< Marko 14 >
1 Ilikuwa siku mbili tu kabla ya sikukuu ya Pasaka na ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Makuhani wakuu na walimu wa Sheria walikuwa wakitafuta njia ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue.
It was now two days before the Passover and the Feast of Unleavened Bread, and the chief priests and the scribes sought how they might seize him by deception and kill him.
2 Lakini walisema, “Tusimtie nguvuni wakati wa sikukuu, watu wasije wakafanya ghasia.”
For they said, “Not during the feast, because there might be a riot among the people.”
3 Yesu alikuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni, Mkoma. Alipokuwa mezani kula chakula, mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya nardo safi ya thamani kubwa alikuja, akaivunja hiyo chupa, akammiminia Yesu marashi hayo kichwani.
While he was at Bethany, in the house of Simon the leper, as he sat at the table, a woman came having an alabaster jar of ointment of pure nard—very costly. She broke the jar and poured it over his head.
4 Baadhi ya watu waliokuwa hapo walikasirika wakajisemea, “Kwa nini kupoteza ovyo marashi haya?
But there were some who were indignant among themselves, saying, “Why has this ointment been wasted?
5 Yangaliweza kuuzwa kwa fedha kiasi cha denari mia tatu, wakapewa maskini!” Wakamkemea huyo mama.
For this might have been sold for more than three hundred denarii and given to the poor.” So they grumbled against her.
6 Lakini Yesu akawaambia, “Mwacheni; kwa nini mnamsumbua? Amenitendea jambo jema.
But Yeshua said, “Leave her alone. Why do you trouble her? She has done a good work for me.
7 Maskini mnao daima pamoja nanyi; mnaweza kuwasaidia wakati wowote mnaopenda. Lakini mimi sitakuwapo pamoja nanyi daima.
For you always have the poor with you, and whenever you want to, you can do them good; but you will not always have me.
8 Yeye amefanya alivyoweza; ameupaka mwili wangu marashi kuutayarisha kwa maziko.
She has done what she could. She has anointed my body beforehand for the burying.
9 Nawaambieni kweli, popote ulimwenguni Habari Njema itakapohubiriwa, kitendo hiki alichofanya kitatajwa kwa ajili ya kumkumbuka.”
Most certainly I tell you, wherever this Good News may be preached throughout the whole world, that which this woman has done will also be spoken of for a memorial of her.”
10 Kisha Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili, alienda kwa makuhani wakuu ili kumsaliti Yesu.
Judah Iscariot, who was one of the twelve, went away to the chief priests, that he might deliver him to them.
11 Makuhani wakuu waliposikia habari hiyo, walifurahi, wakaahidi kumpa fedha. Basi, Yuda akaanza kutafuta nafasi ya kumsaliti Yesu.
They, when they heard it, were glad, and promised to give him money. He sought how he might conveniently deliver him.
12 Siku ya kwanza ya sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wakati ambapo mwana kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wake walimwuliza, “Wataka tukuandalie wapi karamu ya Pasaka?”
On the first day of unleavened bread, when they sacrificed the Passover, his disciples asked him, “Where do you want us to go and prepare that you may eat the Passover?”
13 Basi Yesu akawatuma wawili wa wanafunzi wake akiwaambia, “Nendeni mjini, nanyi mtakutana na mtu anayebeba mtungi wa maji. Mfuateni
He sent two of his disciples and said to them, “Go into the city, and there a man carrying a pitcher of water will meet you. Follow him,
14 mpaka katika nyumba atakayoingia, mkamwambie mwenye nyumba, Mwalimu anasema: wapi chumba changu ambamo nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu?
and wherever he enters in, tell the master of the house, ‘The Rabbi says, “Where is the guest room, where I may eat the Passover with my disciples?”’
15 Naye atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani kilichotayarishwa na kupambwa. Tuandalieni humo.”
He will himself show you a large upper room furnished and ready. Get ready for us there.”
16 Wanafunzi wakaondoka, wakaenda mjini, wakakuta kila kitu sawa kama Yesu alivyokuwa amewaambia. Wakaandaa karamu ya Pasaka.
His disciples went out, and came into the city, and found things as he had said to them, and they prepared the Passover.
17 Ilipokuwa jioni, Yesu alifika pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili.
When it was evening he came with the twelve.
18 Walipokuwa mezani wakila, Yesu alisema, “Kweli nawaambieni, mmoja wenu anayekula pamoja nami, atanisaliti.”
As they sat and were eating, Yeshua said, “Most certainly I tell you, one of you will betray me—he who eats with me.”
19 Hapo wanafunzi wake wakaanza kuhuzunika, wakamwuliza mmojammoja, “Je, ni mimi?”
They began to be sorrowful, and to ask him one by one, “Surely not I?” And another said, “Surely not I?”
20 Yesu akawaambia, “Ni mmoja wenu ninyi kumi na wawili, anayechovya mkate pamoja nami katika bakuli.
He answered them, “It is one of the twelve, he who dips with me in the dish.
21 Kweli Mwana wa Mtu anakwenda zake kama Maandiko Matakatifu yanavyosema juu yake; lakini, ole wake mtu yule anayemsaliti Mwana wa Mtu! Ingalikuwa afadhali kwa mtu huyo kama hangalizaliwa!”
For the Son of Man goes as it is written about him, but woe to that man by whom the Son of Man is betrayed! It would be better for that man if he had not been born.”
22 Walipokuwa wanakula, Yesu alitwaa mkate, akashukuru, akaumega na kuwapa wanafunzi wake akisema, “Twaeni; huu ni mwili wangu.”
As they were eating, Yeshua took bread, and when he had blessed it, he broke it and gave to them, and said, “Take, eat. This is my body.”
23 Kisha akatwaa kikombe, akamshukuru Mungu, akawapa; nao wote wakanywa katika kikombe hicho.
He took the cup, and when he had given thanks, he gave to them. They all drank of it.
24 Akawaambia, “Hii ni damu yangu inayothibitisha agano la Mungu, damu inayomwagwa kwa ajili ya watu wengi.
He said to them, “This is my blood of the new covenant, which is poured out for many.
25 Kweli nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka siku ile nitakapoinywa upya katika Ufalme wa Mungu.”
Most certainly I tell you, I will no more drink of the fruit of the vine until that day when I drink it anew in God’s Kingdom.”
26 Kisha wakaimba wimbo, wakaondoka, wakaenda katika mlima wa Mizeituni.
When they had sung the Hallel, they went out to the Mount of Olives.
27 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Ninyi nyote mtakuwa na mashaka nami; maana Maandiko Matakatifu yasema: Nitampiga mchungaji nao kondoo watatawanyika.
Yeshua said to them, “All of you will be made to stumble because of me tonight, for it is written, ‘I will strike the shepherd, and the sheep will be scattered.’
28 Lakini nikisha fufuka, nitawatangulieni kule Galilaya.”
However, after I am raised up, I will go before you into Galilee.”
29 Petro akamwambia “Hata kama wote watakuwa na mashaka nawe na kukuacha, mimi sitakukana kamwe!”
But Peter said to him, “Although all will be offended, yet I will not.”
30 Yesu akamwambia, “Kweli nakwambia, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.”
Yeshua said to him, “Most certainly I tell you that you today, even this night, before the rooster crows twice, you will deny me three times.”
31 Lakini Petro akasisitiza, “Hata kama ni lazima nife pamoja nawe, sitakuacha kamwe.” Wanafunzi wote pia wakasema vivyo hivyo.
But he spoke all the more, “If I must die with you, I will not deny you.” They all said the same thing.
32 Basi, wakafika katika bustani iitwayo Gethsemane. Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa wakati mimi nasali.”
They came to a place which was named Gethsemane. He said to his disciples, “Sit here while I pray.”
33 Kisha akawachukua Petro, Yakobo na Yohane; akaanza kufadhaika sana na kuhangaika.
He took with him Peter, Jacob, and Yochanan, and began to be greatly troubled and distressed.
34 Akawaambia, “Nina huzuni kubwa moyoni hata karibu kufa. Kaeni hapa mkeshe.”
He said to them, “My soul is exceedingly sorrowful, even to death. Stay here and watch.”
35 Akaenda mbele kidogo, akajitupa chini kifudifudi, akasali kwamba, kama ingewezekana, asiipitie saa hiyo ya mateso.
He went forward a little, and fell on the ground, and prayed that if it were possible, the hour might pass away from him.
36 Akasema, “Baba yangu, kwako mambo yote yanawezekana. Uniondolee kikombe hiki; lakini isiwe kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.”
He said, “Abba, Father, all things are possible to you. Please remove this cup from me. However, not what I desire, but what you desire.”
37 Kisha akarudi kwa wanafunzi wale watatu, akawakuta wamelala. Basi, akamwuliza Petro, “Simoni, je umelala? Hukuweza kukesha hata saa moja?”
He came and found them sleeping, and said to Peter, “Simon, are you sleeping? Couldn’t you watch one hour?
38 Kisha akawaambia, “Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.”
Watch and pray, that you may not enter into temptation. The spirit indeed is willing, but the flesh is weak.”
39 Akaenda kusali tena akirudia maneno yaleyale.
Again he went away and prayed, saying the same words.
40 Kisha akarudi tena, akawakuta wamelala. Macho yao yalikuwa yamebanwa na usingizi. Hawakujua la kumjibu.
Again he returned and found them sleeping, for their eyes were very heavy; and they didn’t know what to answer him.
41 Alipowajia mara ya tatu aliwaambia, “Mnalala bado na kupumzika? Sasa imetosha! Saa imefika! Mwana wa Mtu anakabidhiwa kwa watu waovu.
He came the third time and said to them, “Sleep on now, and take your rest. It is enough. The hour has come. Behold, the Son of Man is betrayed into the hands of sinners.
42 Amkeni, twendeni zetu. Tazameni, yule atakayenisaliti amekaribia.”
Arise! Let’s get going. Behold, he who betrays me is at hand.”
43 Yesu alipokuwa bado anasema, Yuda, mmoja wa wale kumi na wawili, akafika pamoja na umati wa watu wenye mapanga na marungu. Watu hao walikuwa wametumwa na makuhani wakuu, walimu wa Sheria na wazee.
Immediately, while he was still speaking, Judah, one of the twelve, came—and with him a multitude with swords and clubs, from the chief priests, the scribes, and the elders.
44 Msaliti Yuda alikuwa amewapa ishara: “Yule nitakayembusu ndiye; mkamateni, mkampeleke chini ya ulinzi.”
Now he who betrayed him had given them a sign, saying, “Whomever I will kiss, that is he. Seize him, and lead him away safely.”
45 Yuda alipofika tu, alimwendea Yesu moja kwa moja, akasema, “Mwalimu!” Kisha akambusu.
When he had come, immediately he came to him and said, “Rabbi! Rabbi!” and kissed him.
46 Basi, hao watu wakamkamata Yesu, wakamtia nguvuni.
They laid their hands on him and seized him.
47 Mmoja wa wale waliokuwa wamesimama hapo pamoja na Yesu akauchomoa upanga wake, akampiga mtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.
But a certain one of those who stood by drew his sword and struck the servant of the high priest, and cut off his ear.
48 Yesu akawaambia, “Je, mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang'anyi?
Yeshua answered them, “Have you come out, as against a robber, with swords and clubs to seize me?
49 Kila siku nilikuwa pamoja nanyi nikifundisha Hekaluni, wala hamkunikamata. Lakini sasa lazima Maandiko Matakatifu yatimie.”
I was daily with you in the temple teaching, and you didn’t arrest me. But this is so that the Scriptures might be fulfilled.”
50 Hapo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.
They all left him, and fled.
51 Kulikuwa na kijana mmoja aliyekuwa anamfuata Yesu akiwa amevaa shuka. Nao wakajaribu kumkamata.
A certain young man followed him, having a linen cloth thrown around himself over his naked body. The young men grabbed him,
52 Lakini yeye akaponyoka, akaiachilia ile shuka, akakimbia uchi.
but he left the linen cloth and fled from them naked.
53 Basi, wakampeleka Yesu kwa Kuhani Mkuu ambapo makuhani wakuu wote, wazee na walimu wa Sheria walikuwa wamekutanika.
They led Yeshua away to the high priest. All the chief priests, the elders, and the scribes came together with him.
54 Petro alimfuata Yesu kwa mbali, akaingia ndani ya ya wa Kuhani Mkuu, akaketi pamoja na walinzi akiota moto.
Peter had followed him from a distance, until he came into the court of the high priest. He was sitting with the officers, and warming himself in the light of the fire.
55 Makuhani wakuu na Baraza lote wakatafuta ushahidi wa kumshtaki Yesu wapate kumwua, lakini hawakupata.
Now the chief priests and the whole council sought witnesses against Yeshua to put him to death, and found none.
56 Watu wengi walitoa ushahidi wa uongo juu ya Yesu, lakini ushahidi wao haukupatana.
For many gave false testimony against him, and their testimony didn’t agree with each other.
57 Kisha wengine walisimama, wakatoa ushahidi wa uongo wakisema:
Some stood up and gave false testimony against him, saying,
58 “Tulimsikia mtu huyu akisema, Nitaliharibu Hekalu hili lililojengwa kwa mikono, na kwa siku tatu nitajenga lingine lisilojengwa kwa mikono.”
“We heard him say, ‘I will destroy this temple that is made with hands, and in three days I will build another made without hands.’”
59 Lakini hata hivyo, ushahidi wao haukupatana.
Even so, their testimony didn’t agree.
60 Basi, Kuhani Mkuu akasimama katikati yao, akamwuliza Yesu, “Je, hujibu neno? Watu hawa wanashuhudia nini dhidi yako?”
The high priest stood up in the middle, and asked Yeshua, “Have you no answer? What is it which these testify against you?”
61 Lakini yeye akakaa kimya; hakusema hata neno moja. Kuhani Mkuu akamwuliza tena, “Je, wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu Mtukufu?”
But he stayed quiet, and answered nothing. Again the high priest asked him, “Are you the Messiah, the Son of the Blessed?”
62 Yesu akajibu, “Naam, mimi ndiye. Tena, mtamwona Mwana wa Mtu amekaa upande wa kulia wa Mwenyezi, akija katika mawingu ya mbinguni.”
Yeshua said, “I am. You will see the Son of Man sitting at the right hand of Power, and coming with the clouds of the sky.”
63 Hapo Kuhani Mkuu akararua joho lake, akasema, “Tuna haja gani tena ya mashahidi?
The high priest tore his clothes and said, “What further need have we of witnesses?
64 Mmesikia kufuru yake! Ninyi mwaonaje?” Wote wakaamua kwamba anastahili kuuawa.
You have heard the blasphemy! What do you think?” They all condemned him to be worthy of death.
65 Basi, baadhi yao wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, wakampiga na kumwambia, “Bashiri ni nani aliyekupiga!” Hata watumishi wakamchukua, wakampiga makofi.
Some began to spit on him, and to cover his face, and to beat him with fists, and to tell him, “Prophesy!” The officers struck him with the palms of their hands.
66 Petro alipokuwa bado chini ukumbini, mmoja wa wajakazi wa kuhani Mkuu alikuja.
As Peter was in the courtyard below, one of the maids of the high priest came,
67 Alipomwona Petro akiota moto, alimtazama, akamwambia, “Hata wewe ulikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.”
and seeing Peter warming himself, she looked at him and said, “You were also with the Nazarene, Yeshua!”
68 Lakini Petro akakana, “Sijui, wala sielewi unayosema!” Kisha Petro akaondoka, akaenda nje uani. Hapo jogoo akawika.
But he denied it, saying, “I neither know nor understand what you are saying.” He went out on the porch, and the rooster crowed.
69 Yule mjakazi alipomwona tena Petro, akaanza tena kuwaambia watu waliokuwa wamesimama hapo, “Mtu huyu ni mmoja wao.”
The maid saw him and began again to tell those who stood by, “This is one of them.”
70 Petro akakana tena. Baadaye kidogo, watu waliokuwa wamesimama hapo wakamwambia Petro, “Hakika wewe ni mmoja wao, maana wewe ni Mgalilaya.”
But he again denied it. After a little while again those who stood by said to Peter, “You truly are one of them, for you are a Galilean, and your speech shows it.”
71 Lakini Petro akaanza kulaani na kuapa akisema, “Mimi simjui mtu huyu mnayesema habari zake.”
But he began to curse and to swear, “I don’t know this man of whom you speak!”
72 Hapo jogoo akawika mara ya pili. Basi, Petro akakumbuka jinsi Yesu alivyokuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Petro akabubujika machozi.
The rooster crowed the second time. Peter remembered the words that Yeshua said to him, “Before the rooster crows twice, you will deny me three times.” When he thought about that, he wept.