< Marko 3 >

1 Yesu aliingia tena katika sunagogi na mle ndani mlikuwa na mtu aliyekuwa na mkono uliopooza.
Once again Jesus entered the synagogue, and a man with a withered hand was there.
2 Humo baadhi ya watu walimngojea amponye mtu huyo siku ya sabato ili wapate kumshtaki.
In order to accuse Jesus, they were watching to see if He would heal on the Sabbath.
3 Yesu akamwambia huyo mtu aliyekuwa na mkono uliopooza, “Njoo hapa katikati.”
Then Jesus said to the man with the withered hand, “Stand up among us.”
4 Kisha, akawauliza, “Je, ni halali siku ya Sabato kutenda jambo jema au kutenda jambo baya; kuokoa maisha au kuua?” Lakini wao hawakusema neno.
And He asked them, “Which is lawful on the Sabbath: to do good or to do evil, to save life or to destroy it?” But they were silent.
5 Hapo akawatazama wote kwa hasira, akaona huzuni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Kisha akamwambia huyo mtu, “Nyosha mkono wako!” Naye akaunyosha mkono wake, ukawa mzima tena.
Jesus looked around at them with anger and sorrow at their hardness of heart. Then He said to the man, “Stretch out your hand.” So he stretched it out, and it was restored.
6 Mara Mafarisayo wakatoka nje, wakafanya shauri pamoja na watu wa kikundi cha Herode jinsi ya kumwangamiza Yesu.
At this, the Pharisees went out and began plotting with the Herodians how they might kill Jesus.
7 Yesu aliondoka hapo pamoja na wanafunzi wake, akaenda kando ya ziwa, na umati wa watu ukamfuata. Watu hao walikuwa wametoka Yerusalemu, Yudea,
So Jesus withdrew with His disciples to the sea, accompanied by a large crowd from Galilee, Judea,
8 Idumea, ng'ambo ya mto Yordani, Tiro na Sidoni. Watu hao wengi walimwendea Yesu kwa sababu ya kusikia mambo mengi aliyokuwa ameyatenda.
Jerusalem, Idumea, the region beyond the Jordan, and the vicinity of Tyre and Sidon. The large crowd came to Him when they heard what great things He was doing.
9 Yesu akawaambia wanafunzi wake wamtayarishie mashua moja, ili umati wa watu usije ukamsonga.
Jesus asked His disciples to have a boat ready for Him so that the crowd would not crush Him.
10 Alikuwa amewaponya watu wengi, na wagonjwa wote wakawa wanamsonga ili wapate kumgusa.
For He had healed so many that all who had diseases were pressing forward to touch Him.
11 Na watu waliokuwa wamepagawa na pepo wachafu walipomwona, walijitupa chini mbele yake na kupaaza sauti, “Wewe ni Mwana wa Mungu!”
And when the unclean spirits saw Him, they fell down before Him and cried out, “You are the Son of God!”
12 Lakini Yesu akawaamuru kwa ukali wasimjulishe kwa watu.
But He warned them sternly not to make Him known.
13 Yesu alipanda kilimani, akawaita wale aliowataka. Basi, wakamwendea,
Then Jesus went up on the mountain and called for those He wanted, and they came to Him.
14 naye akawateua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume, wakae naye, awatume kuhubiri
He appointed twelve of them, whom He designated as apostles, to accompany Him, to be sent out to preach,
15 na wawe na mamlaka ya kuwafukuza pepo.
and to have authority to drive out demons.
16 Basi, hao kumi na wawili walioteuliwa ndio hawa: Simoni (ambaye Yesu alimpa jina, Petro),
These are the twelve He appointed: Simon (whom He named Peter),
17 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo (Yesu aliwapa hawa ndugu wawili jina Boanerge, maana yake “wanangurumo”),
James son of Zebedee and his brother John (whom He named Boanerges, meaning “Sons of Thunder”),
18 Andrea na Filipo, Batholomayo, Mathayo, Thoma, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkanani na
Andrew, Philip, Bartholomew, Matthew, Thomas, James son of Alphaeus, Thaddaeus, Simon the Zealot,
19 Yuda Iskarioti ambaye alimsaliti Yesu.
and Judas Iscariot, who betrayed Jesus.
20 Kisha Yesu alikwenda nyumbani. Umati wa watu ukakusanyika tena, hata Yesu na wafuasi wake wasiweze kupata nafasi ya kula chakula.
Then Jesus went home, and once again a crowd gathered, so that He and His disciples could not even eat.
21 Basi, watu wa jamaa yake walipopata habari hiyo wakatoka kwenda kumchukua maana walikuwa wanasema kwamba amepatwa na wazimu.
When His family heard about this, they went out to take custody of Him, saying, “He is out of His mind.”
22 Nao walimu wa Sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu, wakasema, “Ana Beelzebuli! Tena, anawafukuza pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo.”
And the scribes who had come down from Jerusalem were saying, “He is possessed by Beelzebul,” and, “By the prince of the demons He drives out demons.”
23 Hapo Yesu akawaita, akawaambia kwa mifano, “Shetani anawezaje kumfukuza Shetani?
So Jesus called them together and began to speak to them in parables: “How can Satan drive out Satan?
24 Ikiwa utawala mmoja umegawanyika makundimakundi yanayopigana, utawala huo hauwezi kudumu.
If a kingdom is divided against itself, it cannot stand.
25 Tena, ikiwa jamaa moja imegawanyika makundimakundi yanayopingana, jamaa hiyo itaangamia.
If a house is divided against itself, it cannot stand.
26 Ikiwa basi, utawala wa Shetani umegawanyika vikundivikundi hauwezi kudumu, bali utaangamia kabisa.
And if Satan is divided and rises against himself, he cannot stand; his end has come.
27 “Hakuna mtu awezaye kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyang'anya mali yake, isipokuwa kwanza amemfunga huyo mtu mwenye nguvu; hapo ndipo atakapoweza kumnyang'anya mali yake.
Indeed, no one can enter a strong man’s house to steal his possessions unless he first ties up the strong man. Then he can plunder his house.
28 “Kweli nawaambieni, watu watasamehewa dhambi zao zote na kufuru zao zote;
Truly I tell you, the sons of men will be forgiven all sins and blasphemies, as many as they utter.
29 lakini anayesema mabaya dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa kamwe; ana hatia ya dhambi ya milele.” (aiōn g165, aiōnios g166)
But whoever blasphemes against the Holy Spirit will never be forgiven; he is guilty of eternal sin.” (aiōn g165, aiōnios g166)
30 (Yesu alisema hivyo kwa sababu walikuwa wanasema, “Ana pepo mchafu.”)
Jesus made this statement because they were saying, “He has an unclean spirit.”
31 Mama yake Yesu na ndugu zake walifika hapo, wakasimama nje, wakampelekea ujumbe kutaka kumwona.
Then Jesus’ mother and brothers came and stood outside. They sent someone in to summon Him,
32 Umati wa watu ulikuwa umekaa hapo kumzunguka. Basi, wakamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje, wanataka kukuona.”
and a crowd was sitting around Him. “Look,” He was told, “Your mother and brothers are outside, asking for You.”
33 Yesu akawaambia, “Mama yangu na ndugu zangu ni kina nani?”
But Jesus replied, “Who are My mother and My brothers?”
34 Hapo akawatazama watu waliokuwa wamemzunguka, akasema, “Tazameni! Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu.
Looking at those seated in a circle around Him, He said, “Here are My mother and My brothers!
35 Mtu yeyote anayefanya anayotaka Mungu, huyo ndiye kaka yangu, dada yangu na mama yangu.”
For whoever does the will of God is My brother and sister and mother.”

< Marko 3 >