< Matendo 8 >

1 Saulo naye alikiona kitendo hicho cha kumwua Stefano kuwa sawa. Siku hiyo kanisa la Yerusalemu lilianza kuteswa vibaya. Waumini wote, isipokuwa tu wale mitume, walilazimika kutawanyika katika sehemu za mashambani za Yudea na Samaria.
掃祿也贊同殺死他。就在那一日,發生了嚴厲迫害耶路撒冷教會的事;除宗徒外,眾人都逃散到猶太和撒瑪黎雅鄉間。
2 Watu wamchao Mungu, walimzika Stefano na kumfanyia maombolezo makubwa.
虔誠的人共同埋葬了斯德望,也為他大哭了一場。
3 Wakati huohuo, Saulo alijaribu kuliangamiza kanisa. Alikwenda katika kila nyumba, akawatoa nje waumini, wanaume kwa wanawake, akawatia gerezani.
掃祿想摧毀教會,進入各家,連男帶女都拉去,押到監裏。
4 Wale waumini waliotawanyika, walikwenda kila mahali wakihubiri ule ujumbe.
那些逃散的人經過各處,宣講真道的喜訊。
5 Naye Filipo aliingia katika mji wa Samaria na kumhubiri Kristo kwa wenyeji wa hapo.
斐理伯下到撒瑪黎雅城,給他們宣講基督。
6 Watu walijiunga kusikiliza kwa makini ule ujumbe wa Filipo na kuona ile miujiza aliyoifanya.
群眾都留意斐理伯所講的話,都同心合意地聽教,並看到了他所行的奇蹟。
7 Maana pepo wachafu waliokuwa wamewapagaa watu wengi waliwatoka wakipiga kelele kubwa; na pia watu wengi waliokuwa wamepooza viungo na waliolemaa waliponywa.
因為有許多附了邪魔的人,邪魔從他們身上大聲喊叫著出去了。有許多癱瘓和瘸子也被治好了。
8 Kukawa na furaha kubwa katika mji ule.
為此,那城裏的人皆大歡喜。
9 Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Simoni ambaye alikuwa amekwisha fanya uchawi wake katika mji huo kwa muda na kuwashangaza watu wa Samaria, akijiona kuwa yeye ni mtu maarufu.
有一個人,名叫西滿,曾在這城中行過邪術,使撒瑪黎雅的百姓驚服,並稱自己是一位大人物。
10 Watu wote, wadogo na wakubwa, walimsikiliza kwa makini wakisema, “Simoni ndiye ile nguvu ya kimungu inayoitwa Nguvu Kubwa.”
所有的人,從上到下,都聽從他,說:「這人就是那稱為神的大能者。」
11 Walivutiwa sana naye kwa vile alikuwa amewashangaza kwa uchawi wake kwa muda mrefu.
他們聽從他,是因為他很久以來,就用邪術使他們驚服;
12 Lakini walipouamini ujumbe wa Filipo juu ya Habari Njema ya Ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, walibatizwa, wanawake na wanaume.
但當他們信服了那傳報天主的國,和耶穌基督名字的斐理伯時,男女就都受了洗,
13 Hata Simoni aliamini; baada ya kubatizwa ilikuwa akiandamana na Filipo, akastaajabia maajabu na miujiza iliyokuwa inafanyika.
連西滿自己也信服了。他受洗以後,常隨從斐理伯;他看到所顯的奇蹟和大能,稱奇不止。
14 Wale mitume waliokuwa kule Yerusalemu walipopata habari kwamba wenyeji wa Samaria nao wamelipokea neno la Mungu, waliwatuma kwao Petro na Yohane.
當時,在耶路撒冷的宗徒,聽說撒瑪黎雅接受了天主的聖道,便打發伯多祿和若望往他們那裏去。
15 Walipofika waliwaombea hao waumini ili wampokee Roho Mtakatifu;
他們二人一到,就為他們祈禱,使他們領受聖神,
16 maana wakati huo Roho Mtakatifu hakuwa ameshukia yeyote kati yao; walikuwa wamebatizwa tu kwa jina la Bwana Yesu.
因為聖神還沒有降臨在任何人身上,他們只因主耶穌的名受過洗。
17 Basi, Petro na Yohane wakawawekea mikono hao waumini, nao wakampokea Roho Mtakatifu.
那時,宗徒便給他們覆手,他們就領受了聖神。
18 Hapo Simoni aling'amua kwamba kwa kuwekewa mikono ya mitume waumini walipewa Roho Mtakatifu. Hivyo aliwapa Petro na Yohane fedha akisema,
西滿看見藉宗徒們的覆手,賦給人聖神,遂獻給他們銀錢,
19 “Nipeni na mimi uwezo huo ili yeyote nitakayemwekea mikono, apokee Roho Mtakatifu.”
說:「你們也把這個權柄交給我,為叫我無論給誰覆手,誰就領受聖神。」
20 Lakini Petro akamjibu, “Potelea mbali na fedha zako kwa vile unafikiri kwamba unaweza kununua karama ya Mungu kwa fedha!
伯多祿卻向他說:「願你的銀錢與你一起喪亡!因為你想天主的恩賜可用銀錢買得。
21 Huna sehemu yoyote wala haki katika kazi hiyo kwa maana moyo wako hauko sawa mbele ya macho ya Mungu.
在這事上,你沒有股,也沒有分,因為你在天主前心懷不正。
22 Kwa hiyo, tubu ubaya wako huu na umwombe Bwana naye anaweza kukusamehe fikira kama hizo.
所以,你該回心轉意,擺脫你這個惡念,祈求主,或者可給你赦免你心中的妄想,
23 Ni dhahiri kwangu kwamba umejaa wivu mkali na mfungwa wa dhambi!”
因為我明知你心懷苦毒,並在邪惡的束縛中。」
24 Simoni akajibu, “Tafadhali, niombeeni kwa Bwana lisije likanipata lolote kati ya hayo mliyosema.”
西滿回答說:「請你們為我祈求主,好叫你們所說的,一點也不要降在我身上。」
25 Baada ya Petro na Yohane kutoa ushuhuda wao na kuutangaza ujumbe wa Bwana, walirudi Yerusalemu. Walipokuwa wanarudi walihubiri Habari Njema katika vijiji vingi vya Samaria.
二宗徒既作了證,並宣講了主的聖道,就返回耶路撒冷,一路在撒瑪黎雅人的許多鄉村中,宣講了福音。
26 Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, “Jitayarishe uende kusini kupitia njia inayotoka Yerusalemu kwenda Gaza.” (Njia hiyo hupita jangwani.)
上主的天使向斐理伯說:「起來,往南行,沿著由耶路撒冷下到迦薩的路走,即曠野中的那條路。」
27 Basi, Filipo akajiweka tayari, akaanza safari. Wakati huohuo kulikuwa na Mwethiopia mmoja, towashi, ambaye alikuwa anasafiri kuelekea nyumbani. Huyo mtu alikuwa ofisa maarufu wa hazina ya Kandake, malkia wa Ethiopia. Alikuwa amekwenda huko Yerusalemu kuabudu na wakati huo alikuwa anarudi akiwa amepanda gari la kukokotwa.
他就起來去了。看,有個厄提約丕雅人,是厄提約丕雅女王甘達刻的有權勢的太監,也是她寶庫的總管;他曾來到耶路撒冷朝聖。
28 Alipokuwa anasafiri, alikuwa akijisomea kitabu cha nabii Isaya.
他回去的時候,坐在車上誦讀依撒意亞先知。
29 Basi, Roho Mtakatifu akamwambia Filipo, “Nenda karibu na gari hilo ukafuatane nalo.”
聖神就向斐理伯說:「你上前去,走近這輛車子!」
30 Filipo akakimbilia karibu na gari, akamsikia huyo mtu akisoma katika kitabu cha nabii Isaya. Hapo Filipo akamwuliza, “Je, unaelewa hayo unayosoma?”
斐理伯就跑過去,聽見他誦讀依撒意亞先知,便說道: 「你明白所誦讀的嗎﹖」
31 Huyo mtu akamjibu, “Ninawezaje kuelewa bila mtu kunielewesha?” Hapo akamwalika Filipo apande juu, aketi pamoja naye.
他答說:「若沒有人指教我,怎麼能夠﹖」於是,請斐理伯上車與他同坐。
32 Basi, sehemu ya Maandiko Matakatifu aliyokuwa anasoma ilikuwa hii: “Alikuwa kama kondoo anayepelekwa kuchinjwa; kimya kama vile mwana kondoo anaponyolewa manyoya, yeye naye hakutoa sauti hata kidogo.
他所誦讀的那段經正是:『他如同被牽去宰殺的羊,又像羔羊在剪毛者前緘默,他也同樣不開口。
33 Alifedheheshwa na kunyimwa haki. Hakuna atakayeweza kuongea juu ya kizazi chake, kwa maana maisha yake yameondolewa duniani.”
在他屈辱之時,無人為他申辯。誰能描述他的後代呢﹖因為他的生命從地上被奪去了。』
34 Huyo Mwethiopia akamwambia Filipo, “Niambie, huyu nabii anasema juu ya nani? Anasema mambo haya juu yake yeye mwenyewe au juu ya mtu mwingine?”
太監向斐理伯發言說:「請你說: 先知說這話是指誰呢﹖是指自己或是指別人﹖」
35 Basi, Filipo akianzia na sehemu hiyo ya Maandiko Matakatifu, akamweleza Habari Njema juu ya Yesu.
斐理伯便開口,從這段經文開始,給他宣講了耶穌的福音。
36 Walipokuwa bado wanaendelea na safari walifika mahali penye maji na huyo ofisa akasema, “Mahali hapa pana maji; je, kuna chochote cha kunizuia nisibatizwe?”
他們沿路前行的時候,來到了一個有水的地方,那太監就說:「看,這裏有水;還有什麼阻擋我受洗呢﹖」
37 Filipo akasema, “Kama unaamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa.” Naye akajibu, “Naam, ninaamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.”
[斐理伯答說:「你若全心相信,便可以。」他答說:「我信耶穌基督就是天主子。」]
38 Basi, huyo ofisa akaamuru lile gari lisimame; na wote wawili, Filipo na huyo ofisa wakashuka majini, naye Filipo akambatiza.
他就命車停住,斐理伯和太監兩人下到水中,斐理伯給他付了洗。
39 Walipotoka majini Roho wa Bwana akamfanya Filipo atoweke. Na huyo Mwethiopia hakumwona tena; lakini akaendelea na safari yake akiwa amejaa furaha.
當他們從水中上來的時候,主的神把斐理伯提去,太監就再看不見他了。他就喜喜歡歡地往前行自己的路。
40 Filipo akajikuta yuko Azoto, akapita katika miji yote akihubiri Habari Njema mpaka alipofika Kaisarea.
斐理伯卻出現在阿左托,以後經過各城,宣講福音,直到凱撒勒雅。

< Matendo 8 >