< Wahebrania 13 >

1 Endeleeni kupendana kidugu.
Let brotherly love continue.
2 Msisahau kuwakaribisha wageni; maana kwa kufanya hivyo watu wengine walipata kuwakaribisha malaika bila kujua.
Do not forget hospitality to strangers, for in doing so some have entertained angels without knowing it.
3 Wakumbukeni wale waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao. Wakumbukeni wale wanaoteseka kana kwamba nanyi mnateseka kama wao.
Remember the prisoners as if chained with them, those who are being mistreated as if you yourselves were physically there.
4 Ndoa inapaswa kuheshimiwa na watu wote, na haki zake zitekelezwe kwa uaminifu. Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi.
Marriage is honorable among all and the marriage bed undefiled, but God will judge fornicators and adulterers.
5 Msiwe watu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitu mlivyo navyo. Mungu mwenyewe amesema: “Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa.”
Your way of life should be free from the love of money, being content with what you have, because He Himself has said: “I absolutely will not desert you; I most certainly will not abandon you.”
6 Ndiyo maana tunathubutu kusema: “Bwana ndiye msaada wangu, sitaogopa. Binadamu atanifanya nini?”
So we can say with confidence: “The Lord is my helper; I will not fear. What can man do to me?”
7 wakumbukeni viongozi wenu waliowatangazieni ujumbe wa Mungu. Fikirieni juu ya mwenendo wao, mkaige imani yao.
Remember your leaders, those who spoke the Word of God to you, whose faith imitate, considering the outcome of their conduct.
8 Yesu Kristo ni yuleyule, jana, leo na milele. (aiōn g165)
Jesus Christ is Himself, yesterday and today and into the ages. (aiōn g165)
9 Msipeperushwe huku na huku kwa mafundisho tofauti ya kigeni. Neema ya Mungu ndiyo inayoimarisha roho zetu na wala si masharti juu ya chakula; masharti hayo hayakumsaidia kamwe mtu yeyote aliyeyafuata.
Do not be carried away by various and strange teachings, because it is good that the heart be established by grace, not foods, by which those who were so occupied were not benefited.
10 Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaotumikia bado katika hema la Wayahudi, hawana haki ya kula vitu vyake.
We have an altar from which those who serve in the Tabernacle have no right to eat.
11 Kuhani Mkuu wa Kiyahudi huleta damu ya wanyama katika Mahali Patakatifu na kuitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi; lakini nyama za hao wanyama huteketezwa nje ya kambi.
Because the bodies of the animals—whose blood, concerning sin, is brought into the Holies by the high priest—are burned up outside the camp,
12 Ndiyo maana Yesu pia, kusudi apate kuwatakasa watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa na kufa nje ya mji.
therefore Jesus also, so that He might sanctify the people by His own blood, suffered outside the city gate.
13 Basi, tumwendee huko nje ya kambi tukajitwike laana yake.
So then, let us go out to Him, outside the camp, bearing His disgrace;
14 Maana hapa duniani hatuna mji wa kudumu; lakini tunautafuta ule unaokuja.
because here we do not have a permanent city, but we seek the coming one.
15 Basi, kwa njia ya Yesu, tumtolee Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani sifa zinazotolewa na midomo inayoliungama jina lake.
Through Him therefore, at all times, let us offer up a sacrifice of praise to God—the fruit of lips that identify with His name.
16 Msisahau kutenda mema na kusaidiana, maana hizi ndizo dhabihu zinazompendeza Mungu.
(But do not forget to do good and to share, for with such sacrifices God is pleased.)
17 Watiini viongozi wenu na kushika amri zao; wao huchunga roho zenu usiku na mchana, na watatoa ripoti ya utumishi wao mbele ya Mungu. Kama mkiwatii watafanya kazi zao kwa furaha, la sivyo, watazifanya kwa huzuni, na hiyo haitakuwa na faida kwenu.
Obey your leaders and submit, for they keep watch over your souls, as those who must give account, so that they may do it with joy and not sighing (which would be unprofitable for you).
18 Tuombeeni na sisi. Tuna hakika kwamba tunayo dhamiri safi, maana twataka kufanya lililo sawa daima.
Pray for us; for we are confident that we have a good conscience, desiring to live commendably in all things;
19 Nawasihi sana mniombee ili Mungu anirudishe kwenu upesi iwezekanavyo.
I especially urge you to do this so that I may be restored to you more quickly.
20 Mungu amemfufua Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Mchungaji Mkuu wa kondoo kwa sababu ya kumwaga damu yake iliyothibitisha agano la milele. (aiōnios g166)
Now may the God of peace—who through the blood of the eternal covenant brought back from the dead our Lord Jesus, that great Shepherd of the sheep— (aiōnios g166)
21 Mungu wa amani awakamilishe katika kila tendo jema ili mtekeleze mapenzi yake; yeye na afanye ndani yetu kwa njia ya Kristo yale yanayompendeza mwenyewe. Utukufu uwe kwake, milele na milele! Amina. (aiōn g165)
equip you for every good work to do His will, working in you what is well pleasing in His sight, through Jesus Christ, to whom be the glory forever and ever. Amen. (aiōn g165)
22 Basi, ndugu, nawasihi mpokee kwa utulivu ujumbe huu wa kuwatieni moyo. Hii ni barua fupi tu ambayo nimewaandikieni.
Now I appeal to you, brothers, bear with this word of exhortation, for I have written to you in few words.
23 Napenda kuwajulisheni kwamba ndugu yetu Timotheo amekwisha funguliwa gerezani. Kama akifika hapa mapema, nitakuja naye nitakapokuja kwenu.
Know that brother Timothy has been released, with whom I will see you, if he comes quickly.
24 Wasalimieni viongozi wenu wote pamoja na watu wa Mungu! Ndugu wa Italia wanawasalimuni.
Greet all your leaders and all the saints. Those from Italy greet you.
25 Tunawatakieni nyote neema ya Mungu.
The Grace be with you all. Amen.

< Wahebrania 13 >