< Ufunuo 21 >
1 Kisha nikaona mbingu mpya na dunia mpya. Mbingu ile ya kwanza na dunia ile ya kwanza vilikuwa vimetoweka, nayo bahari pia haikuweko tena.
ᏓᎩᎪᎲᎩᏃ ᎢᏤ ᎦᎸᎶᎢ ᎠᎴ ᎢᏤ ᎦᏙᎯ; ᎢᎬᏱᏱᏰᏃ ᎦᎸᎶᎢ ᎠᎴ ᎢᎬᏱᏱ ᎦᏙᎯ ᏥᎨᏒᎩ ᎤᏂᎶᏐᏅᎩ; ᎠᎴ ᎥᏝ ᎿᎭᏉ ᎠᎺᏉᎯ ᏱᎨᏎᎢ.
2 Nikaona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni. Ulikuwa umetayarishwa vizuri kama bibi arusi aliyepambwa tayari kukutana na mumewe.
ᎠᎴ ᎠᏴ ᏣᏂ ᎠᎩᎪᎲᎩ ᎦᎸᏉᏗᏳ ᎦᏚᎲ ᎾᏍᎩ ᎢᏤ ᏥᎷᏏᎵᎻ ᏓᏳᏠᎠᏒᎩ ᎤᏁᎳᏅᎯᏱ ᎦᎸᎶᎢ, ᎤᏛᏅᎢᏍᏛᎩ ᎾᏍᎩᏯ ᎠᏥᏰᎯ ᏣᏙᏚᎢᏍᏗᏍᎪ ᏣᏛᏅᎢᏍᏓᏁᎰ ᎤᏰᎯ.
3 Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka katika kiti cha enzi ikisema, “Tazama! Mungu amefanya makao yake kati ya watu. Atakaa kati yao, nao watakuwa watu wake, naye atakuwa Mungu wao.
ᎠᏆᏛᎦᏅᎩᏃ ᎠᏍᏓᏯ ᎧᏁᎬ ᎩᎶ ᎦᎸᎳᏗ ᏛᏓᎴᎲᏍᎬᎩ ᎯᎠ ᏂᎦᏪᏍᎬᎩ, ᎬᏂᏳᏉ ᎤᏁᎳᏅᎯ ᎤᎵᏦᏛ ᏴᏫ ᎠᏁᎲ ᎤᏓᏑᏯ, ᎠᎴ ᎤᏁᎳᏅᎯ ᎾᏍᎩ ᎠᏁᎲ ᏛᏕᏂ, ᎠᎴ ᎾᏍᎩ ᏧᏤᎵ ᎨᏎᏍᏗ ᏴᏫ, ᎤᏁᎳᏅᎯᏃ ᎤᏩᏒ ᎾᏍᎩ ᎠᏁᎲ ᎡᎮᏍᏗ ᎤᎾᏤᎵ ᎤᏁᎳᏅᎯ ᎨᏎᏍᏗ.
4 Yeye atayafuta machozi yao yote; maana hakutakuwako tena na kifo, wala uchungu, wala kilio, wala maumivu; maana ile hali ya kale imepita!”
ᎠᎴ ᎤᏁᎳᏅᎯ ᏙᏓᎦᏅᎦᎸᎯ ᏂᎦᏛ ᏓᏂᎦᏌᏬᎢᎲᎢ; ᎥᏝ ᎠᎴ ᎿᎭᏉ ᏰᎮᏍᏗ ᎠᏲᎱᎯᏍᏗ, ᎠᎴ ᎤᏲ ᎠᏰᎸᏗ ᎨᏒ, ᎠᎴ ᏗᏠᏯᏍᏗ ᎨᏒᎢ, ᎥᏝ ᎠᎴ ᎿᎭᏉ ᏰᎮᏍᏗ ᎡᎯᏍᏗ ᎨᏒᎢ; ᎢᎬᏱᏱᏰᏃ ᏧᏓᎴᏅᏛ ᏤᎲ ᎤᎶᏐᏅ.
5 Kisha yule aliyeketi juu ya kiti cha enzi akasema, “Tazama, nafanya yote mapya.” Tena akaniambia, “Andika hili, maana maneno haya ni ya kuaminika na ya kweli!”
ᎦᏍᎩᎸᏃ ᎤᏬᎵ, ᎯᎠ ᏄᏪᏒᎩ, ᎬᏂᏳᏉ ᏂᎦᏗᏳ ᏧᏓᎴᏅᏛ ᎢᏤ ᏂᎬᏁᎭ. ᎠᎴ ᎯᎠ ᎾᎩᏪᏎᎸᎩ, ᎰᏪᎸᎦ; ᎯᎠᏰᏃ ᎾᏍᎩ ᎧᏃᎮᏛ ᎬᏜᏓᏏᏛᎡᏗ ᏂᎨᏒᎾ ᎠᎴ ᎤᏙᎯᏳᎯᏯ.
6 Kisha akaniambia, “Yametimia! Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Aliye na kiu nitampa kinywaji cha bure kutoka katika chemchemi ya maji ya uzima.
ᎠᎴ ᎯᎠ ᎾᎩᏪᏎᎸᎩ; ᎾᏍᎩ ᏂᏌᎵᏍᏓ. ᎠᏴ ᎡᎵᏆ ᎠᎴ ᎣᎻᎦ, ᎢᎬᏱᏱ ᎨᏒ ᎠᎴ ᎤᎵᏍᏆᎸᏗ ᎨᏒᎢ. ᎤᏔᏕᎩᏍᎩ ᎠᎹ ᎬᏂᏛ ᎠᏓᏁᎯ ᎦᏄᎪᎬ ᏓᏥᏁᏁᎵ ᏧᎬᏩᎶᏗ ᏂᎨᏒᎾ.
7 Yeyote atakayeshinda atapokea hiki, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
ᎩᎶ ᎠᏓᏎᎪᎩᏍᎨᏍᏗ ᏂᎦᏗᏳ ᏧᏓᎴᏅᏛ ᎤᏤᎵ ᎢᏳᎵᏍᏙᏗ ᎨᏎᏍᏗ; ᎠᎴ ᎠᏴ ᏥᏯᏁᎳᏅᎯ ᎨᏎᏍᏗ, ᎤᏩᏒᏃ ᎠᏴ ᎠᏇᏥ ᎨᏎᏍᏗ.
8 Lakini watu waoga, wasioamini, wapotovu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, na waongo wote, mahali pao patakuwa ndani ya lile ziwa linalowaka moto na kiberiti; hicho ndicho kifo cha pili.” (Limnē Pyr )
ᎤᏂᏍᎦᎡᎾᏍᎩᏂ. ᎠᎴ ᏄᏃᎯᏳᏒᎾ, ᎠᎴ ᎤᏂᏍᎦᎢᏍᏗ, ᎠᎴ ᏗᎾᏓᎯᎯ, ᎠᎴ ᎤᏂᏁᎫᏥᏛ, ᎠᎴ ᏗᎾᏙᏂᏍᎩ, ᎠᎴ ᎤᏁᎳᏅᎯ ᏗᏰᎸᎯ ᏗᎾᏓᏙᎵᏍᏓᏁᎯ, ᎠᎴ ᏂᎦᏗᏳ ᎠᏂᏰᎪᎩ, ᎤᎾᏤᎵ ᎢᎨᎬᏁᏗ ᎨᏎᏍᏗ ᎥᏓᎸ ᎾᎿᎭᎠᏓᏪᎵᎩᏍᎬ ᎠᏥᎸ ᎠᎴ ᏌᎪᏂᎨ ᎠᏓᏪᎵᎩᏍᎩ; ᎾᏍᎩ ᏔᎵᏁ ᎠᏲᎱᎯᏍᏗ ᏥᎩ. (Limnē Pyr )
9 Kisha mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba yaliyokuwa yamejaa mabaa saba ya mwisho, akaja na kuniambia, “Njoo! Mimi nitakuonyesha bibi arusi, mkewe Mwanakondoo!”
ᎠᎩᎷᏤᎸᎩᏃ ᎠᏏᏴᏫ ᎾᏍᎩ Ꮎ ᎦᎵᏉᎩ ᎢᏯᏂᏛ ᏗᏂᎧᎿᎭᏩᏗᏙᎯ, ᎾᏍᎩ ᏥᏓᏂᏰᎲᎩ ᏚᎵᏉᎩ ᎫᎫ ᎦᎵᏉᎩ ᎤᎵᏍᏆᎸᏗ ᎤᏕᏯᏙᏗ ᏗᏟᏍᏗ, ᎠᎴ ᎠᏆᎵᏃᎮᏔᏅᎩ, ᎯᎠ ᏄᏪᏒᎩ; ᎡᎮᎾ, ᏓᎬᏯᏎᎮᎵᏃ ᎠᏥᏰᎯ ᎤᏃᏕᎾ ᎠᎩᎾ ᎤᏓᎵᎢ.
10 Basi, Roho akanikumba, naye malaika akanipeleka juu ya mlima mrefu sana. Akanionyesha mji mtakatifu, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni,
ᎠᏆᏘᎾᏫᏛᎲᎩᏃ ᏗᏆᏓᏅᏛ ᎡᏆ ᎠᎴ ᎢᏅ ᎢᎦᏘ ᏦᏓᎸᎢ ᏩᏆᏘᏅᏍᏔᏅᎩ, ᎠᎴ ᎠᎩᎾᏄᎪᏫᏎᎸᎩ Ꮎ ᎡᏆ ᎦᏚᎲᎢ, ᎾᏍᎩ ᎦᎸᏉᏗ ᏥᎷᏏᎵᎻ, ᎡᎳᏗ ᏅᏓᏳᏍᏗᏗᏒᎩ ᎦᎸᎳᏗ ᎤᏁᎳᏅᎯᏱ ᏛᏓᎴᎲᏍᎬᎩ.
11 uking'aa kwa utukufu wa Mungu. Mwangaza wake ulikuwa kama wa jiwe la thamani kubwa kama yaspi, angavu kama kioo.
ᎦᎸᏉᏗᏳ ᎨᏒ ᎤᏁᎳᏅᎯ ᎤᏤᎵᎦ ᎤᏣᏃᏛᎩ; ᎠᎴ ᎾᏍᎩ ᏚᎸᏌᏛ, ᏅᏯ ᎤᏣᏘ ᏧᎬᏩᎶᏗ ᎾᏍᎩᏯ ᎨᏒᎩ, ᎾᏍᎩ ᏣᏍᏆ ᏅᏯ ᎾᏍᎩᏯᎢ ᏗᎬᏩᎸᏌᏛ ᎨᏒᎩ.
12 Ulikuwa na ukuta mrefu na mkubwa, wenye milango kumi na miwili, na malaika wanangojea kumi na wawili. Majina ya wangoja milango kumi na mawili ya Israeli yalikuwa yameandikwa juu ya milango hiyo.
ᎠᏐᏴᎩᏃ ᎡᏆ ᎢᏅ ᎢᎦᏘ, ᎦᎶᎯᏍᏗᏱᏃ ᏔᎳᏚ ᏕᎪᏢᏒᎩ, ᎠᎴ ᎦᎶᎯᏍᏗᏱ ᏔᎳᏚ ᎢᏯᏂᏛ ᏗᏂᎧᎿᎭᏩᏗᏙᎯ [ ᏓᏂᏙᎬᎩ, ] ᏚᎾᏙᎥᏃ ᏕᎪᏪᎸᎩ ᎦᎶᎯᏍᏗᏱ, ᎾᏍᎩ ᏔᎳᏚ ᎾᏂᎳᏍᏓᎸ ᎢᏏᎵ ᏧᏪᏥ ᏚᎾᏙᎥᎢ.
13 Kila upande ulikuwa na milango mitatu: upande wa mashariki, milango mitatu, kaskazini milango mitatu, kusini milango mitatu na magharibi milango mitatu.
ᏅᏙ ᏗᎧᎸᎬ ᎢᏗᏢ ᏦᎢ ᎦᎶᎯᏍᏗᏱ [ ᏕᎪᏢᏒᎩ, ] ᏧᏴᏢᏃ ᎢᏗᏢ ᏦᎢ ᎦᎶᎯᏍᏗᏱ; ᏧᎦᎾᏮᏃ ᎢᏗᏢ ᏦᎢ ᎦᎶᎯᏍᏗᏱ; ᏭᏕᎵᎬᏃ ᎢᏗᏢ ᏦᎢ ᎦᎶᎯᏍᏗᏱ.
14 Kuta za mji huo zilikuwa zimejengwa juu ya mawe ya msingi kumi na mawili, na juu ya mawe hayo yalikuwa yameandikwa majina na mitume kumi na wawili wa Mwanakondoo.
ᎠᏐᏴᏃ ᎦᏚᎲ ᏔᎳᏚ ᏕᎦᎫᏍᏓᎥᎩ, ᏕᎦᎫᏍᏓᎥᏃ ᏔᎳᏚ ᏚᎾᏙᎥᎢ [ ᏕᎪᏪᎸᎩ, ] ᎾᏍᎩ ᏔᎳᏚ ᎢᏯᏂᏛ ᎤᏃᏕᎾ ᎠᎩᎾ ᏧᏅᏏᏛ ᏚᎾᏙᎥᎢ.
15 Basi, yule malaika aliyekuwa anasema nami alikuwa na kijiti cha dhahabu cha kupimia, kwa ajili ya kuupima huo mji, milango yake na kuta zake.
ᎾᏍᎩᏃ ᎠᏆᎵᏃᎮᏔᏅᎯ ᎦᏁᎲᎩ ᎠᏕᎸᏓᎶᏂᎨ ᎠᏢᏔᏅᎯ ᎠᏟᎶᏍᏗ, ᎦᏚᎲ ᎠᏟᎶᏍᏗ, ᎠᎴ ᎦᎶᎯᏍᏗᏱ ᏗᏟᎶᏍᏗ, ᎠᎴ ᎠᏐᏴ ᎠᏟᎶᏍᏗ.
16 Mji wenyewe ulikuwa wa mraba, upana na urefu wake sawa. Basi, malaika akaupima mji huo kwa kijiti chake: ulikuwa na urefu, upana na urefu wa kwenda juu, kama kilomita elfu mbili na mia nne.
ᎦᏚᎲᏃ ᏅᎩ ᏧᏅᏏᏴ ᎨᏒᎩ, ᎦᏅᎯᏒ ᎠᎴ ᎠᏯᏛᎥ ᎤᏠᏱᏉ ᎨᏒᎩ. ᎤᏟᎶᎥᎩᏃ ᎦᏚᎲ ᎤᏩᏔᏅᎩ ᎠᏟᎶᏍᏗ, ᎯᏍᎩᎦᏚ ᎢᏯᏍᎪᎯᏧᏈ ᎢᏳᏟᎶᏛ ᏂᎬᎩ. ᏂᎦᏅᎯᏒ ᎠᎴ ᎾᏯᏛᎲ ᎠᎴ ᏂᎦᏛᎢ ᎤᏠᏱᏉ ᎨᏒᎩ.
17 Kisha akaupima ukuta wake pia; nao ulikuwa mita sitini kwa kipimo cha macho cha kibinadamu ambacho malaika alitumia.
ᎠᏎᏴᏃ ᎤᏟᎶᎥᎩ ᎠᏍᎪᎯᏧᏈ ᏅᎦᏍᎪᎯ ᏅᎩᎦᎵ ᎢᏯᎩᏳᏍᏈᏛ ᎤᏟᎶᎥᎩ, ᎾᏍᎩ ᏴᏫ ᎤᏟᎶᏍᏗ ᎢᎦᏅᎯᏛ, ᎾᏍᎩ ᏗᎧᎿᎭᏩᏗᏙᎯ ᎤᏟᎶᏍᏗ.
18 Ukuta huo ulikuwa umejengwa kwa mawe mekundu ya thamani, na mji wenyewe ulikuwa umejengwa kwa dhahabu safi, angavu kama kioo.
ᎠᏐᏴᏃ ᏣᏍᏆ ᏅᏯ ᎠᏁᏍᎨᏛᎩ; ᎦᏚᎲᏃ ᎪᎱᏍᏗ ᎾᏑᏴᎾ ᎠᏕᎸ ᏓᎶᏂᎨ ᎪᏢᏛᎩ, ᏧᎸᏌᏛ ᎠᏓᎨᏗ ᎾᏍᎩᏯᎢ.
19 Mawe ya msingi wa ukuta huo yalikuwa yamepambwa kwa kila aina ya mawe ya thamani. Jiwe la kwanza la msingi lilikuwa jiwe la thamani jekundu, la pili yakuti samawati, la tatu kalkedoni, la nne zamaradi,
ᏕᎦᎫᏍᏓᎥᏃ ᎠᏐᏴ ᎦᏚᎲᎢ ᏕᎪᏚᎢᏍᏛᎩ ᏄᏓᎴᏒ ᏗᎦᎸᏉᏗ ᏅᏯ; ᎢᎬᏱᏱ ᎦᎫᏍᏓᎥ ᏣᏍᏆ ᎨᏒᎩ, ᏔᎵᏁᏃ ᏌᏆᏯ, ᏦᎢᏁᏃ ᎦᎵᏏᏙᏂ, ᏅᎩᏁᏃ ᎡᎻᎳ,
20 la tano sardoniki, la sita akiki, la saba krisolito, la nane zabarijadi, la tisa topazi, la kumi krisopraso, la kumi na moja yasinto, na la kumi na mbili amethisto.
ᎯᏍᎩᏃ ᏌᏙᏂᎩ, ᏑᏓᎵᏁᏃ ᏌᏗᏱ, ᎦᎵᏉᎩᏁᏃ ᎩᏐᎳᏗ, ᏧᏁᎵᏁᏃ ᏇᎵ, ᏐᎣᏁᎵᏁᏃ ᏙᏆᏏ, ᎠᏍᎪᎯᏁᏃ ᏟᏌᏇᏌ, ᏌᏚᏏᏁᏃ ᏤᏏᏂ, ᏔᎳᏚᏏᏁᏃ ᎠᎻᏗᏏ.
21 Na ile milango kumi na miwili ilikuwa lulu kumi na mbili; kila mlango ulikuwa umetengenezwa kwa lulu moja. Barabara kuu ya mji ilikuwa imetengenezwa kwa dhahabu safi, angavu kama kioo.
ᏔᎳᏚᏃ ᏕᎪᏢᏒ ᏗᏍᏚᏗ ᏔᎳᏚ ᏓᎬᎾᎢᏳᎾᏍᏗ ᏕᎪᏢᏛᎩ; ᏌᏉ ᎠᏍᏚᏗ ᏌᏉ ᏓᎬᎾᎢᏳᏍᏗ ᎪᏢᏛᎩ ᎡᏓᏍᏗᏱ ᎤᏜᏓᏅᏛ ᎦᏚᎲ ᎪᎱᏍᏗ ᎾᏑᏴᎾ ᎠᏕᎸ ᏓᎶᏂᎨ ᎠᏢᏛᎩ, ᏧᎸᏌᏛ ᎠᏓᎨᏗ ᎾᏍᎩᏯᎢ.
22 Sikuona hekalu katika mji huo, maana Bwana Mungu Mwenye Uwezo na yule Mwanakondoo ndio Hekalu lake.
ᎥᏝ ᎠᎴ ᏯᎩᎪᎮ ᎾᎿᎭᏗᎦᎳᏫᎢᏍᏗᏱ; ᎤᎬᏫᏳᎯᏰᏃ ᎤᏁᎳᏅᎯ ᏫᎾᏍᏛᎾ ᎤᎵᏂᎩᏛ ᎠᎴ ᎤᏃᏕᎾ-ᎠᎩᎾ ᎾᏍᎩ ᏗᎦᎳᏫᎢᏍᏗᏱ ᎢᎩ.
23 Mji huo hauhitaji jua wala mwezi kuangazia, maana utukufu wa Mungu huuangazia, na taa yake ni yule Mwanakondoo.
ᎦᏚᎲᏃ ᎥᏝ ᏳᎾᏚᎵ ᏅᏙ-ᎢᎦ-ᎡᎯ ᎠᎴ ᏅᏙ-ᎡᏃᏱ-ᎡᎯ ᎤᎦᎵᎯᏍᏗᏱ ᎾᎿᎭᏂ; ᎦᎸᏉᏗᏳᏰᏃ ᎨᏒ ᎤᏁᎳᏅᎯ ᎤᏤᎵ ᎢᎦ ᎤᏘᏍᏛ ᎾᎿᎭᏂ, ᎠᎴ ᎤᏃᏕᎾ-ᎠᎩᎾ ᎢᎦ ᎠᏘᏍᏗᏍᎩ ᎢᎩ ᎾᎿᎭᏂ.
24 Watu wa mataifa watatembea katika mwanga wake, na wafalme wa dunia watauletea utajiri wao.
ᏧᎾᏓᎴᏅᏛᏃ ᏴᏫ ᎾᏍᎩ ᎨᏥᏍᏕᎸᏛ ᎨᏒ ᎾᏍᎩ ᏚᎸᏌᏛ ᎠᏁᏙᎮᏍᏗ; ᎤᏂᎬᏫᏳᏃ ᎡᎶᎯ ᎠᏁᎯ ᎾᎿᎭᎠᏂᏴᎯᎭ ᎨᏥᎸᏉᏛ ᎠᎴ ᏧᎾᏤᎵ ᏧᏓᎴᏅᏛ ᏗᎦᎸᏉᏗ.
25 Milango ya mji huo itakuwa wazi mchana wote; maana hakutakuwa na usiku humo.
ᎠᎴ ᎦᎶᎯᏍᏗᏱ ᎾᎿᎭᏕᎪᏢᏒ ᎥᏝ ᏧᏂᏍᏚᏗ ᏱᎨᏎᏍᏗ ᎢᎦ, ᎥᏝᏰᏃ ᏒᏃᏱ ᏱᎨᏎᏍᏗ ᎾᎿᎭᏂ.
26 Fahari na utajiri wa watu wa mataifa utaletwa humo ndani.
ᎠᎴ ᎾᎿᎭᎠᏂᏲᎯᎮᏍᏗ ᏧᎾᏓᎴᏅᏛ ᎠᏴ ᎤᎾᏤᎵ ᎦᎸᏉᏗᏳ ᎨᏒ ᎠᎴ ᏣᏓᎴᏅᏛ ᏗᎦᎸᏉᏗ.
27 Lakini hakuna chochote kilicho najisi kitakachoingia humo; wala mtu yeyote atendaye mambo ya kuchukiza au ya uongo hataingia humo. Ni wale tu walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo ndio watakaoingia ndani.
ᎠᎴ ᎥᏝ ᎠᏎ ᎾᎿᎭᎤᏴᏍᏗ ᏱᎨᏎᏍᏗ ᎪᎱᏍᏗ ᎦᏓᎭ, ᎠᎴ ᎤᏂᏆᏘᏍᏗ ᏧᎸᏫᏍᏓᏁᎯ, ᎠᎴ ᎦᏰᎪᎩ; ᎤᏅᏒᏍᎩᏂ [ ᎤᏂᏴᏍᏗ ᎨᏎᏍᏗ ᏚᎾᏙᎥ ] ᏗᎪᏪᎵ ᎬᏂᏛ ᎠᏓᏁᎯ ᎪᏪᎵᎯ ᎤᏃᏕᎾᎠᎩᎾ ᎤᏤᎵᎦ.