< Waefeso 2 >
1 Ninyi mlikuwa mmekufa kwa sababu ya makosa na dhambi zenu.
你們從前因著你們的過犯和罪惡是死的;
2 Wakati ule mliishi kufuatana na mtindo mbaya wa ulimwengu huu, mkawa mnamtii mtawala wa pepo wenye nguvu wa anga, pepo ambao huwatawala sasa watu wasiomtii Mungu. (aiōn )
那時你們生活在過犯罪惡中,跟隨這世界的風氣,順從空中權能的首領,即現今在悖逆之子身上發生作用的惡神。 (aiōn )
3 Na hata sisi sote tulikuwa kama wao; tuliishi kufuatana na tamaa zetu za kidunia na kufanya tu mambo yale yaliyoipendeza miili na akili zetu. Kidunia, sisi kama vile pia wao, tulistahili ghadhabu ya Mungu.
就連我們從前也都在這樣環境中生活過,放縱肉身的私慾,照肉身和心意所喜好的行事,且生來就是易怒之子,和別人一樣。
4 Lakini Mungu ni mwenye huruma nyingi. Alitupenda kwa mapendo yasiyopimika,
然而富於慈悲的天主,因著祂愛我們的大愛,
5 hata, ingawa tulikuwa tumekufa kwa sababu ya dhambi, alitufanya hai pamoja na Kristo. Kwa neema ya Mungu ninyi mmeokolewa.
竟在我們因過犯死了的時候,使我們同基督一起生活──可見你們得救,是由於恩寵──
6 Kwa kuungana na Kristo Yesu, Mungu alitufufua pamoja naye, tukatawale pamoja naye mbinguni.
且使我們同祂一起復活,在基督耶穌內使我們同祂一起坐在天上,
7 Ndivyo alivyopenda kuonyesha kwa watu wa nyakati za baadaye, ukuu wa neema yake aliyotujalia kwa ukarimu katika kuungana kwetu na Kristo Yesu. (aiōn )
為將自己無限豐富的恩寵,即祂在基督耶穌內,對我們所懷有的慈惠,顯示給未來的世代。 (aiōn )
8 Maana, kwa neema ya Mungu mmekombolewa kwa njia ya imani. Jambo hili si matokeo ya juhudi zenu, bali ni zawadi ya Mungu.
因為你們得救是由於恩寵,藉著信德,所以信德並不是出於你們自己,而是天主的恩惠;
9 Wala halitokani na matendo yenu wenyewe, asije mtu akajivunia kitu.
不是出於功行,免得有人自誇。
10 Sisi ni viumbe vyake Mungu, na kwa kuungana na Kristo Yesu, alituumba kwa ajili ya kuishi maisha ya matendo mema aliyotutayarishia tuyatende.
原來我們是祂的化工,是在基督耶穌內受造的,為行天主所預備的各種善工,叫我們在這些善工中度日。
11 Ninyi mlio kwa asili watu wa mataifa mengine—mnaoitwa, “wasiotahiriwa” na Wayahudi ambao hujiita, “Waliotahiriwa,” (kwa sababu ya kile wanachoifanyia miili yao) —kumbukeni mlivyokuwa zamani.
所以你們應該記得,你們從前生來本是外邦人,被那些受割損的人──割損本是人手在肉身上所行的──稱為未受割損的人;
12 Wakati ule ninyi mlikuwa bila Kristo; mlikuwa nje ya jamii ya Israeli; mlikuwa wageni na hamkuwa na sehemu yoyote katika lile agano la zile ahadi. Mlikuwa bila matumaini Mungu hapa duniani.
記得你們那時沒有默西亞,與以色列社團隔絕,對恩許的盟約是局外人,在這世界上沒有希望,沒有天主。
13 Lakini sasa, kwa kuungana na Kristo Yesu, ninyi ambao hapo awali mlikuwa mbali, mmekaribishwa kwa njia ya damu yake Kristo.
但是現今在基督耶穌內,你們從前遠離天主的人,藉著基督的血,成為親近的了。
14 Maana Kristo mwenyewe ametuletea amani kwa kuwafanya Wayahudi na watu wa mataifa mengine kuwa jamii moja. Kwa mwili wake yeye mwenyewe aliubomoa ule ukuta uliowatenganisha na kuwafanya maadui.
因為基督是我們的和平,祂使雙方合而為一;祂以自己的肉身,拆毀了中間阻隔的牆壁,就是隻方的仇恨,
15 Aliiondoa ile Sheria ya Wayahudi pamoja na amri zake na kanuni zake, ili kutokana na jamii hizo mbili aumbe jamii moja mpya katika umoja naye na hivyo kuleta amani.
並廢除了由規條命令所組成的法律,為把雙方在自己身上造成一個新人,而成就和平。
16 Kwa mwili wake, Kristo aliuangamiza uadui wao; kwa msalaba wake aliziunganisha jamii hizo kuwa moja na kuzipatanisha na Mungu.
祂以十字架誅滅了仇恨,也以十字架使雙方合成一體,與天主和好。
17 Basi, Kristo alikuja akahubiri Habari Njema ya amani kwenu ninyi watu wa mataifa mengine mliokuwa mbali na Mungu, na pia kwa Wayahudi ambao walikuwa karibu na Mungu.
所以祂來,向你們遠離的人傳布了和平的福音,也向那親近的人傳布了和平,
18 Hivyo, kwa njia yake, sisi sote, Wayahudi na watu wa mataifa mengine, tunaweza kumwendea Baba katika Roho mmoja.
因為藉著祂,我們雙方在一個聖神內,才得以進到父面前。
19 Basi, ninyi si wageni tena, wala si watu wa nje; ninyi ni raia pamoja na watu wa Mungu, na ni watu wa jamaa ya Mungu.
所以你們已不再是外方人或旅客,而是聖徒的同胞,是天主的家人;
20 Mmejengwa juu ya msingi uliowekwa na mitume na manabii, naye Kristo mwenyewe ndiye jiwe kuu la msingi.
已被建築在宗徒和先知的基礎上,而基督耶穌自己卻是這建築物的角石,
21 Yeye ndiye mwenye kulitengeneza jengo lote na kulikuza hata liwe hekalu takatifu kwa ajili ya B wana.
靠著祂,整個建築物結構緊湊,逐漸擴大,在主內成為一座聖殿;
22 Katika kuungana naye, ninyi pia mnajengwa pamoja na wote wengine, muwe makao ya Mungu kwa njia ya Roho wake.
並且靠著祂,你們也一同被建築,因著聖神,成為天主的住所。