< Mathayo 24 >
1 Yesu alitoka Hekaluni, na alipokuwa akienda zake, wanafunzi wake walimwendea, wakamwonyesha majengo ya Hekalu.
anantaraM yIzu ryadA mandirAd bahi rgacchati, tadAnIM ziSyAstaM mandiranirmmANaM darzayitumAgatAH|
2 Yesu akawaambia, “Sawa, mnaweza kuyatazama haya yote! Kweli nawaambieni, hakuna hata jiwe moja litakalosalia hapa juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa.”
tato yIzustAnuvAca, yUyaM kimetAni na pazyatha? yuSmAnahaM satyaM vadAmi, etannicayanasya pASANaikamapyanyapASANepari na sthAsyati sarvvANi bhUmisAt kAriSyante|
3 Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni, wanafunzi walimwendea faraghani, wakamwuliza, “Twambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonyesha kuja kwako na mwisho wa nyakati?” (aiōn )
anantaraM tasmin jaitunaparvvatopari samupaviSTe ziSyAstasya samIpamAgatya guptaM papracchuH, etA ghaTanAH kadA bhaviSyanti? bhavata Agamanasya yugAntasya ca kiM lakSma? tadasmAn vadatu| (aiōn )
4 Yesu akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa na mtu.
tadAnIM yIzustAnavocat, avadhadvvaM, kopi yuSmAn na bhramayet|
5 Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu wakisema: Mimi ndiye Kristo, nao watawapotosha watu wengi.
bahavo mama nAma gRhlanta AgamiSyanti, khrISTo'hameveti vAcaM vadanto bahUn bhramayiSyanti|
6 Mtasikia juu ya vita na fununu za vita; lakini msifadhaike, maana hayo hayana budi kutokea, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
yUyaJca saMgrAmasya raNasya cADambaraM zroSyatha, avadhadvvaM tena caJcalA mA bhavata, etAnyavazyaM ghaTiSyante, kintu tadA yugAnto nahi|
7 Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. Hapa na pale patakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi.
aparaM dezasya vipakSo dezo rAjyasya vipakSo rAjyaM bhaviSyati, sthAne sthAne ca durbhikSaM mahAmArI bhUkampazca bhaviSyanti,
8 Yote hayo ni kama mwanzo wa maumivu ya kujifungua mtoto.
etAni duHkhopakramAH|
9 “Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa ajili ya jina langu.
tadAnIM lokA duHkhaM bhojayituM yuSmAn parakareSu samarpayiSyanti haniSyanti ca, tathA mama nAmakAraNAd yUyaM sarvvadezIyamanujAnAM samIpe ghRNArhA bhaviSyatha|
10 Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana.
bahuSu vighnaM prAptavatsu parasparam RtIyAM kRtavatsu ca eko'paraM parakareSu samarpayiSyati|
11 Watatokea manabii wengi wa uongo watakaowapotosha watu wengi.
tathA bahavo mRSAbhaviSyadvAdina upasthAya bahUn bhramayiSyanti|
12 Kwa sababu ya ongezeko la uhalifu, upendo wa watu wengi utafifia.
duSkarmmaNAM bAhulyAJca bahUnAM prema zItalaM bhaviSyati|
13 Lakini atakayevumilia mpaka mwisho, ataokoka.
kintu yaH kazcit zeSaM yAvad dhairyyamAzrayate, saeva paritrAyiSyate|
14 Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njema ya Ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote.
aparaM sarvvadezIyalokAn pratimAkSI bhavituM rAjasya zubhasamAcAraH sarvvajagati pracAriSyate, etAdRzi sati yugAnta upasthAsyati|
15 “Basi, mtakapoona Chukizo Haribifu lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake),
ato yat sarvvanAzakRdghRNArhaM vastu dAniyelbhaviSyadvadinA proktaM tad yadA puNyasthAne sthApitaM drakSyatha, (yaH paThati, sa budhyatAM)
16 hapo, walioko Yudea na wakimbilie milimani.
tadAnIM ye yihUdIyadeze tiSThanti, te parvvateSu palAyantAM|
17 Aliye juu ya paa la nyumba yake asishuke kuchukua kitu nyumbani mwake.
yaH kazcid gRhapRSThe tiSThati, sa gRhAt kimapi vastvAnetum adhe nAvarohet|
18 Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazi lake.
yazca kSetre tiSThati, sopi vastramAnetuM parAvRtya na yAyAt|
19 Ole wao kina mama waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo!
tadAnIM garbhiNIstanyapAyayitrINAM durgati rbhaviSyati|
20 Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe siku za baridi au siku ya Sabato!
ato yaSmAkaM palAyanaM zItakAle vizrAmavAre vA yanna bhavet, tadarthaM prArthayadhvam|
21 Maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka leo, wala haitapata kutokea tena.
A jagadArambhAd etatkAlaparyyanantaM yAdRzaH kadApi nAbhavat na ca bhaviSyati tAdRzo mahAklezastadAnIm upasthAsyati|
22 Kama siku hizo hazingalipunguzwa, hakuna binadamu yeyote ambaye angeokoka; lakini siku hizo zitapunguzwa kwa ajili ya wale walioteuliwa.
tasya klezasya samayo yadi hsvo na kriyeta, tarhi kasyApi prANino rakSaNaM bhavituM na zaknuyAt, kintu manonItamanujAnAM kRte sa kAlo hsvIkariSyate|
23 “Basi, mtu akiwaambieni siku hizo: Kristo yuko hapa au Yuko pale, msimsadiki.
aparaJca pazyata, khrISTo'tra vidyate, vA tatra vidyate, tadAnIM yadI kazcid yuSmAna iti vAkyaM vadati, tathApi tat na pratIt|
24 Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Watafanya ishara kubwa na maajabu ya kuweza kuwapotosha ikiwezekana hata wateule wa Mungu.
yato bhAktakhrISTA bhAktabhaviSyadvAdinazca upasthAya yAni mahanti lakSmANi citrakarmmANi ca prakAzayiSyanti, tai ryadi sambhavet tarhi manonItamAnavA api bhrAmiSyante|
25 Sikilizeni, nimekwisha kuwaonya kabla ya wakati.
pazyata, ghaTanAtaH pUrvvaM yuSmAn vArttAm avAdiSam|
26 Basi, wakiwaambieni, Tazameni, yuko jangwani, msiende huko; au, Tazameni, amejificha ndani, msisadiki;
ataH pazyata, sa prAntare vidyata iti vAkye kenacit kathitepi bahi rmA gacchata, vA pazyata, sontaHpure vidyate, etadvAkya uktepi mA pratIta|
27 maana, kama vile umeme uangazavyo toka mashariki hadi magharibi, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu.
yato yathA vidyut pUrvvadizo nirgatya pazcimadizaM yAvat prakAzate, tathA mAnuSaputrasyApyAgamanaM bhaviSyati|
28 Pale ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.
yatra zavastiSThati, tatreva gRdhrA milanti|
29 “Mara baada ya dhiki ya siku hizo, jua litatiwa giza, mwezi hautaangaza, nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu zitatikiswa.
aparaM tasya klezasamayasyAvyavahitaparatra sUryyasya tejo lopsyate, candramA jyosnAM na kariSyati, nabhaso nakSatrANi patiSyanti, gagaNIyA grahAzca vicaliSyanti|
30 Kisha, ishara ya Mwana wa Mtu itaonekana angani, na hapo makabila yote duniani yatalalamika; watamwona Mwana wa Mtu akija juu ya mawingu ya angani mwenye nguvu na utukufu mwingi.
tadAnIm AkAzamadhye manujasutasya lakSma darziSyate, tato nijaparAkrameNa mahAtejasA ca meghArUDhaM manujasutaM nabhasAgacchantaM vilokya pRthivyAH sarvvavaMzIyA vilapiSyanti|
31 Naye atawatuma malaika wake wenye tarumbeta la kuvuma sana, nao watawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, toka mwisho huu wa mbingu hadi mwisho huu.
tadAnIM sa mahAzabdAyamAnatUryyA vAdakAn nijadUtAn praheSyati, te vyomna ekasImAto'parasImAM yAvat caturdizastasya manonItajanAn AnIya melayiSyanti|
32 “Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
uDumbarapAdapasya dRSTAntaM zikSadhvaM; yadA tasya navInAH zAkhA jAyante, pallavAdizca nirgacchati, tadA nidAghakAlaH savidho bhavatIti yUyaM jAnItha;
33 Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo haya yote yakitendeka, jueni kwamba yuko karibu sana.
tadvad etA ghaTanA dRSTvA sa samayo dvAra upAsthAd iti jAnIta|
34 Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo hayo yote kutukia.
yuSmAnahaM tathyaM vadAmi, idAnIntanajanAnAM gamanAt pUrvvameva tAni sarvvANi ghaTiSyante|
35 Naam, mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
nabhomedinyo rluptayorapi mama vAk kadApi na lopsyate|
36 “Lakini, juu ya siku au saa hiyo, hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake ndiye ajuaye.
aparaM mama tAtaM vinA mAnuSaH svargastho dUto vA kopi taddinaM taddaNDaJca na jJApayati|
37 Kwa maana kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu.
aparaM nohe vidyamAne yAdRzamabhavat tAdRzaM manujasutasyAgamanakAlepi bhaviSyati|
38 Maana nyakati hizo, kabla ya gharika kuu, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka Noa alipoingia ndani ya ile safina.
phalato jalAplAvanAt pUrvvaM yaddinaM yAvat nohaH potaM nArohat, tAvatkAlaM yathA manuSyA bhojane pAne vivahane vivAhane ca pravRttA Asan;
39 Hawakujua kuna nini mpaka ile gharika ilipotokea, ikawakumba wote. Ndivyo itakavyokuwa wakati Mwana wa Mtu atakapokuja.
aparam AplAvitoyamAgatya yAvat sakalamanujAn plAvayitvA nAnayat, tAvat te yathA na vidAmAsuH, tathA manujasutAgamanepi bhaviSyati|
40 Wakati huo watu wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.
tadA kSetrasthitayordvayoreko dhAriSyate, aparastyAjiSyate|
41 Kina mama wawili watakuwa wanasaga nafaka, mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.
tathA peSaNyA piMSatyorubhayo ryoSitorekA dhAriSyate'parA tyAjiSyate|
42 Basi, kesheni, kwa maana hamjui siku atakayokuja Bwana wenu.
yuSmAkaM prabhuH kasmin daNDa AgamiSyati, tad yuSmAbhi rnAvagamyate, tasmAt jAgrataH santastiSThata|
43 Lakini kumbukeni jambo hili: kama mwenye nyumba angejua siku mwizi atakapofika, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe.
kutra yAme stena AgamiSyatIti ced gRhastho jJAtum azakSyat, tarhi jAgaritvA taM sandhiM karttitum avArayiSyat tad jAnIta|
44 Kwa hiyo, nanyi pia muwe tayari, kwa maana Mwana wa Mtu atakuja saa msiyoitazamia.”
yuSmAbhiravadhIyatAM, yato yuSmAbhi ryatra na budhyate, tatraiva daNDe manujasuta AyAsyati|
45 Yesu akaendelea kusema, “Ni nani basi mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watu wake, awape chakula kwa wakati wake?
prabhu rnijaparivArAn yathAkAlaM bhojayituM yaM dAsam adhyakSIkRtya sthApayati, tAdRzo vizvAsyo dhImAn dAsaH kaH?
46 Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakapokuja atamkuta akifanya hivyo.
prabhurAgatya yaM dAsaM tathAcarantaM vIkSate, saeva dhanyaH|
47 Kweli nawaambieni, atamweka mtumishi huyo aisimamie mali yake yote.
yuSmAnahaM satyaM vadAmi, sa taM nijasarvvasvasyAdhipaM kariSyati|
48 Lakini kama mtumishi mbaya akijisemea moyoni: Bwana wangu anakawia kurudi,
kintu prabhurAgantuM vilambata iti manasi cintayitvA yo duSTo dAso
49 kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, akaanza kula na kunywa pamoja na walevi,
'paradAsAn praharttuM mattAnAM saGge bhoktuM pAtuJca pravarttate,
50 bwana wake atakuja siku asiyoitazamia na saa asiyoijua.
sa dAso yadA nApekSate, yaJca daNDaM na jAnAti, tatkAlaeva tatprabhurupasthAsyati|
51 Atamkatilia mbali na kumweka kundi moja na wanafiki. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.
tadA taM daNDayitvA yatra sthAne rodanaM dantagharSaNaJcAsAte, tatra kapaTibhiH sAkaM taddazAM nirUpayiSyati|