< Matendo 26 >
1 Basi, Agripa akamwambia Paulo, “Unaruhusiwa kujitetea.” Hapo Paulo alinyosha mkono wake akajitetea hivi:
Then Agrippa said to Paul, "You are permitted to speak for yourself." So Paul stretched forth his hand and began to make his defense.
2 “Mfalme Agripa, ninajiona mwenye bahati leo kujitetea mbele yako kuhusu yale mashtaka yote ambayo Wayahudi walikuwa wamesema juu yangu.
"I think myself happy, King Agrippa, that I am to make my defense before you this day, in regard to all the accusations brought against me by the Jews;
3 Hasa kwa vile wewe mwenyewe ni mtaalamu wa desturi za Wayahudi na migogoro yao, ninakuomba basi unisikilize kwa uvumilivu.
"especially since you are an export in all Jewish customs and questions. I pray you, expert in all Jewish customs and questions. I pray you, hear me with patience.
4 “Wayahudi wanajua habari za maisha yangu tangu utoto, jinsi nilivyoishi tangu mwanzo kati ya taifa langu huko Yerusalemu.
"The kind of life I have lived from my youth upward among my own nation and at Jerusalem, all that early life of mine, is well known to all the Jews.
5 Wananifahamu kwa muda mrefu, na wanaweza kushuhudia, kama wakipenda, kwamba tangu mwanzo niliishi kama mmoja wa kikundi chenye siasa kali zaidi katika dini yetu, yaani kikundi cha Mafarisayo.
"They know me of old, if they are willing to testify, how that according to the strict sect of our religion, I lived a Pharisee.
6 Na sasa niko hapa nihukumiwe kwa sababu ninaitumainia ile ahadi ambayo Mungu aliwaahidia babu zetu.
"Today I am standing trial because of the hope of the promise made by God to our ancestors,
7 Ahadi hiyo ndiyo ileile inayotumainiwa na makabila kumi na mawili ya taifa letu, wakimtumikia Mungu kwa dhati mchana na usiku. Mheshimiwa mfalme, Wayahudi wananishtaki kwa sababu ya tumaini hilo!
"a promise which our twelve tribes, earnestly serving God night and day, hope to attain. It is concerning this hope, King Agrippa, that I am accused by the Jews.
8 Kwa nini ninyi mnaona shida sana kuamini kwamba Mungu huwafufua wafu?
"Why is it deemed incredible by you all, if God raises the dead?
9 Kwa kweli mimi mwenyewe niliamini kwamba ni wajibu wangu kufanya mambo mengi kulipinga jina la Yesu wa Nazareti.
"I indeed once thought with myself that I ought to do many things against the name of Jesus, the Nazarene.
10 Mambo hayo ndiyo niliyoyafanya huko Yerusalemu. Mimi binafsi, nikiwa nimepewa mamlaka kutoka kwa makuhani wakuu, nilipata kuwatia gerezani wengi wa watu wa Mungu. Nao walipohukumiwa kuuawa, nilipiga kura ya kukubali.
"And this also I did in Jerusalem. Armed with authority from the chief priests, I shut up many of the saints in prison, and when they were condemned to death I gave my vote against them.
11 Mara nyingi niliwafanya waadhibiwe katika masunagogi yote nikiwashurutisha waikane imani yao. Hasira yangu kwao ilikuwa kubwa hata nikawasaka mpaka miji ya mbali.
"In all the synagogues also I punished them oftentimes, and tried to make them blaspheme; and in my mad fury I was pursuing them even to foreign cities.
12 “Kwa mujibu huohuo, nilikwenda Damasko wakati mmoja, nikiwa na mamlaka na maagizo kutoka kwa makuhani wakuu.
"On this errand I was traveling to Damascus one day, armed with authority and commission of the chief priests,
13 Mheshimiwa, wakati nilipokuwa njiani, saa sita mchana, niliona mwanga mkubwa kuliko wa jua ukiangaza kutoka mbinguni, ukanizunguka mimi na wale wasafiri wenzangu.
"when at noon, as I journeyed, O King, I saw a light from heaven, brighter than the sun, shining around me and around those who journeyed with me.
14 Sisi sote tulianguka chini, nami nikasikia sauti ikiniambia kwa Kiebrania: Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa? Unajiumiza bure kama punda anayepiga teke fimbo ya bwana wake.
"We all fell to the ground; and I heard a voice saying to me in Hebrew. "‘Saul, Saul, why are you persecuting me? It is hard for you to kick against the goad.’
15 Mimi nikauliza: Ni nani wewe Bwana? Naye Bwana akajibu: Mimi ni Yesu ambaye wewe unamtesa.
"‘Who are you, Lord?’ I said. "And the Lord said. ‘I am Jesus whom you are persecuting.
16 Haidhuru, inuka sasa; simama wima. Nimekutokea ili nikuweke rasmi kuwa mtumishi wangu. Utawathibitishia watu wengine mambo uliyoyaona leo na yale ambayo bado nitakuonyesha.
"‘But rise and stand on your feet, for I have appeared to you in order to appoint you my minister and my witness both of what you have already seen and of those things in which I will appear to you.
17 Nitakuokoa na watu wa Israeli na watu wa mataifa mengine ambao mimi ninakutuma kwao.
"‘I will deliver you from the Jewish people, and from the Gentiles to whom I am sending you to open their eyes
18 Utayafumbua macho yao na kuwawezesha watoke gizani na kuingia katika mwanga; watoke katika utawala wa Shetani, wamgeukie Mungu; ili kwa kuamini, wapate kusamehewa dhambi na kuchukua nafasi yao kati ya wale ambao wamepata kuwa watu wa Mungu.
"‘so that they may turn from darkness to light, and from the power of Satan unto God, in order to receive remission of sins and an inheritance among those who are sanctified by faith in me.’
19 “Hivyo, mfalme Agripa, sikuweza kuwa mkaidi kwa maono hilo la mbinguni.
"So then, O King Agrippa, I was not disobedient unto the heavenly vision;
20 Ila nilianza kuhubiri kwanza kwa watu wa Damasko, halafu kwa wale wa Yerusalemu na nchi yote ya Yudea, na pia kwa watu wa mataifa mengine. Niliwahimiza wamgeukie Mungu na kuonyesha kwa vitendo kwamba wamebadilisha mioyo yao.
"but I proceeded to preach, first to those in Damascus, and then in Jerusalem and throughout all the country of Judea, and also to the Gentiles, that they must repent and turn to God and do deeds worthy of repentance.
21 Kwa sababu hiyo, Wayahudi walinikamata nikiwa Hekaluni, wakajaribu kuniua.
"For this reason the Jews seized me in the temple, and tried to kill me.
22 Lakini Mungu alinisaidia; na hivyo mpaka siku ya leo nimesimama imara nikitoa ushuhuda kwa wote, wakubwa na wadogo. Ninayosema ni yale ambayo manabii na Mose walisema yatatukia;
"But having obtained the help that comes from God, I stand even to this day witnessing both to small and great, saying nothing except what the prophets and Moses said should come;
23 yaani ilimpasa Kristo ateseke na kuwa wa kwanza kufufuka kutoka wafu, ili atangaze kwamba mwanga wa ukombozi unawaangazia sasa watu wote, Wayahudi na pia watu wa mataifa mengine.”
"how that the Christ must suffer, and how he should be the first to rise from the dead, and should bring a message of light to the Jewish people and to the Gentiles."
24 Paulo alipofika hapa katika kujitetea kwake, Festo alisema kwa sauti kubwa, “Paulo! Una wazimu! Kusoma kwako kwingi kunakutia wazimu!”
As Paul thus made his defense, Festus exclaimed in a loud voice. "Paul, you are raving mad; your great learning is driving you mad."
25 Lakini Paulo akasema, “Sina wazimu mheshimiwa Festo: Ninachosema ni ukweli mtupu.
"I am not mad, most noble Festus," said Paul,
26 Wewe Mfalme unayafahamu mambo haya, kwa hiyo ninaweza kuongea bila uoga mbele yako. Sina mashaka kwamba matukio hayo yanajulikana kwako maana jambo hili halikutendeka mafichoni.
"I am speaking words of sober truth. For the King, to whom I am speaking freely, knows of these matters. I am persuaded that not one of these things has escaped his notice; for these things were not done in a corner.
27 Mfalme Agripa, je, una imani na manabii? Najua kwamba unaamini.”
"King Agrippa, do you believe the prophets? I know that you believe."
28 Agripa akamjibu Paulo, “Kidogo tu utanifanya Mkristo!”
Agrippa answered, "In short, you are doing your best to persuade me to become a Christian."
29 Paulo akamjibu, “Namwomba Mungu kwamba, kwa muda mfupi au mrefu, si wewe tu bali wote wanaonisikia leo wapate kuwa kama nilivyo mimi, lakini bila hii minyororo.”
"Long or short," answered Paul, "my prayer to God is that not only you but all who are my hearers this day might become such as I am, save for these chains."
30 Hapo mfalme Agripa, mkuu wa mkoa, Bernike na wale wote waliokuwa pamoja nao, walisimama.
Then the king rose, and Bernice, and those who were sitting with him.
31 Walipokwisha ondoka, waliambiana, “Mtu huyu hakufanya chochote kinachostahili adhabu ya kifo au kifungo.”
When they had withdrawn they continued talking to one another. "This man is doing nothing," they said, "for which he deserves death or imprisonment."
32 Naye Agripa akamwambia Festo, “Mtu huyu angeweza kufunguliwa kama asingalikuwa amekata rufani kwa Kaisari.”
And Agrippa said to Festus, "If he had not appealed to Caesar, he might have been set free."