members arms of iniquity unto sin; but present yourselves to God, as alive from the dead, and your members arms of righteousness unto God.
14 Maana, dhambi haitawatawala ninyi tena, kwani hamko chini ya Sheria, bali chini ya neema.
For sin shall not have dominion over you: for you are not under the law, but under grace.
15 Basi, tuseme nini? Je, tutende dhambi ati kwa sababu hatuko chini ya Sheria bali chini ya neema? Hata kidogo!
What then? can we commit sin, because we are not under the law, but under grace? it could not be so.
16 Mnajua kwamba mkijitolea ninyi wenyewe kama watumwa na kumtii fulani, mnakuwa kweli watumwa wake mtu huyo—au watumwa wa dhambi, na matokeo yake ni kifo, au wa utii, na matokeo yake ni kukubaliwa kuwa waadilifu.
Do you not know, that to whom you present yourselves servants unto obedience, ye are servants to whom you obey; whether of sin unto death, or obedience unto righteousness?
17 Ingawa mlikuwa watumwa wa dhambi zamani, sasa lakini—namshukuru Mungu—mmetii kwa moyo wote yale maazimio na mafundisho mliyopokea.
But thanks be unto God, that whereas ye were servants of sin, but you have obeyed from the heart the type of teaching into which ye were delivered:
18 Mlikombolewa kutoka utumwa wa dhambi, mkawa watumwa wa uadilifu.
but having been made free from sin, ye became servants unto righteousness.
19 (Hapa natumia lugha ya kawaida ya watu kwa sababu ya udhaifu wenu wenyewe.) Kama vile wakati fulani mlivyojitolea ninyi wenyewe kutumikia uchafu na uhalifu kwa ajili ya uovu, vivyo hivyo sasa jitoleeni nafsi zenu wenyewe kutumikia uadilifu kwa ajili ya utakatifu.
I speak after the manner of a man on account of the weakness of your carnality. For as ye presented your members as servants unto impurity and lawlessness pursuant to lawlessness, so now present your members servants unto righteousness pursuant to sanctification.
20 Mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na uadilifu.
For when you were the servants of sin, you were free from righteousness.
21 Sasa, mlipata faida gani siku zile kutokana na mambo yale ambayo mnayaonea aibu sasa? Maana, matokeo ya mambo haya ni kifo!
What fruit then had you at that time in those things in which you are now ashamed? for the end of these things is death.
22 Lakini sasa, mmekwisha kombolewa kutoka utumwa wa dhambi na mmekuwa watumishi wa Mungu; faida mliyo nayo sasa ni utakatifu, na matokeo yake ni uzima wa milele. (aiōnios )
But now having been made free from sin, and having become servants unto God, you have your fruit unto sanctification, and the end eternal life. (aiōnios )
23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni kifo; lakini zawadi anayotoa Mungu ni uzima wa milele katika kuungana na Kristo Yesu, Bwana wetu. (aiōnios )
For the wages of sin is death; but the free gift of God is eternal life through Jesus Christ our Lord, (aiōnios )