< Ufunuo 13 >
1 Na likajisimamia ukingoni mwa bahari. Kisha nikaona mnyama mmoja akitoka baharini. Alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na kila pembe ilikuwa na taji. Jina la kashfa lilikuwa limeandikwa juu ya vichwa hivyo.
於是牠就站在海灘上。 看見從海裏上來一隻獸,牠有十隻角和七個頭,角上有十個王冠,頭上有褻聖的名號。
2 Mnyama huyo niliyemwona alikuwa kama chui; miguu yake ilikuwa kama ya dubu, na kinywa chake kama cha simba. Lile joka likampa huyo mnyama nguvu yake, kiti chake cha enzi na uwezo mkuu.
我所看見的那獸,相似豹子,牠的腳像熊腳,牠的口像獅子口;那龍遂把自己的能力、寶座和大權交給了牠。
3 Kichwa kimojawapo cha huyo mnyama kilionekana kama kilikwisha jeruhiwa vibaya sana, lakini jeraha hilo lilikuwa limepona. Dunia nzima ilishangazwa na huyo mnyama na kumfuata.
我看見那獸的頭中,有一個似乎受了致死的傷,但牠那致死的傷卻治好了;故此全地的人都驚奇,而跟隨了那獸。
4 Watu wote wakaliabudu lile joka kwa sababu lilimpa huyo mnyama uwezo wake. Wakamwabudu pia huyo mnyama wakisema, “Nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana naye?”
世人遂都朝拜那龍,因為牠把權柄賜給了那獸;世人朝拜那獸說:「誰可與這獸相比?誰能和牠交戰?」
5 Kisha huyo mnyama akaruhusiwa kusema maneno ya kujigamba na kumkufuru Mungu; akaruhusiwa kuwa na mamlaka kwa muda wa miezi arobaini na miwili.
又賜給了那獸一張說大話和褻聖的口,並且賜給了牠可妄為四十二個月的權柄;
6 Basi, akaanza kumtukana Mungu, kulitukana jina lake, makao yake, na wote wakaao mbinguni.
牠便張開自己的口,向天主說褻瀆的話,褻瀆他的聖名、他的帳幕和那些居住在天上的人。
7 Aliruhusiwa kuwapiga vita na kuwashinda watu wa Mungu. Alipewa mamlaka juu ya watu wa kila kabila, ukoo, lugha na taifa.
又允許牠可與聖徒們交戰,且戰勝他們;又賜給牠制服各支派、各民族、各異語和各邦國的權柄。
8 Wote waishio duniani watamwabudu isipokuwa tu wale ambao majina yao yameandikwa tangu mwanzo wa ulimwengu katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo aliyechinjwa.
地上的居民,凡名字從創造之初沒有記錄在被宰殺的羔羊生命冊中的人,都要朝拜牠。
9 “Aliye na masikio, na asikie!
誰若有耳朵,就聽罷!
10 Waliokusudiwa kuchukuliwa mateka lazima watatekwa; waliokusudiwa kuuawa kwa upanga lazima watauawa kwa upanga. Kutokana na hayo ni lazima watu wa Mungu wawe na uvumilivu na imani.”
誰若該被俘擄,就去受俘擄;誰若該受刀殺,就去受刀殺:聖徒們的堅忍和忠信即在於此。
11 Kisha nikamwona mnyama mwingine anatoka ardhini. Alikuwa na pembe mbili kama pembe za kondoo, na aliongea kama joka.
以後我看見另一隻獸由地中上來,牠有兩隻相似羔羊的角,說話卻相似龍。
12 Alikuwa na mamlaka kamili kutoka kwa yule mnyama wa kwanza, na akautumia uwezo huo mbele ya huyo mnyama. Akailazimisha dunia yote na wote waliomo humo kumwabudu huyo mnyama wa kwanza ambaye alikuwa na jeraha la kifo lililokuwa limepona.
牠在那前一隻獸面前,施行前一隻獸所有的一切權柄,使大地和居住在地上的人,朝拜前一隻獸,就是那隻受過致死的傷而被治好的獸。
13 Basi, huyu mnyama wa pili akafanya miujiza mikubwa hata akasababisha moto kutoka mbinguni ushuke duniani mbele ya watu.
牠又行大奇蹟,甚至在眾人面前使火從天降到地上。
14 Aliwapotosha wakazi wa dunia kwa miujiza hiyo aliyojaliwa kutenda mbele ya mnyama wa kwanza. Aliwaambia wakazi wa dunia watengeneze sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi tena.
牠因著在那獸面前所行的那些奇蹟,迷惑了地上的居民,便勸告地上的居民,給那那受過刀傷而還活著的獸,立一個像。
15 Kisha alijaliwa kuipulizia uhai hiyo sanamu ya yule mnyama wa kwanza, hata ikaweza kuongea na kuwaua watu wote ambao hawakuiabudu.
牠又得了能力,把生氣賦給那獸像,甚至叫那獸像說話,並使那些凡不朝拜獸像的人死亡。
16 Aliwalazimisha wote, wadogo na wakubwa, matajiri na maskini, watu huru na watumwa, watiwe alama juu ya mikono yao ya kulia au juu ya paji za nyuso zao.
牠給所有的人,無論大小貧富,自主的和為奴的,都在他們的右手上,或在他們的額上,打了一個印號;
17 Akapiga marufuku mtu yeyote kununua au kuuza kitu isipokuwa tu mtu aliyetiwa alama hiyo, yaani jina la yule mnyama au tarakimu ya jina hilo.
如此,除非有這印號的,就是有那獸的名字或牠名字的數字的,誰也不能買,誰也不能賣。
18 Hapa ni lazima kutumia ujasiri! Mwenye akili anaweza kufafanua maana ya tarakimu ya mnyama huyo, maana ni tarakimu yenye maana ya mtu fulani. Tarakimu hiyo ni mia sita sitini na sita.
在這裏應有智慧:凡有明悟的,就讓他計算一下那獸的數字,因為是人的數字,牠的數字是六百六十六。