< 2 Timotheo 4 >
1 Nakuamuru mbele ya Mungu, na mbele ya Kristo Yesu atakayewahukumu watu walio hai na wafu, na kwa sababu anakuja kutawala akiwa Mfalme:
testificor coram Deo et Christo Iesu qui iudicaturus est vivos ac mortuos et adventum ipsius et regnum eius
2 hubiri huo ujumbe, sisitiza kuutangaza (iwe ni wakati wa kufaa au wakati usiofaa), karipia, onya na himiza watu ukiwafundisha kwa uvumilivu wote.
praedica verbum insta oportune inportune argue obsecra increpa in omni patientia et doctrina
3 Utakuja wakati ambapo watu hawatasikiliza mafundisho ya kweli, ila watafuata tamaa zao wenyewe na kujikusanyia walimu tele watakaowaambia mambo yale tu ambayo masikio yao yako tayari kusikia.
erit enim tempus cum sanam doctrinam non sustinebunt sed ad sua desideria coacervabunt sibi magistros prurientes auribus
4 Watakataa kuusikia ukweli, watageukia hadithi za uongo.
et a veritate quidem auditum avertent ad fabulas autem convertentur
5 Wewe, lakini, uwe macho katika kila hali; vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Habari Njema, timiza kikamilifu utumishi wako.
tu vero vigila in omnibus labora opus fac evangelistae ministerium tuum imple
6 Kwa upande wangu mimi, niko karibu kabisa kutolewa dhabihu na wakati wa kufariki kwangu umefika.
ego enim iam delibor et tempus meae resolutionis instat
7 Nimefanya bidii katika mashindano, nimemaliza safari yote na imani nimeitunza.
bonum certamen certavi cursum consummavi fidem servavi
8 Na sasa imebakia tu kupewa tuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu, tuzo ambalo Bwana Hakimu wa haki, atanipa mimi Siku ile na wala si mimi tu, ila na wale wote wanaotazamia kwa upendo kutokea kwake.
in reliquo reposita est mihi iustitiae corona quam reddet mihi Dominus in illa die iustus iudex non solum autem mihi sed et his qui diligunt adventum eius
9 Fanya bidii kuja kwangu karibuni.
festina venire ad me cito
10 Dema ameupenda ulimwengu huu akaniacha na kwenda zake Thesalonike. Kreske amekwenda Galatia, na Tito amekwenda Dalmatia. (aiōn )
Demas enim me dereliquit diligens hoc saeculum et abiit Thessalonicam Crescens in Galliam Titus in Dalmatiam (aiōn )
11 Luka peke yake ndiye aliye hapa pamoja nami. Mpate Marko uje naye, kwa maana ataweza kunisaidia katika kazi yangu.
Lucas est mecum solus Marcum adsume et adduc tecum est enim mihi utilis in ministerium
12 Nilimtuma Tukiko kule Efeso.
Tychicum autem misi Ephesum
13 Utakapokuja niletee koti langu nililoacha kwa Karpo kule Troa; niletee pia vile vitabu, na hasa vile vilivyotengenezwa kwa ngozi.
paenulam quam reliqui Troade apud Carpum veniens adfers et libros maxime autem membranas
14 Yule sonara aitwaye Aleksanda amenitendea maovu mengi; Bwana atamlipa kufuatana na hayo matendo yake.
Alexander aerarius multa mala mihi ostendit reddat ei Dominus secundum opera eius
15 Jihadhari naye kwa sababu aliupinga ujumbe wetu kwa ukali.
quem et tu devita valde enim restitit verbis nostris
16 Wakati nilipojitetea kwa mara ya kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu; wote waliniacha. Mungu asiwahesabie kosa hilo!
in prima mea defensione nemo mihi adfuit sed omnes me dereliquerunt non illis reputetur
17 Lakini, Bwana alikaa pamoja nami, akanipa nguvu, hata nikaweza kuutangaza ujumbe wote, watu wa mataifa wausikie; tena nikaokolewa katika hukumu ya kifo kama kinywani mwa simba.
Dominus autem mihi adstitit et confortavit me ut per me praedicatio impleatur et audiant omnes gentes et liberatus sum de ore leonis
18 Bwana ataniokoa na mambo yote maovu, na kunichukua salama mpaka katika Utawala wake wa mbinguni. Kwake uwe utukufu milele na milele! Amina. (aiōn )
liberabit me Dominus ab omni opere malo et salvum faciet in regnum suum caeleste cui gloria in saecula saeculorum amen (aiōn )
19 Wasalimu Priska na Akula, pamoja na jamaa ya Onesiforo.
saluta Priscam et Aquilam et Onesifori domum
20 Erasto alibaki Korintho, naye Trofimo nilimwacha Mileto kwa sababu alikuwa mgonjwa.
Erastus remansit Corinthi Trophimum autem reliqui infirmum Mileti
21 Fanya bidii kuja kabla ya majira ya baridi. Ebulo, Pude, Lino na Klaudia wanakusalimu; vilevile ndugu wengine wote.
festina ante hiemem venire salutat te Eubulus et Pudens et Linus et Claudia et fratres omnes
22 Bwana awe nawe rohoni mwako. Nawatakieni nyote neema.
Dominus Iesus cum spiritu tuo gratia nobiscum amen