< Luka 19 >
1 Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa anapita katika njia za mji huo.
耶稣走进耶利哥城,穿城而过。
2 Kulikuwa na mtu mmoja mjini, jina lake Zakayo ambaye alikuwa mkuu wa watoza ushuru tena mtu tajiri.
有一个名叫撒该的税吏长,非常富有。
3 Alitaka kuona Yesu alikuwa nani, lakini kwa sababu ya umati wa watu, na kwa vile alikuwa mfupi, hakufaulu.
他想看看耶稣到底是谁,但在人群中,身材矮小的他无法看见。
4 Hivyo, alitangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona Yesu, kwa maana alikuwa apitie hapo.
于是他跑到前面,爬上一棵无花果树,想在耶稣经过的时候看看他的样子。
5 Basi, Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, “Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako.”
耶稣走到这里后往上一看,对他说:“撒该,快下来,今天我要住在你家中。”
6 Zakayo akashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha.
撒该马上爬下来,高兴地迎接耶稣到他家去。
7 Watu wote walipoona hayo, wakaanza kunung'unika wakisema, “Amekwenda kukaa kwa mtu mwenye dhambi.”
众人见状议论纷纷:“他竟要住在这样的罪人家中!”
8 Lakini Zakayo akasimama akamwambia Yesu, “Sikiliza Bwana! Mimi nitawapa maskini nusu ya mali yangu, na kama nimenyang'anya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne.”
撒该站着对主说:“主啊,你看,我正在把一半的家财分给穷人,如果我曾欺骗谁,就会四倍奉还!”
9 Yesu akamwambia, “Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa vile huyu pia ni wa ukoo wa Abrahamu.
耶稣说:“今天这栋房子迎来了救赎,他也是亚伯拉罕的子孙。
10 Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.”
因为人子来寻找和拯救的就是迷失之人。”
11 Wakati watu walipokuwa bado wanasikiliza hayo, Yesu akawaambia mfano. (Hapo alikuwa anakaribia Yerusalemu, na watu wale walidhani kwamba muda si muda, Ufalme wa Mungu ungefika.)
众人专心听着耶稣的话。由于这里接近耶路撒冷,加上民众都认为上帝之国即将出现,于是耶稣就讲了一个故事。
12 Hivyo akawaambia, “Kulikuwa na mtu mmoja wa ukoo wa kifalme aliyefanya safari kwenda nchi ya mbali ili apokee madaraka ya ufalme, halafu arudi.
他说:“从前有一个贵族,他离开家去远方接受王位加冕,然后再回到家。
13 Basi, kabla ya kuondoka aliwaita watumishi wake kumi, akawapa kiasi cha fedha kila mmoja na kumwambia: Fanyeni nazo biashara mpaka nitakaporudi.
他叫了自己的十个仆人来,将钱平分给他们,然后说:‘你们用这钱去做投资,一直到我回来。’
14 Lakini wananchi wenzake walimchukia na hivyo wakatuma wajumbe waende wakaseme: Hatumtaki huyu atutawale.
但这国家的人都憎恨他,于是派一个代表跟过去,说:‘我们不想这个人做王统治我们。’
15 “Huyo mtu mashuhuri alirudi nyumbani baada ya kufanywa mfalme, na mara akaamuru wale watumishi aliowapa zile fedha waitwe ili aweze kujua kila mmoja amepata faida gani.
贵族获得王位后返回,然后将那些拿钱投资的仆人召来,询问他们做投资的收益情况。
16 Mtumishi wa kwanza akatokea, akasema: Mheshimiwa, faida iliyopatikana ni mara kumi ya zile fedha ulizonipa.
第一个仆人上前说:‘主人,你的钱已经赚了十倍。’
17 Naye akamwambia: Vema; wewe ni mtumishi mwema. Kwa kuwa umekuwa mwaminifu katika jambo dogo, utakuwa na madaraka juu ya miji kumi!
国王说:‘做得好,你是个好仆人,因为你证明了在小事上很忠心,我现在派你去管理十座城。’
18 Mtumishi wa pili akaja, akasema: Mheshimiwa, faida iliyopatikana ni mara tano ya zile fedha ulizonipa.
第二个过来说:‘主人,你的钱已经赚了五倍。’
19 Naye akamwambia pia: Nawe utakuwa na madaraka juu ya miji mitano.
国王说:‘我派你去管理五座城。’
20 “Mtumishi mwingine akaja, akasema: Chukua fedha yako; niliificha salama katika kitambaa,
另一个仆人走进来说:‘主啊,你看,这是你的钱,现在还给你。我用布包着它,确保安全。
21 kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Wewe ni mtu ambaye huchukua yasiyo yako, na huchuma ambacho hukupanda.
你是个严厉的人,我很害怕你。我怕你会拿走不属于你的东西,会收走你没有种下的作物。’
22 Naye akamwambia: Nakuhukumu kutokana na msemo wako, ewe mtumishi mbaya! Ulijua kwamba mimi ni mtu mkali, ambaye huchukua yasiyo yangu na kuchuma nisichopanda.
国王回答:‘我要根据你这番话来审判你。你知道我很严厉,会拿走不属于我的东西,会收走我没有种下的作物。
23 Kwa nini basi, hukuiweka fedha yangu benki, nami ningeichukua pamoja na faida baada ya kurudi kwangu?
那你为什么不把我的钱存入银行,等我回来的时候,就可以连本带息取回来?’
24 Hapo akawaambia wale waliokuwa pale: Mnyang'anyeni hizo fedha, mkampe yule aliyepata faida mara kumi.
国王对身边站着的仆人说:‘把他的钱拿走,交给那赚了十倍的人。’
25 Nao wakamwambia: Lakini Mheshimiwa, huyo ana faida ya kiasi hicho mara kumi!
侍卫说:‘但主人,他已经有了十倍的钱了。’
26 Naye akawajibu: Kila aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
国王说:‘告诉你们吧,那些已经有的,还会有更多。没有的,现在有的也会被拿走。
27 Na sasa, kuhusu hao maadui wangu ambao hawapendi niwe mfalme wao, waleteni hapa, mkawaue papa hapa mbele yangu.”
至于那些不愿意我做国王统治他们的敌人,现在把他们拉到这里来,当着我的面杀掉!’”
28 Yesu alisema hayo, kisha akatangulia mbele yao kuelekea Yerusalemu.
耶稣讲完这个故事,就继续向前朝着耶路撒冷走去。
29 Alipokaribia kufika Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,
快到伯法其和伯大尼时,他来到了橄榄山,在那里叫来两名门徒,对他们说:
30 akawaambia: “Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana punda amefungwa ambaye hajatumiwa na mtu. Mfungeni, mkamlete hapa.
“你们到前面的村子去,进去后会看见有一个地方拴着一头从未有人骑过的小驴,解开它的绳子,把它牵来。
31 Kama mtu akiwauliza, kwa nini mnamfungua, mwambieni, Bwana ana haja naye.”
如果有人问为什么解开它,你们就说:‘主需要它。’”
32 Basi, wakaenda, wakakuta sawa kama alivyowaambia.
两名门徒出发了,后来发生的一切与耶稣所说如出一辙。
33 Walipokuwa wanamfungua yule mwana punda, wenyewe wakawauliza, “Kwa nini mnamfungua mwana punda huyu?”
他们解开小驴的时候,驴主人问:“你们为什么解开它?”
34 Nao wakawajibu, “Bwana anamhitaji.”
他们说:“主需要它。”
35 Basi, wakampelekea Yesu yule mwana punda. Kisha wakatandika mavazi yao juu yake wakampandisha Yesu.
门徒把小驴牵到耶稣那里,把自己的衣服搭在驴背上,耶稣坐在上面。
36 Yesu akaendelea na safari, na watu wakatandaza mavazi yao barabarani.
耶稣骑驴前行,众人把自己的衣服铺在路上。
37 Alipofika karibu na Yerusalemu, katika mteremko wa mlima wa Mizeituni, umati wote na wanafunzi wake, wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa, kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona;
当他走近耶路撒冷,这里也是橄榄山的下山路,门徒们因为看见了所有神迹,开始充满喜悦地大声赞美上帝。
38 wakawa wanasema: “Abarikiwe Mfalme ajaye kwa jina la Bwana. Amani mbinguni, na utukufu juu mbinguni!”
他们大声喊:“奉主之名前来的王,赞颂你!愿和平降临天堂,愿荣耀降临至高天堂!”
39 Hapo baadhi ya Mafarisayo waliokuwako katika lile kundi la watu, wakamwambia Yesu, “Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako!”
民众中有几个法利赛人对他说:“老师,不要让你的门徒说这些!”
40 Yesu akawajibu, “Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, hakika hayo mawe yatapaza sauti.”
耶稣说:“我告诉你们,他们若保持沉默,石头就要呼喊了!”
41 Alipokaribia zaidi na kuuona ule mji, Yesu aliulilia
耶路撒冷越来越近了,耶稣看见这座城,开始为之哭泣,
42 akisema: “Laiti ungelijua leo hii yale yaletayo amani! Lakini sasa yamefichika machoni pako.
他说:“我真希望你们——就是你们啊,在今天能知道通往平安的路,但都隐藏起来了,你们看不到。
43 Maana siku zaja ambapo adui zako watakuzungushia maboma, watakuzingira na kukusonga pande zote.
时间一到,你们的仇敌就会包围过来,搭建斜坡攻击你们,把你们团团围住,困住你们,
44 Watakupondaponda wewe pamoja na watoto wako ndani ya kuta zako; hawatakuachia hata jiwe moja juu jingine, kwa sababu hukuutambua wakati Mungu alipokujia kukuokoa.”
他们会彻底摧毁你们,还有你们的孩子。所有的石头建筑都会轰然倒塌,因为你们在救赎到来之刻拒绝接受。”
45 Kisha, Yesu aliingia Hekaluni, akaanza kuwafukuzia nje wafanyabiashara
耶稣走进神庙,赶走做买卖之人,
46 akisema, “Imeandikwa: Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala; lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.”
他对他们说:“经文上记着:‘我的殿将用于祷告’。你们却把它变成贼窝了。”
47 Yesu akawa anafundisha kila siku Hekaluni. Makuhani wakuu, walimu wa Sheria na viongozi wa watu walitaka kumwangamiza,
然后他每天都在神庙里教导众人。祭司长、宗教老师和首领都想杀害他,
48 lakini hawakuwa na la kufanya, maana watu wote walikuwa wakimsikiliza kwa makini kabisa.
但又不知道如何下手,因为众人都围着他并聆听。