< Mathayo 17 >

1 Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane nduguye, akaenda nao peke yao juu ya mlima mrefu.
After six days, Jesus took with him Peter, James, and John his brother, and brought them up into a high mountain by themselves.
2 Huko, wakiwa wanamtazama, akageuka sura, uso wake ukang'aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
He was transfigured before them. His face shone like the sun, and his garments became as white as the light.
3 Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza naye.
And look, Moses and Elijah appeared to them talking with him.
4 Hapo Petro akamwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri sana kwamba tupo hapa! Ukipenda nitajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Eliya.”
Peter answered, and said to Jesus, "Lord, it is good for us to be here. If you want, let us make three tents here: one for you, one for Moses, and one for Elijah."
5 Alipokuwa bado anasema hivyo, wingu jeupe likawafunika, na sauti ikasikika kutoka katika hilo wingu: “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye, msikilizeni.”
While he was still speaking, look, a bright cloud overshadowed them. And look, a voice came out of the cloud, saying, "This is my beloved Son, in whom I am well pleased. Listen to him."
6 Wanafunzi waliposikia hivyo wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana.
When the disciples heard it, they fell on their faces, and were very afraid.
7 Yesu akawaendea, akawagusa, akasema, “Simameni, msiogope!”
Jesus came and touched them and said, "Get up, and do not be afraid."
8 Walipoinua macho yao hawakumwona mtu, ila Yesu peke yake.
And when they lifted up their eyes, they saw no one except Jesus alone.
9 Basi, walipokuwa wanashuka mlimani, Yesu akawaonya: “Msimwambie mtu mambo mliyoyaona mpaka Mwana wa Mtu atakapofufuliwa kutoka wafu.”
As they were coming down from the mountain, Jesus commanded them, saying, "Do not tell anyone what you saw, until the Son of Man has risen from the dead."
10 Kisha wanafunzi wakamwuliza, “Mbona walimu wa Sheria wanasema ati ni lazima kwanza Eliya aje?”
The disciples asked him, saying, "Then why do the scribes say that Elijah must come first?"
11 Yesu akawajibu, “Kweli, Eliya atakuja kutayarisha mambo yote.
And he answered and said, "Elijah indeed comes, and will restore all things,
12 Lakini nawaambieni, Eliya amekwisha kuja nao hawakumtambua, bali walimtendea jinsi walivyotaka. Mwana wa Mtu atateswa vivyo hivyo mikononi mwao.”
but I tell you that Elijah has come already, and they did not recognize him, but did to him whatever they wanted to. Even so the Son of Man will also suffer by them."
13 Hapo hao wanafunzi wakafahamu kwamba alikuwa akiwaambia juu ya Yohane mbatizaji.
Then the disciples understood that he spoke to them of John the Baptist.
14 Walipojiunga tena na ule umati wa watu, mtu mmoja alimwendea Yesu, akampigia magoti,
When they came to the crowd, a man came to him, kneeling down to him, saying,
15 akasema, “Mheshimiwa, mwonee huruma mwanangu kwa kuwa ana kifafa, tena anateseka sana; mara nyingi yeye huanguka motoni na majini.
"Lord, have mercy on my son, for he is epileptic, and suffers severely; for he often falls into the fire, and often into the water.
16 Nilimleta kwa wanafunzi wako lakini hawakuweza kumponya.”
So I brought him to your disciples, and they could not cure him."
17 Yesu akajibu, “Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka! Nitakaa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia ninyi mpaka lini? Mleteni hapa huyo mtoto.”
Jesus answered, "Faithless and perverse generation. How long will I be with you? How long will I bear with you? Bring him here to me."
18 Basi, Yesu akamkemea huyo pepo, naye akamtoka, na yule mtoto akapona wakati huohuo.
Jesus rebuked him, the demon went out of him, and the boy was cured from that hour.
19 Kisha wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha, wakamwuliza, “Kwa nini sisi hatukuweza kumtoa yule pepo?”
Then the disciples came to Jesus privately, and said, "Why weren't we able to cast it out?"
20 Yesu akawajibu, “Kwa sababu ya imani yenu haba. Nawaambieni kweli, kama tu mkiwa na imani, hata iwe ndogo kama mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima huu: Toka hapa uende pale, nao utakwenda. Hakuna chochote ambacho hakingewezekana kwenu.”
So he said to them, "Because of your little faith. For truly I tell you, if you have faith as a grain of mustard seed, you will tell this mountain, 'Move from here to there,' and it will move; and nothing will be impossible for you."
21 “Pepo wa namna hii hawezi kuondolewa ila kwa sala na kufunga.”
22 Walipokuwa pamoja huko Galilaya, Yesu aliwaambia, “Mwana wa Mtu atakabidhiwa kwa watu.
While they were gathering together in Galilee, Jesus said to them, "The Son of Man is about to be delivered up into the hands of men,
23 Watamuua, lakini siku ya tatu atafufuliwa.” Wanafunzi wakahuzunika mno.
and they will kill him, and the third day he will be raised up." They were exceedingly sorry.
24 Walipofika Kafarnaumu watu wenye kukusanya fedha ya zaka ya Hekalu walimwendea Petro, wakamwuliza, “Je, mwalimu wenu hulipa fedha ya zaka?”
When they had come to Capernaum, those who collected the didrachma coins came to Peter, and said, "Does not your teacher pay the didrachma?"
25 Petro akajibu, “Naam, hulipa.” Basi, Petro alipoingia ndani ya nyumba, kabla hata hajasema neno, Yesu akamwuliza, “Simoni, wewe unaonaje? Wafalme wa dunia hukusanya ushuru au kodi kutoka kwa kina nani? Kutoka kwa wananchi ama kutoka kwa wageni?”
He said, "Yes." When he came into the house, Jesus anticipated him, saying, "What do you think, Simon? From whom do the kings of the earth receive toll or tribute? From their children, or from strangers?"
26 Petro akajibu, “Kutoka kwa wageni.” Yesu akamwambia, “Haya basi, wananchi hawahusiki.
And when he said, "From strangers." Jesus said to him, "Therefore the children are exempt.
27 Lakini kusudi tusiwakwaze, nenda ziwani ukatupe ndoana; chukua samaki wa kwanza atakayenaswa, fungua kinywa chake, na ndani utakuta fedha taslimu ya zaka. Ichukue ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako.”
But, lest we cause them to stumble, go to the sea, cast a hook, and take up the first fish that comes up. When you have opened its mouth, you will find a stater coin. Take that, and give it to them for me and you."

< Mathayo 17 >