< Warumi 12 >
1 Kwa hiyo, ndugu zangu, maadam Mungu ni mwenye huruma nyingi, nawasihi kwa moyo wote: jitoleeni nafsi zenu kwa Mungu kama tambiko iliyo hai, takatifu na yenye kupendeza. Hii ndiyo njia yenu halisi ya kumwabudu.
Therefore I urge you, brothers, by the mercies of God, to present your bodies a living sacrifice, holy, acceptable to God, which is your reasonable service.
2 Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu, kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu. (aiōn )
And do not be conformed to this world, but be transformed by the renewing of your mind, so that you may prove what is the good, well-pleasing, and perfect will of God. (aiōn )
3 Kutokana na neema aliyonijalia Mungu, nawaambieni ninyi nyote: msijione kuwa ni kitu zaidi kuliko mnavyopaswa kuwa. Fikira zenu na ziwe na kiasi kufuatana na kipimo cha imani Mungu aliyomgawia kila mmoja.
For I say, through the grace that was given me, to everyone among you, not to think of himself more highly than he ought to think, but to think with sober judgment, as God has apportioned to each person a measure of faith.
4 Mwili una viungo vingi, kila kimoja na kazi yake.
For even as we have many members in one body, and all the members do not have the same function,
5 Hali kadhalika ingawa sisi ni wengi, tu mwili mmoja kwa kuungana na Kristo, na kila mmoja ni kiungo cha mwenzake.
so we, who are many, are one body in Christ, and individually members one of another.
6 Basi, tunavyo vipaji mbalimbali kufuatana na neema tuliyopewa. Mwenye kipaji cha unabii na akitumie kadiri ya imani yake.
And we have different gifts according to the grace that was given to us. If prophecy, according to the proportion of the faith;
7 Mwenye kipaji cha utumishi na atumikie. mwenye kipaji cha kufundisha na afundishe.
if service, in the service; if teaching, in the teaching;
8 Mwenye kipaji cha kuwafariji wengine na afanye hivyo. Mwenye kumgawia mwenzake alicho nacho na afanye hivyo kwa ukarimu. Msimamizi na asimamie kwa bidii; naye mwenye kutenda jambo la huruma na afanye hivyo kwa furaha.
if exhorting, in exhortation; giving, in generosity; leading, in diligence; showing mercy, in cheerfulness.
9 Mapendo yenu na yawe bila unafiki wowote. Chukieni jambo lolote ovu, zingatieni jema.
Let love be without hypocrisy. Abhor that which is evil. Cling to that which is good.
10 Pendaneni kidugu; kila mmoja amfikirie mwenzake kwanza kwa heshima.
In love of the brothers be tenderly affectionate one to another; outdo one another in showing honor;
11 Msilegee katika bidii, muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia Bwana.
not lagging in diligence; fervent in spirit; serving the Lord;
12 Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida na kusali daima.
rejoicing in hope; enduring in troubles; continuing steadfastly in prayer;
13 Wasaidieni watu wa Mungu katika mahitaji yao; wapokeeni wageni kwa ukarimu.
contributing to the needs of the saints; given to hospitality.
14 Watakieni baraka wote wanaowadhulumu ninyi; naam, watakieni baraka na wala msiwalaani.
Bless those who persecute you; bless, and do not curse.
15 Furahini pamoja na wanaofurahi, lieni pamoja na wanaolia.
Rejoice with those who rejoice. Weep with those who weep.
16 Muwe na wema uleule kwa kila mtu. Msijitakie makuu, bali jishugulisheni na watu wadogo. Msijione kuwa wenye hekima sana.
Live in harmony with one another. Do not be arrogant, but associate with the humble. Do not be conceited.
17 Msilipe ovu kwa ovu. Zingatieni mambo mema mbele ya wote.
Repay no one evil for evil. Respect what is honorable in the sight of all people.
18 Kadiri inavyowezekana kwa upande wenu, muwe na amani na watu wote.
If it is possible, as much as it is up to you, be at peace with all people.
19 Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza asema Bwana.”
Do not seek revenge yourselves, beloved, but leave room for the wrath. For it is written, "Vengeance belongs to me; I will repay, says the Lord."
20 Tena, Maandiko yasema: “Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kinywaji. Maana kwa kufanya hivyo utamfanya apate aibu kali kama makaa ya moto juu ya kichwa chake.”
Therefore "If your enemy is hungry, feed him. If he is thirsty, give him a drink; for by doing this you will heap coals of fire on his head."
21 Usikubali kushindwa na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema.
Do not be overcome by evil, but overcome evil with good.