< Ufunuo 8 >
1 Na Mwanakondoo alipouvunja mhuri wa saba, kukawa kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa.
And when He opened the seventh seal, there was silence in heaven for about half an hour:
2 Kisha nikawaona wale malaika saba wanaosimama mbele ya Mungu wamepewa tarumbeta saba.
and I saw the seven angels, that stood before God; and seven trumpets were given to them.
3 Malaika mwingine akafika, akiwa anachukua chetezo cha dhahabu, akasimama mbele ya madhabahu ya kufukizia ubani. Naye akapewa ubani mwingi autoe sadaka pamoja na sala za watu wote wa Mungu, juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.
And another angel came and stood at the altar, having a golden censer; and there was given to Him much incense, that He might present it with the prayers of all the saints on the golden altar, which was before the throne.
4 Moshi wa ubani ukapanda juu, pamoja na sala za watu wa Mungu, kutoka mikononi mwake huyo malaika aliyekuwa mbele ya Mungu.
And the smoke of the incense went up with the prayers of the saints, out of the hand of the angel, before God.
5 Kisha malaika akakichukua hicho chetezo, akakijaza moto wa madhabahuni akakitupa duniani. Kukawa na ngurumo, sauti, umeme na tetemeko la ardhi.
And the angel took the censer, and filled it with fire of the altar, and cast it upon the earth: and there were voices, and thunders, and lightnings, and an earthquake.
6 Kisha wale malaika saba wenye tarumbeta saba wakajiweka tayari kupiga mbiu ya mgambo.
And the seven angels, that had the seven trumpets, prepared themselves to sound their trumpets.
7 Malaika wa kwanza akapiga tarumbeta yake. Mchanganyiko wa mvua ya mawe na moto, pamoja na damu, ukamwagwa juu ya nchi. Theluthi moja ya nchi ikaungua, theluthi moja ya miti ikaungua, na majani yote mabichi yakaungua.
And the first angel sounded his trumpet, and there was hail and fire mingled with blood, and it was cast down upon the earth: and a third part of the trees and every green herb was burnt up.
8 Malaika wa pili akapiga tarumbeta yake. Na kitu kama mlima mkubwa unaowaka moto ukatupwa baharini. Theluthi moja ya bahari ikawa damu,
And the second angel sounded, and I saw as it were a great mountain on fire cast into the sea, and a third part of the sea became blood.
9 theluthi moja ya viumbe vya baharini vikafa na theluthi moja ya meli zikaharibiwa.
And a third part of the creatures in the sea, that had life, died; and a third part of the ships were destroyed.
10 Kisha malaika wa tatu akapiga tarumbeta yake. Na nyota kubwa ikiwaka kama bonge la moto, ikaanguka kutoka mbinguni, na kutua juu ya theluthi moja ya mito na chemchemi za maji.
And the third angel sounded, and there fell from heaven a great star burning like a torch, and it fell upon a third part of the rivers, and the fountains of waters: and the name of the star is Wormwood;
11 (Nyota hiyo inaitwa “Uchungu.”) Basi, theluthi moja ya maji yakawa machungu; watu wengi wakafa kutokana na maji hayo, kwa sababu yaligeuka kuwa machungu.
and a third part of the waters became as wormwood: and many men died of the waters, because they were bitter.
12 Kisha malaika wa nne akapiga tarumbeta yake. Ndipo theluthi moja ya jua, ya mwezi na ya nyota ikapata pigo; hata mwangaza ukapoteza theluthi moja ya mng'ao wake. Theluthi moja ya mchana ikakosa mwanga, hali kadhalika na theluthi moja ya usiku.
And the fourth angel sounded, and a third part of the sun was smitten, and a third part of the moon, and a third part of the stars; so that the third part of them was darkened, and the day lost a third part of it's light, and the night likewise.
13 Kisha nikatazama, nikasikia tai akiruka juu kabisa angani anasema kwa sauti kubwa, “Ole, ole, ole kwa wanaoishi duniani wakati malaika watatu waliobaki watakapopiga tarumbeta zao!”
And I beheld, and heard an angel flying in the midst of heaven saying with a loud voice, Wo, wo, wo to the inhabitants on the earth from the other voices of the trumpet of the three angels, that are yet to sound.