< Mathayo 25 >
1 “Wakati huo, Ufalme wa mbinguni utafanana na wasichana kumi waliochukua taa zao, wakaenda kumlaki bwana arusi.
Then may the kingdom of heaven be shadowed forth by ten virgins, who took their lamps and went out to meet the bridegroom and bride.
2 Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara.
And five of them were wise, and five were foolish.
3 Wale wapumbavu walichukua taa zao, lakini hawakuchukua akiba ya mafuta.
And the foolish took their lamps, but took no oil with them.
4 Lakini wale wenye busara walichukua mafuta katika chupa pamoja na taa zao.
But the wise took oil in vessels, with their lamps.
5 Kwa kuwa bwana arusi alikawia kuja, wale wanawali wote wote walisinzia, wakalala.
And while the bridegroom delayed, they all became sleepy and fell asleep.
6 Usiku wa manane kukawa na kelele: Haya, haya! Bwana arusi anakuja; nendeni kumlaki.
And at midnight there was an outcry: Behold, the bridegroom cometh; go ye out to meet him.
7 Hapo wale wanawali wote wakaamka, wakazitayarisha taa zao.
Then all those virgins arose, and trimmed their lamps.
8 Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara: Tupeni mafuta yenu kidogo maana taa zetu zinazimika.
And the foolish said to the wise; Give us of your oil; for, behold, our lamps have gone out.
9 Lakini wale wenye busara wakawaambia, Hayatatutosha sisi na ninyi! Afadhali mwende dukani mkajinunulie wenyewe!
The wise answered and said: We must refuse, lest there should not be enough for us and for you: but go ye to them that sell, and buy for yourselves.
10 Basi, wale wanawali wapumbavu walipokwenda kununua mafuta, bwana arusi akafika, na wale wanawali waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye katika jumba la arusi, kisha mlango ukafungwa.
And while they went to buy, the bridegroom came; and they that were ready, went with him into the house of the nuptials, and the door was shut.
11 Baadaye wale wanawali wengine wakaja, wakaita: Bwana, bwana, tufungulie!
And at length came also the other virgins, and said: Our lord, our lord, open to us.
12 Lakini yeye akawajibu, Nawaambieni kweli, siwajui ninyi.”
But he answered, and said to them: Verily I say to you, I know you not.
13 Kisha Yesu akasema, “Kesheni basi, kwa maana hamjui siku wala saa.
Watch, therefore, seeing ye know not the day nor the hour.
14 “Itakuwa kama mtu mmoja aliyetaka kusafiri ng'ambo: aliwaita watumishi wake, akawakabidhi mali yake.
For, as a man that took a journey, called his servants and delivered to them his property;
15 Alimpa kila mmoja kadiri ya uwezo wake: mmoja sarafu tano za fedha ziitwazo talanta, mwingine talanta mbili na mwingine talanta moja, kisha akasafiri.
to one he gave five talents; to another, two; and to another, one: to each, according to his ability: and he immediately departed.
16 Mara yule aliyekabidhiwa talanta tano akafanya kazi nazo akapata faida talanta tano.
Then he that received five talents, went and traded with them, and gained five more.
17 Hali kadhalika na yule aliyekabidhiwa talanta mbili akapata faida talanta mbili.
And likewise: the one of two talents, by trading gained two more.
18 Lakini yule aliyekabidhiwa talanta moja akaenda akachimba shimo ardhini, akaificha fedha ya bwana wake.
But he that received one, went and digged in the earth, and hid his lord's money.
19 “Baada ya muda mrefu, yule bwana alirudi, akaanza kukagua hesabu ya matumizi na mapato ya fedha yake.
And after a long time, the lord of those servants came, and received account from them.
20 Mtumishi aliyekabidhiwa talanta tano akaja amechukua zile talanta tano faida, akamwambia, Bwana, ulinikabidhi talanta tano, hapa pana talanta tano zaidi faida niliyopata.
And he who had received the five talents, came and brought five others; and said, My lord, thou gavest me five talents; behold, I have gained by trading five more to them.
21 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.
His lord said to him: Well done! good and faithful servant: thou hast been faithful with a little; I will set thee over much: enter thou into the joy of thy lord.
22 “Mtumishi aliyekabidhiwa talanta mbili akaja, akatoa talanta mbili faida, akisema, Bwana, ulinikabidhi talanta mbili. Chukua talanta mbili zaidi faida niliyopata.
And he of the two talents came, and said: My lord, thou gavest me two talents; behold, I have by trading gained two more to them.
23 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.
His lord said to him: Well done! good and faithful servant: thou hast been faithful with a little; I will set thee over much: enter thou into the Joy of thy lord.
24 “Lakini yule aliyekabidhiwa talanta moja akaja, akasema, Bwana, najua wewe ni mtu mgumu; wewe huvuna pale ambapo hukupanda, na kukusanya pale ambapo hukutawanya.
And he also that received the one talent, came and said: My lord, I knew thee, that thou art a hard man, reaping where thou hast not sowed, and gathering where thou hast not scattered;
25 Niliogopa, nikaificha fedha yako katika ardhi. Chukua basi mali yako.
and I was afraid, and I went and hid thy talent in the earth. Behold, thou hast what is thine.
26 “Bwana wake akamwambia, Wewe ni mtumishi mwovu na mvivu! Unajua kuwa mimi huvuna mahali ambapo sikupanda, na hukusanya pale ambapo sikutawanya.
His lord answered, and said to him: Wicked and slothful servant! Thou knewest me, that I reap where I have not sowed, and gather where I have not scattered!
27 Ilikupasa basi, kuiweka fedha yangu katika benki, nami ningelichukua mtaji wangu na faida yake!
Thou oughtest to have cast my money into the exchange; and I might have come and demanded my property with its interest.
28 Basi, mnyang'anyeni hiyo fedha mkampe yule mwenye talanta kumi.
Take therefore the talent from him, and give it to him that hath ten talents.
29 Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
For, to him that hath, shall be given, and he shall have more; but from him that hath not, even what he hath shall be taken away.
30 Na kuhusu huyu mtumishi asiye na faida, mtupeni nje gizani! Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.
And cast ye the unprofitable servant into the outer darkness: there will be weeping and gnashing of teeth.
31 “Wakati Mwana wa Mtu atakapokuja katika utukufu wake na malaika wote wakiwa pamoja naye, hapo ataketi juu ya kiti chake cha enzi kitukufu,
And when the Son of man shall come in his glory, and all his holy angels with him, then will he sit upon the throne of his glory.
32 na mataifa yote yatakusanyika mbele yake, naye atawatenganisha watu kama mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi.
And before him will be gathered all nations; and he will separate them one from another, as a shepherd severeth the sheep from the goats.
33 Atawaweka kondoo upande wake wa kulia na mbuzi upande wake wa kushoto.
And he will place the sheep on his right hand, and the goats on his left.
34 “Kisha Mfalme atawaambia wale walio upande wake wa kulia, Njoni enyi mliobarikiwa na Baba yangu; pokeeni Ufalme mliotayarishiwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
Then will the king say to those on his right hand: Come, ye blessed of my Father; inherit the kingdom that was prepared for you from the foundation of the world.
35 Maana nilikuwa na njaa nanyi mkanipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi mkanipa maji; nilikuwa mgeni nanyi mkanikaribisha;
For I was hungry, and ye gave me food; I was thirsty, and ye gave me drink; I was a stranger, and ye took me home;
36 nilikuwa uchi, mkanivika; nilikuwa mgonjwa nanyi mkaja kunitazama; nilikuwa gerezani nanyi mkaja kunitembelea.
I was naked, and ye clothed me; I was sick, and ye visited me; I was in prison, and ye came to me.
37 Hapo, hao watu wema watamjibu mfalme Bwana, ni lini tulikuona mwenye njaa nasi tukakupa chakula, au ukiwa na kiu nasi tukakunywesha maji?
Then will the righteous say to him: Our Lord, when saw we thee hungry, and fed thee? or thirsty, and gave thee drink?
38 Ni lini tulikuona ukiwa mgeni nasi tukakukaribisha, au bila nguo nasi tukakuvika?
And when saw we thee a stranger, and took thee home? or naked, and clothed thee?
39 Ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au mfungwa nasi tukaja kukutazama?
And when saw we thee sick, or in prison, and came to thee?
40 Mfalme atawajibu, Kweli nawaambieni, kila kitu mlichomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.
And the king will answer, and say to them: Verily I Say to you, That inasmuch as ye did so to one of these my little brothers, ye did so to me.
41 “Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, Ondokeni mbele yangu enyi mliolaaniwa! Nendeni katika moto wa milele aliotayarishiwa Ibilisi na malaika wake. (aiōnios )
Then will he say also to them on his left hand: Go from me, ye accursed, into everlasting fire, which was prepared for the Calumniator and his angels, (aiōnios )
42 Maana nilikuwa na njaa nanyi hamkunipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi hamkunipa maji.
For I was hungry, and ye gave me no food; and I was thirsty, and ye gave me no drink;
43 Nilikuwa mgeni nanyi hamkunikaribisha; nilikuwa mgonjwa na mfungwa nanyi hamkuja kunitazama.
and I was a stranger, and ye took me not home; and I was naked, and ye clothed me not; and I was sick and in prison, and ye did not visit me.
44 “Hapo nao watajibu, Bwana, ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, ukiwa mgeni au bila nguo, ukiwa mgonjwa au mfungwa, nasi hatukuja kukuhudumia?
Then will they also answer and say: Our Lord, when saw we thee hungry, or thirsty, or a stranger, or naked, or sick, or in prison, and did not minister to thee?
45 Naye atawajibu, Nawaambieni kweli, kila mlipokataa kumtendea mambo haya mmojawapo wa hawa wadogo, mlikataa kunitendea mimi.
Then will he answer, and say to them: Verily I say to you, That in as much as ye did not so to one of these little ones, ye did not so to me.
46 Basi, hawa watakwenda kwenye adhabu ya milele, lakini wale waadilifu watakwenda kwenye uzima wa milele.” (aiōnios )
And these will go into everlasting torment, and the righteous into everlasting life. (aiōnios )