< 2 Timotheo 2 >

1 Basi, wewe mwanangu, uwe na nguvu katika neema tunayopata katika kuungana na Kristo Yesu.
You therefore, my child, be strengthened in the grace that is in Christ Jesus.
2 Chukua yale mafundisho uliyonisikia nikitangaza mbele ya mashahidi wengi, uyakabidhi kwa watu wanaoaminika, ambao wataweza kuwafundisha wengine pia.
The things which you have heard from me amongst many witnesses, commit the same things to faithful men who will be able to teach others also.
3 Shiriki katika mateso kama askari mwaminifu wa Kristo yesu.
You therefore must endure hardship as a good soldier of Christ Jesus.
4 Mwanajeshi vitani hujiepusha na shughuli za maisha ya kawaida ili aweze kumpendeza mkuu wa jeshi.
No soldier on duty entangles himself in the affairs of life, that he may please him who enrolled him as a soldier.
5 Mwanariadha yeyote hawezi kushinda na kupata zawadi ya ushindi kama asipozitii sheria za michezo.
Also, if anyone competes in athletics, he isn’t crowned unless he has competed by the rules.
6 Mkulima ambaye amefanya kazi ngumu anastahili kupata sehemu ya kwanza ya mavuno.
The farmer who labours must be the first to get a share of the crops.
7 Fikiria hayo ninayosema, kwani Bwana atakuwezesha uyaelewe yote.
Consider what I say, and may the Lord give you understanding in all things.
8 Mkumbuke Yesu Kristo aliyefufuliwa kutoka wafu, aliyekuwa wa ukoo wa Daudi, kama isemavyo Habari Njema ninayoihubiri.
Remember Jesus Christ, risen from the dead, of the offspring of David, according to my Good News,
9 Kwa sababu ya kuihubiri Habari Njema mimi nateseka na nimefungwa minyororo kama mhalifu. Lakini neno la Mungu haliwezi kufungwa minyororo,
in which I suffer hardship to the point of chains as a criminal. But God’s word isn’t chained.
10 na hivyo navumilia kila kitu kwa ajili ya wateule wa Mungu, ili wao pia wapate ukombozi upatikanao kwa njia ya Yesu Kristo, na ambao huleta utukufu wa milele. (aiōnios g166)
Therefore I endure all things for the chosen ones’ sake, that they also may obtain the salvation which is in Christ Jesus with eternal glory. (aiōnios g166)
11 Usemi huu ni wa kweli: “Ikiwa tulikufa pamoja naye, tutaishi pia pamoja naye.
This saying is trustworthy: “For if we died with him, we will also live with him.
12 Tukiendelea kuvumilia, tutatawala pia pamoja naye. Tukimkana, naye pia atatukana.
If we endure, we will also reign with him. If we deny him, he also will deny us.
13 Tukikosa kuwa waaminifu, yeye hubaki mwaminifu daima, maana yeye hawezi kujikana mwenyewe.”
If we are faithless, he remains faithful; for he can’t deny himself.”
14 Basi, wakumbushe watu wako mambo haya, na kuwaonya mbele ya Mungu waache ubishi juu ya maneno. Ubishi huo haufai, ila huleta tu uharibifu mkuu kwa wale wanaousikia.
Remind them of these things, charging them in the sight of the Lord that they don’t argue about words to no profit, to the subverting of those who hear.
15 Jitahidi kupata kibali kamili mbele ya Mungu kama mfanyakazi ambaye haoni haya juu ya kazi yake, na ambaye hufundisha sawa ule ujumbe wa kweli.
Give diligence to present yourself approved by God, a workman who doesn’t need to be ashamed, properly handling the Word of Truth.
16 Jiepushe na majadiliano ya kidunia na ya kipumbavu; kwani hayo huzidi kuwatenga watu mbali na Mungu.
But shun empty chatter, for it will go further in ungodliness,
17 Mafundisho ya aina hiyo ni kama donda linalokula mwili. Miongoni mwa hao waliofundisha hayo ni Humenayo na Fileto.
and those words will consume like gangrene, of whom is Hymenaeus and Philetus:
18 Hawa wamepotoka kabisa mbali na ukweli, na wanatia imani ya watu wengine katika wasiwasi kwa kusema ati ufufuo wetu umekwisha fanyika.
men who have erred concerning the truth, saying that the resurrection is already past, and overthrowing the faith of some.
19 Lakini msingi thabiti uliowekwa na Mungu uko imara, na juu yake yameandikwa maneno haya: “Bwana anawafahamu wale walio wake,” na “Kila asemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachane na uovu.”
However, God’s firm foundation stands, having this seal: “The Lord knows those who are his,” and, “Let every one who names the name of the Lord depart from unrighteousness.”
20 Katika nyumba kubwa kuna mabakuli na vyombo vya kila namna: vingine ni vya fedha na dhahabu, vingine vya mbao na udongo, vingine ni vya matumizi ya pekee na vingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
Now in a large house there are not only vessels of gold and of silver, but also of wood and of clay. Some are for honour and some for dishonour.
21 Basi, kama mtu atajitakasa kwa kujitenga mbali na mambo hayo yote maovu, atakuwa chombo cha matumizi ya pekee, kwa sababu amewekwa wakfu, anamfaa Bwana wake na yupo tayari kwa kila kazi njema.
If anyone therefore purges himself from these, he will be a vessel for honour, sanctified, and suitable for the master’s use, prepared for every good work.
22 Jiepushe na tamaa za ujana, fuata uadilifu, imani, upendo, amani, pamoja na watu wote ambao wanamwomba Bwana kwa moyo safi.
Flee from youthful lusts; but pursue righteousness, faith, love, and peace with those who call on the Lord out of a pure heart.
23 Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu; wajua kwamba hayo huleta magomvi.
But refuse foolish and ignorant questionings, knowing that they generate strife.
24 Mtumishi wa Bwana asigombane. Anapaswa kuwa mpole kwa watu wote, mwalimu mwema na mvumilivu,
The Lord’s servant must not quarrel, but be gentle towards all, able to teach, patient,
25 ambaye ni mpole anapowaonya wapinzani wake, kwani huenda Mungu akawajalia nafasi ya kutubu, wakapata kuujua ukweli.
in gentleness correcting those who oppose him. Perhaps God may give them repentance leading to a full knowledge of the truth,
26 Hapo fahamu zao zitawarudia tena, wakaponyoka katika mtego wa Ibilisi aliyewanasa na kuwafanya wayatii matakwa yake.
and they may recover themselves out of the devil’s snare, having been taken captive by him to do his will.

< 2 Timotheo 2 >