< Wahebrania 6 >

1 Basi, tusonge mbele kwa yale yaliyokomaa na kuyaacha nyuma yale mafundisho ya mwanzo ya Kikristo. Hatuhitaji kuweka msingi tena kwa kurudia yale mafundisho ya mwanzo kama vile kuachana na matendo ya kifo, kumwamini Mungu;
因此,讓我們擱下論基督的初級教理,而努力向成全的課程邁進;不必再樹立基礎,就是講論悔改,死亡的行為,信賴天主
2 mafundisho juu ya ubatizo na kuwekewa mikono; ufufuo wa wafu na hukumu ya milele. (aiōnios g166)
及各種的洗禮,覆手,死者復活和永遠審判的道理。 (aiōnios g166)
3 tusonge mbele! Hayo tutayafanya, Mungu akitujalia.
如果天主准許,我們就這育樣去作。
4 Maana watu wanaoiasi imani yao inawezekanaje kuwarudisha watubu tena? Watu hao walikwisha kuwa katika mwanga wa Mungu, walikwisha onja zawadi ya mbinguni na kushirikishwa Roho Mtakatifu;
的確,那些曾一次被光照,嘗過天上的恩賜,成了有分於聖神,
5 walikwisha onja wema wa neno la Mungu na nguvu za ulimwengu ujao, (aiōn g165)
並嘗過天主甘美的言語,及未來世代德能的人 (aiōn g165)
6 kisha wakaiasi imani yao! Haiwezekani kuwarudisha watubu tena, kwa sababu wanamsulubisha tena Mwana wa Mungu na kumwaibisha hadharani.
如果背棄了正道,再叫衪們自新悔改,是不可能的,因為衪們親自又把天主子釘在十字架上,公開加以凌辱。
7 Mungu huibariki ardhi ambayo huipokea mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuotesha mimea ya faida kwa mkulima.
就如一塊田地,時有雨水降於其上,時受潤澤:若出產有益於那種植者的蔬菜,就必蒙受天主的祝福;
8 Lakini kama ardhi hiyo ikiota miti ya miiba na magugu, haina faida; karibu italaaniwa na Mungu na mwisho wake ni kuchomwa moto.
但若生出荊棘疾藜來,就必被廢棄,必要受詛咒,它的結局就市焚燒。
9 Lakini, ingawa twasema namna hii, wapenzi wetu, tunalo tumaini kubwa juu ya hali yenu. Tunajua kwamba mmepokea baraka zile bora za wokovu wenu.
可是,親愛的諸位,我們雖這樣說,但對你們,我們確信你們將有更好的表現,更近於救恩,
10 Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au upendo mlioonyesha kwa ajili ya jina lake katika huduma mliyowapa na mnayowapa sasa watu wake.
因為天主不是不公義的,甚至於忘掉了你們的善工和愛德,即你們為了衪的名,在過去和現在,在服事聖徒的事上所表現的愛德。
11 Hamu yetu ni kwamba kila mmoja wenu aonyeshe bidii hiyohiyo mpaka mwisho, ili yale mnayotumainia yapate kutimia.
我們只願你們每一位表現同樣的熱,心以答達成你們的希望,一直到底。
12 Msiwe wavivu, bali muwe kama wale wanaoamini na wenye uvumilivu na hivyo wanapokea yake aliyoahidi Mungu.
這樣,你們不但不會懈怠,而且還會效法那些因信德和耐心而繼承恩許的人。
13 Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa jina lake mwenyewe, maana hakuna aliye mkuu kuliko Mungu ambaye kwa huyo angeweza kuapa.
當天主應許亞巴郎的時後,因為沒有一個比天主大而能指著起誓的,就指著自己起誓,
14 Mungu alisema: “Hakika nitakubariki na nitakupa wazawa wengi.”
說:『我必多多祝福你,使你的後裔繁多。
15 Abrahamu alisubiri kwa uvumilivu na hivyo alipokea kile alichoahidiwa na Mungu.
這樣亞巴郎因耐心等待,而獲得了恩許。
16 Watu wanapoapa, huapa kwa mmoja aliye mkuu zaidi kuliko wao, na kiapo hicho husuluhisha ubishi wote.
人都是指著比自己大的起誓;以起誓作擔保,了結一切爭端。
17 Naye Mungu aliimarisha ahadi yake kwa kiapo; na kwa namna hiyo akawaonyesha wazi wale aliowaahidia kwamba hatabadili nia yake.
為此天主願意向繼承恩許的人,充分顯示自己不可更改的旨意,就以起誓來自作擔保,
18 Basi, kuna vitu hivi viwili: ahadi na kiapo, ambavyo haviwezi kubadilika na wala juu ya hivyo Mungu hawezi kusema uongo. Kwa hiyo sisi tuliokimbilia usalama kwake, tunapewa moyo wa kushikilia imara tumaini lililowekwa mbele yetu.
好叫我們這些尋求避難所的人,因這兩種不可更改的事----在這些事上天主決不會撒謊----得到一種強有力的鼓勵,去抓住那擺在目前的希望。
19 Tunalo tumaini hilo kama nanga ya maisha yetu. Tumaini hilo ni imara na thabiti, nalo lapenya lile pazia la hekalu la mbinguni mpaka patakatifu ndani.
我們拿這希望,當作靈魂的安全而又堅固的錨,深深地拋入帳幔的內部。
20 Yesu ametangulia kuingia humo kwa niaba yetu, na amekuwa kuhani mkuu milele, kufuatana na utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki. (aiōn g165)
作前驅的耶穌已為我們進入了那帳幔內部,按照默基瑟德品位做了永遠的大司祭。 (aiōn g165)

< Wahebrania 6 >