< Mathayo 27 >

1 Kulipopambazuka, makuhani wakuu wote na wazee wa watu walifanya mashauri juu ya Yesu wapate kumwua.
When morning came, all the chief priests and elders of the people conspired against Jesus to put Him to death.
2 Wakamfunga pingu, wakamchukua, wakamkabidhi kwa Pilato, mkuu wa mkoa.
They bound Him, led Him away, and handed Him over to Pilate the governor.
3 Hapo, Yuda ambaye ndiye aliyemsaliti, alipoona kwamba wamekwisha mhukumu Yesu, akajuta, akawarudishia makuhani wakuu zile sarafu thelathini za fedha.
When Judas, who had betrayed Him, saw that Jesus was condemned, he was filled with remorse and returned the thirty pieces of silver to the chief priests and elders.
4 Akawaambia, “Nimekosa kwa kumtoa mtu asiye na hatia auawe.” Lakini wao wakasema, “Yatuhusu nini sisi? Hilo ni shauri lako.”
“I have sinned by betraying innocent blood,” he said. “What is that to us?” they replied. “You bear the responsibility.”
5 Naye akazitupa zile fedha Hekaluni, akatoka nje, akaenda akajinyonga.
So Judas threw the silver into the temple and left. Then he went away and hanged himself.
6 Makuhani wakuu wakazichukua zile fedha, wakasema, “Haifai kuziweka katika hazina ya Hekalu kwa maana ni fedha za damu.”
The chief priests picked up the pieces of silver and said, “It is unlawful to put this into the treasury, since it is blood money.”
7 Basi, wakashauriana, wakazitumia kununua shamba la mfinyanzi liwe mahali pa kuzika wageni.
After conferring together, they used the money to buy the potter’s field as a burial place for foreigners.
8 Ndiyo maana mpaka leo shamba hilo linaitwa Shamba la Damu.
That is why it has been called the Field of Blood to this day.
9 Hivyo maneno ya nabii Yeremia yakatimia: “Walizichukua sarafu thelathini za fedha, thamani ya yule ambaye watu wa Israeli walipanga bei,
Then what was spoken through Jeremiah the prophet was fulfilled: “They took the thirty pieces of silver, the price set on Him by the people of Israel,
10 wakanunua nazo shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyoniagiza.”
and they gave them for the potter’s field, as the Lord had commanded me.”
11 Yesu alisimamishwa mbele ya mkuu wa mkoa. Basi, mkuu wa mkoa akamwuliza, “Je, wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akamwambia, “Wewe umesema.”
Meanwhile Jesus stood before the governor, who questioned Him: “Are You the King of the Jews?” “You have said so,” Jesus replied.
12 Lakini makuhani wakuu na wazee walipokuwa wanamshtaki, hakujibu neno.
And when He was accused by the chief priests and elders, He gave no answer.
13 Hivyo Pilato akamwuliza, “Je, husikii mashtaka hayo yote wanayotoa juu yako?”
Then Pilate asked Him, “Do You not hear how many charges they are bringing against You?”
14 Lakini Yesu hakumjibu hata neno moja; hata huyo mkuu wa mkoa akashangaa sana.
But Jesus gave no answer, not even to a single charge, much to the governor’s amazement.
15 Ilikuwa kawaida wakati wa Sikukuu ya Pasaka mkuu wa mkoa kuwafungulia Wayahudi mfungwa mmoja waliyemtaka.
Now it was the governor’s custom at the feast to release to the crowd a prisoner of their choosing.
16 Wakati huo kulikuwa na mfungwa mmoja, jina lake Baraba.
At that time they were holding a notorious prisoner named Barabbas.
17 Hivyo, watu walipokusanyika pamoja, Pilato akawauliza, “Mwataka nimfungue yupi kati ya wawili hawa, Baraba ama Yesu aitwae Kristo?”
So when the crowd had assembled, Pilate asked them, “Which one do you want me to release to you: Barabbas, or Jesus who is called Christ?”
18 Alisema hivyo maana alijua wazi kwamba walimleta kwake kwa sababu ya wivu.
For he knew it was out of envy that they had handed Jesus over to him.
19 Pilato alipokuwa amekaa katika kiti cha hukumu, mke wake akampelekea ujumbe: “Usijitie katika shauri la mtu huyu mwema, maana leo nimeteseka sana katika ndoto kwa sababu yake.”
While Pilate was sitting on the judgment seat, his wife sent him this message: “Have nothing to do with that innocent man, for I have suffered terribly in a dream today because of Him.”
20 Lakini makuhani wakuu na wazee wakawashawishi watu waombe Baraba afunguliwe na Yesu auawe.
But the chief priests and elders persuaded the crowds to ask for Barabbas and to have Jesus put to death.
21 Mkuu wa mkoa akawauliza, “Ni yupi kati ya hawa wawili mnayetaka nimfungue?” Wakamjibu, “Baraba!”
“Which of the two do you want me to release to you?” asked the governor. “Barabbas,” they replied.
22 Pilato akawauliza, “Sasa, nifanye nini na Yesu aitwaye Kristo?” Wote wakasema, “Asulubiwe!”
“What then should I do with Jesus who is called Christ?” Pilate asked. They all answered, “Crucify Him!”
23 Pilato akauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Wao wakazidi kupaaza sauti: “Asulubiwe!”
“Why?” asked Pilate. “What evil has He done?” But they shouted all the louder, “Crucify Him!”
24 Basi, Pilato alipotambua kwamba hafanikiwi chochote na kwamba maasi yalikuwa yanaanza, alichukua maji, akanawa mikono mbele ya ule umati wa watu, akasema, “Mimi sina lawama juu ya kifo cha mtu huyu; shauri lenu wenyewe.”
When Pilate saw that he was accomplishing nothing, but that instead a riot was breaking out, he took water and washed his hands before the crowd. “I am innocent of this man’s blood,” he said. “You bear the responsibility.”
25 Watu wote wakasema, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!”
All the people answered, “His blood be on us and on our children!”
26 Hapo Pilato akawafungulia Baraba kutoka gerezani, lakini akamtoa Yesu asulubiwe.
So Pilate released Barabbas to them. But he had Jesus flogged, and handed Him over to be crucified.
27 Kisha askari wa mkuu wa mkoa wakamwingiza Yesu ndani ya ikulu, wakamkusanyikia kikosi kizima.
Then the governor’s soldiers took Jesus into the Praetorium and gathered the whole company around Him.
28 Wakamvua nguo zake, wakamvika joho la rangi nyekundu.
They stripped Him and put a scarlet robe on Him.
29 Kisha wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani, wakamwekea pia mwanzi katika mkono wake wa kulia. Wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki wakisema, “Shikamoo mfalme wa Wayahudi!”
And they twisted together a crown of thorns and set it on His head. They put a staff in His right hand and knelt down before Him to mock Him, saying, “Hail, King of the Jews!”
30 Wakamtemea mate, wakauchukua ule mwanzi, wakampiga nao kichwani.
Then they spit on Him and took the staff and struck Him on the head repeatedly.
31 Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.
After they had mocked Him, they removed the robe and put His own clothes back on Him. Then they led Him away to crucify Him.
32 Walipokuwa wakienda, wakamkuta mtu mmoja jina lake Simoni, mwenyeji wa Kurene, wakamlazimisha kuuchukua msalaba wake Yesu.
Along the way they found a man from Cyrene, named Simon, and they forced him to carry the cross of Jesus.
33 Walipofika mahali paitwapo Golgotha, maana yake, “Mahali pa Fuvu la kichwa,”
And when they came to a place called Golgotha, which means The Place of the Skull,
34 wakampa mchanganyiko wa divai na nyongo. Lakini Yesu alipoonja akakataa kunywa.
they offered Him wine to drink, mixed with gall; but after tasting it, He refused to drink it.
35 Walimsulubisha, kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
When they had crucified Him, they divided up His garments by casting lots.
36 Wakaketi, wakawa wanamchunga.
And sitting down, they kept watch over Him there.
37 Juu ya kichwa chake wakaweka shtaka dhidi yake lilioandikwa, “Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi.”
Above His head they posted the written charge against Him: THIS IS JESUS, THE KING OF THE JEWS.
38 Wanyang'anyi wawili walisulubishwa pia pamoja naye, mmoja upande wa kushoto na mwingine upande wa kulia.
Two robbers were crucified with Him, one on His right hand and the other on His left.
39 Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana wakitikisa vichwa vyao na kusema,
And those who passed by heaped abuse on Him, shaking their heads
40 “Wewe! Si ulijidai kulivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu? Sasa jiokoe mwenyewe. Kama wewe ni Mwana wa Mungu, basi shuka msalabani!”
and saying, “You who are going to destroy the temple and rebuild it in three days, save Yourself! If You are the Son of God, come down from the cross!”
41 Hali kadhalika na makuhani wakuu pamoja na walimu wa Sheria na wazee walimdhihaki wakisema,
In the same way, the chief priests, scribes, and elders mocked Him, saying,
42 “Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi! Eti yeye ni mfalme wa Wayahudi! Basi, sasa na ashuke msalabani, nasi tutamwamini.
“He saved others, but He cannot save Himself. He is the King of Israel! Let Him come down now from the cross, and we will believe in Him.
43 Alimtumainia Mungu na kusema eti yeye ni Mwana wa Mungu; basi, Mungu na amwokoe kama anamtaka.”
He trusts in God. Let God deliver Him now if He wants Him. For He said, ‘I am the Son of God.’”
44 Hali kadhalika na wale waliosulubiwa pamoja naye wakamtukana.
In the same way, even the robbers who were crucified with Him berated Him.
45 Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi yote ikawa katika giza.
From the sixth hour until the ninth hour darkness came over all the land.
46 Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kubwa, “Eli, Eli, lema sabakthani?” Maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”
About the ninth hour Jesus cried out in a loud voice, “Eli, Eli, lema sabachthani?” which means, “My God, My God, why have You forsaken Me?”
47 Lakini wale waliosimama pale waliposikia hivyo wakasema, “Anamwita Eliya.”
When some of those standing there heard this, they said, “He is calling Elijah.”
48 Mmoja wao akakimbia, akachukua sifongo, akaichovya katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe.
One of them quickly ran and brought a sponge. He filled it with sour wine, put it on a reed, and held it up for Jesus to drink.
49 Wengine wakasema, “Acha tuone kama Eliya anakuja kumwokoa.”
But the others said, “Leave Him alone. Let us see if Elijah comes to save Him.”
50 Basi, Yesu akalia tena kwa sauti kubwa, akakata roho.
When Jesus had cried out again in a loud voice, He yielded up His spirit.
51 Hapo pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili, toka juu mpaka chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
At that moment the veil of the temple was torn in two from top to bottom. The earth quaked and the rocks were split.
52 makaburi yakafunguka na watu wengi wa Mungu waliokufa wakafufuliwa;
The tombs broke open, and the bodies of many saints who had fallen asleep were raised.
53 nao, baada ya kufufuka kwake, wakatoka makaburini, wakaingia katika Mji Mtakatifu, wakaonekana na watu wengi.
After Jesus’ resurrection, when they had come out of the tombs, they entered the holy city and appeared to many people.
54 Basi, jemadari na wale waliokuwa wakimlinda Yesu walipoona tetemeko la ardhi na yale mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”
When the centurion and those with him who were guarding Jesus saw the earthquake and all that had happened, they were terrified and said, “Truly this was the Son of God.”
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia.
And many women were there, watching from a distance. They had followed Jesus from Galilee to minister to Him.
56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo.
Among them were Mary Magdalene, Mary the mother of James and Joseph, and the mother of Zebedee’s sons.
57 Ilipokuwa jioni, akaja mtu mmoja tajiri mwenyeji wa Armathaya, jina lake Yosefu. Yeye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu.
When it was evening, there came a rich man from Arimathea named Joseph, who himself was a disciple of Jesus.
58 Akamwendea Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu. Basi, Pilato akaamuru apewe.
He went to Pilate to ask for the body of Jesus, and Pilate ordered that it be given to him.
59 Yosefu akauchukua ule mwili akauzungushia sanda safi ya kitani,
So Joseph took the body, wrapped it in a clean linen cloth,
60 akauweka ndani ya kaburi lake jipya alilokuwa amelichonga katika mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.
and placed it in his own new tomb that he had cut into the rock. Then he rolled a great stone across the entrance to the tomb and went away.
61 Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikuwa wameketi kulielekea kaburi.
Mary Magdalene and the other Mary were sitting there opposite the tomb.
62 Kesho yake, yaani siku iliyofuata ile ya Maandalio, makuhani wakuu na Mafarisayo walimwendea Pilato,
The next day, the one after Preparation Day, the chief priests and Pharisees assembled before Pilate.
63 Wakasema, “Mheshimiwa, tunakumbuka kwamba yule mdanganyifu alisema kabla ya kufa ati, Baada ya siku tatu nitafufuka.
“Sir,” they said, “we remember that while He was alive that deceiver said, ‘After three days I will rise again.’
64 Kwa hiyo amuru kaburi lilindwe mpaka siku ya tatu ili wanafunzi wake wasije wakamwiba na kuwaambia watu kwamba amefufuka. Uongo huu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa awali.”
So give the order that the tomb be secured until the third day. Otherwise, His disciples may come and steal Him away and tell the people He has risen from the dead. And this last deception would be worse than the first.”
65 Pilato akawaambia, “Haya, mnao walinzi; nendeni mkalinde kadiri mjuavyo.”
“You have a guard,” Pilate said. “Go, make the tomb as secure as you know how.”
66 Basi, wakaenda, wakalilinda kaburi, wakatia mhuri juu ya lile jiwe na kuacha hapo askari walinzi.
So they went and secured the tomb by sealing the stone and posting the guard.

< Mathayo 27 >