< Luka 5 >

1 Siku moja Yesu alikuwa amesimama kando ya ziwa Genesareti, na watu wengi walikuwa wamemzunguka wakisongana wanalisikiliza neno la Mungu.
One day, as Jesus was standing beside the Sea of Galilee, people crowded around him to hear the word of God.
2 Akaona mashua mbili ukingoni mwa ziwa; wavuvi wenyewe walikuwa wametoka, wanaosha nyavu zao.
Jesus noticed two boats lying on the shore, left there by fishermen who were washing their nets.
3 Baada ya Yesu kuingia katika mashua moja, iliyokuwa ya Simoni, alimtaka Simoni aisogeze majini, mbali kidogo na ukingo wa ziwa. Akaketi, akafundisha umati wa watu akiwa ndani ya mashua.
Jesus got into a boat, the one that belonged to Simon, and asked him to push it out into the water, just offshore. Then Jesus sat down in the boat and taught the people from there.
4 Alipomaliza kufundisha, akamwambia Simoni, “Peleka mashua mpaka kilindini, mkatupe nyavu zenu mpate kuvua samaki.”
After he'd finished speaking, he told Simon, “Go out into deeper water, and let down your nets for a catch.”
5 Simoni akamjibu, “Bwana, tumejitahidi kuvua samaki usiku kucha bila kupata kitu, lakini kwa kuwa umesema, nitatupa nyavu.”
“Lord, we worked hard all night, and didn't catch anything. But if you say so, I'll let down the nets,” Simon replied.
6 Baada ya kufanya hivyo, wakavua samaki wengi, hata nyavu zao zikaanza kukatika.
Having done this, a large shoal of fish filled the nets full to breaking point.
7 Wakawaita wenzao waliokuwa katika mashua nyingine waje kuwasaidia. Wakaja, wakazijaza mashua zote mbili samaki, hata karibu zingezama.
They waved to their partners in the other boat, asking them to come over and help. The others came over and together they filled both of the boats with fish. The boats were so full that they began to sink.
8 Simoni Petro alipoona hayo, akapiga magoti mbele ya Yesu akisema, “Ondoka mbele yangu, ee Bwana, kwa kuwa mimi ni mwenye dhambi!”
When Simon Peter saw what had happened, he dropped to his knees before Jesus. “Lord, please stay away from me, for I am a sinful man!” he exclaimed.
9 Simoni pamoja na wenzake wote walishangaa kwa kupata samaki wengi vile.
For he and everybody with him were completely amazed by the catch of fish that they had landed.
10 Hali kadhalika Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, waliokuwa wavuvi wenzake Simoni. Yesu akamwambia Simoni, “Usiogope; tangu sasa utakuwa ukivua watu.”
James and John, the sons of Zebedee, Simon's partners, felt the same way. “Don't be afraid,” Jesus told Simon. “From now on you'll be fishing for people!”
11 Basi, baada ya kuzileta zile mashua ukingoni mwa ziwa, wakaacha yote, wakamfuata.
So they dragged the boats onto the shore, left everything, and followed Jesus.
12 Ikawa, Yesu alipokuwa katika mmojawapo wa miji ya huko, mtu mmoja mwenye ukoma mwili mzima akamwona. Basi, mtu huyo akaanguka kifudifudi akamwomba Yesu: “Mheshimiwa, ukitaka, waweza kunitakasa.”
Once when Jesus was visiting one of the towns, he met a man there who had a very bad case of leprosy. The man fell with his face to the ground and begged Jesus, “Please Lord, if you're willing, you can make me clean.”
13 Yesu akaunyosha mkono wake, akamgusa na kusema, “Nataka, takasika!” Mara ule ukoma ukamwacha.
Jesus reached out and touched the man. “I am willing,” he said. “Be clean!” Immediately the leprosy disappeared.
14 Yesu akamwamuru: “Usimwambie mtu yeyote; bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe sadaka kwa ajili ya kutakasika kwako kama inavyotakiwa na Sheria ya Mose, iwe uthibitisho kwao kwamba umepona.”
“Say nothing to anyone,” Jesus instructed him. “Go and show yourself to the priest and make the ceremonial offerings as required by the law of Moses as proof that you've been healed.”
15 Lakini habari za Yesu zilizidi kuenea kila mahali. Watu makundi mengi wakakusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.
Yet the news about Jesus spread more and more. Large crowds came to hear Jesus and to be healed from their diseases.
16 Lakini yeye alikwenda zake mahali pasipo na watu, akawa anasali huko.
But Jesus often used to retreat to quiet places and pray.
17 Siku moja Yesu alikuwa akifundisha. Mafarisayo na walimu wa Sheria kutoka katika kila kijiji cha Galilaya, Yudea na Yerusalemu, walikuwa wameketi hapo. Nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye kwa ajili ya kuponyea wagonjwa.
One day when Jesus was teaching, the Pharisees and religious teachers who had come from all over Galilee, Judea, and Jerusalem were sitting there. The power of the Lord to heal was with him so he could heal.
18 Mara watu wakaja wamemchukua mtu mmoja aliyepooza maungo, amelala kitandani; wakajaribu kumwingiza ndani wamweke mbele ya Yesu.
Some men arrived carrying a paralyzed man on a mat. They tried to take him in and lay him in front of Jesus.
19 Lakini kwa sababu ya wingi wa watu, hawakuweza kuingia ndani. Basi, wakapanda juu ya dari, wakaondoa vigae, wakamshusha huyo aliyepooza pamoja na kitanda chake, wakamweka mbele ya Yesu.
But they couldn't find any way through the crowd, so they went up on the roof and made a hole in the roof tiles. Then they lowered the man down on the mat, right into the crowd in front of Jesus.
20 Yesu alipoona jinsi walivyokuwa na imani kubwa, akamwambia huyo mtu, “Rafiki, umesamehewa dhambi zako.”
When Jesus saw the trust they had in him, he said to the man, “Your sins are forgiven.”
21 Walimu wa Sheria na Mafarisayo wakaanza kujiuliza: “Nani huyu anayemkufuru Mungu kwa maneno yake? Hakuna mtu awezaye kusamehe dhambi ila Mungu peke yake!”
The religious teachers and the Pharisees began to argue with that. “Who is this who's speaking blasphemies?” they asked. “Who can forgive sins? Only God can do that!”
22 Yesu alitambua mawazo yao, akawauliza, “Mnawaza nini mioyoni mwenu?
Jesus knew what they were arguing about, so he asked them, “Why are you thinking to question this?
23 Ni lipi lililo rahisi zaidi: kusema, Umesamehewa dhambi, au kusema, Simama utembee?
What is easier? To say your sins are forgiven, or to say get up and walk?
24 Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kusamehe dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Simama, chukua kitanda chako uende zako nyumbani.”
However, I will prove to you that the Son of man has the authority here on earth to forgive sins.” Then he said to the paralyzed man, “I tell you: Get up, pick up your mat, and go home.”
25 Mara, huyo mtu aliyepooza akasimama mbele yao wote, akachukua kitanda chake akaenda zake nyumbani huku akimtukuza Mungu.
Immediately the man stood up in front of them. He picked up the mat he'd been lying on, and went home, praising God as he went.
26 Wote wakashangaa na kushikwa na hofu; wakamtukuza Mungu wakisema: “Tumeona maajabu leo.”
Everyone was completely astonished at what had happened, and in great awe they praised God, saying, “What we saw today was amazing!”
27 Baada ya hayo, Yesu akatoka nje, akamwona mtoza ushuru mmoja aitwaye Lawi, ameketi ofisini. Yesu akamwambia, “Nifuate!”
Later, as Jesus was leaving the town, he saw a tax collector called Levi sitting at his tax booth. “Follow me,” Jesus told him.
28 Lawi akaacha yote, akamfuata.
Levi stood up, left everything, and followed Jesus.
29 Kisha Lawi akamwandalia Yesu karamu kubwa nyumbani mwake; na kundi kubwa la watoza ushuru na watu wengine walikuwa wameketi pamoja nao.
Levi organized a large banquet at his home in Jesus' honor. Many tax collectors and others were in the crowd that sat down to eat with them. But the Pharisees and the religious teachers complained to Jesus' disciples, asking,
30 Mafarisayo na walimu wa Sheria wakawanung'unikia wafuasi wake wakisema: “Mbona mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?”
“Why do you eat and drink with tax collectors and sinners?”
31 Yesu akawajibu, “Wenye afya hawahitaji daktari, lakini wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa.
“Healthy people don't need a doctor—but sick people do,” Jesus replied.
32 Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi, ili wapate kutubu.”
“I didn't come to call those who are living right to repentance—I came to call sinners.”
33 Watu wengine wakamwambia Yesu, “Wafuasi wa Yohane mbatizaji hufunga mara nyingi na kusali; hata wafuasi wa Mafarisayo hufanya vivyo hivyo. Lakini wafuasi wako hula na kunywa.”
“Well, John's disciples often fast and pray, and the Pharisees' disciples do so as well. But your disciples don't—they go on eating and drinking,” they told him.
34 Yesu akawajibu, “Je, mnaweza kuwataka wale walioalikwa arusini wafunge hali bwana arusi yuko pamoja nao?
“Should the groomsmen fast while the bridegroom is with them?” Jesus asked.
35 Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kati yao, na wakati huo ndipo watakapofunga.”
“No—but the time is coming when the bridegroom will be taken away from them. Then they can fast.”
36 Yesu akawaambia mfano huu: “Hakuna mtu akataye kiraka cha nguo mpya na kukitia katika vazi kuukuu; kama akifanya hivyo, atakuwa amelikata hilo vazi jipya, na hicho kiraka hakitachukuana na hilo vazi kuukuu.
Then he gave them an illustration: “You don't tear out a patch from new clothes to mend old clothes. Otherwise you'd ruin new clothes, and the patch from the new wouldn't match the old.
37 Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu; kwani hiyo divai mpya itavipasua hivyo viriba, divai itamwagika, na viriba vitaharibika.
You don't put new wine into old wineskins, because if you did the new wine would burst the wineskins. Then both wine and wineskins would be wasted.
38 Divai mpya hutiwa katika viriba vipya!
You put new wine in new wineskins.
39 Wala hakuna mtu ambaye hutamani kunywa divai mpya baada ya kunywa ya zamani, kwani husema: Ile ya zamani ni nzuri zaidi.”
And nobody after drinking old wine wants new wine, for they say, ‘the old tastes good.’”

< Luka 5 >