< Yohana 15 >
1 “Mimi ni mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.
I am the true vine, and my Father is the vine-dresser.
2 Yeye huliondoa ndani yangu kila tawi lisilozaa matunda, na kila tawi lizaalo hulisafisha lipate kuzaa zaidi.
Every branch in me that bears no fruit, he takes away; and every branch that bears fruit, he prunes, that it may bear more fruit.
3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya ule ujumbe niliowaambieni.
Now are you pure, through the word which I have spoken to you.
4 Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Tawi haliwezi peke yake kuzaa matunda lisipokaa katika mzabibu hali kadhalika nanyi hamwezi kuzaa matunda msipokaa ndani yangu.
Abide in me, and I will abide in you. As the branch can not bear fruit of itself, unless it abide in the vine, so neither can you, unless you abide in me.
5 “Mimi ni mzabibu, nanyi ni matawi yake. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo atazaa matunda mengi, maana bila mimi hamwezi kufanya chochote.
I am the vine, you are the branches. He that abides in me and I in him, he will bear much fruit; for apart from me you can do nothing.
6 Mtu yeyote asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi litupwalo nje hata likakauka. Watu huliokota tawi la namna hiyo na kulitupa motoni liungue.
If any one abide not in me, he is thrown out as a branch, and withers; and such are gathered, and thrown into the fire, and burned.
7 Mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, basi, ombeni chochote mtakacho nanyi mtapewa.
If you abide in me, and my words abide in you, you shall ask what you will, and it shall be done for you.
8 Baba yangu hutukuzwa kama mkizaa matunda mengi na kuwa wanafunzi wangu.
In this is my Father glorified, that you bear much fruit; and in this you will be my disciples.
9 Mimi nimewapenda ninyi kama vile Baba alivyonipenda mimi. Kaeni katika pendo langu.
As the Father has loved me, so have I loved you; abide in my love.
10 Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama vile nami nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.
If you keep my commandments, you shall abide in my love, even as I have kept my Father’s commandments, and abide in his love.
11 Nimewaambieni mambo haya ili furaha yangu ikae ndani yenu, na furaha yenu ikamilike.
These things have I spoken to you, that my joy may remain in you, and that your joy may be full.
12 Hii ndiyo amri yangu: pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda ninyi.
This is my commandment: That you love one another, as I have loved you.
13 Hakuna upendo mkuu zaidi kuliko upendo wa mtu atoaye uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.
Greater love has no man than this, that one should lay down his life for his friends.
14 Ninyi ni rafiki zangu mkifanya ninayowaamuru.
You are my friends, if you do whatever I command you.
15 Ninyi siwaiti tena watumishi, maana mtumishi hajui anachofanya bwana wake. Lakini mimi nimewaita ninyi rafiki, kwa sababu nimewajulisha yote ambayo nimeyasikia kutoka kwa Baba yangu.
I no longer call you servants, because the servant knows not what his master does. But I have called you friends; for all things that I have heard from my Father, I have made known to you.
16 Ninyi hamkunichagua mimi; mimi niliwachagueni na kuwatuma mwende mkazae matunda, matunda yadumuyo, naye Baba apate kuwapa ninyi chochote mumwombacho kwa jina langu.
You have not chosen me, but I have chosen you, and appointed you, that you may go and bring forth fruit, and that your fruit may remain; that whatever you ask of the Father in my name, he may give you.
17 Basi, amri yangu kwenu ndiyo hii: pendaneni.
These things I command you, that you may love one another.
18 “Kama ulimwengu ukiwachukia ninyi, kumbukeni kwamba umenichukia mimi kabla haujawachukia ninyi.
If the world hates you, you know that it hated me before it hated you.
19 Kama mngalikuwa watu wa ulimwengu, ulimwengu ungaliwapenda ninyi kama watu wake. Lakini kwa vile ninyi si wa ulimwengu, ila mimi nimewachagueni kutoka ulimwenguni, kwa sababu hiyo ulimwengu unawachukieni.
If you were of the world, the world would love its own. But because you are not of the world, but I have chosen you out of the world, therefore the world hates you.
20 Kumbukeni niliyowaambieni: mtumishi si mkuu zaidi kuliko bwana wake. Ikiwa wamenitesa mimi, watawatesa na ninyi pia; kama wameshika neno langu, watalishika na lenu pia.
Remember the word which I spoke to you, The servant is not greater than his master. If they have persecuted me, they will also persecute you; if they have kept my word, they will keep yours also.
21 Lakini hayo yote watawatendeeni ninyi kwa sababu ya jina langu, kwani hawamjui yeye aliyenituma.
But all these things they will do to you on my account, because they know not him that sent me.
22 Kama nisingalikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia; lakini sasa hawawezi kujitetea kwamba hawana dhambi.
If I had not come and spoken to them, they would not have had sin; but now they have no excuse for their sin.
23 Anayenichukia mimi, anamchukia na Baba yangu pia.
He that hates me, hates my Father also.
24 Kama nisingalifanya kwao mambo ambayo hakuna mtu mwingine amekwisha yafanya wasingalikuwa na hatia; lakini sasa wameona niliyoyafanya wakinichukia mimi, wakamchukia na Baba yangu pia.
If I had not done among them the works that no other man has done, they would have had no sin; but now they have both seen, and hated both me and my Father.
25 Na hivi ni lazima yatimie yale yaliyoandikwa katika Sheria yao: Wamenichukia bure!
But this is so, that the word may be fulfilled which is written in their law, They hated me without a cause.
26 “Atakapokuja huyo Msaidizi nitakayemtuma kwenu kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi.
But when the Paraclete has come, whom I will send to you from my Father, the Spirit of the truth, which proceeds from the Father, he will testify of me;
27 Nanyi pia mtanishuhudia kwa kuwa mmekuwa nami tangu mwanzo.
and you also will testify, because you have been with me from the beginning.