< Ufunuo 15 >

1 Kisha nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na ya kushangaza. Palikuwa hapo malaika saba wenye mabaa makubwa saba ya mwisho. Kwa mabaa hayo makubwa saba, ghadhabu ya Mungu imekamilishwa.
And I saw another sign in heaven, great and wonderful: seven angels that had seven plagues which are the last; for by them the wrath of God is brought to an end.
2 Kisha nikaona kitu kama bahari ya kioo, imechanganywa na moto. Nikawaona pia wale watu waliomshinda yule mnyama na sanamu yake na ambaye jina lake lilitajwa kwa ile tarakimu. Watu hao walikuwa wamesimama kando ya hiyo bahari ya kioo, wakiwa na vinubi walivyopewa na Mungu.
And I saw, as it were, a sea of glass mingled with fire, and those who had obtained the victory over the beast, and over his image, and over the number of his name, standing on the sea of glass, having the harps of God.
3 Walikuwa wakiimba wimbo wa Mose, mtumishi wa Mungu, na wimbo wa Mwanakondoo: “Bwana Mungu Mwenye Uwezo, matendo yako ni makuu mno! Ewe Mfalme wa mataifa, njia zako ni za haki na za kweli!
And they sung the song of Moses the servant of God, and the song of the Lamb, saying: Great and wonderful are thy works, Lord God Almighty; just and true are thy ways, thou King of saints.
4 Bwana, ni nani asiyekucha wewe? Nani asiyelitukuza jina lako? Wewe peke yako ni Mtakatifu. Mataifa yote yatakujia na kukuabudu maana matendo yako ya haki yameonekana na wote.”
Who will not fear thee, O Lord, and glorify thy name? For thou alone art holy; for all nations shall come and worship before thee: because thy judgments are made manifest.
5 Baada ya hayo nikaona Hekalu limefunguliwa mbinguni, na ndani yake hema ionyeshayo kuwapo kwa Mungu.
And after this I saw, and the temple of the tabernacle of the testimony in heaven was opened;
6 Basi, wale malaika saba wenye mabaa saba wakatoka humo Hekaluni, wakiwa wamevaa nguo za kitani safi zenye kung'aa, na kanda za dhahabu vifuani mwao.
and the seven angels that had the seven plagues came out of the temple, clothed in pure white linen, and girded about the breasts with golden girdles.
7 Kisha, mmojawapo wa vile viumbe vinne akawapa hao malaika saba mabakuli ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu, aishiye milele na milele. (aiōn g165)
And one of the four living creatures gave to the seven angels seven golden cups full of the wrath of God, who lives from age to age. (aiōn g165)
8 Hekalu likajaa moshi uliosababishwa na utukufu na nguvu ya Mungu, na hakuna mtu aliyeweza kuingia Hekaluni mpaka mwisho wa mabaa makubwa saba ya wale malaika saba.
And the temple was filled with smoke from the glory of God, and from his power; and no one was able to enter the temple, till the seven plagues of the seven angels were completed.

< Ufunuo 15 >