< Marko 11 >
1 Walipokuwa wanakaribia Yerusalemu walifika Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni. Hapo aliwatuma wawili wa wanafunzi wake,
他們將近耶路撒冷,到了貝特法革和伯達尼,在橄欖山那裏時,耶穌就打發兩個門徒,
2 akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia humo, mtakuta mwana punda amefungwa ambaye bado hajatumiwa na mtu. Mfungueni mkamlete.
對他們說:「你們往對面的村莊裏去,一進村莊,立時會看見一匹拴著的驢駒,是從來沒有人騎過的;把牠解開牽來。
3 Kama mtu akiwauliza, Mbona mnafanya hivyo? Mwambieni, Bwana anamhitaji na atamrudisha hapa mara.”
若有人對你們說:「你們做什麼﹖你們就說:主要用牠,但是會立刻把牠牽回這裏來。」
4 Basi, wakaenda, wakamkuta mwana punda barabarani amefungwa mlangoni. Walipokuwa wakimfungua,
去了,便見一匹驢駒,拴在門外街道上,就把牠解開。
5 baadhi ya watu waliokuwa wamesimama hapo wakawauliza “Kwa nini mnamfungua huyo mwana punda?”
在那裏站著的人,有人對他們說:「你們解開驢駒作什麼﹖」
6 Wanafunzi wakajibu kama Yesu alivyokuwa amewaambia; nao wakawaacha waende zao.
門徒就按照耶穌所吩咐的對他們說了; 那些人遂容許了他們。
7 Wakampelekea Yesu huyo mwana punda. Wakatandika mavazi yao juu ya huyo mwana punda, na Yesu akaketi juu yake.
他們把驢駒牽到耶穌跟前,把自己的外衣搭在上面,耶穌就騎了上去。
8 Watu wengi wakatandaza mavazi yao barabarani; wengine wakatandaza matawi ya miti waliyoyakata mashambani.
有許多人把自己的外衣,另有些人把從田間砍來的綠樹枝,鋪在路上,
9 Watu wote waliotangulia na wale waliofuata wakapaaza sauti zao wakisema, “Hosana! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana!
前行後隨的都喊著說:「賀三納! 因上主之名而來的,應受讚頌!
10 Ubarikiwe Ufalme ujao wa baba yetu Daudi. Hosana juu mbinguni!”
那要來的我們祖先達味之國,應受讚頌! 賀三納於至高之天!」
11 Yesu aliingia mjini Yerusalemu akaenda moja kwa moja mpaka Hekaluni, akatazama kila kitu kwa makini. Lakini kwa vile ilikwisha kuwa jioni, akaenda Bethania pamoja na wale kumi na wawili.
耶穌進了耶路撒冷,到聖殿裏,周圍察看了一切,時辰已晚, 遂同十二門徒出來,往伯達尼去了。
12 Kesho yake, walipokuwa wanatoka Bethania, Yesu aliona njaa.
第二天,他們從伯達尼出來,耶穌餓了。
13 Basi, akaona kwa mbali mtini wenye majani mengi. Akauendea ili aone kama ulikuwa na tunda lolote. Alipoufikia, aliukuta bila tunda lolote ila majani matupu, kwa vile hayakuwa majira ya mtini kuzaa matunda.
他從遠處望見了一棵茂盛的無花果樹,就上前去,看是否在樹上可以找到什麼;及至走到那裏,除了葉子外,什麼也沒有找著,因為還不是無花果的時節。
14 Hapo akauambia mtini, “Tangu leo hata milele mtu yeyote asile matunda kwako.” Nao wanafunzi wake walisikia maneno hayo. (aiōn )
耶穌就開口對它說:「永遠再沒有人吃你的果子了! 」他的門徒也都聽見了。 (aiōn )
15 Basi, wakafika Yerusalemu. Yesu akaingia Hekaluni, akaanza kuwafukuza nje watu waliokuwa wanauza na kununua vitu humo ndani. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilishana fedha na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa.
他們來到耶路撒冷。耶穌一進殿院,就開始把在殿院裏的買賣人趕出去,把錢莊的桌子和賣鴿子的凳子推翻,
16 Hakumruhusu mtu yeyote kupitia Hekaluni akichukua kitu.
也不許人帶著器皿由殿院裏經過,
17 Kisha akawafundisha, “Imeandikwa: Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa ajili ya mataifa yote! Lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi!”
教訓他們說:「經上不是記載:『我的殿宇將稱為萬民的祈禱之所』麼﹖你們竟把它作成了賊窩! 」
18 Makuhani wakuu na walimu wa Sheria waliposikia hayo, walianza kutafuta njia ya kumwangamiza. Lakini walimwogopa kwa sababu umati wa watu ulishangazwa na mafundisho yake.
司祭長和經師聽了,就設法要怎樣除掉他,卻又害怕他,因為全群眾對他的教訓都驚奇不已。
19 Ilipokuwa jioni, Yesu na wanafunzi wake waliondoka mjini.
到了晚上,他們就出了城。
20 Asubuhi na mapema, walipokuwa wanapita, waliuona ule mtini umenyauka wote, hata mizizi.
早晨,他們從那裏經過時,看見那棵無花果樹連根都枯乾了。
21 Petro aliukumbuka, akamwambia Yesu, “Mwalimu, tazama! Ule mtini ulioulaani, umenyauka!”
伯多祿想起來,就對耶穌說:「師傅! 看,你所咒罵的無花果樹已枯乾了。」
22 Yesu akawaambia, “Mwaminini Mungu.
耶穌回答他們說:「你們對天主當有信德!
23 Nawaambieni kweli, mtu akiuambia mlima huu: Ng'oka ukajitose baharini bila kuona shaka moyoni mwake, ila akaamini kwamba mambo yote anayosema yanafanyika, atafanyiwa jambo hilo.
我實在告訴你們:無論誰對這座山說:起來,投到海裏去! 他心裏若不懷疑,反相信他說的必成就,就必給他成就。
24 Kwa hiyo nawaambieni, mnaposali na kuomba kitu, aminini kwamba mmekipokea, nanyi mtapewa.
因此,我告訴你們:你們祈禱,不論求矢麼,祇要你們相信必得,必給你們成就。
25 Mnaposimama kusali, sameheni kila mtu aliyewakosea chochote, ili Baba yenu aliye mbinguni awasamehe ninyi makosa yenu.
當你們立著祈禱時,若你們有什麼怨人的事,就寬恕罷! [
26 Lakini msipowasamehe wengine, hata Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.”
好叫你們在天之父, 也寬恕你們的過犯。」]
27 Basi, wakafika tena Yerusalemu. Yesu alipokuwa akitembea Hekaluni, makuhani wakuu, walimu wa Sheria na wazee walimwendea,
他們又來到耶路撒冷。當耶穌在殿裏徘徊時,司祭長、經師和長老來到他跟前,
28 wakamwuliza, “Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Nani aliyekupa mamlaka ya kufanya mambo haya?”
對他說:「你憑什麼權柄作這些事﹖或者,是誰給了你權柄作這些事﹖」
29 Lakini Yesu akawaambia, “Nitawaulizeni swali moja; mkinijibu, na pia nitawaambieni ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.
耶穌對他們說:「我也要問你們一句話,你們回答我,我就告訴你們:我憑什麼權柄作這些事。
30 Je, mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka mbinguni ama kwa watu? Nijibuni.”
若翰的洗禮是從天上來的,還是從人來的﹖答覆我罷!」
31 Wakaanza kujadiliana, “Tukisema, Yalitoka mbinguni, atatuuliza, Basi, mbona hamkumsadiki?
他們心中思量說:「若我們說:是從天上來的,他就要說:那麼你們為什麼不信他﹖
32 Na tukisema, Yalitoka kwa watu...” (Waliogopa umati wa watu maana wote waliamini kwamba Yohane alikuwa kweli nabii.)
但我們怎敢說:是從人來的呢﹖」──他們是害怕民眾,因為眾人都以若翰實在是一位先知。
33 Basi, wakamjibu Yesu, “Sisi hatujui.” Naye Yesu akawaambia, “Nami pia sitawaambieni ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani.”
他們便回答耶穌說:「我們不知道。」耶穌也對他們說:「我也不告訴你們:我憑什麼權柄作這些事。」