< 2 Timotheo 1 >

1 Mimi Paulo, ambaye Mungu alitaka niwe mtume wa Kristo Yesu ili niutangaze ule uzima tulioahidiwa katika kuungana na Kristo Yesu,
PAUL, a legate of Jesus the Messiah by the pleasure of God, according to the promise of life which is in Jesus the Messiah;
2 nakuandikia wewe mwanangu mpenzi Timotheo. Nakutakia neema, huruma na amani kutoka kwa Mungu Baba na Kristo Yesu Bwana wetu.
to Timothy a beloved son; grace, and mercy, and peace, from God the Father, and from our Lord Jesus the Messiah.
3 Ninamshukuru Mungu ambaye ninamtumikia kwa dhamiri safi kama walivyofanya wazee wangu; namshukuru kila ninapokukumbuka daima katika sala zangu.
I thank God, whom I serve from my forefathers with a pure conscience, that I continually remember thee in my prayers, by night and by day:
4 Nakumbuka machozi yako na ninatamani usiku na mchana kukuona, ili nijazwe furaha.
and I desire to see thee, and I call to mind thy tears; that I may be filled with joy,
5 Naikumbuka imani yako ya kweli, imani aliyokuwa nayo nyanya yako Loisi, na pia mama yako Eunike. Nina hakika kwamba wewe pia unayo.
by the recollection which I have, by thy genuine faith, which dwelt first in thy grandmother Lois, and in thy mother Eunice, and also, I am persuaded, in thee.
6 Ndio maana nakukumbusha ukiweke motomoto kile kipaji ulichopewa na Mungu wakati nilipokuwekea mikono yangu.
Wherefore I remind thee, that thou excite the gift of God, that is in thee by the imposition of my hands.
7 Kwa maana Mungu hakutupa Roho wa kutufanya tuwe waoga, bali alitupa Roho wa kutujalia nguvu, upendo na nidhamu.
For God hath not given us a spirit of fear, but of energy, and of love, and of instruction.
8 Basi, usione haya kumshuhudia Bwana wetu, wala usione haya kwa sababu yangu mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Lakini shiriki katika mateso kwa ajili ya Habari Njema, kadiri ya nguvu unazopewa na Mungu.
Therefore be not thou ashamed of the testimony of our Lord, nor of me his prisoner; but endure evils in connection with the Gospel, through the power of God;
9 Yeye alituokoa, akatuita tuwe watu wake yeye mwenyewe, si kwa sababu ya matendo yetu wenyewe bali kwa sababu ya kusudi lake na neema yake. Alitujalia neema hiyo katika Kristo Yesu kabla mwanzo wa nyakati; (aiōnios g166)
who hath vivified us, and called us with a holy calling; not according to our works, but according to his good pleasure, and his grace that was given us in Jesus the Messiah from time before the ages, (aiōnios g166)
10 lakini sasa imefunuliwa kwetu kwa kuja kwake Mwokozi wetu Yesu Kristo. Yeye amekomesha nguvu za kifo, na kwa njia ya Habari Njema akadhihirisha uzima usio kufa.
and is now made known by the appearing of our Vivifier, Jesus the Messiah; who hath abolished death, and hath made manifest life and immortality, by the gospel:
11 Mungu amenichagua mimi niwe mtume na mwalimu kwa ajili ya kuhubiri Habari Njema,
of which I am constituted a herald and a legate, and a teacher of the Gentiles.
12 nami nateseka mambo haya kwa sababu hiyo. Lakini niko bado timamu kabisa kwani namjua yule niliyemwamini, tena nina hakika kwamba yeye aweza kukilinda salama kile alichonikabidhi, mpaka Siku ile.
Therefore I suffer these things: and I am not ashamed; for I know in whom I have believed, and I am persuaded that he is competent to keep for me my deposit against that day.
13 Shika kwa makini mafundisho yale ya kweli niliyokufundisha, na kubaki katika hiyo imani na huo upendo wetu katika kuungana na Kristo Yesu.
Let the form of sound words, which thou hast heard from me, abide with thee; with faith and love, in Jesus the Messiah.
14 Jambo lile bora ulilokabidhiwa lilinde kwa nguvu ya Roho Mtakatifu anayeishi ndani yetu.
Keep thou the good deposit, by the Holy Spirit who dwelleth in us.
15 Kama unavyojua, watu wote mkoani Asia wameniacha, miongoni mwao wakiwa Fugelo na Hermogene.
This thou knowest, that all those in Asia have turned from me; and that among them are Phygellus and Hermogenes.
16 Bwana aihurumie jamaa ya Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha rohoni mara nyingi, wala hakuona haya kwa kuwa nilikuwa kifungoni,
May our Lord bestow mercy on the house of Onesiphorus; for, many times, he refreshed me, and was not ashamed of the chains of my imprisonment.
17 ila mara tu alipofika Roma, alianza kunitafuta kwa bidii mpaka akanipata.
But also, when he came to Rome, he sought for me with diligence, and found me.
18 Bwana amjalie huruma katika Siku ile! Nawe wajua vizuri mengi aliyonifanyia huko Efeso.
May our Lord grant him, that he may find mercy with our Lord, in that day. And how he ministered to me at Ephesus, thou very well knowest.

< 2 Timotheo 1 >