< Warumi 11 >

1 Basi, nauliza: je, Mungu amewakataa watu wake? Hata kidogo! Mini binafsi ni Mwisraeli mzawa wa Abrahamu, wa kabila la Benyamini.
Pravim torej: Jeli Bog zavrgel, ljudstvo svoje? Bog ne daj! kajti tudi jaz sem Izraelec, iz semena Abrahamovega, iz rodu Benjaminovega.
2 Mungu hakuwakataa watu wake aliowateua tangu mwanzo. Mnakumbuka yasemavyo Maandiko Matakatifu juu ya Eliya wakati alipomnung'unikia Mungu kuhusu Israeli:
Ni zavrgel Bog ljudstva svojega, kterega je najprej spoznal. Jeli ne veste, kaj pravi za Elija pismo? kakor se toži Bogu na Izraela govoreč:
3 “Bwana, wamewaua manabii wako na kubomoa madhabahu yako. Ni mimi tu peke yangu niliyebaki, nao wanataka kuniua?”
"Gospod, preroke tvoje so poubili in oltare tvoje so razkopali, in jaz sem ostal sam in iščejo dušo mojo."
4 Je, Mungu alimjibu nini? Alimwambia: “Nimejiwekea elfu saba ambao hawakumwabudu Baali.”
Ali kaj pravi njemu Božji odgovor? "Pustil sem sebi sedem tisoč mož, kteri niso pripognili kolena pred Baalom."
5 Basi, ndivyo ilivyo pia wakati huu wa sasa: ipo idadi ya waliobaki ambao Mungu aliwateua kwa sababu ya neema yake.
Tako je torej tudi v sedanjem času ostanek po izbiri milosti.
6 Uteuzi wake unatokana na neema yake, na si kwa sababu ya matendo yao. Maana, kama uteuzi wake ungetegemea matendo ya watu, neema yake haingekuwa neema tena.
Če pa iz milosti, ni več iz del, kajti bi milost več ne bila milost; a če iz del, več ni milost, kajti bi delo več ne bilo delo.
7 Sasa, je? Watu wa Israeli hawakukipata kile walichokuwa wanakitafuta; lakini wote walioteuliwa walikipata. Wengine walipumbazwa,
Kaj torej? Česar je iskal Izrael, tega ni dobil, a izbira je dobila, drugi pa so bili zaslepljeni,
8 kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mungu ameifanya mioyo yao kuwa mizito, na mpaka leo hii hawawezi kuona kwa macho yao wala kusikia kwa masikio yao.”
(Kakor je pisano: "Dal jim je Bog duha brljavega, oči, da ne vidijo, in ušesa, da ne slišijo, ) noter do današnjega dné.
9 Naye Daudi anasema: “Karamu zao na ziwe mtego wa kuwanasa, waanguke na kuadhibiwa.
In David pravi: "Postane naj jim njih miza za zanjko in za lov, in za pohujšanje in za povračilo;
10 Macho yao yatiwe giza wasiweze kuona. Migongo yao ipindike kwa taabu daima!”
Potamné naj njih oči, da ne vidijo, in njih hrbet čisto upogni."
11 Basi, nauliza: je, Wayahudi wamejikwaa hata wakaangamia kabisa? Hata kidogo! Kutokana na kosa lao ukombozi umewajia watu wa mataifa mengine, ili Wayahudi wapate kuwaonea wivu.
Pravim torej: Jeli so se spotaknili, da padejo? Bog ne daj! nego od njih pregrehe je zveličanje za pogane, da bi jih na posnemanje razdražili.
12 Kosa la Wayahudi limesababisha baraka nyingi kwa ulimwengu, na utovu wao kwa kiroho umeleta baraka nyingi kwa watu wa mataifa mengine. Basi, ni dhahiri zaidi kwamba utimilifu wao utasababisha baraka nyingi zaidi.
Če je pa njih pregreha bogastvo za svet in njih izguba bogastvo za pogane, koliko bolje njih polnost!
13 Basi, sasa nawaambieni ninyi watu wa mataifa mengine: Maadamu mimi nimekuwa mtume kwa watu wa mataifa mengine, ninajivunia huduma yangu,
Kajti vam poganom govorim, in dokler sem jaz apostelj poganov, hvalim svojo službo,
14 nipate kuwafanya wananchi wenzangu wawaonee ninyi wivu, na hivyo nipate kuwaokoa baadhi yao.
Ne bi li kako na posnemanje razdražil svoje meso in zveličal ktere izmed njih;
15 Maana ikiwa kukataliwa kwao kulisababisha ulimwengu upatanishwe na Mungu, itakuwaje wakati watakapokubaliwa na Mungu? Wafu watafufuka!
Ker če je njih zavrženje sprava sveta, kaj bi bilo sprejetje, če ne življenje iz mrtvih?
16 Ikiwa kipande cha kwanza cha mkate kimewekwa wakfu, mkate wote umewekwa wakfu; mizizi ya mti ikiwa mizuri, na matawi yake huwa mazuri pia.
Če je pa prvina sveta, tudi je testo, in če je korenina sveta, tudi so veje.
17 Naam, baadhi ya matawi ya mzeituni bustanini yalikatwa, na mahali pake tawi la mzeituni mwitu likapandikizwa. Ninyi watu wa mataifa mengine ndio hilo tawi la mzeituni mwitu; na sasa mnashiriki nguvu na utomvu wa mzeituni bustanini.
Če so se pa nektere veje odlomile, a ti, ker si bil divja olika, vcepil si se na nje in postal sodeležnik olikove korenine in tolšče,
18 Basi, msiwadharau wale waliokatwa kama matawi! Na, hata kama kuna la kujivunia, kumbukeni kwamba si ninyi mnaoitegemeza mizizi, bali mizizi ndiyo inayowategemeza ninyi.
Ne hvali se z vejami; če pa hvališ, ne nosiš ti korenine, nego korenina tebe.
19 Lakini utasema: “Matawi yalikatwa kusudi mimi nipandikizwe mahali pake.”
Porečeš torej: Odlomile so se veje, da bi se jaz vcepil.
20 Sawa! Yalikatwa kwa sababu ya kukosa imani, bali wewe unasimama kwa imani yako. Lakini usijivune; ila uwe na tahadhari.
Dobro, za voljo nevere so se odlomile, ti pa z vero stojiš. Ne prevzetuj, nego boj se.
21 Kwa maana, ikiwa Mungu hakuwahurumia Wayahudi ambao ni kama matawi ya asili, je, unadhani atakuhurumia wewe?
Ker če Bog naravnim vejam ni prizanesel, da tudi tebi kako ne prizanese.
22 Kumbuka, basi, jinsi Mungu alivyo mwema na mkali. Yeye ni mkali kwa wale walioanguka, na ni mwema kwako wewe ikiwa utaendelea katika wema wake; la sivyo, nawe pia utakatwa.
Glej torej dobroto in ostrost Božjo: nad temi, kteri so padli, ostrost, a nad teboj dobroto, če ostaneš v dobroti; če ne, tudi ti boš posekan.
23 Nao Wayahudi, hali kadhalika; wakiacha utovu wao wa imani, watapandikizwa tena. Maana Mungu anao uwezo wa kuwapandikiza tena.
A oni, če ne ostanejo v neveri, vcepili se bodo, kajti Bog je mogoč zopet jih vcepiti.
24 Ninyi watu wa mataifa mengine, kwa asili ni kama tawi la mzeituni mwitu, lakini mmeondolewa huko, mkapandikizwa katika mzeituni bustanini mahali ambapo kwa asili si penu. Lakini, Wayahudi kwa asili ni kama mzeituni bustanini, na itakuwa jambo rahisi zaidi kwao kupandikizwa tena katika mti huohuo wao.
Kajti če si ti odsekan od olike po naravi divje in si se vcepil proti naravi na pravo oliko, koliko bolje ti le, kteri se bodo vcepili na lastno oliko?
25 Ndugu zangu, napenda mjue ukweli huu uliofichika msije mkajiona wenye akili sana. Ukaidi wa Wayahudi ulikuwa ni wa muda tu, mpaka watu wa mataifa mengine watakapokuwa wamemfikia Mungu.
Kajti ne čem, da bi vi, bratje, ne vedeli skrivnosti, (da bi ne bili sami v sebi razumni, ) da je trdokornost Izraela deloma zadela, dokler ne vnide polnost poganov.
26 Hapo ndipo taifa lote la Israeli litakapookolewa, kama yesemavyo Maandiko Matakatifu: “Mkombozi atakuja kutoka Sioni, atauondoa uovu wa Yakobo.
In tako se bo zveličal ves Izrael, kakor je pisano: "Prišel bo iz Siona rešitelj in odvrnil nepobožnost od Jakoba;
27 Hili ndilo agano nitakalofanya nao wakati nitakapoziondoa dhambi zao.”
In to jim je od mene zaveza, kedar odvzamem njih grehe."
28 Kwa sababu wanaikataa Habari Njema, Wayahudi wamekuwa adui wa Mungu, lakini kwa faida yenu nyinyi watu wa mataifa. Lakini, kwa kuwa waliteuliwa, bado ni rafiki wa Mungu kwa sababu ya baba zao.
Poleg evangelja so sicer sovražniki za voljo vas, a poleg izbire so ljubljenci za voljo očetov.
29 Maana Mungu akisha wapa watu zawadi zake na kuwateua, hajuti kwamba amefanya hivyo.
Kajti brez kesanja so darovi in klicanje Božje,
30 Hapo awali ninyi mlikuwa mmemwasi Mungu, lakini sasa mmepata huruma yake kutokana na kuasi kwao.
Ker kakor tudi vi nekdaj niste verjeli Bogu, a sedaj ste usmiljenje dobili po njih neveri;
31 Hali kadhalika, kutokana na huruma mliyojaliwa ninyi, Wayahudi wanamwasi Mungu sasa ili nao pia wapokee sasa huruma ya Mungu.
Tako tudi ti sedaj niso verjeli, po vašem usmiljenji da bi tudi oni usmiljenje dobili.
32 Maana Mungu amewafunga watu wote katika uasi wao ili wapate kuwahurumia wote. (eleēsē g1653)
Kajti zaprl je Bog vse v neverstvo, da bi se vseh usmilil. (eleēsē g1653)
33 Utajiri, hekima na elimu ya Mungu ni kuu mno! Huruma zake hazichunguziki, na njia zake hazieleweki! Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:
O globočina bogastva in modrosti in znanja Božjega! kako neizvedljive so njegove sodbe in kako nezasledljive njegove poti!
34 “Nani aliyepata kuyajua mawazo ya Bwana? Nani awezaye kuwa mshauri wake?
Kajti: "kdo je spoznal misel Gospodovo?"
35 Au, nani aliyempa yeye kitu kwanza hata aweze kulipwa tena kitu hicho?”
Ali: "kdo je bil njemu svetovalec?" Ali: "kdo je njemu naprej dal, ter mu se bo nazaj dajalo?"
36 Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, vyote vipo kwa uwezo wake na kwa ajili yake. Utukufu na uwe kwake hata milele! Amina. (aiōn g165)
Kajti od njega in po njem in v njem je vse, njemu slava na veke! Amen. (aiōn g165)

< Warumi 11 >