< Mathayo 13 >

1 Siku hiyohiyo, Yesu alitoka katika ile nyumba, akaenda na kuketi kando ya ziwa.
On that same day, after Jesus had left the house, he took his seat on the seashore;
2 Makundi makubwa ya watu yalimzunguka hata Yesu akapanda mashua, akaketi. Hao watu walisimama kwenye ukingo wa ziwa,
and such a great crowd gathered about him that he got into a boat and sat in it, while all the crowd stood on the beach.
3 naye Yesu akawaambia mambo mengi kwa mifano. “Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu.
Then he told them many truths in parables. "Behold," he said, "the sower went forth to sow;
4 Alipokuwa akipanda, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila.
and as he sowed, some seed fell by the roadside, and the birds came and ate it.
5 Nyingine zilianguka penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi. Zikaota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina.
Some fell on rocky ground where there was not much earth. Now because it had no depth of soil, it sprang up at once;
6 Jua lilipochomoza, zilichomeka; na kwa kuwa mizizi yake haikuwa na nguvu, zikanyauka.
but when the sun rose it was scorched, and withered away because it had no root.
7 Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga.
Some fell among thorns, and the thorns sprang up and choked it.
8 Lakini nyingine zilianguka penye udongo mzuri, zikaota, zikazaa: nyingine punje mia moja, nyingine sitini na nyingine thelathini.
But some fell on good soil, and bore a crop, some a hundredfold, some sixty, some thirty.
9 Mwenye masikio na asikie!”
He who has ears, let him hear!"
10 Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwuliza, “Kwa nini unasema na watu kwa mifano?”
Now when his disciples came up to him, they said,
11 Yesu akawajibu, “Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za Ufalme wa mbinguni, lakini wao hawakujaliwa.
"Why do you speak to them in parables?" Jesus answered. "To you it has been granted to understand the mysteries of the kingdom of heaven; but to them it has not been granted.
12 Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa; lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
"For whoever holds, to him shall more be given, and he shall have abundance; but whoever does not hold, from him shall be taken away even what he holds.
13 Ndiyo maana ninasema nao kwa mifano, kwa sababu wanatazama lakini hawaoni, wanasikiliza lakini hawasikii, wala hawaelewi.
"This is why I speak to them in parables, because seeing they do not see, and hearing they do not hear, nor do they understand.
14 Kwao yametimia yale aliyosema nabii Isaya: Kusikia mtasikia, lakini hamtaelewa; Kutazama mtatazama, lakini hamtaona.
And in them is being fulfilled that prophecy of Isaiah which says. "Hearing you will hear and not understand; Seeing you will see and not perceive;
15 Maana akili za watu hawa zimepumbaa, wameyaziba masikio yao, wameyafumba macho yao. La sivyo, wangeona kwa macho yao. wangesikia kwa masikio yao, wangeelewa kwa akili zao, na kunigeukia, asema Bwana, nami ningewaponya.
For the heart of his people is made fat, Their ears are dull of hearing; Their eyes, too, have they closed, Lest some day their eyes should perceive, And their ears should hear, And their heart should understand and turn, And I should heal them.
16 “Lakini heri yenu ninyi, maana macho yenu yanaona na masikio yenu yanasikia.
"But happy are your eyes, because they see, and your ears because they hear.
17 Kweli nawaambieni, manabii na watu wengi wema walitamani kuyaona yale mnayoyaona, wasiyaone, na kuyasikia yale mnayoyasikia, wasiyasikie.
"In solemn truth I tell you that many prophets and holy men have seen it not, and to hear what you are hearing, and have not heard it.
18 “Basi, ninyi sikilizeni maana ya mfano huo wa mpanzi.
"Listen then, to the parable of the sower.
19 Yeyote asikiaye ujumbe wa ufalme bila kuuelewa, ni kama zile mbegu zilizoanguka njiani; yule Mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake.
"Whenever any one hears the message of the kingdom, and does not understand it, the Evil One comes and snatches away what was sown in his heart.
20 Ile mbegu iliyopandwa penye mawe ni mfano wa mtu asikiaye ujumbe huo na mara akaupokea kwa furaha.
"This is the seed sown by the wayside. And the word, and at once receives it with joy.
21 Lakini haumwingii na kuwa na mizizi ndani yake; huendelea kuuzingatia ujumbe huo kwa kitambo tu, na wakati taabu au udhalimu vinapotokea kwa sababu ya ujumbe huo, anakata tamaa mara.
"But he has no root in himself; he continues for a time, but when trouble arises, or persecutions, on account of the word, at once he stumbles and falls.
22 Ile mbegu iliyoanguka kati ya miti ya miiba, ni mfano wa mtu asikiaye huo ujumbe, lakini wasiwasi wa ulimwengu huu na anasa za mali huusonga ujumbe huo, naye hazai matunda. (aiōn g165)
"And the seed sown among thorns is he who hears the word, but the anxieties of the age and the deceitfulness of riches choke the word, and it becomes unfruitful. (aiōn g165)
23 Ile mbegu iliyopandwa katika udongo mzuri ni mfano wa mtu ausikiaye ujumbe huo na kuuelewa, naye huzaa matunda; mmoja mia, mwingine sitini na mwingine thelathini.”
"But the seed sown in good soil is he who hears the word and understands it, who indeed bears fruit, and makes now an hundredfold, now sixty, now thirty."
24 Yesu akawaambia watu mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake.
He told them another parable. "The kingdom of heaven," he said, "is like a man who sowed good seed in his field;
25 Lakini watu wakiwa wamelala, adui yake akaja akapanda magugu kati ya ngano, akaenda zake.
"but while men were asleep his enemy came and sowed tares among his wheat and went away.
26 Basi, mimea ilipoota na kuanza kuchanua, magugu pia yakaanza kuonekana.
"And when the blade shot up and formed the wheat-kernel, then the tares also appeared.
27 Watumishi wa yule mwenye shamba wakamwendea, wakamwambia, Mheshimiwa, bila shaka ulipanda mbegu nzuri katika shamba lako. Sasa magugu yametoka wapi?
"The slaves of the owner went to him and said. "‘Was it not good seed, sir, that you sowed in your field? From whence then, do you get tares?’
28 Yeye akawajibu, Adui ndiye aliyefanya hivyo. Basi, watumishi wake wakamwuliza, Je, unataka twende tukayang'oe
"‘It is an enemy who has done this,’ he answered. "The slaves said to him, ‘Do you want us to go and collect them?’
29 Naye akawajibu, La, msije labda mnapokusanya magugu, mkang'oa na ngano pia.
"‘No,’ he answered, ‘for fear lest while you are collecting the tares, you at the same time pull up the wheat.
30 Acheni vikue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji: kusanyeni kwanza magugu mkayafunge mafungumafungu ya kuchomwa. Lakini ngano ikusanyeni mkaiweke ghalani mwangu.”
"Let both grow together until harvest, and at harvest-time I will tell the reapers to first gather the tares and tie them in bundles for burning, but to bring all the wheat into my store-house.’"
31 Yesu akawaambia watu mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni unafanana na mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja, akaipanda katika shamba lake.
He set forth to them another parable, saying. "The kingdom of heaven is like a mustard-seed which a man took and planted in his field.
32 Yenyewe ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini ikishaota huwa kubwa kuliko mimea yote. Hukua ikawa mti, na ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake.”
"This is indeed the smallest of seeds, but when it is grown it is greater than any herb, and becomes a tree, so that the winged things of the sky come and roost in its branches."
33 Yesu akawaambia mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mama mmoja, akaichanganya na unga pishi tatu, hata unga wote ukaumuka.”
He told them another parable. He said, "The kingdom of heaven is like leaven which a woman took and hid in three measures of flour, until the whole was leavened."
34 Yesu aliwaambia watu hayo yote kwa mifano. Hakuwaambia chochote bila kutumia mifano,
Jesus told all this to the crowd in parables; indeed he never spoke to them except in parables,
35 ili jambo lililonenwa na nabii litimie: “Nitasema kwa mifano; nitawaambia mambo yaliyofichika tangu kuumbwa ulimwengu.”
in fulfilment of the word spoken by the prophet, I will open my mouth in parables, I will utter things kept secret since the foundation of the world."
36 Kisha Yesu aliwaaga wale watu, akaingia nyumbani. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwambia, “Tufafanulie ule mfano wa magugu shambani.”
After he had sent the people away and gone into the house, his disciples came to him and said, "Explain to us the parable about the weeds in the field."
37 Yesu akawaambia, “Mpanzi wa zile mbegu nzuri ni Mwana wa Mtu.
"The sower of the seed," he answered, "is the Son of man;
38 Lile shamba ni ulimwengu. Zile mbegu nzuri ni watu wale ambao Ufalme ni wao. Lakini yale magugu ni wale watu wa yule Mwovu.
"the field is the world; the good seed is the sons of the kingdom; the weeds, the sons of the Evil One.
39 Adui aliyepanda yale magugu ni Ibilisi. Mavuno ni mwisho wa nyakati na wavunaji ni malaika. (aiōn g165)
"The enemy who sows the weeds is the Devil. The harvest is the end of the age. The reapers are the angels. (aiōn g165)
40 Kama vile magugu yanavyokusanywa kuchomwa moto, ndivyo itakavyokuwa mwishoni mwa nyakati; (aiōn g165)
"Just as the weeds are collected together and burnt with fire, so will it be at the end of the age. (aiōn g165)
41 Mwana wa Mtu atawatuma malaika wake wawakusanye kutoka katika Ufalme wake wale wote wenye kusababisha dhambi, na wote wenye kutenda maovu,
"The son of man will send forth his angels, and they will gather out of his kingdom all hindrances, and whoever practises iniquity,
42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, na huko watalia na kusaga meno.
"and will throw them into the fiery furnace. There will be the weeping and the gnashing of teeth.
43 Kisha, wale wema watang'ara kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Sikieni basi, kama mna masikio!
"And then shall the just shine forth like the sun in the kingdom of their Father. Let him who has ears to hear, listen!
44 “Ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyofichika shambani. Mtu mmoja aliigundua, akaificha tena. Alifurahi sana hata akaenda kuuza yote aliyokuwa nayo, akalinunua shamba lile.
"The kingdom of heaven is like a treasure buried in the ground, which a man finds but buries again, and then in his joy goes and sells all that he has and buys that land.
45 “Tena, Ufalme wa mbinguni umefanana na mfanyabiashara mmoja mwenye kutafuta lulu nzuri.
"Again, the kingdom of heaven is like a merchant in search of beautiful pearls.
46 Alipopata lulu moja ya thamani kubwa, alienda akauza yote aliyokuwa nayo, akainunua lulu ile.
"When he finds one of great price, he goes and sells everything he has and buys it.
47 “Tena, Ufalme wa mbinguni unafanana na wavu uliotupwa baharini, ukanasa samaki wa kila aina.
"Again, the kingdom of heaven is like a net that was cast into the sea and gathered fish of every kind.
48 Ulipojaa, watu waliuvuta pwani, wakaketi, wakachagua samaki wazuri wakawaweka ndani ya vikapu vyao, na wabaya wakawatupa.
"When it was full they hauled it upon the beach, and sat down and sorted the good fish into baskets, but threw the worthless fish away.
49 Ndivyo itakavyokuwa mwishoni mwa nyakati: malaika watatokea, watawatenganisha watu wabaya na watu wema, (aiōn g165)
"So will it be at the end of the age. The angels will go forth and separate the wicked from the righteous, and fling them into the furnace of fire. (aiōn g165)
50 na kuwatupa hao wabaya katika tanuru ya moto. Huko watalia na kusaga meno.”
"There shall be the weeping and the gnashing of teeth.
51 Yesu akawauliza, “Je, mmeelewa mambo haya yote?” Wakamjibu, “Naam.”
"Have you understood all this?" he asked. "We have," they answered him.
52 Naye akawaambia, “Hivyo basi, kila mwalimu wa Sheria aliye mwanafunzi wa Ufalme wa mbinguni anafanana na mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.”
"Then," said he, "every scribe who has been instructed in the kingdom of heaven is like a householder who brings out of his storehouse new things and old."
53 Yesu alipomaliza kusema mifano hiyo alitoka mahali hapo,
After Jesus had finished these parables, he withdrew from that place,
54 akaenda kijijini kwake. Huko akawa anawafundisha watu katika sunagogi hata wakashangaa, wakasema, “Huyu amepata wapi hekima hii na maajabu?
and came into his own country, where he continued teaching the people in their synagogues, until they were amazed. "Where did he get such wisdom?" they said, "and such wondrous powers?
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda?
"Is not this the carpenter’s son? Is not his mother called Mary? and his brothers Jamesand Joseph and Simon and Judas?
56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?”
"Are not his sisters all living among us? Where, then, did he get all these powers?"
57 Basi, wakawa na mashaka naye. Lakini Yesu akawaambia, “Nabii hakosi kuheshimiwa, isipokuwa katika nchi yake na nyumbani mwake!”
This kept them from believing in him. Wherefore Jesus said, "A prophet is not without honor except in his own country and among his own family."
58 Kwa hiyo, hakutenda miujiza mingi pale kwa sababu ya kutoamini kwao.
And he did no mighty works there, because of their lack of faith.

< Mathayo 13 >