< Luka 11 >

1 Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulani akisali. Alipomaliza kusali, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana, tunakuomba utufundishe kusali kama Yohane mbatizaji alivyowafundisha wanafunzi wake.”
一次,耶穌在一個地方祈禱,停止以後,祂的一個門徒對祂說:「主,請教給我們祈禱,如同若翰教給了他的門徒一樣。」
2 Yesu akawaambia, “Mnaposali, semeni: Baba! Jina lako litukuzwe; Ufalme wako ufike.
耶穌給他們說:「你們時要說:父啊! 願你的名被尊為聖,願你的國來臨,
3 Utupe daima chakula chetu cha kila siku.
我們的日用糧,求你天天賜給我們,
4 Utusamehe dhambi zetu, maana sisi tunawasamehe wote waliotukosea; wala usitutie katika majaribu.”
寬免我們的罪過,因為我們自己也寬免所有虧負我們的人;不要讓我們陷入誘惑。」
5 Kisha akawaambia, “Tuseme mmoja wenu anaye rafiki, akaenda kwake usiku wa manane, akamwambia: Rafiki, tafadhali niazime mikate mitatu,
耶穌對他們說:「你們中間誰有一個朋友,半夜去他那裏,給他說:朋友,借給我三個餅罷!
6 kwa kuwa rafiki yangu amepitia kwangu akiwa safarini nami sina cha kumpa.
因為我的朋友行路到了我這裏,我沒有什麼可以款待他。
7 Naye, akiwa ndani angemjibu: Usinisumbue! Nimekwisha funga mlango. Mimi na watoto wangu tumelala; siwezi kuamka nikupe!
那人從裏面回答說:不要煩擾我了! 門己經關上,我的孩子們同我一起在床上,我不能起來給你。
8 Hakika, ingawa hataamka ampe kwa sababu yeye ni rafiki yake, lakini, kwa sababu ya huyo mtu kuendelea kumwomba, ataamka ampe chochote anachohitaji.
我告訴你們:他縱然不為了他是朋友的緣故,而起來給他,也要因他恬不知恥地切求而起來,給他所需要的一切。
9 Kwa hiyo, ombeni, nanyi mtapewa, tafuteni, nanyi mtapata, bisheni nanyi mtafunguliwa.
所以,我告訴你們:你們求,必要給你們;你們找,必要找著;你們敲,必要給你們開門。
10 Maana yeyote aombaye hupewa, atafutaye hupata na abishaye hufunguliwa.
因為凡求的,就必得到;找的,就必找到;敲的,就必給他開。
11 Mtoto akimwomba baba yake samaki, je, atampa nyoka badala ya samaki?
你們中間那有為父親的,兒子向他求餅,反而給他石頭呢﹖或是求魚,反將蛇當魚給他呢﹖
12 Na kama akimwomba yai, je, atampa ng'e?
或者求雞蛋,反將蝎子給他呢﹖
13 Ninyi, ingawa ni waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri. Basi, baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi; atawapa Roho Mtakatifu wale wanaomwomba.”
你們縱然不善,尚且知道把好東西給你們的兒女,何況在天之父,有不更將聖神賜與求他的人嗎﹖」
14 Siku moja Yesu alikuwa anamfukuza pepo aliyemfanya mtu mmoja kuwa bubu. Basi, huyo pepo alipomtoka, yule mtu akaweza kuongea hata umati wa watu ukashangaa.
耶穌驅逐一個魔鬼──他是使人瘖啞的魔鬼;他出去以後,啞吧便說出話來,群眾都驚訝不止。
15 Lakini baadhi ya watu hao wakasema, “Anamfukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, mkuu wa pepo.”
但是,其中有人說:「他是仗賴魔王貝則步驅魔。」
16 Wengine, wakimjaribu, wakamtaka afanye ishara kuonyesha kama alikuwa na idhini kutoka mbinguni.
另一些人試探耶穌,向他要求一個自天而來的徵兆。
17 Lakini yeye, akiwa anayajua mawazo yao, akawaambia, “Ufalme wowote uliofarakana wenyewe, hauwezi kudumu; kadhalika, jamaa yeyote inayofarakana huangamia.
耶穌知道了他們的心意,便給他們說:「凡是一國自相紛爭,必成廢墟,一家一家的敗落。
18 Kama Shetani anajipinga mwenyewe, utawala wake utasimamaje? Mnasemaje, basi, kwamba ninawafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli?
如果撒殫自相紛爭,他的國如何能存立呢﹖因為你們說我仗賴貝耳則步驅魔。
19 Kama ninafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, watoto wenu huwafukuza kwa uwezo wa nani? Kwa sababu hiyo, wao ndio watakaowahukumu ninyi.
如果我仗賴貝耳則步驅,你們的子弟們是仗賴誰驅魔呢﹖為此,他們將是你們的裁判者。
20 Lakini ikiwa ninawafukuza pepo kwa uwezo wa Mungu, basi jueni kwamba Ufalme wa Mungu umekwisha fika kwenu.
如果我是仗賴天主的手指驅魔,那麼,天主的國已來到你們中間了。
21 “Mtu mwenye nguvu anapolinda jumba lake kwa silaha, mali yake yote iko salama.
幾時壯士配帶武器,看守自己的宅舍,他的財產必能安全。
22 Lakini akija mwenye nguvu zaidi akamshambulia na kumshinda, huyo huziteka silaha zake alizotegemea na kugawanya nyara.
但是,如果有個比他強壯的來戰勝他,必會把他所依仗的一切器械都奪去,而瓜分他的贓物。
23 Yeyote asiyejiunga nami, ananipinga; na yeyote asiyekusanya pamoja nami, hutawanya.
不隨同我的,就是反對我;不同我收集的,就是分散。」
24 “Pepo mchafu akifukuzwa kwa mtu fulani, huzururazurura jangwani akitafuta mahali pa kupumzikia. Asipopata, hujisemea: Nitarudi kwenye makao yangu nilikotoka.
邪魔從人身上出去後,走遍乾旱之地,尋找一個安息之所,卻沒有找著;他於是說:我要回到我出來的那屋裏去。
25 Anaporudi, huikuta ile nyumba imefagiwa na kupambwa.
他來到後,見裏面已打掃清潔,裝飾整齊,
26 Basi, huenda na kuwachukua pepo wengine saba waovu zaidi kuliko yeye; wote huenda na kumwingia mtu yule. Hivyo, basi hali ya mtu huyo sasa huwa mbaya zaidi kuliko pale mwanzo.”
就去,另外帶了七個比自己更惡的魔鬼來,進去,住在那裏;那人末後的處境,比先前就更壞了。」
27 Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika lile kundi la watu, akasema kwa sauti kubwa: “Heri tumbo lililokuzaa, na maziwa yaliyokunyonyesha!”
耶穌說這些話的時候,人群中,有一個婦人高聲向他說:「懷過你的胎,及你所吮吸過的乳房,是有福的! 」
28 Lakini Yesu akasema, “Lakini heri zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kulishika.”
耶穌卻說:「可是那聲天主的話而遵行的,更是有福的! 」
29 Umati wa watu ulipozidi kuongezeka, Yesu akawaambia, “Kizazi hiki ni kizazi kiovu. Kinataka ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ya Yona.
群眾合攏來的時候,耶穌開始說:「這一世代是一個邪惡的世代:它要求徵兆,除了約納的徵兆外,必不給它任何其他徵兆。
30 Jinsi Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninewi, ndivyo pia Mwana wa Mtu atakavyokuwa ishara kwa kizazi hiki.
因為,有如約納為尼尼微人是個徵兆,將來人子為這一世代也是這樣的。
31 Malkia wa kusini atatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, naye atashuhudia kwamba kina hatia. Yeye alisafiri kutoka mbali, akaja kusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni; kumbe hapa pana mkuu zaidi kuliko Solomoni.
南方的女王,在審判時,將同這一世代的人起來,定他們的罪,因為她從地極來,聽撒羅滿的智慧;看,這裏有一位大於撒羅滿的!
32 Watu wa Ninewi watatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, na watashuhudia kwamba kizazi hiki kina hatia. Hao watu wa Ninewi walitubu kwa sababu ya mahubiri ya Yona; na hapa pana mkuu zaidi kuliko Yona!
尼尼微人在審判時,將同這一代的人起來,定他們的罪,因為尼尼微人因了約納的宣講而悔改了;看,這裏有一位大於約納的! 」
33 “Hakuna mtu anayewasha taa na kuifunika kwa pishi, bali huiweka juu ya kinara ili watu wanaoingia ndani wapate kuona mwanga.
沒有人點燈放在窖中,或置於斗下的,而是放在燈台上,讓進來的人看見光明。
34 Jicho lako ni kama taa ya mwili wako; likiwa zima, mwili wako wote utakuwa katika mwanga. Jicho lako likiwa bovu, na mwili wako pia utakuwa katika giza.
你的眼睛就是身體的燈。幾時你的眼睛純潔,你全身就光明;但如果邪惡,你全身就黑暗。
35 Uwe mwangalifu basi mwanga ulio ndani yako usije ukawa giza.
為此,你要小心,不要叫你內裏的光成了黑暗。
36 Basi, kama mwili wako wote una mwanga, bila kuwa na sehemu yoyote yenye giza, mwili huo utang'aa kikamilifu kama vile taa inavyokuangazia kwa mwanga wake.”
所以,如果你全身光明,絲毫沒有黑暗之處,一切必要光明,有如燈光照耀你一樣。」
37 Yesu alipokuwa akiongea, Mfarisayo mmoja alimkaribisha chakula nyumbani kwake, naye akaenda, akaketi kula chakula.
耶穌正說話的時候,有一個法利賽人請他到自己家中用飯,耶穌進去便入了席。
38 Huyo Mfarisayo alistaajabu kuona kwamba alikula chakula bila kunawa.
那個法利賽人一看見,就怪異耶穌飯前不先洗手。
39 Bwana akamwambia, “Ninyi Mafarisayo huosha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani mmejaa udhalimu na uovu.
但主對他說:「你們法利賽人洗淨杯盤的外面,而你們心中卻滿是劫奪與邪惡。
40 Wapumbavu ninyi! Je, aliyetengeneza nje si ndiye aliyetengeneza ndani pia?
糊塗人哪! 那造外面的,不是也造了裏面嗎﹖
41 Toeni kwa maskini vile vitu vilivyomo ndani, na vingine vyote vitakuwa halali kwenu.
只要把你們杯盤裏面的施捨了,那麼,一切對你們便都潔淨了。
42 “Lakini ole wenu Mafarisayo, kwa sababu mnatoza watu zaka hata juu ya majani ya kukolezea chakula, mchicha na majani mengine, na huku hamjali juu ya haki na upendo kwa Mungu. Mambo haya iliwapasa muwe mmeyazingatia bila kuyasahau yale mengine.
但是,禍哉,你們法利賽人! 因為你們把薄荷茴香及各種菜蔬捐獻十分之一,反而將公義及愛天主的義務忽略過去:這些固然該作,那些也不可忽略。
43 “Ole wenu ninyi Mafarisayo, kwa sababu mnapenda kuketi mbele mahali pa heshima katika masunagogi, na kusalimiwa kwa heshima hadharani.
禍哉,你們法利賽人! 因為你們在會堂裏愛坐上座,在街市上愛受人致敬。
44 Ole wenu, kwa sababu mko kama makaburi yaliyofichika; watu hutembea juu yake bila kufahamu.”
禍哉,你們! 因為你們就如同不顯露的墳墓,人在上面行走,也不知道。」
45 Mmoja wa walimu wa Sheria akamwambia, “Mwalimu, maneno yako yanatukashifu na sisi pia.”
有一個法學士回答耶穌說:「師傅,你說這些話,連我們也悔辱了。」
46 Yesu akamjibu, “Na ninyi walimu wa Sheria, ole wenu; maana mnawatwika watu mizigo isiyochukulika, huku ninyi wenyewe hamnyoshi hata kidole kuwasaidia.
耶穌說:「禍哉,你們這些法學士! 因為你們加給人不堪負荷的重擔,而你們自己對重擔連一個指頭也不肯動一下。
47 Ole wenu, kwa kuwa mnajenga makaburi ya manabii wale ambao wazee wenu waliwaua.
禍哉,你們! 你們修建先知的墳墓,而你們的祖先卻殺害了他們,
48 Kwa hiyo mnashuhudia na kukubaliana na matendo ya wazee wenu; maana wao waliwaua hao manabii, nanyi mnajenga makaburi yao.
可見你們證明,並讚成你們祖先所行的事,因為他們殺害了先知,而你們卻修建先知的墳墓。
49 Kwa hiyo, Hekima ya Mungu ilisema hivi: Nitawapelekea manabii na mitume, lakini watawaua baadhi yao, na kuwatesa wengine.
為此,天主的智慧曾說過:我將要派遣先知及使者到他們那裏,其中有的,他們要殺死;有的,他們要迫害,
50 Matokeo yake ni kwamba kizazi hiki kitaadhibiwa kwa sababu ya damu ya manabii wote iliyomwagika tangu mwanzo wa ulimwengu;
為使從創造世界以來,所流眾先知的血,都要向這一代追討,
51 tangu kumwagwa damu ya Abeli mpaka kifo cha Zakariya ambaye walimuua kati ya madhabahu na mahali patakatifu. Naam, hakika kizazi hiki kitaadhibiwa kwa matendo haya.
從亞伯爾的血,到喪亡在祭壇與聖所之間的則加黎雅的血,的確,我告訴你們:都要向這一代追討。
52 “Ole wenu ninyi walimu wa Sheria, kwa sababu mmeuficha ule ufunguo wa mlango wa elimu; ninyi wenyewe hamkuingia na mmewazuia waliokuwa wanaingia wasiingie.”
禍哉,你們法學士! 因為你們拿走了智識的鑰匙,自己不進去,那願意進去的,你們也加以阻止。」
53 Alipokuwa akitoka pale, wale Mafarisayo na walimu wa Sheria wakaanza kumshambulia vikali na kumsonga kwa maswali mengi
耶穌從那裏出來以後,經師們同法利賽人開始嚴厲追逼他,盤問他許多的事,
54 ili wapate kumnasa kwa maneno yake.
窺伺他,要從他口中抓到語病。

< Luka 11 >