< Mathayo 28 >

1 Baada ya Sabato, karibu na mapambazuko ya siku ile ya Jumapili, Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikwenda kutazama lile kaburi.
Now after the Sabbath, at the dawning of the first day of the week, Mary Magdalene, and the other Mary, came to see the tomb.
2 Ghafla kutatokea tetemeko kubwa la nchi; malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akalivingirisha lile jiwe, akalikalia.
Now then, a big earthquake had occurred, because an angel of the Lord, descending out of heaven, had come and rolled back the stone from the door, and sat on it!
3 Alionekana kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji.
And his appearance was like lightning and his clothing as white as snow.
4 Walinzi wa lile kaburi wakatetemeka kwa hofu kubwa, hata wakawa kama wamekufa.
So the guards were shaken for fear of him, and became like dead men.
5 Lakini yule malaika akawaambia wale wanawake, “Ninyi msiogope! Najua kwamba mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa.
Now the angel spoke up and said to the women: “Do not be afraid! I know that you are looking for the Jesus who was crucified.
6 Hayupo hapa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni mkaone mahali alipokuwa amelala.
He is not here, because He is risen, just like He said! Come, see the place where the Lord was lying.
7 Basi, nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake kwamba amefufuka kutoka wafu, na sasa anawatangulieni kule Galilaya; huko mtamwona. Haya, mimi nimekwisha waambieni.”
Now go quickly and tell His disciples that He is risen from the dead; and get this, He is going before you into Galilee; there you will see Him. There, I have told you!”
8 Wakiwa wenye hofu na furaha kubwa, hao wanawake walitoka upesi kaburini, wakakimbia kwenda kuwaambia wanafunzi wake.
So they went out quickly from the tomb with fear and great joy, and ran to report to His disciples.
9 Mara, Yesu akakutana nao, akawasalimu: “Salamu.” Hao wanawake wakamwendea, wakapiga magoti mbele yake, wakashika miguu yake.
But as they were going to report to His disciples, wow, Jesus met them saying, “Rejoice!” So approaching, they held His feet and worshiped Him.
10 Kisha Yesu akawaambia, “Msiogope! Nendeni mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, na huko wataniona.”
Then Jesus says to them: “Do not be afraid! Go report to my brothers that they must go to Galilee, and there they will see me.”
11 Wale wanawake walipokuwa wanakwenda zao, baadhi ya walinzi wa lile kaburi walikwenda mjini kutoa taarifa kwa makuhani wakuu juu ya mambo yote yaliyotukia.
Now while they were going, get this, some of the guard went into the city and reported to the chief priests all that had happened.
12 Basi, wakakutana pamoja na wazee, na baada ya kushauriana, wakawapa wale askari kiasi kikubwa cha fedha
When they had met with the elders and consulted together, they gave plenty of money to the soldiers
13 wakisema, “Ninyi mtasema hivi: Wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba sisi tukiwa tumelala.
saying: “Say that his disciples came at night and stole him while you were sleeping.
14 Na kama mkuu wa mkoa akijua jambo hili, sisi tutasema naye na kuhakikisha kuwa ninyi hamtapata matatizo.”
And should this get to the governor, we will persuade him and make you safe.”
15 Wale walinzi wakazichukua zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Habari hiyo imeenea kati ya Wayahudi mpaka leo.
So taking the money they did as they were instructed. Their tale is widely spread among the Jews until this day.
16 Wale wanafunzi kumi na mmoja walikwenda Galilaya kwenye ule mlima aliowaagiza Yesu.
The eleven disciples went into Galilee to the mountain that Jesus had indicated to them.
17 Walipomwona, wakamwabudu, ingawa wengine walikuwa na mashaka.
When they saw Him they worshiped Him; but some doubted.
18 Yesu akaja karibu, akawaambia, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
And approaching Jesus asserted to them saying: “All authority in heaven and on earth has been given to me.
19 Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu; mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.
As you go, make disciples in all ethnic nations: baptizing them in the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit;
20 Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati.” (aiōn g165)
teaching them to obey everything that I commanded you; and take note, I am with you every day, until the end of the age!” Amen. (aiōn g165)

< Mathayo 28 >