< Waefeso 6 +

1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu Kikristo maana hili ni jambo jema.
Children, obey your parents in the Lord: for this is right.
2 “Waheshimu Baba na mama yako,” hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani,
Honour thy father and mother; ( which is the first commandment with promise; )
3 “Upate fanaka na miaka mingi duniani.”
That it may be well with thee, and thou mayest live long on the earth.
4 Nanyi akina baba, msiwachukize watoto wenu ila waleeni katika nidhamu na mafundisho ya Kikristo.
And, ye fathers, provoke not your children to wrath: but bring them up in the nurture and admonition of the Lord.
5 Enyi watumwa, watiini mabwana zenu hapa duniani kwa hofu na tetemeko; fanyeni hivyo kwa unyofu wa moyo kana kwamba mnamtumikia Kristo.
Servants, be obedient to them that are your masters according to the flesh, with fear and trembling, in singleness of your heart, as to Christ;
6 Fanyeni hivyo si tu wakati wanapowatazama ili mjipendekeze kwao, bali tumikieni kwa moyo kama atakavyo Mungu kwa sababu ninyi ni watumishi wa Kristo.
Not with eyeservice, as menpleasers; but as the servants of Christ, doing the will of God from the heart;
7 Muwe radhi kutumikia kwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya watu.
With good will doing service, as to the Lord, and not to men:
8 Kumbukeni kwamba kila mtu mwenye kutenda mema, awe mtumwa au mtu huru, atapokea tuzo lake kutoka kwa Bwana.
Knowing that whatever good thing any man doeth, the same shall he receive from the Lord, whether he be bond or free.
9 Nanyi mnaotumikiwa, watendeeni vivyo hivyo watumwa wenu, na acheni kutumia vitisho. Kumbukeni kwamba ninyi pia kama vile wao, mnaye Bwana yuleyule mbinguni, kwake cheo cha mtu si kitu.
And, ye masters, do the same things to them, forbearing threatening: knowing that your Master also is in heaven; neither is there respect of persons with him.
10 Hatimaye, nawatakeni muwe imara katika kuungana na Bwana na kwa msaada wa nguvu yake kuu.
Finally, my brethren, be strong in the Lord, and in the power of his might.
11 Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi.
Put on the whole armour of God, that ye may be able to stand against the wiles of the devil.
12 Maana vita vyenu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu wanaomiliki ulimwengu huu wa giza. (aiōn g165)
For we wrestle not against flesh and blood, but against principalities, against powers, against the rulers of the darkness of this world, against spiritual wickedness in high places. (aiōn g165)
13 Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika muweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, muwe bado thabiti.
Therefore take up the whole armour of God, that ye may be able to withstand in the evil day, and having done all, to stand.
14 Basi, simameni imara! Ukweli uwe kama ukanda kiunoni mwenu, uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani,
Stand therefore, having your loins girt about with truth, and having on the breastplate of righteousness;
15 na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu.
And your feet shod with the preparation of the gospel of peace;
16 Zaidi ya hayo yote, imani iwe daima kama ngao mikononi mwenu, iwawezeshe kuizima mishale ya moto ya yule Mwovu.
Above all, taking the shield of faith, with which ye shall be able to put out all the fiery darts of the wicked.
17 Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno la Mungu kama upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu.
And take the helmet of salvation, and the sword of the Spirit, which is the word of God:
18 Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati kwa nguvu ya Roho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa Mungu.
Praying always with all prayer and supplication in the Spirit, and watching for this purpose with all perseverance and supplication for all saints;
19 Niombeeni nami pia ili niongeapo Mungu anijalie cha kusema, niweze kuwajulisha watu fumbo la Habari Njema kwa uthabiti.
And for me, that utterance may be given to me, that I may open my mouth boldly, to make known the mystery of the gospel,
20 Mimi ni balozi kwa ajili ya Habari Njema hiyo ingawa sasa niko kifungoni. Ombeni, basi, ili niweze kuwa hodari katika kuitangaza kama inipasavyo.
For which I am an ambassador in bonds: that in it I may speak boldly, as I ought to speak.
21 Tukiko, ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifu wa Bwana, atawapeni habari zangu zote mpate kujua ninachofanya.
But that ye also may know my affairs, and how I do, Tychicus, a beloved brother and faithful minister in the Lord, shall make known to you all things:
22 Namtuma kwenu awapeni habari zetu mpate kuwa na moyo.
Whom I have sent to you for the same purpose, that ye may know our affairs, and that he may comfort your hearts.
23 Ninawatakieni ninyi ndugu amani, upendo na imani kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo.
Peace be to the brethren, and love with faith, from God the Father and the Lord Jesus Christ.
24 Nawatakia neema ya Mungu wote wanaompenda Bwana wetu Yesu Kristo kwa mapendo yasiyo na mwisho.
Grace be with all them that love our Lord Jesus Christ in sincerity. Amen. To the Ephesians written from Rome, by Tychicus.

< Waefeso 6 +