< Marko 15 >

1 Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya shauri pamoja na wazee, walimu wa Sheria na Baraza lote, wakamfunga Yesu pingu, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato.
ᎩᎳᏉᏃ ᎢᏴᏛ ᏭᎩᏨᏅ ᏄᏂᎬᏫᏳᏒ ᎠᏥᎸ-ᎠᏁᎶᎯ, ᎠᎴ ᏧᎾᏛᏐᏅᎯ, ᎠᎴ ᏗᏃᏪᎵᏍᎩ, ᎠᎴ ᏂᎦᏛ ᏗᏂᎳᏫᎩ ᎤᎾᎵᏃᎮᎸ ᎤᎾᎸᎴ ᏥᏌ, ᎠᎴ ᎤᎾᏘᎾᏫᏛᎮᎢ, ᎠᎴ ᏆᎴᏗ ᏫᏚᏂᏲᎯᏎᎴᎢ.
2 Pilato akamwuliza Yesu, “Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe umesema.”
ᏆᎴᏗᏃ ᎤᏛᏛᏁ ᎯᎠ ᏄᏪᏎᎴᎢ, ᏂᎯᏍᎪ ᏣᎬᏫᏳᎯ ᎠᏂᏧᏏ ᎤᎾᏤᎵᎦ? ᎤᏁᏨᏃ ᎯᎠ ᏄᏪᏎᎴᎢ, ᏰᎵᏉ ᏂᏫ.
3 Makuhani wakuu wakamshtaki Yesu mambo mengi.
ᏄᏂᎬᏫᏳᏒᏃ ᎠᏥᎸ-ᎠᏁᎶᎯ ᎤᏣᏖ ᏧᏓᎴᏅᏛ ᎬᏭᎯᏍᏗᏍᎨᎢ.
4 Pilato akamwuliza tena Yesu, “Je, hujibu neno? Tazama wanavyotoa mashtaka mengi juu yako.”
ᏆᎴᏗᏃ ᏔᎵᏁ ᎤᏛᏛᏁ ᎯᎠ ᏄᏪᏎᎢ; ᏝᏍᎪ ᎪᎱᏍᏗ ᏯᏗᎭ? ᎬᏂᏳᏉ ᎤᏣᏘ ᏧᏓᎴᏅᏛ ᎠᏂᏃᎮᎭ ᎨᏣᏡᏗᎭ.
5 Lakini Yesu hakujibu neno, hata pilato akashangaa.
ᎠᏎᏃ ᏥᏌ ᎠᏏ ᎥᏝ ᎪᎱᏍᏗ ᏯᏗᏍᎨᎢ; ᎾᏍᎩ ᎢᏳᏍᏗ ᏆᎴᏗ ᎤᏍᏆᏂᎪᏎᎢ.
6 Kila wakati wa sikukuu ya Pasaka, Pilato alikuwa na desturi ya kuwafungulia mfungwa mmoja waliyemtaka.
ᏓᎾᎵᏍᏓᏴᎲᏍᎬᏃ ᎢᏳᎢ ᏓᏲᎯᏎᎮ ᎠᏏᏴᏫ ᎠᏴᎩ, ᎾᏍᎩᏉ ᎠᏂᏔᏲᎭ.
7 Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Baraba, ambaye alikuwa amefungwa pamoja na waasi wengine kwa kusababisha uasi na mauaji.
ᎠᏏᏴᏫᏃ ᎡᎮ ᏆᎳᏆ ᏧᏙᎢᏛ ᎾᏍᎩ ᎢᏧᎳᎭ ᏕᎨᎦᎸᎡ ᎬᏩᎵᎪᏁᎸᎯ ᎤᎾᏓᏑᏰᏛ ᎤᎾᎵᏖᎸᏅᎯ, ᎾᏍᎩ ᎤᎾᏓᎸᎯ ᎨᏎ ᎾᎯᏳ ᎤᎾᏓᏑᏰᏛ ᎤᎾᎵᏖᎸᏅᎢ.
8 Watu wengi wakamwendea Pilato wakamwomba awafanyie kama kawaida yake.
ᎤᏂᏣᏘᏃ ᎠᏍᏓᏯ ᎤᎾᎵᏍᏕᎢ, ᎤᎾᎴᏅᎮ ᎤᏂᏔᏲᎴ ᎾᏍᎩᏯ ᏂᏚᏛᏁᎸ ᏧᏩᎫᏔᏅᏒ ᎢᏧᏛᏁᏗᏱ.
9 Pilato akawauliza, “Je, mwataka niwafungulieni Mfalme wa Wayahudi?”
ᏆᎴᏗᏃ ᏚᏁᏤᎴ ᎯᎠ ᏄᏪᏎᎢ, ᎢᏣᏚᎵᏍᎪ ᎤᎬᏫᏳᎯ ᎠᏂᏧᏏ ᎤᎾᏤᎵᎦ ᏗᏳᏲᎯᏎᏗᏱ.
10 Alisema hivyo kwa sababu alijua wazi kwamba makuhani wakuu walimkabidhi Yesu kwake kwa sababu ya wivu.
ᎠᎦᏔᎮᏰᏃ ᎾᏍᎩ ᏄᏂᎬᏫᏳᏒ ᎠᏥᎸ-ᎠᏁᎶᎯ ᎠᏅᏳᏤᎲᏉ ᏅᏗᎦᎵᏍᏙᏗᏍᎬ ᏕᎬᏩᏲᏒᎢ.
11 Lakini makuhani wakuu wakawachochea watu wamwombe Pilato awafungulie Baraba.
ᎠᏎᏃ ᏄᏂᎬᏳᏒ ᎠᏥᎸ-ᎠᏁᎶᎯ ᏄᏅᏂᏌᏁ ᎤᏂᏣᏘ ᏴᏫ, ᎾᏍᎩ ᏆᎳᏆ ᎤᏂᏔᏲᏍᏗᏱ ᏧᏲᎯᏎᏗᏱ.
12 Pilato akawauliza tena, “Basi, sasa mwataka nifanye nini na mtu huyu mnayemwita Mfalme wa Wayahudi?”
ᏆᎴᏗᏃ ᏔᎵᏁ ᎤᏁᏨ, ᎯᎠ ᏂᏚᏪᏎᎴᎢ, ᎦᏙᏃ ᎢᏣᏚᎵ ᏥᏴᏁᏗᏱ ᎾᏍᎩ Ꮎ ᎤᎬᏫᏳᎯ ᎠᏂᏧᏏ ᎤᎾᏤᎵᎦ ᏤᏦᏎᎭ?
13 Watu wote wakapaaza sauti tena: “Msulubishe!”
ᏔᎵᏁᏃ ᎤᏁᎷᏁᎢ ᎯᏯᏛᎥᎦ ᎤᎾᏛᏁᎢ.
14 Lakini Pilato akawauliza, “Kwa nini! Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakazidi kupaaza sauti, “Msulubishe!”
ᏆᎴᏗᏃ ᎯᎠ ᏂᏚᏪᏎᎴᎢ, ᎦᏙᏃ, ᎦᏙ ᎤᏍᏗ ᎤᏲ ᏚᎸᏫᏍᏓᏁᎸ? ᎠᏎᏃ ᎤᏟᏉ ᎢᏯᏍᏓᏯ ᎤᏁᎷᏁᎢ, ᎯᏯᏛᎥᎦ, ᎤᎾᏛᏁᎢ.
15 Pilato alitaka kuuridhisha huo umati wa watu; basi, akamwachilia Baraba kutoka gerezani. Akaamuru Yesu apigwe viboko, kisha akamtoa asulubiwe.
ᏆᎴᏗᏃ ᎣᏏᏳ ᎤᏰᎸᏎ ᎣᏍᏛ ᏧᏓᏅᏓᏗᏍᏙᏗᏱ ᎤᏂᏣᏘ, ᏚᏲᎯᏎᎴ ᏆᎳᏆ, ᏥᏌᏃ ᎤᎵᎥᏂᎸ ᏚᏲᏎ ᎠᎦᏛᏗᏱ.
16 Kisha askari walimpeleka Yesu ndani ukumbini, katika ikulu, wakakusanya kikosi kizima cha askari.
ᎠᏂᏯᏫᏍᎩᏃ ᎬᏩᏘᎾᏫᏛᎮ ᏫᎬᏩᏴᏔᏁ ᎤᎬᏫᏳᎯᏱ ᎠᏓᏁᎸᎢ ᎾᏍᎩ ᎤᎬᏫᏳᎯ ᏣᏥᎳᏫᏤᏗᏱ, ᏂᎦᏛᏃ ᏑᎾᏓᏡᎩ ᏫᏚᏂᏯᏅᎮᎢ.
17 Wakamvika vazi la rangi ya zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamwekea kichwani.
ᎩᎦᎨᏃ ᎬᏩᏄᏪᎡᎢ, ᎠᎴ ᎠᎵᏍᏚᎶ ᏧᏣᏲᏍᏗ ᎪᏢᏔᏅᎯ ᎤᏂᏍᏕᏲᏅ, ᎾᏍᎩ ᎤᏂᏍᏚᎶᏔᏁᎢ.
18 Wakaanza kumsalimu, “Shikamoo Mfalme wa Wayahudi!”
ᎠᎴ ᎤᎾᎴᏅᎮ ᎠᏂᏲᎵᎮᎢ, ᎢᏨᏲᎵᎦ, ᏣᎬᏫᏳᎯ ᎠᏂᏧᏏ ᎤᎾᏤᎵᎦ, ᎠᎾᏗᏍᎨᎢ.
19 Wakampiga kichwani kwa mwanzi, wakamtemea mate; wakampigia magoti na kumsujudia.
ᎠᏍᎪᎵᏃ ᏕᎬᏩᏂᎮ ᎦᎾᏍᏓ ᎬᏗ, ᎠᎴ ᏕᎬᏩᎵᏥᏍᏆᏍᎨᎢ, ᎠᎴ ᏓᎾᎵᏂᏆᏅᎥᏍᎨ ᎬᏩᏓᏙᎵᏍᏓᏁᎮᎢ.
20 Baada ya kumdhihaki, walimvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.
ᎤᎾᏕᎰᏔᏃᏅᏃ, ᎬᏩᏄᏪᏎ ᎩᎦᎨᎢ, ᎠᎴ ᎤᏩᏒ ᏧᏄᏬ ᏕᎬᏩᏄᏬᎡᎢ, ᎠᎴ ᏫᎬᏩᏘᏅᏍᏔᏁ ᎬᏩᏛᏗᏱ.
21 Walipokuwa njiani, walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, mwenyeji wa Kurene. Yeye alikuwa baba wa Aleksanda na Rufo, na wakati huo alikuwa akitoka shambani. Basi, wakamlazimisha auchukue msalaba wa Yesu.
ᎩᎶᏃ ᎢᏳᏍᏗ ᏌᏩᏂ ᏧᏙᎢᏛ ᏌᎵᏂ ᎡᎯ ᎠᎢᏎᎢ, ᏙᏗᎦᎶᎨᏒ ᏅᏓᏳᎶᏒᎯ, ᎾᏍᎩ ᎡᎵᎩ ᎠᎴ ᎷᏆᏏ ᎤᏂᏙᏓ, ᎾᏍᎩ ᎤᏤᎵ ᏧᏓᎿᎭᏩᏛ ᎤᏪᏅᏍᏗᏱ ᏄᏅᏁᎴᎢ.
22 Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgotha, maana yake, “Mahali pa Fuvu la Kichwa.”
ᎪᎵᎦᏓᏃ ᏚᏙᎥ ᏫᎬᏩᏘᏅᏔᏁᎢ, ᎾᏍᎩ ᎠᏁᏢᏔᏅᎯ ᎨᏒ ᎤᏍᏆᎷᎪ ᎦᏛᎦ.
23 Wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini yeye akaikataa.
ᎬᏩᏁᏁᎴᏃ ᎤᏗᏔᏍᏗ ᎩᎦᎨᎠᏗᏔᏍᏗ ᎻᎳ ᎠᏑᎵ; ᎠᏎᏃ ᎥᏝ ᏳᏁᎩᏎᎢ.
24 Basi, wakamsulubisha, wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura waamue nani angepata nini.
ᎿᎭᏉᏃ ᏓᏓᎿᎭᏩᏍᏛ ᎬᏩᏛᏅ ᎤᏂᏯᏙᎴ ᏧᏄᏬᎢ, ᎤᎾᏎᏒᎮ ᎤᎾᏙᎴᎰᎯᏍᏗᏱ ᎾᏍᎩ ᎠᏂᏏᏴᏫᎭ ᏧᏂᏁᏒᏍᏗ ᎨᏒᎢ.
25 Ilikuwa saa tatu asubuhi walipomsulubisha.
ᏐᎣᏁᎳᏃ ᎢᏳᏟᎶᏛ ᎧᎳᏩᏗᏒ ᎨᏎᎢ, ᎠᎴ ᎬᏩᏛᏁᎢ.
26 Na mshtaka wake ulikuwa umeandikwa: “Mfalme wa Wayahudi.”
ᎦᎸᎳᏗᏢᏃ ᎪᏪᎴ ᏄᏍᏛ ᎠᎫᎢᏍᏛᎢ, ᎯᎠ ᏂᎬᏁᎢ, ᎤᎬᏫᏳᎯ ᎠᏂᏧᏏ ᎤᎾᏤᎵᎦ.
27 Pamoja naye waliwasulubisha wanyang'anyi wawili, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wake wa kushoto.
ᎢᏧᎳᎭᏃ ᏕᎨᎦᏛᏁ ᎠᏂᏔᎵ ᏗᎾᏓᎾᏌᎲᏍᎩ; ᎠᏏᏴᏫ ᎠᎦᏘᏏᏗᏢ, ᏐᎢᏃ ᎠᎦᏍᎦᏂ ᎢᏗᏢ.
28 Hapo yakatimia Maandiko Matakatifu yanayosema, “Aliwekwa kundi moja na waovu.”
ᎪᏪᎸᏃ ᎤᏙᎯᏳᏁᎢ, ᎯᎠ ᏥᏂᎦᏪᎭ, ᎤᏂᏍᎦᏅᏨᎯ ᎨᎦᏎᎸ ᎠᎦᏠᏯᏍᏔᏅᎩ.
29 Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana, wakitikisa vichwa vyao na kusema, “Aha! Wewe mwenye kuvunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu!
ᎠᏂᎶᏍᎩᏃ ᎦᎬᏩᏐᏢᏗᏍᎨᎢ, ᎠᎴ ᏓᎾᎵᏍᏛᏂᎮ ᎯᎠ ᎾᏂᏪᏍᎨᎢ, Ᏺ, ᎤᏛᏅ-ᏗᎦᎳᏫᎢᏍᏗᏱ ᎯᏲᏍᏗᏍᎩ, ᎠᎴ ᏦᎢᏉᏉ ᎢᎦ ᎯᏱᎵᏙᎯ ᎭᏁᏍᎨᏍᎩ,
30 Sasa, shuka msalabani ujiokoe mwenyewe!”
ᏨᏒ ᎭᎵᏍᏕᎸ, ᎠᎴ ᎡᎭᏠᎠᎯ ᏓᏓᎿᎭᏩᏍᏛᎢ.
31 Nao makuhani wakuu pamoja na walimu wa Sheria walimdhihaki wakisema, “Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi!
ᎾᏍᎩᏯ ᎾᏍᏉ ᏄᏂᎬᏫᏳᏒ ᎠᏥᎸ ᎠᏁᎶᎯ ᎠᎴ ᏗᏃᏪᎵᏍᎩ ᎬᏩᏕᎰᏗᏍᎬ, ᎯᎠ ᏂᏓᎾᏓᏪᏎᎮᎢ, ᏅᏩᎾᏓᎴ ᏓᏍᏕᎵᏍᎬᎩ; ᎤᏩᏒ ᎥᏝ ᏴᎬᎵᏍᏕᎸ.
32 Eti yeye ni Kristo, Mfalme wa Israeli! Basi, na ashuke msalabani ili tuone na kuamini.” Hata watu wale waliosulubiwa pamoja naye walimtukana.
ᎦᎶᏁᏛ ᎤᎬᏫᏳᎯ ᎢᏏᎵ ᎤᎾᏤᎵᎦ ᎿᎭᏉ ᏩᏠᎠᎯ ᏓᏓᎿᎭᏩᏍᏛᎢ, ᎾᏍᎩ ᎣᎩᎪᏩᏛᏗᏱ ᎠᎴ ᎣᎪᎯᏳᏗᏱ. ᎠᎴ ᎾᏍᎩ ᎢᏧᎳᎭ ᏗᎨᎦᏛᏅᎯ ᎦᎬᏩᏐᏢᏕᎢ.
33 Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa kulikuwa giza nchini kote.
ᏔᎳᏚᏃ ᎢᏳᏟᎶᏛ ᎤᎵᏰᎢᎶᎸ ᎤᎵᏏᎲᏎ ᏂᎬᎾᏛ ᎾᎿᎭᎦᏙᎯ, ᏦᎢ ᎢᏳᏟᎶᏛ ᎢᏯᏍᏘ.
34 Saa tisa alasiri Yesu akalia kwa sauti kubwa, “Eloi, Eloi, lema sabakthani?” Maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”
ᏦᎢᏁ ᎢᏳᏟᎶᏛ ᎤᎵᏰᎢᎶᎸ ᏥᏌ ᎠᏍᏓᏯ ᎤᏪᎷᏁᎢ, ᎯᎠ ᏄᏪᏎᎢ, ᎢᎶᎢ, ᎢᎶᎢ, ᎳᎹ ᏌᏆᏓᏂ? ᎾᏍᎩ ᎠᏁᏢᏔᏅᎯ ᎯᎠ ᏄᏍᏗ ᎦᏛᎦ, ᎠᏆᏁᎳᏅᎯ, ᎠᏆᏁᎳᏅᎯ, ᎦᏙᏃ ᎥᏍᏋᏕᎩ?
35 Baadhi ya watu waliosimama pale waliposikia hivyo, walisema, “Sikiliza! Anamwita Eliya!”
ᎢᎦᏛᏃ ᎾᎥ ᎠᏂᏙᎾᎢ ᎤᎾᏛᎦᏅ, ᎯᎠ ᏄᏂᏪᏎᎢ, ᎬᏂᏳᏉ, ᎢᎳᏯ ᎠᏯᏂᎭ.
36 Mtu mmoja akakimbia, akachovya sifongo katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe akisema, “Hebu tuone kama Eliya atakuja kumteremsha msalabani!”
ᎠᏎᏴᏫᏃ ᏚᏍᏆᎸᏔᏅ, ᎠᎴ ᏚᏬᎵ ᏧᏂᏦᏯᏍᏗ ᏭᎧᎵᎢᏍᏔᏅ, ᎠᎴ ᎦᎾᏍᏙᎯ ᎤᏪᏆᏔᏅ, ᎤᏁᏁᎸ ᎤᏗᏔᏍᏗ; ᎯᎠ ᏄᏪᏎᎢ, ᎤᏁᎳᎩ, ᎢᏓᏙᎴᎰᎯ, ᏥᎪᏃ ᎢᎳᏯ ᏓᎦᎷᏥ ᏓᏳᏠᎥᏔᏂᎵ.
37 Yesu akapaaza sauti kubwa, akakata roho.
ᏥᏌᏃ ᎠᏍᏓᏯ ᎤᏪᎷᏅ, ᎤᎵᏍᏆᏕᎴᎢ.
38 Basi, pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili toka juu mpaka chini.
ᎠᏰᏙᎳᏛᏗᏃ ᎤᏛᏅ-ᏗᎦᎳᏫᎢᏍᏗᏱ ᎦᏛ ᎤᏓᏣᎦᎸᎮ ᏔᎵ ᏄᏓᏕᎢ, ᎦᎸᎳᏗ ᏅᏓᏳᏓᎴᏅᏛ ᎡᎳᏗ ᏩᏍᏗ.
39 Jemadari mmoja aliyekuwa amesimama mbele yake aliona jinsi Yesu alivyolia kwa sauti na kukata roho, akasema, “Kweli mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”
ᎠᏍᎪᎯᏧᏈᏃ ᏗᏘᏂᏙᎯ ᎠᎢᏗᏢ ᏧᏳᎪᏗ ᎦᏙᎩ, ᎤᏙᎴᎰᏒ ᎾᏍᎩ ᎤᏪᎷᏅᎢ, ᎠᎴ ᎤᎵᏍᏆᏕᎸᎢ, ᎯᎠ ᏄᏪᏎᎢ, ᎤᏙᎯᏳᎯ ᎯᎠ ᎠᏍᎦᏯ ᎤᏁᎳᏅᎯ ᎤᏪᏥ ᎨᏎᎢ.
40 Walikuwako pia wanawake waliotazama kwa mbali, miongoni mwao akiwa Maria toka mji wa Magdala, Salome, na Maria mama wa kina Yakobo mdogo na Yose.
ᎠᏂᎨᏴᏃ ᎾᏍᏉ Ꭸ ᎢᏴᏛ ᏙᏗᏂᎧᏁᎢ; ᎾᎿᎭᏃ ᎠᏁᎴ ᎺᎵ ᏑᎩᏕᎵ ᎡᎯ, ᎠᎴ ᎺᎵ ᏥᎻ ᎤᏍᏗ ᎠᎴ ᏦᏏ ᎤᏂᏥᎢ, ᎠᎴ ᏌᎶᎻ.
41 Hawa walimfuata Yesu alipokuwa Galilaya na kumtumikia. Kulikuwa na wanawake wengine wengi waliokuja Yerusalemu pamoja naye.
ᎾᏍᎩ ᎾᏍᏉ ᎨᎵᎵ ᏤᏙᎮ ᎬᏩᏍᏓᏩᏗᏙᎮ ᎠᎴ ᎬᏩᏍᏕᎸᎯᏙᎮᎢ; ᎠᎴ ᎤᏂᏣᏖ ᏅᏩᎾᏓᎴ ᎠᏂᎨᏴ ᏥᎷᏏᎵᎻ ᏅᏓᎬᏩᏍᏓᏩᏙᎸᎯ.
42 Wakati wa jioni ulikuwa umekwisha fika. Hiyo ilikuwa siku ya Maandalio, yaani siku inayotangulia Sabato.
ᎿᎭᏉᏃ ᎤᏒ ᏄᎵᏍᏔᏅ, ᎾᏍᎩ ᎠᏛᏅᎢᏍᏙᏗᏱ ᎨᏒ ᎢᏳᏍᏗ, ᎾᏍᎩ ᎤᎾᏙᏓᏈᏕᎾ ᎢᎦ ᎨᏒᎢ.
43 Hapo akaja Yosefu mwenyeji wa Armathaya, mjumbe wa Baraza Kuu, aliyeheshimika sana. Yeye pia alikuwa anatazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. Basi, alimwendea Pilato bila uoga, akaomba apewe mwili wa Yesu.
ᏦᏩ ᎠᎵᎹᏗᏱ ᎡᎯ ᎠᏥᎸᏉᏗ ᏗᎦᎳᏫᎩ, ᎾᏍᎩ ᎾᏍᏉ ᎠᎦᏘᏰ ᎤᏁᎳᏅᎯ ᎤᎬᏫᏳᎯ ᎨᏒ ᎤᎷᎯᏍᏗᏱ, ᎾᏍᎩ ᎤᎷᏤᎢ, ᎠᎴ ᎾᏍᎦᎢᎲᎾ ᏭᏴᎴ ᏆᎴᏗᏱ, ᎠᎴ ᎤᏔᏲᎴ ᏥᏌ ᎠᏰᎸᎢ.
44 Pilato alishangaa kusikia kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa. Basi, akamwita jemadari, akamwuliza kama Yesu alikuwa amekufa kitambo.
ᏆᎴᏗᏃ ᎤᏍᏆᏏᎪᏎ ᎤᏜᏓᏏᏛᎡᎮ ᎾᏞᎬ ᎤᏲᎱᏒᎢ; ᏭᏯᏅᎲᏃ ᎠᏍᎪᎯᏧᏈ ᏗᏘᏂᏙᎯ, ᎤᏛᏛᏁ, ᏰᎵᏍᎪ ᎪᎯᎩ ᎬᏩᏲᎱᏒᎯ, ᎤᏛᏁᎢ.
45 Pilato alipoarifiwa na huyo jemadari kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa, akamruhusu Yosefu auchukue mwili wake.
ᎬᏂᎨᏒᏃ ᏄᏩᏁᎸ ᎠᏍᎪᎯᏧᏈ ᏗᏘᏂᏙᎯ, ᏦᏩ ᏚᏲᎯᏎᎴ ᎠᏰᎸᎢ.
46 Hapo Yosefu akanunua sanda ya kitani, akauteremsha chini huo mwili, akauzungushia sanda. Akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa mwambani, kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango.
ᎤᏩᏒᏃ ᎤᏏᏙᎵ ᏙᎴᏛ ᎠᏄᏬ, ᎠᎴ ᎤᏕᏒ ᎠᏰᎸᎢ, ᎠᎴ ᎠᏄᏬᎩᎯ ᏙᎴᏛ ᎤᏪᏣᏄᎳᏅ, ᎠᏤᎵᏍᏛ ᎤᏅᏁ ᎾᏍᎩ ᏅᏲᎯ ᎠᏍᎪᏒᎢ, ᎠᎴ ᏅᏯ ᎤᏪᏌᏆᎴᎴᎢ ᎠᏤᎵᏍᏛ ᎦᎶᎯᏍᏗᏱ ᎤᏁᎢ.
47 Nao Maria Magdalene na Maria mama yake Yose walipaona hapo alipolazwa.
ᎺᎵᏃ ᎹᎩᏕᎵ ᎡᎯ, ᎠᎴ ᎺᎵ ᏦᏏ ᎤᏥ ᎤᏂᎪᎮ ᎾᎿᎭᎤᏂᏅᏅᎢ.

< Marko 15 >