< Ufunuo 17 >
1 Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na bakuli akaja, akaniambia, “Njoo, mimi nitakuonyesha adhabu aliyopewa yule mzinzi mkuu, mji ule uliojengwa juu ya maji mengi.
七位拿著七個盂的天使中,有一位前來, 向我說道:「你來,我要指給你看,那在多水之旁為王的大淫婦受的懲罰;
2 Wafalme wa dunia wamefanya uzinzi pamoja naye; na wakazi wa dunia wamelewa divai ya uzinzi wake.”
世上的諸王都同她行過邪淫,地上的居民也都喝醉了她淫亂的酒。」
3 Kisha, Roho akanikumba, akaniongoza mpaka jangwani. Huko nikamwona mwanamke ameketi juu ya mnyama mwekundu. Mnyama huyo alikuwa ameandikwa kila mahali majina ya makufuru; alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.
於是天使叫我神魂超拔,提我到了曠野,我便看見了一個婦人,坐在一隻朱紅色且滿了褻瀆名號的獸身上,牠有七個頭,十隻角。
4 Mwanamke huyo alikuwa amevaa vazi la rangi ya zambarau na nyekundu; alikuwa amejipamba kwa dhahabu, mawe ya thamani na lulu. Mkononi mwake alishika kikombe cha dhahabu ambacho kilikuwa kimejaa machukizo na mambo machafu yanayoonyesha uzinzi wake.
這婦人身穿紫紅和朱紅色的衣服,全身點綴著金子、寶石和珍珠;她手裏拿著滿盛可憎之物和她淫污的金杯。
5 Alikuwa ameandikwa juu ya paji la uso wake jina la fumbo “Babuloni mkuu, mama wa wazinzi na wa mambo yote ya kuchukiza sana duniani.”
她的額上寫著一個含有奧秘的名字:「偉大的巴比倫!淫亂和地上可憎之物的母親。」
6 Nikamwona huyo mwanamke amelewa damu ya watu wa Mungu, na damu ya watu waliouawa kwa sababu ya kumtangaza Yesu. Nilipomwona nilishangaa mno.
我又看見這婦人痛飲了聖徒的血,和為耶穌殉道者的血; 我一看見她,遂大為驚奇。
7 Lakini malaika akaniambia, “Kwa nini unashangaa? Mimi nitakuambia maana iliyofichika ya mwanamke huyu na mnyama huyo amchukuaye ambaye ana vichwa saba na pembe kumi.
天使便對我說:「你為什麼驚奇?我要告訴你這婦人和馱著她,而有七個頭和十隻角的那獸的奧秘:
8 Huyo mnyama uliyemwona alikuwa hai hapo awali, lakini sasa amekufa. Hata hivyo, karibu sana atapanda kutoka shimoni kuzimu, lakini ataangamizwa. Wanaoishi duniani watashangaa; naam, watu wote ambao majina yao hayakupata kuandikwa katika kitabu cha uzima tangu mwanzo wa ulimwengu, watashangaa kumwona huyo mnyama ambaye hapo awali, aliishi, kisha akafa na sasa anatokea tena! (Abyssos )
你所看見的那獸, 先前在而今不在,可是牠又要從深淵中上來,自趨於喪亡;地上的居民,凡他們的名字從創世之初,沒有記錄在生命冊中的,看見那先前在,而今不在,將來又在的獸,都必要驚奇。 (Abyssos )
9 “Hapa panahitaji akili na hekima! Hivyo vichwa saba ni vilima saba, na huyo mwanamke anaketi juu yake. Vichwa hivyo pia ni wafalme saba.
這裏需要一個有智慧的明悟去理解:七個頭是指那婦人所坐的七座山,也是指七位君王;
10 Kati ya hao wafalme saba, watano wamekwisha angamia, mmoja anatawala bado, na yule mwingine bado hajafika; na atakapofika atabaki kwa muda mfupi.
五位已經倒了,一位仍在,另一位還沒有來到;當他來到時,必要存留片刻。
11 Huyo mnyama ambaye alikuwa anaishi hapo awali lakini sasa haishi tena ni mfalme wa nane, naye pia ni miongoni mwa hao saba, na anakwenda zake kuharibiwa.
至於那先前在而今不在的獸,是第八位,也屬於那七位中之一,牠要趨於喪亡。
12 “Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme ambao bado hawajaanza kutawala. Lakini watapewa mamlaka ya kutawala kwa muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.
你所看見的那十隻角,是指十個君王,他們還沒有領受王位,但必要同那獸一起得到權柄;他們當國王,只一個時辰。
13 Shabaha ya hawa kumi ni moja, na watampa yule mnyama nguvu na mamlaka yao yote.
他們的意見都一致:就是把自己的能力和權柄都交給那獸。
14 Watapigana na Mwanakondoo, lakini Mwanakondoo pamoja na wale aliowaita na kuwachagua, ambao ni waaminifu, atawashinda kwa sababu yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme.”
他們要同羔羊交戰,羔羊卻要戰勝他們,因為他是萬主之主,萬王之王,同他在一起的蒙召、被選和忠信的人,也必要獲勝。 」
15 Malaika akaniambia pia, “Yale maji uliyoyaona pale alipokaa yule mzinzi, ni mataifa, watu wa kila rangi na lugha.
天使又對我說:「你看見那淫婦所統治的水,是指諸民族、群眾、邦國和異語人民。
16 Pembe zile kumi ulizoziona na yule mnyama watamchukia huyo mzinzi. Watachukua kila kitu alicho nacho na kumwacha uchi; watakula nyama yake na kumteketeza kwa moto.
你看見的那十隻角和那獸,必要憎恨那淫婦,使她成為孤獨淒涼,赤身裸體的,並吞食她的肉,且用火焚燒她,
17 Maana Mungu ametia mioyoni mwao nia ya kutekeleza shabaha yake, yaani kwa kukubaliana wao kwa wao na kumpa huyo mnyama mamlaka yao ya kutawala, mpaka hapo neno la Mungu litakapotimia.
因為天主使牠們的心中有這意念,叫牠們實行天主的計劃,就是叫牠們一心,把牠們的王權交給那獸,直到天主的話完全應驗為止。
18 “Na yule mwanamke uliyemwona ndio ule mji mkuu unaowatawala wafalme wa dunia.”
你所看見的那婦人,是指那座對地上的諸王握有王權的大城。」