< Mathayo 18 >

1 Wakati ule wanafunzi walimwendea Yesu, wakamwuliza, “Ni nani aliye mkuu katika Ufalme wa mbinguni?”
In that hour the disciples came to Jesus, saying, "Who then is greatest in the kingdom of heaven?"
2 Yesu akamwita mtoto mmoja, akamsimamisha kati yao,
He called a little child to himself, and set him in the midst of them,
3 kisha akasema, “Nawaambieni kweli, msipogeuka na kuwa kama watoto, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni.
and said, "Truly I tell you, unless you turn, and become as little children, you will in no way enter into the kingdom of heaven.
4 Yeyote anayejinyenyekesha kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkubwa katika Ufalme wa mbinguni.
Whoever therefore humbles himself as this little child, the same is the greatest in the kingdom of heaven.
5 Yeyote anayemkaribisha mtoto mmoja kama huyu kwa jina langu, ananikaribisha mimi.
Whoever receives one such little child in my name receives me,
6 “Yeyote atakayemkosesha mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini, ingekuwa afadhali afungwe shingoni jiwe kubwa la kusagia na kuzamishwa kwenye kilindi cha bahari.
but whoever causes one of these little ones who believe in me to stumble, it would be better for him that a huge millstone should be hung around his neck, and that he should be sunk in the depths of the sea.
7 Ole wake ulimwengu kwa sababu ya vikwazo vinavyowaangusha wengine. Vikwazo hivyo ni lazima vitokee lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha.
"Woe to the world because of stumbling blocks. For there will always be something to cause people to stumble, but woe to the person through whom the stumbling block comes.
8 “Kama mkono au mguu wako ukikukosesha, ukate na kuutupa mbali nawe. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima bila mkono au mguu, kuliko kutupwa katika moto wa milele ukiwa na mikono miwili na miguu yako miwili. (aiōnios g166)
If your hand or your foot causes you to stumble, cut it off, and cast it from you. It is better for you to enter into life maimed or crippled, rather than having two hands or two feet to be cast into the everlasting fire. (aiōnios g166)
9 Na kama jicho lako likikukosesha, ling'oe na kulitupa mbali nawe. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa chongo, kuliko kutupwa katika moto wa Jehanamu ukiwa na macho yako yote mawili. (Geenna g1067)
If your eye causes you to stumble, pluck it out, and cast it from you. It is better for you to enter into life with one eye, rather than having two eyes to be cast into the fire of hell. (Geenna g1067)
10 “Jihadharini! Msimdharau mmojawapo wa wadogo hawa. Nawaambieni, malaika wao huko mbinguni wako daima mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
See that you do not despise one of these little ones, for I tell you that in heaven their angels always see the face of my Father who is in heaven.
11 Maana Mwana wa Mtu alikuja kuwaokoa wale waliopotea.
12 Mnaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, akimpoteza mmoja, hufanyaje? Huwaacha wale tisini na tisa mlimani, na huenda kumtafuta yule aliyepotea.
"What do you think? If someone has one hundred sheep, and one of them goes astray, does he not leave the ninety-nine, go to the mountains, and seek that which has gone astray?
13 Akimpata, nawaambieni kweli, humfurahia huyo kuliko awafurahiavyo wale tisini na tisa ambao hawakupotea.
If he finds it, truly I tell you, he rejoices over it more than over the ninety-nine which have not gone astray.
14 Hali kadhalika, Baba yenu wa mbinguni hapendi hata mmoja wa hawa wadogo apotee.
Even so it is not the will of my Father who is in heaven that one of these little ones should perish.
15 “Ndugu yako akikukosea, mwendee ukamwonye mkiwa ninyi peke yenu. Akikusikia utakuwa umempata ndugu yako.
"If your brother sins against you, go, show him his fault between you and him alone. If he listens to you, you have gained back your brother.
16 Asipokusikia, chukua mtu mmoja au wawili pamoja nawe, ili kwa mawaidha ya mashahidi wawili au watatu, kila tatizo litatuliwe.
But if he does not listen, take one or two more with you, that at the mouth of two or three witnesses every word may be established.
17 Asipowasikia hao, liambie kanisa. Na kama hatalisikia kanisa, na awe kwako kama watu wasiomjua Mungu na watoza ushuru.
If he refuses to listen to them, tell it to the church. If he refuses to hear the church also, let him be to you as an unbeliever or a tax collector.
18 “Nawaambieni kweli, mtakachofunga duniani kitafungwa mbinguni, na mtakachofungua duniani kitafunguliwa mbinguni.
Truly I tell you, whatever you bind on earth will be bound in heaven, and whatever you loose on earth will be loosed in heaven.
19 Tena nawaambieni, wawili miongoni mwenu wakikubaliana hapa duniani kuhusu jambo lolote la kuomba, Baba yangu wa mbinguni atawafanyia jambo hilo.
Again, truly I tell you, that if two of you agree on earth concerning anything that they will ask, it will be done for them by my Father who is in heaven.
20 Kwa maana popote pale wanapokusanyika wawili au watatu kwa jina langu, mimi nipo hapo kati yao.”
For where two or three are gathered together in my name, there I am in the midst of them."
21 Kisha Petro akamwendea Yesu, akamwuliza, “Je, ndugu yangu akinikosea, nimsamehe mara ngapi? Mara saba?”
Then Peter came to him and said, "Lord, how often can my brother sin against me, and I forgive him? Up to seven times?"
22 Yesu akamjibu, “Sisemi mara saba tu, bali sabini mara saba.
Jesus said to him, "I do not tell you up to seven times, but up to seventy times seven.
23 Ndiyo maana Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyeamua kukagua hesabu za watumishi wake.
Therefore the kingdom of heaven is like a certain king, who wanted to reconcile accounts with his servants.
24 Ukaguzi ulipoanza, akaletewa mtu mmoja aliyekuwa na deni la fedha talanta elfu kumi.
When he had begun to reconcile, one was brought to him who owed him ten thousand talents.
25 Mtu huyo hakuwa na chochote cha kulipa; hivyo bwana wake aliamuru wauzwe, yeye, mke wake, watoto wake na vitu vyote alivyokuwa navyo, ili deni lilipwe.
But because he could not pay, his lord commanded him to be sold, with his wife and children, and all that he had, and payment to be made.
26 Basi, huyo mtumishi akapiga magoti mbele yake, akasema, Unisubiri nami nitakulipa deni lote.
The servant therefore fell down and kneeled before him, saying, 'Lord, have patience with me, and I will repay you all.'
27 Yule bwana alimwonea huruma, akamsamehe lile deni, akamwacha aende zake.
The lord of that servant, being moved with compassion, released him, and forgave him the debt.
28 “Lakini huyo mtumishi akaondoka, akamkuta mmoja wa watumishi wenzake aliyekuwa na deni lake fedha denari mia moja. Akamkamata, akamkaba koo akisema, Lipa deni lako!
"But that servant went out, and found one of his fellow servants, who owed him one hundred denarii, and he grabbed him, and took him by the throat, saying, 'Pay what you owe.'
29 Huyo mtumishi mwenzake akapiga magoti, akamwomba, Unisubiri nami nitalipa deni langu lote.
"So his fellow servant fell down at his feet and begged him, saying, 'Have patience with me, and I will repay you all.'
30 Lakini yeye hakutaka, bali alimtia gerezani mpaka hapo atakapolipa lile deni.
He would not, but went and cast him into prison, until he should pay back that which was due.
31 “Basi, watumishi wenzake walipoona jambo hilo walisikitika sana, wakaenda kumpasha habari bwana wao juu ya mambo hayo yaliyotukia.
So when his fellow servants saw what was done, they were exceedingly sorry, and came and told to their lord all that was done.
32 Hapo yule bwana alimwita huyo mtumishi, akamwambia, Wewe ni mtumishi mbaya sana! Uliniomba, nami nikakusamehe deni lako lote.
Then his lord called him in, and said to him, 'You wicked servant. I forgave you all that debt, because you begged me.
33 Je, haikukupasa nawe kumhurumia mtumishi mwenzako kama nilivyokuhurumia?
Should you not also have had mercy on your fellow servant, even as I had mercy on you?'
34 “Basi, huyo bwana alikasirika sana, akamtoa huyo mtumishi aadhibiwe mpaka hapo atakapolipa deni lote.
His lord was angry, and delivered him to the tormentors, until he should pay all that was due.
35 Na baba yangu aliye mbinguni atawafanyieni vivyo hivyo kama kila mmoja wenu hatamsamehe ndugu yake kwa moyo wake wote.”
So my heavenly Father will also do to you, if you do not each forgive your brother his trespasses from your heart."

< Mathayo 18 >