< Warumi 16 >

1 Napenda kumjulisha kwenu dada yetu Foibe ambaye ni mtumishi katika kanisa la Kenkrea.
I commend to you our sister Phoebe, who is a servant of the congregation in Cenchrea,
2 Mpokeeni kwa ajili ya Bwana kama iwapasavyo watu wa Mungu. Mpeni msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, maana yeye amekuwa mwema sana kwa watu wengi na kwangu pia.
so that you may receive her in the Lord in a manner worthy of the saints, and assist her in whatever matter she may need from you; for indeed she herself has been a helper of many, including my own self.
3 Salamu zangu ziwafikie Priska na Akula, wafanyakazi wenzangu katika utumishi wa Kristo Yesu.
Greet Prisca and Aquila, my fellow workers in Christ Jesus,
4 Wao walihatarisha maisha yao kwa ajili yangu. Wanastahili shukrani; si tu kutoka kwangu, bali pia kutoka kwa makanisa yote ya watu wa mataifa mengine.
who risked their own necks for my life; to whom not only I give thanks, but also all the congregations of the Gentiles.
5 Salamu zangu pia kwa kanisa linalokutana nyumbani kwao. Salamu zangu zimfikie rafiki yangu Epaineto ambaye ni kwa kwanza katika mkoa wa Asia kumwamini Kristo.
And greet the congregation that is in their house. Greet my beloved Epaenetus, who is the first convert to Christ from Achaia.
6 Nisalimieni Maria ambaye amefanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu.
Greet Mary, who worked very hard for you.
7 Salamu zangu kwa Androniko na Yunia, wananchi wenzangu waliofungwa gerezani pamoja nami; wao wanajulikana sana kati ya mitume; tena walikuwa Wakristo kabla yangu mimi.
Greet Andronicus and Junias, my countrymen and my fellow prisoners, who are outstanding among the apostles, and who were in Christ before me.
8 Salamu zangu kwa Ampliato, rafiki yangu katika kuungana na Bwana.
Greet Amplias, my beloved in the Lord.
9 Salamu zangu zimfikie Urbano, mfanyakazi mwenzangu katika utumishi wa Kristo; salamu zangu pia kwa rafiki yangu Staku.
Greet Urbanus, our fellow worker in Christ, and my beloved Stachys.
10 Nisalimieni Apele ambaye uaminifu wake kwa Kristo umethibitishwa. Salamu zangu kwa wote walio nyumbani mwa Aristobulo.
Greet Apelles, approved in Christ. Greet those who are of the household of Aristobulus.
11 Salamu zangu kwa Herodiana, mwananchi mwenzangu; na kwa jamaa yote ya Narkisi iliyojiunga na Bwana.
Greet Herodian, my countryman. Greet those who are of the household of Narcissus, who are in the Lord.
12 Nisalimieni Trufena na Trufosa wanaofanya kazi katika utumishi wa Bwana, na rafiki yangu Persi ambaye amefanya mengi kwa ajili ya Bwana.
Greet Tryphena and Tryphosa, who have worked hard in the Lord. Greet the beloved Persis, who has worked very hard in the Lord.
13 Nisalimieni Rufo, mtu hodari sana katika kazi ya Bwana, na mama yake ambaye ni mama yangu pia.
Greet Rufus, chosen in the Lord, also his mother, and mine.
14 Nisalimieni Asunkrito, Flegoni, Herme Patroba, Herma na ndugu wote walio pamoja nao.
Greet Asyncritus, Phlegon, Hermas, Patrobas, Hermes, and the brothers who are with them.
15 Nisalimieni Filologo na Yulia, Nerea na dada yake, na Olumpa, pamoja na watu wote wa Mungu walio pamoja nao.
Greet Philologus and Julia, Nereus and his sister, also Olympus and all the saints who are with them.
16 Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa ishara ya upendo. Salamu kwenu kutoka kwa makanisa yote ya Kristo.
Greet one another with a holy kiss. The congregations of Christ greet you.
17 Ndugu zangu, nawasihi muwafichue wote wanaosababisha mafarakano na kuwafanya watu wengine waanguke, kinyume cha mafundisho mliyofundishwa. Jiepusheni na watu hao,
Now I exhort you, brothers, to watch out for those who cause divisions and offenses, contrary to the doctrine you have learned, and avoid them.
18 maana watu wa namna hiyo hawamtumikii Kristo Bwana wetu, bali wanayatumikia matumbo yao wenyewe. Kwa maneno yao matamu na hotuba za kubembeleza hupotosha mioyo ya watu wanyofu.
Because such people do not serve our Lord Jesus Christ, but their own belly, and by smooth talk and flattery they deceive the hearts of the unsuspecting.
19 Kila mtu amesikia juu ya utii wenu na hivyo mmekuwa sababu ya furaha yangu. Nawatakeni muwe na hekima katika mambo mema, na bila hatia kuhusu mambo mabaya.
I rejoice over you because your obedience has become known to all, but I want you to be wise as to what is good, yet innocent as to what is evil.
20 Naye Mungu aliye chanzo cha amani hatakawia kumponda Shetani chini ya miguu yenu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi.
The God of peace will quickly crush Satan under your feet! The grace of our Lord Jesus Christ be with you.
21 Timotheo, mfanyakazi mwenzangu, anawasalimu. Hali kadhalika Lukio, Yasoni, na Sosipatro, wananchi wenzangu, wanawasalimu.
Timothy, my fellow worker, greets you, as do Lucius, Jason and Sosipater, my countrymen.
22 Nami Tertio, ninayeandika barua hii nawasalimuni katika Bwana.
I, Tertius, who penned this letter in the Lord, greet you.
23 Gayo, mwenyeji wangu, pamoja na kanisa lote linalokutana kwake, anawasalimu. Erasto, mweka hazina wa mji huu, pamoja na Kwarto, wanawasalimu.
Gaius, host to me and the whole congregation, greets you. Erastus, the city treasurer, greets you, as does brother Quartus.
24 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote. Amina.
The grace of our Lord Jesus Christ be with us all! Amen.
25 Basi, sasa na tumsifu Mungu! Yeye anaweza kuwaimarisheni katika ile Habari Njema niliyohubiri juu ya ujumbe wa Yesu Kristo, na katika ile siri iliyofunuliwa na ambayo ilikuwa imefichika kwa karne nyinyi zilizopita. (aiōnios g166)
Now to Him who has power to establish you according to my Gospel and the proclamation of Jesus Christ, according to the revelation of the mystery kept secret through long ages, (aiōnios g166)
26 Lakini, sasa ukweli huo umefunuliwa kwa njia ya maandiko ya manabii; na kwa amri ya Mungu wa milele umedhihirisha kwa mataifa yote ili wote waweze kuamini na kutii. (aiōnios g166)
but now revealed and made known through the prophetic Scriptures, according to the command of the eternal God, with a view to obedience of faith among all ethnic nations (aiōnios g166)
27 Kwake Mungu aliye peke yake mwenye hekima, uwe utukufu kwa njia ya Yesu Kristo, milele na milele! Amina. (aiōn g165)
—to the only wise God, through Jesus Christ—to Him be the glory forever! Amen. (aiōn g165)

< Warumi 16 >