< Ufunuo 5 >
1 Kisha katika mkono wa kulia wa huyo aliyeketi juu ya kiti cha enzi, nikaona kitabu; nacho kilikuwa kimeandikwa ndani na nje na kufungwa na mihuri saba.
我看見在那坐於寶座者的右手上,有一書卷,內外都寫著字,用七個印密封著。
2 Tena nikamwona malaika mwenye nguvu akitangaza kwa sauti kubwa: “Nani anayestahili kuvunja hiyo mihuri na kukifungua kitabu hicho?”
我又看見一位強有力的天使大聲宣佈說:「誰當得起展開這書卷,開啟它的印呢?」
3 Lakini hakupatikana mtu yeyote mbinguni, wala duniani, wala chini Kuzimu, aliyeweza kukifungua hicho kitabu au kukitazama ndani. ()
但是,不論在天上、地上、或地下,沒有一個能展開那書卷的,沒有能閱讀它的。
4 Basi, mimi nikalia sana kwa sababu hakupatikana mtu aliyestahili kukifungua, au kukitazama ndani.
我就大哭起來,因為沒有找著一位當得起展開那書卷,和閱讀它的。
5 Kisha mmoja wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama! Simba wa kabila la Yuda, mjukuu maarufu wa Daudi, ameshinda. Yeye anaweza kuivunja mihuri yake saba na kukifungua hicho kitabu.”
長老中有一位對我說:「不要哭!看,那出於猶大支派中的獅子,達味的苗裔已得了勝利,他能展開那書卷和那七個印。」
6 Kisha nikaona pale katikati ya kiti cha enzi Mwana kondoo amesimama, akizungukwa kila upande na vile viumbe hai vinne, na wale wazee. Huyo Mwanakondoo alionekana kana kwamba amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba ambayo ni roho saba za Mungu zilizokuwa zimepelekwa kila mahali duniani.
我就看見在寶座和四個活物中間,並在長老們中間,站著一隻羔羊,好像被宰殺過的,他有七個角和七隻眼:那眼睛就是被派往全地的天主的七神。
7 Mwanakondoo akaenda, akakitwaa hicho kitabu kutoka mkono wa kulia wa yule aliyeketi juu ya kiti cha enzi.
他於是前來,從坐在寶座上的那位右手中接了那書卷。
8 Mara tu alipokwisha twaa hicho kitabu, vile viumbe hai vinne pamoja na wale wazee ishirini na wanne walianguka kifudifudi mbele ya Mwanakondoo. Kila mmoja, alikuwa na kinubi na bakuli za dhahabu zilizojaa ubani, ambao ni sala za watu wa Mungu.
當他接那書卷的時候,那四個活物和那二十四位長老,都俯伏在羔羊前,各拿著弦琴和盛滿了香料的金盂--這香料即是眾聖徒的祈禱,
9 Basi, wakaimba wimbo huu mpya: “Wewe unastahili kukitwaa hicho kitabu na kuivunja mihuri yake. Kwa sababu wewe umechinjwa, na kwa damu yako umemnunulia Mungu watu kutoka katika kila kabila, lugha, jamaa na taifa.
並唱新歌說:「惟有你當得起接受那書卷和開啟它的印,因為你曾被宰殺,曾用你的血,從各支派、各異語、各民族、各邦國中,把人贖來歸於天主,
10 Wewe umewafanya wawe ufalme wa makuhani wamtumikie Mungu wetu nao watatawala duniani.”
並使他們成為國度和司祭,事奉我們的天主;他們必要為王,統治世界。」
11 Kisha nikatazama, nikasikia sauti ya malaika wengi sana, idadi isiyohesabika, maelfu na maelfu. Walikuwa wamekaa kuzunguka kiti cha enzi, vile viumbe hai vinne na wale wazee;
我又看見,且聽見在寶座、活物和長老的四周,有許多天使的聲音,他們的數目千千萬萬,
12 wakasema kwa sauti kuu: “Mwanakondoo aliyechinjwa anastahili kupokea uwezo, utajiri, hekima, nguvu, utukufu na sifa.”
大聲喊說:「被宰殺的羔羊堪享權能、富裕、智慧、勇毅、尊威、光榮、和讚頌!」
13 Nikasikia viumbe vyote mbinguni, duniani, chini kuzimuni na baharini—viumbe vyote ulimwenguni—vikisema: “Kwake yeye aketiye katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo, iwe sifa na heshima na utukufu na enzi milele na milele.” (aiōn , questioned)
此後我又聽見一切受造物,即天上、地上、地下和海中的萬物都說:「願讚頌、尊威、光榮和權力,歸於坐在寶座上的那位和羔羊,至於無窮之世!」 (aiōn )
14 Na vile viumbe vinne hai vikasema, “Amina!” Na wale wazee wakaanguka kifudifudi, wakaabudu.
那四個活物就答說:「阿們。」長老們遂俯伏朝拜。