< Mathayo 14 >

1 Wakati huo, mtawala Herode alisikia sifa za Yesu.
At that time, Herod the tetrarch heard the report concerning Jesus,
2 Basi, akawaambia watumishi wake, “Mtu huyu ni Yohane mbatizaji, amefufuka kutoka wafu; ndiyo maana nguvu za miujiza zinafanya kazi ndani yake.”
and said to his servants, “This is John the Baptiser. He is risen from the dead. That is why these powers work in him.”
3 Herode ndiye aliyekuwa amemtia Yohane nguvuni, akamfunga minyororo na kumtia gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake. Sababu hasa ni
For Herod had arrested John, bound him, and put him in prison for the sake of Herodias, his brother Philip’s wife.
4 kwamba alikuwa amemwambia Herode, “Si halali kwako kuishi na huyo mwanamke!”
For John said to him, “It is not lawful for you to have her.”
5 Herode alitaka kumwua Yohane, lakini aliogopa watu kwa sababu kwao Yohane alikuwa nabii.
When he would have put him to death, he feared the multitude, because they counted him as a prophet.
6 Katika sherehe za sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti ya Herodia alicheza mbele ya wageni. Herode alifurahiwa,
But when Herod’s birthday came, the daughter of Herodias danced amongst them and pleased Herod.
7 hata akaahidi kwa kiapo kumpa huyo msichana chochote atakachoomba.
Therefore he promised with an oath to give her whatever she should ask.
8 Naye, huku akichochewa na mama yake, akaomba, “Nipe papahapa katika sinia kichwa cha Yohane mbatizaji.”
She, being prompted by her mother, said, “Give me here on a platter the head of John the Baptiser.”
9 Mfalme alihuzunika, lakini kwa sababu ya kile kiapo chake na kwa sababu ya wale wageni karamuni, akaamuru apewe.
The king was grieved, but for the sake of his oaths and of those who sat at the table with him, he commanded it to be given,
10 Basi, Herode akatuma mtu gerezani amkate kichwa Yohane.
and he sent and beheaded John in the prison.
11 Kichwa chake kikaletwa katika sinia, wakampa yule msichana, naye akampelekea mama yake.
His head was brought on a platter and given to the young lady; and she brought it to her mother.
12 Wanafunzi wa Yohane wakaja, wakauchukua mwili wake, wakauzika. Kisha wakaenda kumpasha habari Yesu.
His disciples came, took the body, and buried it. Then they went and told Jesus.
13 Yesu alipopata habari hiyo, aliondoka mahali pale kwa mashua, akaenda mahali pa faragha peke yake. Lakini watu walipata habari, wakamfuata kwa miguu toka mijini.
Now when Jesus heard this, he withdrew from there in a boat to a deserted place apart. When the multitudes heard it, they followed him on foot from the cities.
14 Basi, aliposhuka pwani, aliona umati mkubwa wa watu, akawaonea huruma, akawaponya wagonjwa wao.
Jesus went out, and he saw a great multitude. He had compassion on them and healed their sick.
15 Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa zimepita. Basi, uwaage watu ili waende vijijini wakajinunulie chakula.”
When evening had come, his disciples came to him, saying, “This place is deserted, and the hour is already late. Send the multitudes away, that they may go into the villages, and buy themselves food.”
16 Yesu akawaambia, “Si lazima waende, wapeni ninyi chakula.”
But Jesus said to them, “They don’t need to go away. You give them something to eat.”
17 Lakini wao wakamwambia, “Tunayo mikate mitano tu na samaki wawili.”
They told him, “We only have here five loaves and two fish.”
18 Yesu akawaambia, “Nileteeni hapa.”
He said, “Bring them here to me.”
19 Akawaamuru watu waketi katika nyasi. Kisha akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akamshukuru Mungu. Halafu akaimega hiyo mikate, akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu.
He commanded the multitudes to sit down on the grass; and he took the five loaves and the two fish, and looking up to heaven, he blessed, broke and gave the loaves to the disciples; and the disciples gave to the multitudes.
20 Watu wote wakala, wakashiba. Kisha wanafunzi wakakusanya mabaki, wakajaza vikapu kumi na viwili.
They all ate and were filled. They took up twelve baskets full of that which remained left over from the broken pieces.
21 Jumla ya waliokula ilikuwa wanaume wapatao elfu tano, bila kuhesabu wanawake na watoto.
Those who ate were about five thousand men, in addition to women and children.
22 Mara, Yesu akawaamuru wanafunzi wake wapande mashua, wamtangulie ng'ambo ya ziwa wakati yeye anawaaga watu.
Immediately Jesus made the disciples get into the boat and go ahead of him to the other side, while he sent the multitudes away.
23 Baada ya kuwaaga, alipanda mlimani peke yake kusali. Ilipokuwa jioni, yeye alikuwa huko peke yake,
After he had sent the multitudes away, he went up into the mountain by himself to pray. When evening had come, he was there alone.
24 na wakati huo ile mashua ilikwishafika karibu katikati ya ziwa, lakini ilikuwa inakwenda mrama kwa sababu upepo ulikuwa unaipinga.
But the boat was now in the middle of the sea, distressed by the waves, for the wind was contrary.
25 Usiku, karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji.
In the fourth watch of the night, Jesus came to them, walking on the sea.
26 Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji waliingiwa na hofu, wakasema, “Ni mzimu!” Wakapiga kelele kwa hofu.
When the disciples saw him walking on the sea, they were troubled, saying, “It’s a ghost!” and they cried out for fear.
27 Mara, Yesu akasema nao, “Tulieni, ni mimi. Msiogope!”
But immediately Jesus spoke to them, saying, “Cheer up! It is I! Don’t be afraid.”
28 Petro akamwambia, “Bwana, ikiwa ni wewe kweli, amuru nitembee juu ya maji nije kwako.”
Peter answered him and said, “Lord, if it is you, command me to come to you on the waters.”
29 Yesu akasema, “Haya, njoo.” Basi, Petro akashuka kutoka ile mashua, akatembea juu ya maji, akamwendea Yesu.
He said, “Come!” Peter stepped down from the boat and walked on the waters to come to Jesus.
30 Lakini alipouona ule upepo, aliogopa, akaanza kuzama; akalia kwa sauti, “Bwana, niokoe!”
But when he saw that the wind was strong, he was afraid, and beginning to sink, he cried out, saying, “Lord, save me!”
31 Hapo, Yesu akaunyosha mkono wake, akamshika na kumwambia, “Ewe mwenye imani haba! Kwa nini uliona shaka?”
Immediately Jesus stretched out his hand, took hold of him, and said to him, “You of little faith, why did you doubt?”
32 Basi, wakapanda mashuani, na upepo ukatulia.
When they got up into the boat, the wind ceased.
33 Wote waliokuwa ndani ya mashua walimsujudia, wakasema, “Hakika wewe ni Mwana wa Mungu.”
Those who were in the boat came and worshipped him, saying, “You are truly the Son of God!”
34 Walivuka ziwa, wakafika nchi ya Genesareti.
When they had crossed over, they came to the land of Gennesaret.
35 Watu wa huko walipomtambua, wakaeneza habari pote katika sehemu hizo. Basi, wakamletea Yesu wagonjwa wote,
When the people of that place recognised him, they sent into all that surrounding region and brought to him all who were sick;
36 wakamwomba awaruhusu waguse tu pindo la vazi lake; wote waliomgusa walipona.
and they begged him that they might just touch the fringe of his garment. As many as touched it were made whole.

< Mathayo 14 >