< Ufunuo 11 >

1 Kisha nikapewa mwanzi uliokuwa kama kijiti cha kupimia, nikaambiwa, “Inuka, ukalipime Hekalu la Mungu, madhabahu ya kufukizia ubani, na ukawahesabu watu wanaoabudu ndani ya Hekalu.
I was given a reed like a measuring rod. And the angel stood saying: “Rise and measure the temple of God and the altar, and those who worship there.
2 Lakini uache ukumbi ulio nje ya Hekalu; usiupime, maana huo umekabidhiwa watu wa mataifa mengine, ambao wataukanyanga mji Mtakatifu kwa muda wa miezi arobaini na miwili.
But leave out the outer court of the temple and do not measure it, because it has been given to the nations; and they will trample the holy city for forty-two months.
3 Nami nitawatuma mashahidi wangu wawili ili watangaze ujumbe wa Mungu kwa muda huo wa siku elfu moja mia mbili na sitini wakiwa wamevaa mavazi ya magunia.”
And I will give authority to my two witnesses, and they will prophesy one thousand two hundred and sixty days, clothed in sackcloth.”
4 Hao mashahidi wawili ni miti miwili ya Mizeituni na taa mbili zinazosimama mbele ya Bwana wa dunia.
These are the two olive trees, even the two lampstands that stand before the Lord of the earth.
5 Kama mtu akijaribu kuwadhuru, moto hutoka kinywani mwao na kuwaangamiza adui zao; na kila mtu atakayejaribu kuwadhuru atakufa namna hiyo.
And if anyone wants to harm them fire comes out of their mouths and consumes their enemies. So if anyone wants to harm them he must be killed in this way.
6 Hao wanayo mamlaka ya kufunga anga, mvua isinyeshe wakati wanapotangaza ujumbe wa Mungu. Tena wanayo mamlaka ya kuzigeuza chemchemi zote za maji ziwe damu, na ya kusababisha maafa ya kila namna duniani kila mara wapendavyo.
They have authority to shut up the sky so that no rain falls during the days of their prophecy; and they have authority over the waters to turn them into blood, and to strike the earth with every plague, as often as they wish.
7 Lakini wakisha maliza kutangaza ujumbe huo, mnyama atokaye shimoni kuzimu atapigana nao, atawashinda na kuwaua. (Abyssos g12)
When they finish their witness, the Beast of prey that comes up out of the Abyss will make war with them, overcome them and kill them (Abyssos g12)
8 Maiti zao zitabaki katika barabara za mji mkuu ambapo Bwana wao alisulubiwa; jina la kupanga la mji huo ni Sodoma au Misri.
—and leave their corpses in the street of the great city! (which is called Sodom and Egypt, spiritually speaking), even where their Lord was crucified.
9 Watu wa kila kabila, lugha, taifa na rangi wataziangalia maiti hizo kwa muda wa siku tatu na nusu, na hawataruhusu zizikwe.
And those from the peoples, tribes, languages and ethnic nations look at their corpses three and a half days, and will not allow their corpses to be buried.
10 Watu waishio duniani watafurahia kifo cha hao wawili. Watafanya sherehe na kupelekeana zawadi maana manabii hawa wawili walikuwa wamewasumbua mno watu wa dunia.
And those who dwell on the earth rejoice over them, and they will enjoy themselves and send gifts to one another, because these two prophets tormented those who dwell on the earth.
11 Lakini baada ya zile siku tatu na nusu pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu iliwaingia, nao wakasimama; wote waliowaona wakaingiwa na hofu kuu.
And after three and a half days a breath of life from God entered them and they stood on their feet, and a great fear fell on those who were watching them.
12 Kisha hao manabii wawili wakasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikiwaambia, “Njoni hapa juu!” Nao wakapanda juu mbinguni katika wingu, maadui wao wakiwa wanawatazama.
And I heard a loud voice from the heaven saying to them, “Come up here!” And they went up to heaven in a cloud, and their enemies watched them.
13 Wakati huohuo, kukatokea tetemeko kubwa la ardhi, sehemu moja ya kumi ya ardhi ikaharibiwa. Watu elfu saba wakauawa kwa tetemeko hilo la ardhi. Watu waliosalia wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.
And in that day there was a severe earthquake and a tenth of the city fell, and seven thousand individuals were killed in the earthquake. And the rest became fearful and gave glory to the God of heaven.)
14 Maafa ya pili yamepita; lakini tazama! Maafa ya tatu yanafuata hima.
The second woe is past. Look out, here comes the third woe!
15 Kisha malaika wa saba akapiga tarumbeta yake. Na sauti kuu zikasikika mbinguni zikisema, “Sasa utawala juu ya ulimwengu ni wa Bwana wetu na Kristo wake. Naye atatawala milele na milele!” (aiōn g165)
So the seventh angel trumpeted, and there were loud voices in heaven saying: “The kingdom of the world has become the kingdom of our Lord and of His Christ, and He shall reign forever and ever!” (aiōn g165)
16 Kisha wale wazee ishirini na wanne walioketi mbele ya Mungu katika viti vyao vya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu,
And the twenty-four elders, who sit on their thrones in God's presence, fell on their faces and worshiped God
17 wakisema: “Bwana Mungu Mwenye uwezo, uliyeko na uliyekuwako! Tunakushukuru, maana umetumia nguvu yako kuu ukaanza kutawala!
saying: “We thank You, O Lord God Almighty, He who is and who was and who is coming, because You have taken up your great power and begun to reign.
18 Watu wa mataifa waliwaka hasira, maana wakati wa ghadhabu yako umefika, wakati wa kuwahukumu wafu. Ndio wakati wa kuwatuza watumishi wako manabii, watu wako na wote wanaolitukuza jina lako, wakubwa kwa wadogo. Ni wakati wa kuwaangamiza wale wanaoangamiza dunia.”
The nations were angry and your wrath came, even the time for the dead to be judged and to give the reward to Your slaves the prophets, and to the saints and those who fear your name, small and great, and to destroy those who have corrupted the earth.”
19 Hekalu la Mungu mbinguni likafunguliwa, na Sanduku la Agano lake likaonekana Hekaluni mwake. Kisha kukatokea umeme, sauti, ngurumo, tetemeko la ardhi, na mvua kubwa ya mawe.
And the temple of God in heaven was opened, and the ark of the covenant of the Lord was seen in His temple. And there were lightnings, noises, thunderings and huge hail.

< Ufunuo 11 >