< Waefeso 1 >
1 Mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, nawaandikia ninyi watu wa Mungu huko Efeso, mlio waaminifu katika kuungana na Kristo Yesu.
Paul, an apostle of Jesus Christ by the will of God, to the saints who are in Ephesus and to the faithful in Christ Jesus,
2 Nawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
grace to you and peace from God our father and the Lord Jesus Christ.
3 Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Maana, katika kuungana na Kristo ametubariki kwa kutujalia zawadi zote za kiroho mbinguni.
Blessed be the God and Father of our Lord Jesus Christ, who has blessed us in every spiritual blessing in the heavenly realms in Christ.
4 Kabla ya kuumbwa ulimwengu, Mungu alituteua tuwe wake katika kuungana na Kristo ili tuwe watakatifu na bila hitilafu mbele yake. Kwa sababu ya upendo wake,
Even as he chose us in him before the foundation of the world to be holy and without blemish in his sight.
5 Mungu alikuwa ameazimia tangu zamani kutuleta kwake kama watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo. Ndivyo alivyopenda na kunuia.
For in his love he predestined us (such was the good pleasure of his will) to adoption for himself as sons through Jesus Christ,
6 Basi, tumsifu Mungu kwa sababu ya neema yake tukufu katika Mwanae mpenzi!
and to the praise of his glorious grace which he graciously bestowed upon us in the Beloved.
7 Maana kwa damu yake Kristo sisi tunakombolewa, yaani dhambi zetu zinaondolewa. Ndivyo ulivyo ukuu wa neema yake
It is in him we have deliverance, the forgiveness of our trespasses, through his blood;
8 aliotukirimia bila kipimo! Kwa hekima na ujuzi wake wote
so abundantly did he lavish upon us the riches of his grace in all wisdom and understanding,
9 Mungu alitekeleza kile alichonuia, akatujulisha mpango wake uliofichika, ambao alikuwa ameazimia kuutekeleza kwa njia ya Kristo.
when he made known to us, I say, that good pleasure which he purposed in himself
10 Mpango huo ambao angeutimiza wakati utimiapo ni kukusanya pamoja viumbe vyote, kila kitu mbinguni na duniani, chini ya Kristo.
for the government of the fulness of the ages, that all things in heaven and earth are alike should be gathered up in Christ, as Head.
11 Kila kitu hufanywa kufuatana na mpango na uamuzi wa Mungu; naye Mungu ametuteua sisi tuwe watu wake kwa mapenzi yake katika kuungana na Kristo, kufuatana na azimio alilofanya tangu mwanzo.
It is he in whom we Jews also have our inheritance, having been chosen beforehand according to the purpose of Him who executes all things according to the counsel of his will,
12 Basi, sisi tuliotangulia kumtumainia Kristo tunapaswa kuusifu utukufu wa Mungu!
that we who first hoped in Christ should be for the praise of his glory.
13 Nanyi pia watu wa mataifa mengine, mliusikia ujumbe wa kweli yaani Habari Njema iliyowaletea wokovu, mkamwamini Kristo; naye Mungu, ili kuonyesha kuwa ninyi ni wake, akawapiga mhuri kwa kuwapeni yule Roho Mtakatifu aliyetuahidia.
And in him, because you listened to the proclamation of the truth, the evangel of your salvation, and trusted it, you Gentiles too were sealed with the promised Holy Spirit,
14 Huyu Roho ni dhamana ya kurithi yote yale Mungu aliyowaahidia watu wake, na jambo hili latuhakikishia kwamba Mungu atawakomboa kabisa wote walio wake. Tuusifu utukufu wake!
who for the praise of his glory is the pledge of our common heritage, unto the complete redemption of his purchased property.
15 Kwa sababu hiyo, tangu niliposikia juu ya imani yenu kwa Bwana Yesu na mapendo yenu kwa watu wa Mungu,
For this reason I also, from the time when I heard of the faith in the Lord Jesus which prevails among you, and your love to all the saints,
16 sijaacha kamwe kumshukuru Mungu kwa ajili yenu. Ninawakumbuka katika sala zangu
do not cease to praise God for you, whenever I mention you in my prayers.
17 ili Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo Baba mtukufu, awajalieni Roho wake atakayewapa hekima na kuwafunulieni Mungu mpate kumjua.
I am praying that the God of our Lord Jesus Christ, the Father most glorious, may grant you a spirit of wisdom and revelation, through an intimate knowledge of himself;
18 Namwomba Mungu aifunue mioyo yenu iweze kuuona mwanga wake, mpate kutambua lile tumaini alilowaitieni na utukufu mkuu wa zawadi alizowawekea watu wake,
and that the eyes of your heart may be flooded with light so that you may understand what is the hope of his calling, what the wealth of the glory of his inheritance in the saints,
19 mpate kutambua jinsi uwezo wake ulivyo mkuu mno kwa ajili yetu sisi tunaoamini. Uwezo huo unaofanya kazi ndani yetu, ni sawa na nguvu ile kuu mno
and what the surpassing greatness of his might in us who believe, as seen in the energy of that resistless might
20 aliyomfufua nayo Kristo kutoka wafu, akamketisha kulia kwake mbinguni.
which he exercised in raising Christ from the dead, and in seating him at his right hand in the heavenly heights,
21 Huko, Kristo anatawala juu ya kila tawala, mamlaka, enzi na ukuu; anatawala juu ya kila cheo kiwezacho kutajwa katika ulimwengu huu na katika ulimwengu ujao. (aiōn )
far above all hierarchies and authorities and powers and dominions and every name that is named, not only in this age but in that which is to come. (aiōn )
22 Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake, akamkabidhi kwa kanisa akiwa mkuu wa vitu vyote.
God has put all things under Christ’s feet, and placed him as Head over all in the church,
23 Kanisa ni mwili wa Kristo, na ukamilifu wake yeye anayekamilisha vitu vyote kila mahali.
which is his body, the fulness of Him who fills the universe.