< Wahebrania 11 >
1 Kuwa na imani ni kuwa na hakika ya mambo tunayotumainia; kusadiki kabisa mambo tusiyoyaona.
德是所希望之事的擔保,是未見之事的確證。
2 Maana wazee wa kale walipata kibali cha Mungu kwa sababu ya imani yao.
因這信德,先人們都曾得了褒揚。
3 Kwa imani sisi tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu; vitu vinavyoonekana kutoka vitu visivyoonekana. (aiōn )
因著信德,我們知道普世是藉天主的形成,看得見的是由看不見的化成的。 (aiōn )
4 Kwa imani Abeli alimtolea Mungu dhabihu iliyokuwa bora zaidi kuliko ile ya Kaini. Kwa imani yake alikubaliwa na Mungu kuwa mwadilifu; Mungu mwenyewe alizikubali sadaka zake. Kwa imani yake ingawa amekufa, bado ananena.
因著信德,亞伯爾向天主奉獻了比加音因高貴的祭品;因著信德,因著信德,亞伯爾被褒揚為義人,因為有天主為衪的供品作證;因這信德,衪雖死了,卻仍發言。
5 Kwa imani Henoki alichukuliwa na Mungu, asipate kufa. Hakuonekana tena kwa sababu Mungu alikuwa amemchukua. Maandiko yasema kwamba kabla ya kuchukuliwa kwake, yeye alikuwa amempendeza Mungu.
因著信德,哈諾客被接去了,叫他不見死亡,世人也找不著他了,因為天主已將他接去;原來被接去之前,已有了中悅天主的明證
6 Basi, pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwa maana kila mtu anayemwendea Mungu ni lazima aamini kwamba Mungu yuko, na kwamba huwatuza wale wanaomtafuta.
沒有信德是不可能中悅天主的因為凡接近天主的人,應該信衪存在,且信衪對信衪的人是賞報者。
7 Kwa imani Noa alionywa na Mungu juu ya mambo ya baadaye ambayo hakuweza kuyaona bado. Alimtii Mungu, akajenga ile safina ambamo aliokolewa yeye pamoja na jamaa yake. Kutokana na hayo ulimwengu ulihukumiwa, naye Noa akapokea uadilifu unaotokana na imani.
因著信德,諾厄對尚未見得的事得了啟示,懷著敨畏製造了方舟,為自己的家庭;因著信德,衪定了世界的罪,且成了由信德得正義的承繼者。
8 Kwa imani Abrahamu alimtii Mungu alipoitwa aende katika nchi ambayo Mungu angempa iwe yake. Ingawa hakujua alikokuwa anakwenda, Abrahamu alihama.
因著信德,亞巴郎一蒙召選,就聽命往他將要承受為產業的地方去了:他出走時,還不知道要到那裏去。
9 Kwa imani aliishi kama mgeni katika nchi aliyoahidiwa na Mungu. Aliishi huko katika hema kama walivyoishi Isaka na Yakobo, ambao pia walishiriki ahadi ileile.
因著信德,他旅居在所應許的地域,好像是在外邦,與有同樣恩許的承繼人依撒格和雅各伯寄居在帳幕內,
10 Maana Abrahamu alikuwa akingojea mji wenye misingi imara, mji ambao Mungu mwenyewe ndiye fundi aliyeubuni na kuujenga.
因為他期待著那有堅固基礎的城,此城的工程師和建築師是天主。
11 Kwa imani hata Sara aliamini kwamba Mungu hutimiza ahadi zake, kwa hiyo akajaliwa kuchukua mimba ingawaje alikuwa amepita umri.
因著信德,連石女撒辣雖然過了適當的年齡,也蒙受了懷孕生子的能力,因為她相信那應許者是忠信的。
12 Kwa hiyo, kutoka katika mtu huyo mmoja, Abrahamu, ambaye alikuwa kama amekufa, walitokea watu wengi wasiohesabika kama vile nyota za mbinguni na mchanga wa pwani.
為此由一個人,且是由一個已近於死的人,生了子孫,有如天上的星辰那麼多,又如海岸上的沙粒那麼不可勝數。
13 Watu hawa wote walikufa wakiwa na imani. Walikufa kabla ya kupokea mambo ambayo Mungu alikuwa ameahidi, lakini kwa mbali waliyaona, wakashangilia, na kukiri wazi kwamba wao walikuwa wageni na wakimbizi duniani.
這些人都懷著信德死了,沒有獲得所恩許的,只由遠處觀望,表示歡迎明認自己在世上只是外方人和旅客。
14 Watu wanaosema mambo kama hayo, huonyesha wazi kwamba wanaitafuta nchi yao wenyewe.
的確,那些說這樣話的人,表示自己是在尋求一個家鄉。
15 Kama wangalikuwa wanaifikiria nchi walikotoka zamani, wangalipata nafasi ya kurudi huko.
如果他們是懷念所離開的家鄉,他們還有返回的機會;
16 Lakini sasa wanataka nchi iliyo bora zaidi, yaani nchi ya mbinguni. Ndiyo maana Mungu haoni haya wakimwita yeye Mungu wao, kwa sababu yeye mwenyewe amekwisha watayarishia mji.
其實他們如今所渴望的,實是一個更美麗的家鄉,即天上的家鄉。為此,天主自稱是他們的天主,不以他們為羞恥,因為衪已給他們準備了一座城。
17 Kwa imani, Abrahamu alimtoa mwanae Isaka sadaka wakati Mungu alipomjaribu. Huyo Abrahamu ndiye aliyekuwa amepokea ahadi ya Mungu, lakini, hata hivyo, alikubali kumtoa dhabihu mwanae wa pekee,
因著信德,亞巴郎在受試探的時候,獻上了依撒格,就是那承受了恩許的人,獻上了自己的獨生子;
18 ingawa Mungu alikuwa amemwambia: “Wazawa wako watatokana na Isaka.”
原來天主曾向他說過:『只有由依撒格所生的,才稱為你的後裔。』
19 Abrahamu aliamini kwamba Mungu anaweza kuwafufua wafu: na kwa namna fulani kweli Abrahamu alimpata tena mwanae kutoka wafu.
他想天主也有使人從死者中復活的能力,為此他又把依撒格得了回來以作預像。
20 Kwa imani Isaka aliwabariki Yakobo na Esau, wapate baraka zitakazokuja baadaye.
因著信德,依撒格也關於未來的事是有福的,因為祝福了雅各伯和厄撒烏。
21 Kwa imani Yakobo alipokuwa karibu kufa, aliwabariki kila mmoja wa wana wa Yosefu, akamwabudu Mungu akiegemea ile fimbo yake.
因著信德,臨死的雅各伯祝福了若瑟的每一個兒子,也扶著若瑟的扙頭朝拜了天主。
22 Kwa imani Yosefu alipokuwa karibu kufa, alinena juu ya kutoka kwa Waisraeli katika nchi ya Misri, na pia akawaachia maagizo kuhusu mifupa yake.
因著信德,臨終的若瑟提及以色列子民出離埃及的事,並對他自己的骨骸有所吩咐。
23 Kwa imani wazazi wa Mose walimficha huyo mtoto kwa muda wa miezi mitatu baada ya kuzaliwa kwake. Walimwona kuwa ni mtoto mzuri, wala hawakuiogopa amri ya mfalme.
因著信德,梅瑟一誕生就被他父母隱藏了三個月,因為他們見嬰孩俊美,便不怕君王的諭令。
24 Kwa imani Mose alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mwana wa binti Farao.
因著信德,梅瑟長大以後,拒絕被稱為法郎公主的兒子,
25 Aliona ni afadhali kuteseka pamoja na watu wa Mungu kuliko kufurahia raha ya dhambi kwa kitambo kidogo.
他寧願同天主的百姓一起受苦,也不願有犯罪的暫時享受,
26 Alitambua kwamba kuteseka kwa ajili ya Masiha kuna faida kubwa zaidi kuliko utajiri wote wa nchi ya Misri, maana alikuwa anatazamia tuzo la baadaye.
因為他以默西亞的恥辱比埃及的寶藏更為寶貴,因為他所注目的是天主的賞報。
27 Kwa imani Mose alihama kutoka nchi ya Misri bila kuogopa hasira ya mfalme; na wala hakurudi nyuma, kwani alikuwa kama mtu aliyemwona yule Mungu asiyeonekana.
因著信德,他不害怕君王的憤怒,而離開了埃及,因為他好像看見了那看不見的一位,而堅定不移。
28 Kwa imani aliadhimisha siku ya Pasaka, akaamuru damu inyunyizwe juu ya milango, ili yule Malaika Mwangamizi asiwaue wazaliwa wa kwanza wa Israeli.
因著信德,他舉行了逾越節,行了灑血禮,免得那消滅首生者觸犯以色列子民的首生者。
29 Kwa imani watu wa Israeli walivuka bahari ya Shamu, kana kwamba ilikuwa nchi kavu; lakini Wamisri walipojaribu kufanya hivyo walikufa maji.
因著信德,他們渡過了紅海,如過旱地;埃及人一嘗試,就被淹沒了。
30 Kwa imani kuta za mji wa Yeriko zilianguka watu wa Israeli walipokwisha zunguka kwa muda wa siku saba.
因著信德,耶利哥城牆,被繞行七天之後,就倒塌了。
31 Kwa imani Rahabu aliyekuwa malaya hakuangamia pamoja na wale waliomwasi Mungu, kwa sababu aliwakaribisha wale wapelelezi.
因著信德,妓女辣哈布平安地接待了偵探,沒有同抗命的人一起滅亡。
32 Basi, niseme nini zaidi? Wakati hauniruhusu kueleza juu ya Gedeoni, Baraki, Samsoni, Yeftha, Daudi, Samweli na manabii.
此外,我還說什麼呢﹖我的確沒有足夠時間再論述基德紅、巴辣克、三松、依弗大、達味和撒慕爾以及眾先知的事:
33 Kwa imani hawa wote walipigana vita na wafalme, wakashinda. Walitenda mambo adili, wakapokea yale aliyoahidi Mungu. Walifunga vinywa vya simba,
他們藉著信德征服列國,執行正義,得到恩許,杜往獅子的口,
34 Walizima mioto mikali, waliepuka kuuawa kwa upanga. Walikuwa dhaifu lakini walipata nguvu. Walikuwa hodari katika vita wakashinda majeshi ya kigeni.
熄滅烈火的威力,逃脫利劍,轉弱為強,成為戰爭中的英雄,擊潰外國的軍隊。
35 Na, wanawake walioamini walirudishiwa wafu wao wakiwa wamefufuliwa. Baadhi yao walikataa kufunguliwa, wakateswa mpaka kufa ili wapate kufufuliwa na kuingia katika maisha bora zaidi.
有些女人得了她們的復活,有些人受了酷刑拷打,不願接受釋放,為獲得更好的復活;
36 Wengine walidhihakiwa na kupigwa mijeledi, na wengine walifungwa minyororo na kutupwa gerezani.
另有些人受了淩辱和鞭打,甚至鎖押和監禁,
37 Walipigwa mawe, walipasuliwa vipandevipande, waliuawa kwa upanga. Walizungukazunguka wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi, walikuwa watu maskini, walioteswa na kudhulumiwa.
被石頭砸死,被鋸死死,被拷問,被利劍殺死,披著山羊皮到處流浪,受貧乏,受磨難,受虐待。
38 Ulimwengu haukustahili kuwa na watu hao. Walitangatanga jangwani na mlimani, wakaishi katika mashimo na mapango ya ardhi.
世界原配不上他們,他們遂在曠野、山嶺、山洞和地中穴中漂流無定。
39 Watu hawa wote walionekana kuwa mashujaa kwa sababu ya imani yao. Hata hivyo, hawakupokea yale ambayo Mungu aliwaahidia,
這一切人雖然因著信德獲得了褒揚,但是沒有獲得恩許的,
40 maana Mungu alikuwa ameazimia mpango ulio bora zaidi kwa ajili yetu; yaani wao wangeufikia ukamilifu wakiwa pamoja nasi.
因為天主早己為我們預備了一種更好的事,以致若沒有我們,他們決得不到成全。