< Ufunuo 18 >

1 Baada ya hayo, nilimwona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni. Alikuwa na uwezo mkuu, na dunia ikamulikwa na mng'ao wake.
After this I saw another angel coming down from heaven. He had great authority, and the earth was illuminated with his glory.
2 Basi, akapaaza sauti kwa nguvu akisema, “Umeanguka; Babuloni mkuu umeanguka! Sasa umekuwa makao ya mashetani na pepo wachafu; umekuwa makao ya ndege wachafu na wa kuchukiza mno.
He cried out with a mighty voice, “Fallen is Babylon the great! She has become a dwelling place for demons, a haunt for every unclean spirit, and a haunt for every unclean and hated bird.
3 Maana mataifa yote yalileweshwa kwa divai kali ya uzinzi wake, nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi naye. Nao wafanyabiashara wa dunia wametajirika kutokana na anasa zake zisizo na kipimo.”
For all the nations have fallen because of the wine of the wrath of her fornication. The kings of the earth have committed fornication with her, and the merchants of the earth have become rich from the power of her luxury.”
4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema, “Watu wangu, ondokeni kwake, ili msishirikiane naye katika dhambi zake, msije mkaipata adhabu yake.
Then I heard another voice from heaven say, “Come out of her, my people, so that you do not participate in her sins, and so that you do not receive any of her plagues;
5 Kwa maana dhambi zake zimekuwa nyingi mno, zimelundikana mpaka mbinguni, na Mungu ameyakumbuka maovu yake.
for her sins are heaped as high as heaven, and God has remembered her unrighteous acts.
6 Mtendeeni kama alivyowatendea ninyi; mlipeni mara mbili kwa yale aliyoyatenda. Jazeni kikombe chake kwa kinywaji kikali mara mbili zaidi ya kile alichowapeni.
Render to her as she herself has rendered; make it double, as she has done, even according to her works. Mix a double portion for her in the cup she has mixed.
7 Mpeni mateso na uchungu kadiri ya kujigamba kwake, na kuishi kwake kwa anasa. Maana anajisemea moyoni: Ninaketi hapa; mimi ni malkia. Mimi si mjane, wala sitapatwa na uchungu!
As much as she has glorified herself and lived in luxury, give her the same amount of torment and mourning, for in her heart she says, ‘I am like a queen; I am not a widow and will never see mourning.’
8 Kwa sababu hiyo mabaa yake yatampata kwa siku moja: ugonjwa, huzuni na njaa. Atachomwa moto, maana Bwana Mungu mwenye kumhukumu ni Mwenye Uwezo.”
Therefore her plagues will come in a single day— death, mourning, and famine. She will be burned up with fire, for mighty is the Lord God who has judged her.”
9 Wafalme wa Dunia waliofanya uzinzi naye na kuishi naye maisha ya anasa wataomboleza na kulia wakati watakapoona moshi wa mji huo unaoteketea.
The kings of the earth who have committed fornication with her and lived in luxury with her will weep and wail over her when they see the smoke of her burning.
10 Wanasimama kwa mbali kwa sababu ya kuogopa mateso yake, na kusema, “Ole! Ole kwako Babuloni, mji maarufu na wenye nguvu! Kwa muda wa saa moja tu adhabu yako imekupata.”
In fear of her torment they will stand at a distance and say, “Alas, alas, for the great city, Babylon, the mighty city! For in a single hour yoʋr judgment has come.”
11 Wafanyabiashara wa dunia watalia na kumfanyia matanga, maana hakuna mtu anayenunua tena bidhaa zao;
The merchants of the earth will weep and mourn over her, because no one buys their cargo anymore,
12 hakuna tena wa kununua dhahabu yao, fedha, mawe ya thamani na lulu, kitani na nguo za rangi ya zambarau, hariri na nguo nyekundu; vyombo vya kila aina ya miti ya pekee, vyombo vya pembe za ndovu, vya miti ya thamani kubwa, vya shaba, chuma na marmari;
cargo of gold, silver, precious stones, pearls, fine linen, purple cloth, silk, scarlet cloth, all kinds of citron wood, all kinds of articles made of ivory, all kinds of articles made of costly wood, bronze, iron, and marble;
13 mdalasini, viungo, ubani, manemane, udi, divai, mafuta, unga na ngano, ng'ombe na kondoo, farasi na magari ya kukokotwa, watumwa wao na hata maisha ya watu.
cargo of cinnamon, incense, myrrh, frankincense, oil, fine flour, wheat, sheep, cattle, horses and chariots, and bodies and souls of men.
14 Wafanyabiashara wanamwambia: “Faida yote uliyotazamia imetoweka, na utajiri na fahari vimekuponyoka; hutaweza kuvipata tena!”
“The ripe fruit that was the desire of yoʋr soul has gone from yoʋ, and all yoʋr delicacies and splendors are lost to yoʋ; yoʋ will never find them again!”
15 Wafanya biashara waliotajirika kutokana na mji huo, watasimama mbali kwa sababu ya hofu ya mateso yake, watalalamika na kuomboleza,
The merchants of these wares, who became rich from her, will stand at a distance in fear of her torment, weeping and mourning aloud,
16 wakisema, “Ole! Ole kwa mji huu mkuu. Ulizoea kuvalia nguo za kitani, za rangi ya zambarau na nyekundu, na kujipamba kwa dhahabu, mawe ya thamani na lulu!
“Alas, alas, for the great city that was clothed in fine linen, in purple and scarlet, adorned with gold, with precious stone and pearls!
17 Kwa saa moja tu utajiri wako umetoweka!” Halafu manahodha wote na wasafiri wao, wanamaji na wote wanaofanya kazi baharini, walisimama kwa mbali,
For in a single hour such great wealth has been laid waste!” And every shipmaster and seafaring man, sailors and all whose trade is on the sea, stood at a distance
18 na walipouona moshi wa moto ule uliouteketeza, wakalia kwa sauti: “Hakujapata kuwako mji kama mji huu mkuu!”
and cried out as they saw the smoke of her burning, “What city is like the great city?”
19 Wakajimwagia vumbi juu ya vichwa vyao wakilia kwa sauti na kuomboleza: “Ole! Ole kwako mji mkuu! Ni mji ambamo wote wenye meli zisafirizo baharini walitajirika kutokana na utajiri wake. Kwa muda wa saa moja tu umepoteza kila kitu!”
They threw dust on their heads and cried out, weeping and mourning aloud, “Alas, alas, for the great city, where all who had ships at sea grew rich from her valuable merchandise! For in a single hour she has been laid waste.
20 Furahi ee mbingu, kwa sababu ya uharibifu wake. Furahini watu wa Mungu, mitume na manabii! Kwa maana Mungu ameuhukumu kwa sababu ya mambo uliyowatenda ninyi!
Rejoice over her, O heaven, and you saints, apostles, and prophets, for God has given judgment for you against her.”
21 Kisha malaika mmoja mwenye nguvu sana akainua jiwe mfano wa jiwe kubwa la kusagia, akalitupa baharini akisema, “Ndivyo, Babuloni atakavyotupwa na kupotea kabisa.
Then a mighty angel picked up a stone like a great millstone and threw it into the sea, and said, “With such violence Babylon the great city will be thrown down, never to be found again.
22 Sauti za vinubi za muziki, sauti za wapiga filimbi na tarumbeta hazitasikika tena ndani yako. Hakuna fundi wa namna yoyote ile atakayepatikana tena ndani yako; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikika tena ndani yako.
The sound of harpists, musicians, flutists, and trumpeters will never be heard in yoʋ again. No craftsman of any trade will ever be found in yoʋ again. The sound of a mill will never be heard in yoʋ again.
23 Mwanga wa taa hautaonekana tena ndani yako; sauti za bwana arusi na bibi arusi hazitasikika tena ndani yako. Wafanyabiashara wako walikuwa wakuu duniani, na kwa uchawi wako mataifa yote yalipotoshwa!”
The light of a lamp will never shine in yoʋ again. The voice of bridegroom and bride will never be heard in yoʋ again. For yoʋr merchants were the magnates of the earth, and all the nations were deceived by yoʋr sorcery.”
24 Mji huo uliadhibiwa kwani humo mlipatikana damu ya manabii, damu ya watu wa Mungu na damu ya watu wote waliouawa duniani.
And in her was found the blood of prophets and of saints, and of all who have been slain on the earth.

< Ufunuo 18 >