< Marko 13 >
1 Yesu alipokuwa anatoka Hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, “Mwalimu, tazama jinsi mawe haya na majengo haya yalivyo ya ajabu!”
穌從聖殿裏出來的時候,他的門徒中有一個對他說:「師傅! 看,這是何等的石頭! 何等的建築!」
2 Yesu akamwambia, “Je, unayaona majengo haya makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalosalia juu ya lingine; kila kitu kitabomolewa.”
耶穌對他說:「你看見這些偉大的建築嗎﹖將來這裏決沒有一塊石頭留在另一塊石頭上,而不被拆毀的。」
3 Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni akielekea Hekalu, Petro, Yakobo, Yohane na Andrea wakamwuliza kwa faragha,
耶穌在橄欖山上,面對聖殿坐著的時候,伯多祿、雅各伯、若望和安德肋私下問他說:「
4 “Twambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonyesha kwamba mambo haya karibu yatimizwe?”
請告訴我們:什麼時候發生這事﹖一切事要完成時,將有什麼先兆﹖」
5 Yesu akaanza kuwaambia, “Jihadharini msije mkadanganywa na mtu.
耶穌就開始對他們說:「你們要謹慎,免得有人欺騙了你們。
6 Maana wengi watakuja wakilitumia jina langu, wakisema, Mimi ndiye! nao watawapotosha watu wengi.
將有許多人假冒我的名字來說:我就是[默西亞] ;並且要欺騙許多人。
7 Mtakaposikia juu ya vita na fununu za vita, msifadhaike. Mambo hayo lazima yatokee, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
當你們聽到戰爭和戰爭的風聲時,不要驚慌,因為這是必須發生的,但還不是結局。
8 Taifa moja litapigana na taifa lingine; utawala mmoja utapigana na utawala mwingine; kila mahali kutakuwa na mitetemeko ya ardhi na njaa. Mambo haya ni kama tu maumivu ya kwanza ya kujifungua mtoto.
因為民族要起來攻擊民族,國家攻擊國家;到處要有地震,要有饑荒;但這只是苦痛的開始。」
9 “Lakini ninyi jihadharini. Maana watu watawapelekeni mahakamani, na kuwapigeni katika masunagogi. Mtapelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa sababu yangu ili mpate kunishuhudia kwao.
你們自己要謹慎! 人要把你們解送到公議會,你們在會堂裏要受鞭打,並且也要為我的緣故,站在總督和君王面前,對他們作證。
10 Lakini lazima kwanza Habari Njema ihubiriwe kwa mataifa yote.
但福音必須先傳於萬國。
11 Nao watakapowatieni nguvuni na kuwapeleka mahakamani, msiwe na wasiwasi juu ya yale mtakayosema; saa ile itakapofika, semeni chochote mtakachopewa, maana si ninyi mtakaosema, bali Roho Mtakatifu.
人把你們拉去解送到法庭時,你們不要預先思慮該說什麼;在那時刻賜給你們什麼話,你們就說什麼,因為說話的不是你們,而是聖神。
12 Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe; baba atamsaliti mwanae; watoto watawashambulia wazazi wao na kuwaua.
兄弟將把兄弟,父親將把兒子置於死地;兒女將起來反對父母,把他們處死。
13 Watu wote watawachukieni ninyi kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokolewa.
你們為了我的字,將為眾人所惱恨;但那堅持到底的,必要得救。」
14 “Mtakapoona Chukizo Haribifu limesimama mahali ambapo si pake, (msomaji na atambue maana yake!) Hapo watu walioko Yudea wakimbilie milimani.
幾時你們看見那『招致荒涼的可憎之物』立在不應在的地方──讀者應明白;那時在猶太的,該逃往山中;
15 Mtu aliye juu ya paa la nyumba asishuke kuingia nyumbani mwake kuchukua kitu.
在屋頂上的,不要下來,也不要進去,從屋裏取什麼東西;
16 Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazi lake.
在田地裏的,不要回來取自己的外衣。
17 Ole wao waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo!
在那些日子裏,懷孕的和哺乳的是有禍的!
18 Ombeni ili mambo hayo yasitukie nyakati za baridi.
但你們當祈禱, 不要叫這事逢到冬天。」
19 Maana wakati huo kutakuwa na dhiki ambayo haijatokea tangu Mungu alipoumba ulimwengu mpaka leo, wala haitatokea tena.
因為在那些日子裏,必有災難,這是從天主開始,直到如今從未有過的,將來也不會再有。
20 Kama Bwana asingepunguza siku hizo, hakuna binadamu ambaye angeokolewa. Lakini kwa ajili ya wateule wake, Bwana amezipunguza siku hizo.
若不是上主縮短了那些時日,凡有血肉的人都不會得救; 但為了他所揀選的被選者,他縮短了那些時日。
21 “Basi mtu akiwaambieni, Tazama, Kristo yupo hapa! au Yupo pale! msimsadiki.
那時,若有人對你們說:看,默西亞在這裏! 看,在那裏! 你們不要相信!
22 Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo, watafanya ishara na maajabu, ili kuwapotosha wateule wa Mungu, kama ikiwezekana.
因為將有假默西亞和假先知興起,行異跡和奇事,如果可能的話,他們連被選者都要欺騙。
23 Lakini ninyi jihadharini. Mimi nimewaambieni mambo yote kabla hayajatokea.
所以,你們要謹慎! 看,凡事我都預先告訴了你們!
24 “Basi, siku hizo baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza na mwezi hautaangaza.
但是,在那些日子裏,在那災難以後,太陽將要昏暗,月亮不再發光;
25 Nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu zitatikiswa.
星辰要從天上墜下,天上的萬象也要動搖。
26 Hapo watamwona Mwana wa Mtu akija katika mawingu kwa nguvu nyingi na utukufu.
那時,人要看見人子帶著大威能和光榮乘雲降來。
27 Kisha atawatuma malaika wake; atawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho wa dunia mpaka mwisho wa mbingu.
那時,他要派遣天使,由四方,從地極到天邊,聚集他的被選者。」
28 “Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
你們恁由無花果樹取個比喻:幾時它的枝條已經發嫩,生出葉子,你們就知道夏天近了。
29 Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo hayo yakitendeka, jueni kwamba Mwana wa Mtu yuko karibu sana.
同樣,你們幾時看見這些事發生了,就該知道:他已近在門口了。
30 Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo hayo yote kutukia.
我實在告訴你們:非到這一切發生了,這一世代決不會過去。
31 Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
天地要過去,但是我的話決不會過去。
32 “Lakini hakuna mtu ajuaye siku au saa hiyo itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye.
至於那日子和那時刻,除了父以外,誰也不知道,連天上的天使和子都不知道。」
33 Muwe waangalifu na kesheni, maana hamjui wakati huo utafika lini.
你們要當心,要醒寤,因為你們不知道那日期什麼時候來到。
34 Itakuwa kama mtu anayeondoka nyumbani kwenda safari akiwaachia watumishi wake madaraka, kila mmoja na kazi yake; akamwambia mlinzi wa mlango awe macho.
正如一個遠行的人,離開自己的家時,把權柄交給自己的僕人,每人有每人的工作;又囑咐看門的須醒寤。
35 Kesheni, basi, kwa maana hamjui mwenye nyumba atarudi lini; huenda ikawa jioni, usiku wa manane, alfajiri au asubuhi.
所以,你們要醒寤,因為你們不知道,家主什麼時候回來:或許傍晚,或許夜半,或許雞叫,或許清晨;
36 Kesheni ili akija ghafla asije akawakuta mmelala.
免得他忽然來到,遇見你們正在睡覺。
37 Ninayowaambieni ninyi, nawaambia wote: Kesheni!”
我對你們說的,我也對眾人說:你們要醒寤!」