< Mathayo 5 >
1 Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda mlimani, akaketi. Wanafunzi wake wakamwendea,
耶穌一見群眾,就上了山,坐下;他的門徒上他跟前來,
2 naye akaanza kuwafundisha:
他遂開口教訓他們說:
3 “Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
神貧的人是有福的,因為天國是他們的。
4 Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.
哀慟的人是有福的,因為他們要受安慰。
5 Heri walio wapole, maana watairithi nchi.
溫良的人是有福的,因為他們要承受土地。
6 Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.
飢渴慕義的人是有福的,因為他們要得飽飫。
7 Heri walio na huruma, maana watahurumiwa.
憐憫人的人是有福的,因為他們要受憐憫。
8 Heri wenye moyo safi, maana watamwona Mungu.
心裏潔淨的人是有福的,因為他們要看見天主。
9 Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu.
締造和平的人是有福的,因為他們要稱為天主的子女。
10 Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
為義而受迫害的是有福的,因為天國是他們的。
11 “Heri yenu ninyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu.
幾時人為了我而辱罵迫害你們,你們是有福的,捏造一切壞話毀謗你們,你們是有福的。
12 Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Hivyo ndivyo walivyowadhulumu manabii waliokuwako kabla yenu.
你們歡喜踴躍罷!因為你們在天上的賞報是豐富的,因為在你們以的先知,人也曾這樣迫害過他們。
13 “Ninyi ni chumvi ya dunia! Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
你們是地上的鹽,鹽若失了味,可用什麼使它再鹹呢﹖它再毫無用途,只好拋在外邊,任人踐踏罷了。
14 “Ninyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika.
你們是世界的光,建在山上的城是不能隱藏的。
15 Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa chungu, ila huiweka juu ya kinara ili iwaangazie wote waliomo nyumbani.
人點燈,並不是於在斗底下,而是於在燈台上,照耀屋人所有的人。
16 Vivyo hivyo, ni lazima mwanga wenu uangaze mbele ya watu, ili wayaone matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.”
照樣,你們的光也當在人前照耀,好使他們看見你們的善行,光耀你們在天之父。
17 “Msidhani ya kuwa nimekuja kutangua Sheria ya Mose na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha.
你們不要以為我來是廢除法律或先知;我來不為廢除,而是為成全。
18 Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya Sheria itakayoondolewa, mpaka yote yametimia.
我實在告訴你們:既使天地過去了,一撇或一劃也決不會從法律上過,必待一切完成。
19 Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika Ufalme wa mbiguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine, huyo atakuwa mkubwa katika Ufalme wa mbinguni.
所以,誰若廢除這些誡命中最小的一條,也這樣教訓人,在天國裏他將稱為最小的;但誰若實行,也這樣教訓人,這人在天國裏將稱為大的。
20 Ndiyo maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa Mafarisayo na walimu wa Sheria, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni.
我告訴你們:除非你們的義德超過經師和法利賽人的義德,你們決進不了天國。
21 “Mmekwisha sikia ya kuwa watu wa kale waliambiwa: Usiue! Atakayeua lazima ahukumiwe.
你們一向聽過給古人說:『不可殺人!』誰吝殺了人,應受裁判。
22 Lakini mimi nawaambieni, yeyote anayemkasirikia ndugu yake, lazima ahukumiwe. Anayemdharau ndugu yake atapelekwa mahakamani. Anayemwita ndugu yake: Pumbavu atastahili kuingia katika moto wa Jehanamu. (Geenna )
我卻對你們說:凡向自己弟兄發怒的,就要受裁判,誰若向自己的弟兄說「傻子」,就要受議會的裁判;誰若說「瘋子」就要受火獄的罰。 (Geenna )
23 Basi, ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka kwamba ndugu yako ana ugomvi nawe,
所以,你們若在祭壇前,要獻你們的禮物時,在那裏想起你們的弟兄有什麼怨你的事,
24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, nenda kwanza ukapatane na ndugu yako, ndipo urudi ukatoe sadaka yako.
就把你們的禮物留在那裏,留在祭壇前,先去和你們的弟兄和好,然後再來獻你的禮物。
25 “Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani, kwenda mahakamani. La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa askari, nawe utafungwa gerezani.
當你和你的對頭還在路上,趕快與他和解,免得對頭把你交給判官,判官交給差役,把你投在獄裏。
26 Kweli nakwambia, hutatoka humo mpaka umemaliza kulipa senti ya mwisho.
我實在告訴你。非到你還了最後的一文,決不能從那裏出來。
27 “Mmesikia ya kuwa watu waliambiwa: Usizini!
你們一向聽說過:不可奸淫!』
28 Lakini mimi nawaambieni, atakayemtazama mwanamke kwa kumtamani, amekwisha zini naye moyoni mwake.
我卻對你們說:凡注視婦女,有意貪戀她的,他已在心裏奸淫了她。
29 Basi, kama jicho lako la kulia linakukosesha, ling'oe ukalitupe mbali. Afadhali zaidi kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako, kuliko mwili wako wote kutupwa katika moto wa Jehanamu. (Geenna )
若是你的右眼使你跌倒,剜出它來,從你身上扔掉,因為喪失你一個肢體,比你全身投入地獄裏,為你更好; (Geenna )
30 Na kama mkono wako wa kulia unakukosesha, ukate ukautupe mbali. Afadhali zaidi kupoteza kiungo kimoja cha mwili, kuliko mwili wako wote uende katika moto wa Jehanamu. (Geenna )
若你的右手手使你跌倒,砍下它來,從你身上扔掉,因為喪失你一個肢體,比你全身投入地獄裏為你更好。 (Geenna )
31 “Ilikwisha semwa pia: Anayemwacha mke wake, yampasa ampe hati ya talaka.
又說過『誰若休妻,就該給她休書。』
32 Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mtu akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.
我卻對你們說:除了姘居外,凡休自已的妻子的,便是叫她受奸污;並且誰若娶被休的婦人,就是犯奸淫。
33 “Tena mmesikia kuwa watu wa kale waliambiwa: Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.
你們又一向聽過對古人說:『不可發虛誓,要向上主償還你的誓願!』
34 Lakini mimi nawaambieni, msiape kamwe; wala kwa mbingu, maana ni kiti cha enzi cha Mungu;
我卻對你們說:你們總不可發誓:不可指天,因為天是天主的寶座;
35 wala kwa dunia, maana ni kiti chake cha kuwekea miguu; wala kwa Yerusalemu, maana ni mji wa Mfalme mkuu.
不可指地,地是他的腳凳,不可指耶路撒冷,因它是大王的城市;
36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
也不可指你的頭發誓,因為你不能使一根頭髮變白或變黑。
37 Ukisema, Ndiyo, basi iwe Ndiyo; ukisema Siyo, basi iwe kweli Siyo. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu.
你們的話當是:是就說是,非就說非;其他多餘的便是出於邪惡。
38 “Mmesikia kwamba ilisemwa: Jicho kwa jicho, jino kwa jino.
你們一向聽說過:『以眼還眼,以牙還牙。』
39 Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia shavu la pili.
我卻對你們說:不要抵抗惡人:而且,若有人掌擊你的右頰,你把另一面也轉給他。
40 Mtu akikupeleka mahakamani kutaka kukuchukulia shati lako, mwache achukue pia koti lako.
那願與你爭訟,拿你的內衣的,你連外衣也讓給他。
41 Mtu akikulazimisha kubeba mzigo wake kilomita moja, ubebe kilomita mbili.
若有人強迫你走一千步,你就同他走兩千步。
42 Akuombaye mpe, na mtu akitaka kukukopa kitu usimnyime.
求你的,就給他;願向你借貸的,你不要拒絕。
43 “Mmesikia kwamba ilisemwa: Mpende jirani yako na kumchukia adui yako.
你們一向聽說過:『你應愛你的近人,恨你的仇人!』
44 Lakini mimi nawaambieni, wapendeni adui zenu na kuwaombea wale wanaowadhulumu ninyi
我卻對你們說:你們當愛你們的仇人,當為迫害你們的人祈禱,
45 ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu wabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watu wanyofu na waovu.
好使你們成為你們在天之父的子女,因為衪使太陽上升,光照惡人,也光照善人;降雨給義,也給不義的人。
46 Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda ninyi? Hakuna! Kwa maana hata watoza ushuru hufanya hivyo!
你們若只愛那愛你們的人,你們還有什麼賞報呢? 稅吏不是也這樣做嗎﹖
47 Kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mmefanya kitu kisicho cha kawaida? Hata watu wasiomjua Mungu nao hufanya vivyo hivyo.
你們若只問候你們的弟兄,你們做了什麼特別的呢? 外邦人不是也這樣做嗎﹖
48 Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
所以你們應當是成全的,如同你們的父是成全的一樣。