< Ufunuo 2 >
1 “Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika hivi: “Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye ashikaye nyota saba katika mkono wake wa kulia, na ambaye hutembea katikati ya vinara saba vya taa vya dhahabu.
你給厄弗所教會的天使寫:「那右手握著七顆星,而在那七盞金燈臺當中行走的這樣說:
2 Najua mambo yako yote; najua bidii yako na uvumilivu wako. Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume na kumbe sio, ukagundua kwamba ni waongo.
我知道你的作為、你的苦勞和你的堅忍;也知道你不能容忍惡人,並且你也會查驗出那些自稱為宗徒而實非宗徒的人,發現他們是撒謊的人;
3 Wewe unayo saburi, umestahimili taabu nyingi kwa ajili ya jina langu, wala hukuvunjika moyo.
也知道你有堅忍,為了我的名字受了苦,而毫不厭倦。
4 Lakini ninayo hoja moja juu yako: wewe hunipendi tena sasa kama pale awali.
可是,我有反對你的一條,就是你拋棄了你起初的愛德,
5 Basi, pakumbuke pale ulipokuwa kabla ya kuanguka, ukayaache madhambi yako, na kufanya kama ulivyofanya pale awali. La sivyo, naja kwako na kukiondoa kinara chako mahali pake.
所以你該回想你是從那裏跌下的,你該悔改,行先前所行的事:若你不悔改,我就要臨於你,把你的燈臺從原處挪去。
6 Lakini nakusifu juu ya kitu kimoja: wewe unayachukia wanayoyatenda Wanikolai kama ninavyoyachukia mimi.
不過你有一條:就是你惱恨了尼苛勞黨人的行為,這也是我所惱恨的。
7 “Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Wale wanaoshinda nitawapa haki ya kula matunda ya mti wa uzima ulioko ndani ya bustani ya Mungu.
有耳朵的,應聽聖神向各教會說的話:勝利的,我要把天主樂園中生命樹的果實,賜給他吃。」
8 “Kwa malaika wa kanisa la Smurna andika hivi: “Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye wa kwanza na wa mwisho, ambaye alikufa na akaishi tena.
你給斯米那教會的天使寫:「那身為元始和終末,曾死過而復生的這樣說:
9 Najua taabu zako; najua pia umaskini wako, ingawaje kwa kweli wewe ni tajiri; najua kashfa walizokufanyia wale wanaojiita Wayahudi lakini si Wayahudi wa kweli, bali ni kundi lake Shetani.
我知道你的困苦和貧窮,其實你是富足的;也知道你由那些自稱為猶太人的人受的誹謗,其實他們不是猶太人,而是撒殫的會眾。
10 Usiogope hata kidogo yale ambayo itakulazimu kuteseka. Sikiliza! Ibilisi anataka kuwajaribu kwa kuwatia baadhi yenu gerezani; nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Muwe waaminifu hata mpaka kufa, nami nitawapeni taji ya uzima.
不要怕你要受的苦!看,魔鬼要把你們中的一些人投在監裏,叫你們受試探;你們要遭受困難十天之久。你應當忠信至死,我必要賜給你生命的華冠。
11 “Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Wale wanaoshinda hawataumizwa na kifo cha pili.
有耳朵的,應聽聖神向各教會說的話:勝利的必不受第二次死亡的害。」
12 “Kwa malaika wa kanisa la Pergamoni andika hivi: “Huu ndio ujumbe wake yeye aliye na upanga mkali wenye kuwili.
你給培爾加摩教會的天使寫:「那持有雙刃利劍的這樣說:
13 Najua unakoishi: Wewe unaishi kwenye makao makuu ya Shetani! Lakini bado unashikilia jina langu; hukuikana imani yako kwangu hata siku zile Antipa shahidi wangu mwaminifu, alipouawa pale mahali anapoishi Shetani.
我知道你居住的地方,在那裏有撒殫的寶座;當我忠信的見證安提帕在你們中間,即在撒殫居住的地方被殺的時日,你仍堅持了我的名字,從未否認對我的信仰。
14 Lakini ninayo machache dhidi yako: baadhi yenu ni wafuasi wa Balaamu aliyemfundisha Balaki kuwatega wana wa Israeli wale vyakula vilivyotambikiwa sanamu za kufanya uzinzi.
可是,我有反對你的幾條,就是:在你們那裏,你容忍了一些堅持巴郎教訓的人;巴郎曾教巴拉克在以色列子民前安放了絆腳石,叫他們吃祭肉,行邪淫;
15 Vivyo hivyo, wako pia miongoni mwenu watu wanaofuata mafundisho ya Wanikolai.
同樣,你也容忍了一些堅持尼苛勞黨人教訓的人。
16 Basi, achana na madhambi yako. La sivyo, nitakuja kwako upesi na kupigana na watu hao kwa upanga utokao kinywani mwangu.
所以你應當悔改,不然,我就要迅速臨於你,用我口中的利劍攻擊他們。
17 “Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Wale wanaoshinda nitawapa ile mana iliyofichika. Nitawapa pia jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya ambalo hakuna mtu aliyelijua isipokuwa tu wale wanaolipokea.
有耳朵的,應聽聖神向各教會說的話:勝利的,我要賜給他隱藏的「瑪納」,也要賜給他一塊刻有新名號的白石,除領受的人外,誰也不認得這名號。」
18 “Kwa malaika wa kanisa la Thuatira andika hivi: “Huu ndio ujumbe wa Mwana wa Mungu, ambaye macho yake yametameta kama moto, na miguu yake inang'aa kama shaba iliyosuguliwa.
你給提雅提辣教會的天使寫:「那位眼睛有如火燄,雙腳有如光銅的天主子這樣說:
19 Najua mambo yako yote. Najua upendo wako, imani yako, utumishi wako na uvumilivu wako. Wewe unafanya vizuri zaidi sasa kuliko pale awali.
我知道你的作為、你的愛德、信德、服務和堅忍,也知道你末後的作為比先前的更多。
20 Lakini nina hoja moja juu yako: wewe unamvumilia yule mwanamke Yezabeli anayejiita nabii wa Mungu. Yeye huwafundisha na kuwapotosha watumishi wangu wafanye uzinzi na kula vyakula vilivyotambikiwa sanamu.
可是我有反對你的一條,就要你曾容許那自稱為先知的婦人依則貝耳教訓我的僕人,並引誘他們行邪淫,吃祭肉。
21 Nimempa muda wa kutubu dhambi zake, lakini hataki kuachana na uzinzi wake.
我原給了她悔改的時間,可是她不肯悔改自己的淫行。
22 Sikiliza! Sasa namtupa kitandani ambapo yeye pamoja na wote waliofanya uzinzi naye watapatwa na mateso makali. Naam, nitafanya hivyo, kama wasipotubu matendo yao mabaya waliyotenda naye.
看,我要把她投在病床上,並且把那些與她行邪淫的人,若他們對她的惡行不予以悔改,也投到重大的困苦中,
23 Tena nitawaua wafuasi wake, ili makanisa yote yatambue kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo na fikira za watu.
並將她的子女置於死地;這樣各教會都知道我是洞察人心和肺腑的主,並且我要按照你們的行為,報應你們每一個人。
24 “Lakini ninyi wengine mlioko huko Thuatira ambao hamfuati mafundisho yake Yezabeli, na ambao hamkujifunza kile wanachokiita Siri ya Shetani, nawaambieni kwamba sitawapeni mzigo mwingine.
至於你們其餘的提雅提辣人,凡不隨從這種教訓,不認識那所謂「撒殫奧義」的人,我對你們說:我不再把別的重擔加在你們身上,
25 Lazima mzingatie yale mliyo nayo sasa mpaka nitakapokuja.
可是你們應該堅持已有的,直到我來。
26 “Wanaoshinda, na wale watakaozingatia mpaka mwisho kutenda ninayotaka, nitawapa mamlaka juu ya mataifa.
勝利的,並且到最末堅守我事業的人,我必賜給他治理萬民的權柄--
27 Naam, nitawapa uwezo uleule nilioupokea kwa Baba: yaani, watayatawala mataifa kwa fimbo ya chuma na kuyavunjavunja kama chombo cha udongo.
他將用鐵杖管轄他們,有如打碎瓦器--
28 Tena nitawapa nyota ya asubuhi.
正如我由我父所領受的權柄一樣;我還要賜給他那顆晨星。
29 “Aliye na masikio, basi, na ayasikie yale Roho anayoyaambia makanisa!
有耳朵的,應聽聖神向各教會說的話。」