< Wahebrania 3 >
1 Ndugu zangu watu wa Mungu ambao mmeitwa na Mungu, fikirini juu ya Yesu ambaye Mungu alimtuma awe Kuhani Mkuu wa imani tunayoiungama.
Therefore, holy brothers, partakers of a heavenly calling, consider the Apostle and High Priest of our confession: Jesus,
2 Yeye alikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemteua kufanya kazi yake kama vile Mose alivyokuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu.
who was faithful to him who appointed him, as also Moses was in all his house.
3 Mjenzi wa nyumba hupata heshima zaidi kuliko hiyo nyumba yenyewe. Hali kadhalika naye Yesu anastahili heshima kubwa zaidi kuliko Mose.
For he has been counted worthy of more glory than Moses, because he who built the house has more honor than the house.
4 Kila nyumba hujengwa na mjenzi fulani—na Mungu ndiye mjenzi wa vitu vyote.
For every house is built by someone; but he who built all things is God.
5 Mose alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Bwana kama mtumishi, na alinena juu ya mambo ambayo Mungu atayasema hapo baadaye.
Moses indeed was faithful in all his house as a servant, for a testimony of those things which were afterward to be spoken,
6 Lakini Kristo ni mwaminifu kama Mwana mwenye mamlaka juu ya nyumba ya Mungu. Sisi ni nyumba yake kama tukizingatia uhodari wetu na uthabiti wetu katika kile tunachotumainia.
but Christ is faithful as a Son over his house. We are his house, if we hold fast our confidence and the glorying of our hope firm to the end.
7 Kwa hiyo, basi, kama asemavyo Roho Mtakatifu: “Kama mkisikia sauti ya Mungu leo,
Therefore, even as the Holy Spirit says, “Today if you will hear his voice,
8 msiifanye mioyo yenu kuwa migumu kama wazee wenu walivyokuwa wakati walipomwasi Mungu; kama walivyokuwa siku ile kule jangwani,
do not harden your hearts as in the rebellion, in the day of the trial in the wilderness,
9 Huko wazee wenu walinijaribu na kunichunguza, asema Bwana, ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu kwa miaka arobaini.
where your fathers tested me and tried me, and saw my deeds for forty years.
10 Kwa sababu hiyo niliwakasirikia watu hao nikasema, Fikira za watu hawa zimepotoka, hawajapata kamwe kuzijua njia zangu.
Therefore I was displeased with that generation, and said, ‘They always err in their heart, but they did not know my ways.’
11 Basi, nilikasirika, nikaapa: Hawataingia huko ambako ningewapa pumziko.”
As I swore in my wrath, ‘They will not enter into my rest.’”
12 Basi ndugu, jihadharini asije akawako yeyote miongoni mwenu aliye na moyo mbaya hivyo na asiyeamini hata kujitenga na Mungu aliye hai.
Beware, brothers, lest perhaps there might be in any one of you an evil heart of unbelief, in falling away from the living God;
13 Maadamu hiyo “Leo” inayosemwa katika Maandiko bado inatuhusu sisi, mnapaswa kusaidiana daima, ili mtu yeyote miongoni mwenu asidanganywe na dhambi na kuwa mkaidi.
but exhort one another day by day, so long as it is called “today”, lest any one of you be hardened by the deceitfulness of sin.
14 Maana sisi tunashirikiana na Kristo ikiwa tutazingatia kwa uthabiti tumaini tulilokuwa nalo mwanzoni.
For we have become partakers of Christ, if we hold the beginning of our confidence firm to the end,
15 Maandiko yasema hivi: “Kama mkisikia sauti ya Mungu leo, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu kama wazee wenu walivyokuwa wakati walipomwasi Mungu.”
while it is said, “Today if you will hear his voice, do not harden your hearts, as in the rebellion.”
16 Ni akina nani basi, waliosikia sauti ya Mungu wakamwasi? Ni wale wote walioongozwa na Mose kutoka Misri.
For who, when they heard, rebelled? Was not it all those who came out of Egypt led by Moses?
17 Mungu aliwakasirikia akina nani kwa miaka arobaini? Aliwakasirikia wale waliotenda dhambi, maiti zao zikatapakaa kule jangwani.
With whom was he displeased forty years? Was not it with those who sinned, whose bodies fell in the wilderness?
18 Mungu alipoapa: “Hawataingia huko ambako ningewapa pumziko,” alikuwa anawasema akina nani? Alikuwa anasema juu ya hao walioasi.
To whom did he swear that they would not enter into his rest, but to those who were disobedient?
19 Basi, twaona kwamba hawakuingia huko kwa sababu hawakuamini.
We see that they were not able to enter in because of unbelief.