< 2 Timotheo 3 >
1 Kumbuka kwamba, katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za taabu.
But understand this: In the last days terrible times will come.
2 watu watakuwa na ubinafsi, wenye tamaa ya fedha, wenye majivuno, wenye kujiona, wenye kumtukana Mungu, wasiowatii wazazi wao, wasio na shukrani na waovu;
For men will be lovers of themselves, lovers of money, boastful, arrogant, abusive, disobedient to their parents, ungrateful, unholy,
3 watatokea watu wasio na upendo moyoni, wasio na huruma, wachongezi, walafi na wakali; watachukia chochote kilicho chema;
unloving, unforgiving, slanderous, without self-control, brutal, without love of good,
4 watakuwa wahaini, wakaidi na waliojaa kiburi; watapenda anasa kuliko kumpenda Mungu.
traitorous, reckless, conceited, lovers of pleasure rather than lovers of God,
5 Kwa nje wataonekana kama watu wenye kumcha Mungu, lakini wataikana nguvu yake. Jiepushe kabisa na watu wa namna hiyo.
having a form of godliness but denying its power. Turn away from such as these!
6 Baadhi yao huenda katika nyumba za watu na huwateka wanawake dhaifu waliolemewa mizigo ya dhambi na ambao wanaongozwa na tamaa za kila aina;
They are the kind who worm their way into households and captivate vulnerable women who are weighed down with sins and led astray by various passions,
7 wanawake ambao wanajaribu daima kujifunza lakini hawawezi kuufikia ujuzi wa huo ukweli.
who are always learning but never able to come to a knowledge of the truth.
8 Watu hao huupinga ukweli kama vile Yane na Yambre walivyompinga Mose.
Just as Jannes and Jambres opposed Moses, so also these men oppose the truth. They are depraved in mind and disqualified from the faith.
9 Lakini hawataweza kuendelea zaidi kwa maana upumbavu wao utaonekana wazi kwa wote. Ndivyo ilivyokuwa kwa akina Yane na Yambre.
But they will not advance much further. For just like Jannes and Jambres, their folly will be plain to everyone.
10 Wewe lakini, umeyafuata mafundisho yangu, mwenendo wangu, makusudi yangu katika maisha, imani yangu, uvumilivu wangu, upendo wangu, subira yangu,
You, however, have observed my teaching, my conduct, my purpose, my faith, my patience, my love, my perseverance,
11 udhalimu na mateso yangu. Unayajua mambo yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Lustra. Nilivumilia udhalimu mkubwa mno! Lakini Bwana aliniokoa katika mambo hayo yote.
my persecutions, and the sufferings that came upon me in Antioch, Iconium, and Lystra. What persecutions I endured! Yet the Lord rescued me from all of them.
12 Kila mtu anayetaka kuishi maisha ya kumcha Mungu katika kuungana na Kristo Yesu lazima adhulumiwe.
Indeed, all who desire to live godly lives in Christ Jesus will be persecuted,
13 Watu waovu na wadanyanyifu watazidi kuwa waovu zaidi na zaidi kwa kuwadanganya wengine na kudanganyika wao wenyewe.
while evil men and imposters go from bad to worse, deceiving and being deceived.
14 Lakini wewe dumu katika ukweli ule uliofundishwa, ukaukubali kabisa. Unawajua wale waliokuwa walimu wako.
But as for you, continue in the things you have learned and firmly believed, since you know from whom you have learned them.
15 Unakumbuka kwamba tangu utoto wako umeyajua Maandiko Matakatifu ambayo yaweza kukupatia hekima iletayo wokovu kwa njia ya imani kwa Kristo Yesu.
From infancy you have known the Holy Scriptures, which are able to make you wise for salvation through faith in Christ Jesus.
16 Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yanafaa katika kufundishia ukweli, kuonya, kusahihisha makosa, na kuwaongoza watu waishi maisha adili,
All Scripture is God-breathed and is useful for instruction, for conviction, for correction, and for training in righteousness,
17 ili mtu anayemtumikia Mungu awe mkamilifu, na tayari kabisa kufanya kila tendo jema.
so that the man of God may be complete, fully equipped for every good work.